Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

INVISIBLE 

A Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa. 

Rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA KWANZA

★★★★★★★★★★★★★

 

Niliamka kutoka usingizini na kutazama ndani ya chumba nilichokuwa nimelala. Mwanga ulikuwa umetawala vyema, nami nikajisogeza kwenye upande wa pembeni wa kitanda kisha kuiwasha simu niangalie saa. Ilikuwa saa 4 asubuhi, na jambo hilo halikunishangaza kutokana na tabia niliyokuwa nayo ya kulala nimechelewa sana. Mambo yaliyofanya nichelewe kulala hasa ilikuwa ni kazi za kiofisi nilizofanya hadi usiku wa manane.

Nikanyanyuka kutoka kitandani kivivu, bila haraka yoyote, kwa kuwa leo singekwenda kazini. Ilikuwa sikukuu ya Iddi na ndiyo sababu nilijiamini vya kutosha kulala mpaka saa 4. Boss wangu angenitafuna kama ningechelewa namna ile siku ya kazi. Nikaingia mlango wa bafuni, bafu ambalo lilikuwa humo humo ndani ya chumba hiki pamoja na choo, kisha nikafanya usafi wa mwili kama kawaida yangu.

Usiku wa jana sikucheleweshwa kulala na kazi, bali ilikuwa kwa sababu ya kuchat na washkaji zangu na kuperuzi mitandao ya kijamii baada ya kutoka kuangalia movie mbili. Nilikuwa na laptop aina ya Samsung, niliyoiwekea makolokolo mengi ya kazini na movie na muziki. Nilipenda sana movie pamoja na katuni. 

Baada ya kumaliza kuoga, nilitoka bafuni na kurudi kuvaa nguo. Kwa kuwa sikuwa na mpango wa kutoka, niliamua tu kukaa ndani siku hiyo na kuangalia movie. Kama ni siku ya mapumziko kwangu, basi masuala ya kazi ilikuwa tupa kule. Nilikuwa na TV iliyounganishiwa waya wa cable, hivyo nikaiwasha na kuweka channel ya muziki. Niliona muziki uliokuwepo unaboa, kwa hiyo nikawa natafuta chaneli nyingine nzuri ambayo ingekuwa na kipindi chenye kuburudisha. Baada ya kuzunguka kwa kuzirudia-rudia, nikaacha kwenye chaneli ya Nickelodeon, ambayo ilionesha katuni. 

Niliwasha jiko langu dogo la gesi ili kupasha chai. Nikaiweka kwenye kikombe baada ya kupata moto, kisha nikakaa kwenye sofa langu moja lililokuwa humo. Nilishika simu na kuanza kuangalia udaku insta, nikishushia na chai yangu taratibu. Nilizama sana kwenye simu kiasi kwamba sikutambua jinsi muda ulivyopita haraka sana. Nikasikia mlango wangu ukigongwa na kwenda kuufungua.

"Woyooo!" nikasema kwa shauku.

"Ah mzee mzima nakuona ndani ya bukta. Tai mbona hujavaa?" akasema mtu aliyesimama mlangoni pale. 

Huyu alikuwa Justine. Alikuwa rafiki yangu na tulifanya kazi pamoja. Nilikuwa najua angekuja leo, lakini sikutarajia afike muda huo.

"We fala nini... nimeificha kwa ndani. Ebu ingia bana," nikamwambia kiutani. 

Aliingia kisha nikafunga mlango. Alibeba mfuko mkubwa kiasi mkononi, nami tayari ningeweza kukisia kulikuwa na nini ndani yake. Tulikuwa tumepanga aje kwangu leo tukae na kupoteza muda kwa kupeana company. Haikuwa mara yake ya kwanza kufika hapa, alikuwa ameshakuja mara kadhaa kipindi cha nyuma.

"Mbona umewahi sana?" nikamuuliza.

"Hivi unajua sa'hivi sa'ngapi?" akaniuliza pia.

Nikachukua simu na kushangaa baada ya kuangalia muda. "Eeh! Saa saba! Ilikuwa saa 5 tu sa'hivi!" 

"Unapenda mno makatuni bwege wewe."

"Dah mwanangu ubarikiwe. Katuni ndiyo maisha yangu. Em' leta msosi huo," nilimwambia huku nikiuchukua ule mfuko aliobeba. Baada ya kuchungulia ndani nikamwambia, "aaaaa oya umechakachua."

"Nimechakachua nini sasa?" akaniuliza huku akiwa ameshaketi kwenye sofa lile.

"Ulipaswa uje na nyama kilo mbili hapa, hii ni nusu. Umeilia njiani?"

"Bwege wewe, umeniona?"

"Tulia hapo hapo, nakuja kuitoa," nikamwambia na kisha kufata kisu. 

Nilimfata na kuanza kumtania kuwa nalikata tumbo lake ili niitoe nyama aliyokula njiani. Tulipenda sana kutaniana na Justine. Tulikuwa tumepanga kuwa siku hiyo tungenunua nyama choma na kuipiga na vinywaji. Na ndiyo vitu vilivyokuwa ndani ya mfuko aliobeba. Kwa nje tuliweza kusikia sauti ya juu ya muziki, labda ya watu waliosherehekea sikukuu. Nikaanza kuzishughulikia nyama zile kwa kuzitengenezea 'roast' nzuri yenye pilipili, ili tuje tuzikamue na vinywaji vyetu. Tulikuwa tukipiga story muda wote na kucheka pamoja. 

Mambo yetu ya makamuzi yalipokaa sawa na tayari, niliweka vitu vile chini na sote tukaketi ili tuanze kukamua. Justine alikuwa ametoa chaneli yangu ya katuni, hivyo nikaifata remote kuirudisha. Alianza kuniita mimi pimbi na kwamba ninaboa kwa kuwa aliziona katuni kuwa za watoto; lakini hakujua sababu iliyofanya nizipende. 

Nilifungua kinywaji changu; Grand Malta ya kopo, na kunywa kidogo. Justine alikuwa na bia kama zote, lakini mimi sikupendelea bia. Kiukweli, sikuwahi kunywa bia. Wine kadhaa nilikuwa nakunywa kipindi cha nyuma, lakini sasa ulikuwa umepita muda sijaweka kileo mdomoni.

Baada ya kutosheka, nilinyanyuka kwenda kunawa mikono bafuni. Justine bado alikuwa anagombana na mifupa ya nyama. Nilimwangalia na kucheka sana. Alipenda nyama mno. Hazikupita dakika nyingi nikasikia mlango wangu ukigongwa tena. Justine alinitazama na kuniuliza kama kulikuwa na mtu mwingine anakuja, nami nikakataa. Nikanyanyuka kutoka kitandani nilipokuwa nimeketi na kwenda kuufungua mlango.

Mlangoni pale, alisimama mdada mweupe kiasi aliyevaa ushungi kichwani, akiwa na sahani ya udongo mikononi iliyofunikwa kwa sahani nyingine tena. Nilimtambua haraka na kutabasamu. Yeye pia akatabasamu.

"Mambo vipi Salma?" nikamsalimia.

"Poa."

"Aaam... hongera ya sikukuu. Sijui ndo' napaswa kusema hivyo?" nikamuuliza kiutani.

Akacheka kidogo kisha akasema, "Asante. Nimekuletea chakula kama zawadi ya sikukuu. Karibu." 

Niliifahamu hii kawaida ya kupeana chakula wakati wa sikukuu, lakini kwa siku hiyo sikutarajia kuletewa chakula. Nikamwambia 'asante' na kukipokea. Kwa kuwa mikono yake ilikuwa imeshikilia sahani kwa pamoja, hiyo ilifanya mikono yangu iishike ya kwake kwa chini nilipokipokea. Nilimtazama machoni, naye akaniangalia; kisha nikatabasamu kwa mbali, na yeye akatabasamu huku amebana midomo yake na kuangalia chini. 

Hali hiyo niliipenda sana. Sijui ni kwa nini lakini toka nimemjua Salma, hatukuwahi kukaa kuzungumza mambo mengi, zaidi ya kusalimiana mara kwa mara tulipoonana nilipokuwa nakwenda kazini au nikiwa narudi nyumbani hapo.

Salma alikuwa mdada mwenye sura nzuri, nyeupe kiasi na sikuwahi kulichora umbo lake vizuri kabla kwa kuwa mara nyingi alivaa baibui au dera na Sari kama zile za wahindi, ila ningeweza kwa haraka kusema alikuwa na hips nene. Alionekana kama kwenye miaka 20 mpaka 23 hivi kwa kukadiria, na alinukia vizuri balaa. 

Nyumba hii niliyoishi ilikuwa ya kupanga, lakini mpangaji pekee ilikuwa ni mimi. Ilikuwa nyumba yenye ghorofa moja ambalo chumba chake ndiyo nilikaa. Huko chini iliishi familia ya Salma, yaani baba na mama yake, mdogo wake mwingine wa kike na msichana wa kazi. Pia, baba yake ndiye alikuwa mwenye nyumba hii. Walikuwa waislamu, hivyo mara kwa mara wangekuja watu pale kutoka msikitini kwao kuwatembelea.

Salma alirudi chini kisha nikafunga mlango. Tabasamu lake na jinsi alivyonitazama vilipeleka taarifa fulani kichwani kwangu ambayo nilikuwa nikijaribu kuipotezea. 

"Oya, huyo mtoto wa wapi?" akaniuliza Justine.

"Anakaa huku chini ya ghorofa," nikamjibu huku naweka chakula kile mezani.

"Dah, we boya uko vizuri sana. Umepata demu tayari af' hatuambiani?"

"Siyo demu wangu bana. Namchukulia kama mdogo wangu na... rafiki pia.'

"Unazingua mwana. Nimecheki alivyokuwa anakuangalia. Anakutaka huyo. Usiniangushe sasa."

"Utajiangusha mwenyewe, mjinga wewe. Umekula nyama kilo nzima na nusu na chupa 5 za bia umemaliza. Usije kusingizia huwezi kutembea, haulali hapa," nikamtania.

"Aaaa asa' hiyo tu? Hata kilo tano ningemaliza," akajibu huku anatoa nyama zilizong'ang'ania kwenye meno kwa 'toothpick.'

Baada ya kukaa mpaka jioni tukipiga story, kuangalia movie na kupitia mambo machache ya kazi za kesho, Justine alipigiwa simu nyumbani kwao kuwa alihitajika kutokana na dharura. Hakutaka kuondoka kwa kuwa aliona wamemharibia wakati wake wa burudani. Ila nikamsihi akawasikilize maana kukiwa na shida muhimu, ni lazima mwanaume akaitatue. 

"Dah, aisee nilikuwa nataka nilale hapa kabisa, una geto zuri kama umeoa," akaniambia.

"Ujing'ate? Yaani siku ukilala hapa labda imenyesha mvua ya moto," nikamtania.

Akacheka kisha akasema, "Anyway, tutaonana kesho boy. Halafu usisahau kuhusu ile ishu."

"Ishu gani?"

"We' naye mbona unazingua? Tumeongea nini muda ule? Mtoto huyo nataka unisogezee."

"Nimekwambia sina ukaribu naye sana. Siwezi tu nikamfata nimwambie 'Justine anakutaka' af' akubali."

"Aaaaa... siyo fresh hivyo," akaanza kulalamika.

"Me nakwambia ukweli tu. Siwezi nikakupa uhakikisho wakati najua mambo kihalisi jinsi yalivyo."

"We' unakaa naye hapa. Unategeshea tu mida fulani unamwita unampanga unanipa namba yake; me nitamaliza kila kitu. Demu mzuri ki****, yaani nimemkubali."

"Oya, lugha hiyo mwanangu. Baba mwenye nyumba ni kifimbocheza. Halafu, je kama ana mtu wake? Na lazima awe na mtu wake, unataka kunisumbua tu," nikamwambia.

"We' fanya nilivyokwambia tu. Ukishanipa namba yake mie nitayajenga kwake maana kila mwanaume ana swaga yake. Na yangu ataikubali tu," akajigamba.

"Una kichwa kigumu wewe! Haya poa nitamsemesha," hatimaye nikalegeza.

"Sasa je! Hayo ndiyo maneno. Nakubali sana mwanangu; ndo' maana ukapewa sura nzuri kama demu."

Nilicheka na kumwoneshea kidole cha kati. 

Nikamsindikiza nje ya geti dogo la mbele la kutokea na kuagana naye alipoondoka kuelekea nyumbani. Nilitaka kwenda dukani ninunue vitu kwa ajili ya chakula, lakini nikakumbuka kuwa Salma aliniletea chakula, hivyo nikaahirisha na kurudi kwenye chumba changu.

Ilikuwa ni mida ya saa moja jioni na giza lilikuwa limeanza kuingia. Nikawa chumbani nimeketi kwenye sofa nikiangalia katuni fulani Nickelodeon iliyoitwa Fairy Godparents, pale mlango wangu ulipogongwa. Nikanyanyuka na kwenda mlangoni nikifikiri labda ni Justine kasahau kitu fulani, na kukuta ni Salma baada ya kufungua mlango.

"Salma, vipi? Za toka muda ule?" nikamuuliza huku nikitabasamu.

"Safi tu. Nilikuwa nimekuja kuchukua zile sahani," akaniambia huku akitabasamu pia.

"Oooh... aam... pole nilikuwa sijazisafisha bado. Ngoja nikuoshee nikupatie, sawa?"

"Sawa," akajibu huku akibana midomo yake.

Nilimwangalia kidogo kisha nikamwambia, "Tafadhali ingia uketi wakati unasubiri."

Aliingia kisha nikafunga mlango. Nilipogeuka kumtazama, hakuwa ameketi kwenye lile sofa, bali aliketi kwenye upande wa kitanda huku akitazama TV. Nikaenda kwenye kile chakula na kukifunua. Hadi kufikia wakati huu sikuwa nimekifunua, na sasa niliona jinsi chakula kilivyokuwa kizuri. Pilau na wali mweupe pembeni, maharage, kabichi na mchicha kwa pembeni, nyama ya ng'ombe na paja la kuku kwa pembeni pia. Kilikuwa kingi. Ningejinoma sana leo usiku!

Nikafanya kukihamishia kwenye sahani yangu moja, kisha nikaziosha sahani zile mbili.

"Na we' unaangaliaga katuni?" aliniuliza Salma wakati nikizikausha kwa kitambaa.

"Ee ndiyo. Wewe je?" nikamuuliza.

"Hata mimi naziangaliaga. Napendeleaga sanasana za 3D, ila hata za hivi naangalia," akasema.

Hiki ni kitu ambacho sikuwa nimetarajia. Alisema kwa usahihi kabisa AINA ya katuni anazopenda. Ilinifanya nijihisi vizuri kuwa karibu na mtu ambaye alijua mambo mengi kuhusu vitu ambavyo mimi pia nilipenda. Nilitabasamu huku nikimwangalia sana, na yeye akageukia TV kuendelea kuangalia.

"Nimezisafisha tayari," nikamwambia.

"Aah... sawa, asante. Rafiki yako yule mwingine ameondoka?" akauliza.

"Ndiyo ameondoka muda si mrefu," nikamjibu.

Kitendo cha yeye kumuulizia Justine, kilinikumbusha 'mission' ambayo Justine alikuwa amenipa. Na sasa nilikuwa nimepata nafasi nzuri ya kumuunganishia mitambo msela wangu. Salma alianza kucheka huku akiwa anatazama TV bado, hivyo nikakaa pembeni yake kwenye kitanda.

"Nini kimekufurahisha?" nikamuuliza.

"Hiyo scene... imenichekesha," akajibu.

"Aaaa... imenipita sikuiona."

"Ahahah... yaani wameonyesha huyu mtoto alikuwa amelala huku simu yake inaita. Sasa alikuwa anajivuta kuichukua, kwa hiyo kichwa cha aliyekuwa anapiga kikatokea kutoka ndani ya simu na kumpigia kelele apokee," akaeleza.

"Ahaa... ahahahah... kweli hiyo noma."

"Ila kilichonichekesha ni kwamba baada ya kupokea, huyo jamaa tena akamwambia aingie WhatsApp kuna kitu anataka kumwambia. Asa' si angemwambia tu hapo hapo!" akasema huku akianza kucheka tena.

Nilicheka pamoja naye huku nikitambua kuwa kiukweli katuni zilimfurahisha pia. Hakuona kile ambacho watu wengi hufikiri ndiyo dhumuni la katuni; kwamba ni za watoto tu, bali mawazo na utunzi wenye kufurahisha uliotolewa kwenye story. Nilimwangalia usoni mwake huku nikijipanga kumwambia jambo ambalo lingepelekea nimwombe namba kwa ajili ya Justine.

"Ona, Salma, kuna jambo nilikuwa nataka nikuulize," nikaanzisha.

Alinitazama na kubana midomo yake kama kawaida, kisha akaangalia chini kidogo na kuniambia, "Uliza tu."

"Najua hatufahamiani sana, hivyo naomba samahani kabla ya kukuuliza hivi, in case nikakukwaza."

"Usijali. Niulize tu," akasema kistaarabu.

"Uko kwenye... uhusiano na mtu yeyote?" niliuliza vile. 

Lakini tena kimoyomoyo nikawa najilaumu kwa nini nilianza kwa kumuuliza hivyo badala ya kumwambia tu kuwa jamaa yangu alim-feel sana. 

"Hapana. Siko kwenye uhusiano. Niko single," akajibu huku ananitazama kwa macho fulani hivi ambayo, sikuweza kuyaelewa kidogo.

"Anhaa... sawa. Sasa... me kuna jambo nilikuwa nataka nikwambie. Kwanza, kiukweli wewe ni mwanamke mwenye kuvutia sana. Unaweza kuvutia wanaume hata zaidi ya elfu moja kwa siku tu... siyo kwa uzuri huo."

Alicheka kwa sauti ya chini kisha kuniambia, "Unadanganya... me wa kawaida sana."

"Hamna bwana, lazima nikusifie inapostahili. Asiyekusifia lazima awe anakuonea gere," nilimtania, naye akaanza tena kucheka.

"Asante," akajibu kisha kuibana midomo yake.

"Sawa. Sasa... nilikuwa nataka ujue kwamba..." 

Nilipokuwa sijamalizia kusema nilichotaka kusema, aliniwekea kidole chake juu ya mdomo wangu, kama kuninyamazisha. Nilishangaa kiasi lakini nikaweza kutulia.

"Usijali. Najua unachotaka kuniambia," akasema.

Kiukweli sikuwa nimetegemea kwamba angeweza kujua jambo nililotaka kusema. Lakini muda siyo mrefu nikatambua kuwa nilichowaza kilikuwa tofauti na kile alichowaza yeye. 

Akasogeza uso wake karibu na wangu, kisha kutoa kidole chake mdomoni kwangu. Nilielewa kwa haraka alichokuwa anakusudia kufanya, na nikajikuta nashindwa kufanya lolote zaidi ya kukaa kimya na kumtazama machoni. Alisogeza midomo yake karibu kabisa na yangu, na hapa sasa nikaanza kupata zile hisia kali za mahaba. Akafungua kinywa chake na kuanza kulamba lips zangu ambazo bado nilikuwa nimefunga. Alinifanya nikose cha kufanya na kuanza kufungua midomo yangu ili kupokea ulimi wake. Aliuzungusha ndani ya mdomo wangu taratibu huku amefumba macho; na kwa ukaribu ule, harufu yake nzuri iliingia puani mwangu.

Akautoa mdomo wake kidogo kutoka kwangu, huku uso wake bado ukiwa karibu kabisa na wa kwangu, kisha akasema kwa sauti nyororo, "Hata mi' nakuhitaji pia."

Hapa sasa ndiyo pakanichanganya. Kiukweli, kama ningekuwa nimeweka nia ya kumtokea kimapenzi Salma, ningefanya hivyo kitambo tokea nilipohamia kwenye nyumba yao. Alikuwa mrembo sana, na ndiyo kitu kilichofanya nisimkazie fikira kwa kuwa nilidhani lazima angekuwa na mwanaume; aliyemgharamia pia. 

Hisia alizokuwa ameziamsha kwangu ni hisia ambazo sikuwa nimeziamsha karibia mwaka mzima sasa, kwa kuwa tokea nilipoanza hii kazi, sikuwahi kutoka kimapenzi na yeyote yule. Nilifurahia zaidi kutokuwa na mahusiano, maana jambo hilo lilinifanya nijihisi uhuru sana. Lakini baada ya Salma kusema hivyo, nikatambua kwamba kwa kipindi fulani amekuwa akitamani kuwa pamoja na mimi, lakini huenda hakuweza kuniambia kwa jinsi nilivyokuwa 'busy' na mambo yangu.

Sasa nikaanza kuwaza niitikie vipi jambo hili. Hapa nilikuwa najaribu kumtengenezea mazingira rafiki yangu ili achukue ngai, ngai ikageukia kwangu. Nilianza kumtamani Salma, na hilo likanifanya nihisi kama namsaliti Justine. Nimwambie Salma kuwa hicho alichofikiri hakikuwa sahihi au? Niliwaza kwa ufupi huku binti akinitazama kwa macho malegevu yenye hamu.

Kwa jinsi alivyoitengeneza hali hiyo kuwa moja yenye kuamsha hisia zangu zote nilizokuwa nimefungia, mashine yangu ilianza kuvimba. Ilisimama na kukaza kwa nguvu sana mpaka nikahisi kama inataka kutoboa kaptura yangu. Niliiangalia midomo yake iliyokuwa imelowa mate, nami sasa sikuweza kujizuia tena. 

Nikaifata na kuanza kuinyonya taratibu kwa mahaba. Nilihisi mwili wangu ukipatwa na msisimko mkubwa sana kadiri tulivyoendelea kupeana busu hiyo. Nilikuwa nikisikia sauti za miguno ya Salma ndani ya mdomo wangu, akiitikia kwa upendo denda ile takatifu. Nikapeleka mkono wangu kwenye titi lake moja na kufanya kama nalizungusha-zungusha kwa kulibonyeza huku nikiendelea kuusikilizia ulimi wake ndani ya mdomo wangu. Hisia nyingi zilikuwa zimenipanda, hivyo sikuwa nikifikiria la kufanya, nilifanya tu. 

Nilijitoa mdomoni mwake na kuanza kuivuta taratibu blauzi ya mikono mirefu nyeusi yenye kubana aliyovaa. Alinyoosha mikono yake juu kuniruhusu, nami nikaitoa yote pamoja na ushungi aliovaa. Kwa mara ya kwanza niliweza kumwona akiwa bila ushungi, na alikuwa amesuka nywele ndefu zilizobanwa kwa nyuma. Hakuwa amevaa sidiria, hivyo matiti yake madogo kiasi yakawa wazi mbele ya macho yangu. Mashine yangu ilishtua mara mbili kwa msisimko, huku akinitazama kwa macho yaliyoonyesha... njaa ya mahaba.

Nikashika kiuno chake na kunyonya taratibu chuchu zake, naye akawa akitoa pumzi juu juu za raha. Alianza kulegea, nami nikamruhusu aulaze mgongo wake kitandani huku bado namumunya matunda yake laini. Nilishika pindo za sketi ndefu ya samawati (blue) aliyovaa, na kuivuta yote kisha kuitupia pembeni chini. Sasa akawa amebaki na nguo ya ndani nyekundu tu. Nikajinyanyua na kuweka goti moja kitandani huku nikivua T-shirt niliyovaa, naye akajinyanyua na kushika pande za kaptura yangu na kuishusha; kisha kuniangalia machoni baada ya kuiona mashine yangu ndefu ikiwa imesimama vyema.

Nilimfata mdomoni mwake na kuanza kumpa denda tena huku nikimsukumia kitandani taratibu. Nilizungusha vidole vyangu kwenye titi zake huku nikizifinya-finya chuchu zake zilizokuwa ngumu kwa hamu. Nilimbusu kotekote; usoni, kwenye sikio, kwenye mabega na shingoni ambapo alivaa cheni ya dhahabu (nafikiri).

"We' ni mtundu," aliniambia kwa sauti legevu, nami nikatabasamu kidogo na kuendelea na kazi.

Niliendelea kumbusu na kumlamba kuelekea chini ya mwili wake, nikinyonya titi zake, nikilamba kitovu chake, na kuyabusu mapaja yake kuelekea hadi kwenye miguu yake. Kisha nikaanza kupandisha juu tena. Muda wote Salma alikuwa akiguna na kuunyonga mwili wake kwa wororo sana taratibu. Kisha, nilipokaribia katikati ya mapaja yake, nikaisogeza sehemu ya nguo yake ya ndani ya mbele iliyofunika, na hapa mbele yangu, kitoweo cha Salma kikawa wazi. Nilipitisha ulimi wangu kwa juu kidogo na kufanya ashtuke, kisha kuniangalia, nami nikamwangalia na kuendelea kuuchezesha ulimi juu yake huku akirudisha kichwa kitandani taratibu.

Nikauingiza ulimi wangu ndani yake na kufanya atoe mguno wa sauti ya juu kidogo. Alianza kuvuta shuka huku akiguna na kuzungusha kiuno chake kadiri nilivyoendelea kuuzungusha ulimi ndani yake. Kisii chake kilikuwa kimevimba kwa hamu kubwa kikiniomba nikinyonye pia, na bila kuchelewa nikakitii na kukibugia na kumumunya kwa ustadi uliompoteza akili kabisa Salma. Alianza kuongea maneno ambayo sikuelewa, ya kiarabu nafikiri, huku akishika nywele za kichwa changu na kuuzungusha mkono wake kichwani huku akikivutia kwake kwa nguvu.

Zilipita dakika chache na Salma alifikia mshindo wa kwanza ulioutetemesha mwili wake sana. Nikajinyanyua na kuendelea kuchezea matiti yake kwa mikono yangu naye akaishika shingo yangu kwa nguvu na kunivutia kinywani mwake. Hilo lilinishangaza kiasi maana tokea tulipoanza alikuwa mpole kweli; sasa akaonyesha utamu ulikuwa umemkolea. Aliishika mashine yangu, huku midomo yetu bado ikiwa karibu, na kuiingiza kwenye kitoweo chake yeye mwenyewe. Nilitenda haki kwa kuwa nilimsugua vyema huku akitoa vilio vya mahaba kwa sauti. Niliwaza ingekuwa vipi ikiwa wazazi wake wangemsikia, lakini sijui ilikuwa ni nini tu kilichofanya nisiendelee kujali.

Nilimsugua huku nikimbadilishia mikao, naye alikuwa akifatisha chochote nilichomfanyia. Nilishughulika vile kwa kama nusu saa hivi, kisha akapiga mshindo wa pili. Tuliendelea kwa dakika kumi na tano hivi, ndipo nikaanza kuhisi watoto wangu wakija na kuitoa mashine yangu ndani yake ili niwamwagie pembeni. Lakini nilishangaa Salma alipoiwahi mashine yangu na kuipeleka mdomoni mwake, kitu ambacho kilifanya nijiachie mdomoni mwake. Lakini alionekana kufurahia jambo hilo, na kuendelea kuilamba-lamba huku akiniangalia machoni.

Nikajilaza kitandani pamoja naye na kuanza kushikana-shikana naye. Alikuwa akirembua macho yake kama kwa uchovu huku ameweka mguu wake juu yangu kama kapiga nne.

"Nimefurahi sana Tristan... nakupenda," aliniambia huku akipitisha vidole vyake kwenye nywele zangu.

Ndiyo. Jina langu ni Tristan. Sikuwahi kumsikia akilitaja tena tokea mara ya kwanza nilipojitambulisha kwake; ijapokuwa mimi nilikuwa na kawaida ya kusema lake, yeye hakuwa nayo. Hivyo kusikia akilitaja sasa, kulisisimua. Hili ni jambo ambalo kihalisi sikutarajia, na ikaanza kuonekana kama vile mambo yalikwenda haraka sana, ijapokuwa tulicheza mechi saa zima. Pamoja na kwamba sikutazamia hili, mimi pia nilifurahi. Nikampa tabasamu huku vidole vyangu vikizungukia mapaja yake na mgongoni.

"Mimi pia Salma," nikamjibu.

"Nimeisubiria siku hii kwa muda mrefu sasa," akasema.

"Kweli? Mbona sikutambua hilo?"

"Nilikuwa nashindwa kukwambia kama wewe tu."

Huku nikijua akilini kwamba kwa upande wangu hiyo haikuwa jinsi alivyofikiri, nikampa tu tabasamu bandia kukubali.

"Me nilijua utakuwa na mtu wako tayari maana kwa uzuri kama wako, ni nadra sana kupata mwanamke kama wewe akiwa single," nikamweleza.

"Nilikuwa na mpenzi miezi michache iliyopita ila akaniacha."

"Mh! Binti mzuri namna hii uachwe?"

"Basi tu, ndiyo wanaume wengi walivyo. Nilikuwa nimeshaamua kwamba sitakuwa na mtu yeyote tena, mpaka nilipokuja kukuona," akaniambia.

"Uliona utofauti gani kwangu? Mimi pia ni mwanaume," nikamtega.

"Wewe sikuwahi kukuona na mwanamke hii miezi yote uliyokaa hapa, na hata kuleta tu mwanamke humu chumbani kwako sikuwahi kukuona. Lakini pia... kuna siku ulimkuta mama anapalilia hapo pembeni ya ukuta, na ndiyo ulikuwa tu umetoka kazini, umechoka, ila ukaanza kumsaidia kupalilia na ulipomaliza ukafagia eneo lote... nilipenda sana."

"Ulinionaje?"

"Nilikuwa ndani napika, ila ningeweza kukuona dirishani."

"Kwa hiyo kwa sababu nilifagia uwanja ndiyo ukanipenda?"

"Hapana. Nilichopenda zaidi ilikuwa utayari wako wa kusaidia mtu hata kama umechoka... lakini pia... ni macho yako..." akasema huku akitabasamu.

"Macho yangu yamefanyaje?" nikamuuliza kichokozi.

"Nayapenda... mazuri sana."

Nikacheka kidogo, naye akacheka pia.

"Una miaka mingapi?" nikamuuliza.

"21."

"Oooh... okay. Kiukweli umenivutia sana. Sikuwa nimetarajia tulichofanya leo, lakini nimefurahi sana. Halafu... vipi wazazi wako sasa? Watakuwa wametusikia huko chini."

"Usijali, wametoka. Tulitakiwa tuondoke pamoja lakini me nikawaambia ninajisikia vibaya... so... nikabaki," akaeleza.

"Mmm... na kilichokufanya ubaki ni nini? Maana kwa jinsi ulivyocheza mechi kwa bidii, sidhani kama kweli unaumwa!" nikamtania.

Akacheka, kisha akasema, "Nilitaka kuwa nawe. Baada ya kukuona mchana wa leo, nilijisikia vizuri sana. Na sasa najisikia bora hata zaidi."

Alikuwa anasema vitu kwa njia iliyovutia sana. Nilianza kuvutiwa naye hata zaidi, huku nikijua nimeshamharibia Justine mishe yake tayari. Nikafikiri hata kama ningemwambia tu huyu dada tayari ana mtu na kagoma kutoa namba, ingetosha na angeacha kujisumbua, ili mie niendelee kujilia vyangu.

Zilipita kama dakika 20 tukiendelea kupiga story za kufurahisha, pale tuliposikia honi za gari nje ya geti. Salma alishtuka na kusema ni baba yake amerudi, kisha kuanza kuvuta nguo zake avae haraka. 

Nilimwangalia huku natabasamu, kisha nikamtuliza kwa kumpiga denda iliyofanya atulie kidogo. Nikampa sahani zake, naye akatoka chumbani kwangu ila alipofika mlangoni, akageuka na kunipa tabasamu tena. 'Horn' za gari ziliendelea kusikika hivyo akawahi ili awafungulie. Eneo la nyumba hii halikuwa kubwa sana na gari yao ilikuwa spacio ndogo nyeusi, hivyo ingeweza kubananishwa vizuri kwenye kona za ukuta.

Nilirudi kukaa kitandani nikianza kurudia matukio ya muda mfupi uliopita akilini mwangu. Nilijikuta natabasamu kwa kiburi nilipowaza kuwa leo kiukweli nilikula bata haswa; tena hata bila kusumbuka, bata zote zililika chumbani kwangu. 

"Ooh no..." 

Nikajisemea hivyo baada ya kukumbuka sikuwa nimemwomba namba ya simu Salma. Bila shaka, nilikuwa nina hamu ya kuyajenga naye tena wakati mwingine hivyo mawasiliano yangekuwa muhimu. Sikujua kama ningepata nafasi nyingine nzuri ili niweze kuipata yake au kumpa yangu, lakini nilitazamia kwa hamu kuwa naye tena. 

Muda ulikuwa ukipita haraka, nami nilianza kuandaa nguo za kuvaa kesho kazini, nikatoa mashuka yaliyomwagikiwa juisi ya moto ya mtoto na kuyabadili, kisha nikaketi na kula chakula chake mtoto alichoniletea. Pindi kwa pindi ningejichekea mwenyewe kila nilipofikiria Justine angeitikia vipi kama ningemwambia ngai yake nimeichukua. Angenitoa meno! Ilifika saa sita usiku baada ya kuwa nimeridhika na TV, hivyo nikaizima ili niingie kulala. Nafikiri kwa kuwa kwa jinsi matukio yalivyojitengeneza mpaka kisa changu na Salma kikatokea, ilifanya iwe ngumu kutomuwaza sana. 


★★★


Ilinichukua saa zima usiku huo nikihangaika kutafuta usingizi kitandani, lakini mwisho wa siku, nilijikuta naamka ikiwa ni saa kumi na mbili asubuhi. Nikajiandaa upesi na kuondoka, huku nikiangalia nje pale kama ningeweza kumwona Salma, lakini sikumwona. Hivyo, nikawahi kuondoka kuelekea kazini ambako tulipaswa kuingia saa moja juu ya alama. Nilikuwa na kawaida ya kutembea mwendo mfupi kufikia sehemu ambayo nilisubiri usafiri ulionipeleka mpaka maeneo ya kazini.

Nilikuwa nimesimama pembezoni mwa barabara nikisubiri gari nililohitaji kuelekea kazini, pale nilipomwona mwanamke fulani mzee aliyekuwa akitembelea mkongojo, akivuka barabara kuelekea upande wa pili. Lakini ilionekana kama hakuweza kuona Lori lililokuwa likija upande wake, na alikuwa ameanza tu kuvuka wakati Lori hilo lilipokuwa bado kwenye mwendo wa kasi.

Bila kukaa kufikiri, nilikimbia haraka sana kwenda sehemu ile na kumshika yule mwanamke kiunoni, kisha kumvutia upande wa pili wa barabara. Sote tuliangukia pembeni karibu sana na nguzo ndogo ya chuma yenye taa ya barabarani, mwanamke yule akiwa juu yangu, mimi nikiwa chini. Nilihisi maumivu kwenye bega langu la kulia, lakini nilijikaza bila kutoa sauti yoyote ya maumivu. Lori lile lilipiga breki ya ghafla huku begi langu nililobebea laptop likiwa limeangukia chini yake.

Mwanamke huyo mzee akajitoa kifuani kwangu, nami nikamsaidia kusimama. Mkongojo wake ulikuwa wa chuma na uliangukia karibu yetu, nikamwokotea na kumpa. Watu kadhaa walisogea pale na kutuuliza kama tulikuwa sawa, kutia ndani dereva wa Lori lile. Nilisema niko sawa na kisha nikamuuliza huyo mwanamke kama kuna sehemu yoyote aliumia. 

Mwanamke huyo, aliyekuwa na nywele nyeupe sana, alinitazama huku akitabasamu, kisha akaweka mkono wake juu ya kifua changu upande wa kushoto. Alianza kuongea maneno fulani ambayo sikuweza kuyaelewa; sijui ni kiarabu, kichina, kifaransa, sikujua. Lakini mkono wake kifuani kwangu ulinifanya nihisi joto fulani ambalo lilitoka kwenye kiganja chake. 

Kisha akautoa mkono wake na kutabasamu tena. Kwa kuwa sikuelewa alichosema, nilichukulia alikuwa akinishukuru, nami nikampa tabasamu pia. Akaanza kujipangusa vumbi huku watu wakiongezeka kiasi, kisha mimi nikaelekea chini ya lile Lori kufata begi langu. Nilihuzunika sana baada ya kulifungua na kukuta vipande-vipande vya laptop yangu, ambayo ilikanyagwa vibaya na tairi la gari. Dereva wa Lori akanipa pole, nami nikamwambia haina shida kwa kuwa uhai uliokolewa, laptop ningeweza pata nyingine. 

Nilipogeuka nyuma kumwangalia yule mwanamke mzee, sikuweza kumwona tena. Watu bado walikuwa eneo lile, lakini yeye sikumwona. Kwa jinsi alivyokuwa akitembea polepole wakati akivuka barabara, nilitarajia ningemwona baada ya kugeuka huku na kule kumtafuta, lakini alikuwa amepotea ghafla.

'Ameenda wapi?' nilijiuliza kichwani kwangu.

 

 

★★★★★★★★★★

 ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

Next