Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

INVISIBLE

A Story by Elton Tonny

Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Unyanyasaji, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA TANO

★★★★★★★★★★★★


Nikashusha pumzi kidogo na kunyanyuka ili nielekee ofisini kwake. Njia nzima niliwaza ni kitu gani alichotaka kusema, au kufanya, hivyo nilijiweka tayari kwa lolote. Nikafika na kugonga mlango kama kawaida, naye akaniambia nipite. Wakati huu, sikuingia moja kwa moja, ilibidi nichungulie kwanza ili kuhakikisha hajajibanza nyuma ya mlango akiwa ameshika rungu ili nikiingia tu anipige nalo kichwani! Nilimwona akiwa upande mwingine wa ofisi uliokuwa na sofa, na aliketi hapo akiwa amekunja nne.

Nikaingia na kuelekea sehemu hiyo kisha kusimama na kumtazama usoni. Alikuwa akiniangalia kwa njia fulani... ya kawaida. Yaani hakuonyesha hasira wala chuki ndani ya macho yake. Akachukua glass iliyokuwa na 'juice' kisha akanywa kidogo na kuiweka chini.

"Unajiona umeshinda baada ya kunifanyia vile muda mfupi uliopita, siyo?" akauliza kistaarabu sana.

"Kwenye kila mechi, ni lazima mashabiki wasubiri mpaka iishe na kupata matokeo ndiyo ijulikane nani kashinda. Mechi yetu ndiyo imeanza tu, tusubiri matokeo," nikamweleza kwa kumpa mfano.

Akanyanyuka na kuanza kunisogelea karibu zaidi taratibu. Alinitazama machoni akiwa makini sana.

"Ulijuaje kuhusu mimi kufanya masturbation?" akauliza.

"Kwa kukuangalia tu," nikamjibu.

Akanyoosha kidole chake juu kama anataka kusema kitu fulani kwa hasira, kisha akajituliza na kushusha mkono chini.

"Ni Magda, si ndiyo?" akauliza kitulivu.

"Magda hajui lolote. Sihitaji mtu yeyote aniambie jambo ambalo nimejionea mimi mwenyewe," nikamwambia.

"Uliniona vipi?"

"Nina macho mengi."

"Mimi ni boss wako Tristan. Nitakufukuza kazi," akanitisha.

"Sawa tu. Nifukuze. Inaonekana ndiyo ulichobobea hicho. Ila bado msimamo wangu uko pale pale," nikamwambia nikiwa makini kabisa.

"Unawezaje... anyway... wewe una uhusiano gani na Magda mpaka unafanya haya yote kwa ajili yake?" akauliza.

"Sihitaji kuwa na uhusiano wowote na mtu ili kumsaidia. Hata wewe ungekuwa chini ya shida ningekusaidia."

"Ahah... we' unaweza kunisaidia nini mimi?"

"Mambo mengi tu. Tia ndani na hata yale ambayo mume wako ameshindwa."

Sura yake iligeuka na kuwa makini zaidi baada ya mimi kusema hivyo.

"We' ni mwendawazimu," akaniambia.

"Siyo zaidi yako. Unapaswa kuwa mtu anayeheshimiwa, siyo kuogopwa. Lakini kiburi chako ndiyo kinakuzuia kuona mambo kihalisi. Utaendelea kufukuza wafanyakazi mpaka lini? Kampuni inajengwa na wanaoifanyia kazi. Ukiwa unabadilisha-badilisha watu kila mara eti kwa sababu tu unaweza, unaiweka kampuni na reputation yako at stake," nikamweleza ukweli.

Sijui aliuchukuliaje ushauri wangu kwa kuwa akanifata na kunipiga kofi usoni. Lakini ni kama alishangaa kwa nini wakati huu sikumzuia. Nilimwangalia tena usoni na kuona akiwa na hofu fulani ya mbali. Bila shaka, maneno niliyomwambia yalimchoma.

"Vipi boss Ritha? Unashangaa kwa nini sijakuzuia kunipiga kibao sa'hivi? Hicho ndiyo kiburi nachoongelea. Nakwambia huu ukweli siyo kwa sababu nakujali, ijapokuwa unavutia, ila ni kwa sababu nawajali wafanyakazi wenzangu unaowatendea kama mbwa, wakati we' unayoyafanya hata mbwa hawezi kufikiria kuyafanya."

Niliongea maneno hayo kwa hisia kali sana. Alichomwa sana kwa sababu alijua ni ukweli. Ghafla, akashika sehemu yangu ya siri iliyokuwa ndani ya suruali kwa nguvu na kuibana kwenye kiganja chake, huku uso wake ukionyesha hasira. Nilikaza meno yangu na kumshika shingoni, kama namkaba, lakini nilihakikisha simuumizi sana. Alianza kutoa pumzi za juu juu huku akisogea karibu yangu zaidi.

Ni kiburi chake ndiyo alichotanguliza sikuzote, na sasa mimi nilijua huyu mwanamke hakuwa mtu wa kuonyeshwa upole, hivyo kama ni ujeuri ndiyo aliutaka, basi kwangu angeupata. Nilitaka kumfanya aone kuwa kuna mambo mengine ambayo yako juu kuliko pesa; kama utu. Nikaanza kuongeza nguvu kwenye kiganja changu na kumfanya aanze kutoa sauti za kukabwa. Muda wote alijitahidi sana kujikaza asitoe sauti kubwa, huku nami pia nikivumilia maumivu niliyopata kutokana na mkono wake wenye kucha ndefu kuikaza sehemu yangu.

Nikatumia mkono wangu mwingine kuutoa wakwake na kuubana nyuma ya mgongo wake, na sasa alikuwa karibu nami zaidi, nyuso zetu zikitazamana huku bado nimemkaba shingoni. Lakini kwa chini, nilianza kuhisi mkono wake mwingine ukiichezea-chezea sehemu yangu ya siri juu ya suruali huku akinitazama kilegevu. Nikaanza kulegeza mkono uliomkaba kiasi huku nikiwa namtazama kwa makini. Alianza kutoa pumzi kwa midomo yake zilizoonyesha alikosa hewa kiasi kutokana na jinsi nilivyomkaba.

Nilihisi akifungua mkanda wa suruali yangu kwa mkono wake huo huo na kisha kutoa kifungo na kuifungua zipu. Bado niliendelea kumtazama machoni huku nimemkaba shingoni kwa kulegeza mkono, na mkono wake mmoja nikiubana mgongoni kwake, na macho yake yalionyesha kuwa alifurahia jambo hili, naye alitaka lifanywe kwa njia hii. Moja kwa moja nikawa nimeelewa kuwa boss Ritha alipendezwa na mapenzi ya mateso.

"Unafanya nini?" nikamuuliza nikiwa makini.

"Nataka kuona kama kweli unaweza kunipa kile ambacho mume wangu alishindwa," akajibu.

"Is that a challenge?" nikamuuliza.

"Consider it one," akajibu.

Nikatabasamu, kisha nikamwambia, "Well... sahau!"

Nikamsukuma nyuma kidogo na kuanza kuifunga suruali yangu. Alionekana kushangaa kiasi.

"Ikiwa tumemaliza hapa, wacha nikaendelee na kazi... boss," nikamwambia.

Alikaa kimya huku amekunja sura yake, siyo kwa hasira, ila kwa uhitaji. Nikaanza kuondoka kuelekea mlangoni lakini aliwahi na kunipita kisha kuufunga mlango kwa ndani na kuu-lock kwa funguo. Aligeuka na kunitazama huku amesimama mlangoni hapo, kama kunizuia nisipite.

"What are you doing?" nikamuuliza nikiwa nimeshangaa.

Akasogea karibu yangu na kuniambia kwa sauti ya chini, "Nakuhitaji Tristan."

"Excuse me?!" nikashangaa huku nikiachia tabasamu la kutoamini alichosema.

"Ndiyo Tristan... nakuhitaji. Please," akasema huku sura yake ikionyesha upole fulani hivi.

"Boss hauko serious. Mimi siwezi kukusaidia na unachohitaji..."

"Nataka unionyeshe. Nionyeshe wewe kweli mwanaume," akanikatisha.

Nikacheka kidogo na kusema, "Lini ushaniona nimevaa gauni?"

"Nataka unipe mapenzi kama ulivyosema unaweza."

"No. Haiwezekani," nikamwambia.

"Lazima unipatie. Haya yote ni makosa yako," akasema.

"Me nimefanyaje?"

"Nani alikwambia unishike vile? Nani alikwambia uniambie hayo maneno?"

"Boss... nisikilize. Wewe ni mtu ambaye ni ngumu sana kuona jambo jinsi lilivyo hasa kwa kuwa unataka jinsi unavyoliona wewe ndiyo iwe sahihi. Nilifanya vile ili utulie... na nashukuru Mungu hukupiga kelele," nikamweleza.

"Hapana Tristan. Mimi sijali ulifanya ukiwa na nia gani, nakuhitaji now."

"No... impossible," nikamwambia kifupi.

Nilianza kuufata mlango ili nitoke na kujaribu kuuvuta baada ya kumsukumia pembeni, lakini kwa kuwa aliupiga lock, nilihitaji funguo. Nikamwomba funguo, naye akakataa kunipa.

"Boss naomba funguo... nitapiga kelele unanibaka humu!" nikamwambia kiutani.

Niliona akiachia tabasamu ambalo sikutarajia kuliona wakati huo. Nikaanza kumfata naye akawa ananikwepa na kuelekea mpaka mezani kwake. Nilimwahi na kumvuta kiuno chake kisha kumbana kwa nguvu ili nimnyang'anye funguo. Sikuwa nimeiweka akili yangu kutambua kwamba kufikia wakati huu, ilikuwa ni kama tunacheza ofisini humo, kwa sababu wakati nilipokuwa namkimbiza ili nichukue funguo, alikuwa akicheka. Lakini sasa nilikuwa nimemkamata na nia yangu ilikuwa funguo tu. Mwili wake ulitazamana na wangu pindi nilipombana huku akikwepesha mkono ulioshika funguo ili nisiifikie.

"Boss acha basi, huu ni utoto. Naomba funguo nitoke bwana..."

"No. Hautoki hapa..."

Nikaweza kuifikia funguo na kuivuta kwa nguvu kutoka kiganjani mwake. Nikamwachia na kutaka kuufata mlango, lakini akanishika mkono kwa nguvu kunizuia.

"Please Tristan... tafadhali nisikilize," akanisihi.

"Leo ndo' mara ya kwanza nakusikia unasema neno tafadhali," nikamwambia.

'Tristan, umeamsha hisia zangu za ndani kabisa... nakuhitaji sana. Tafadhali..."

"Boss naomba uelewe. Mimi siyo cheap kama unavyofikiri. Sikuzote umekuwa ukitutendea kama vikaragosi. Na mara nyingi unafanya vitu ili vikufaidishe wewe tu. Hata sasa," nikamwambia kistaarabu.

"Hapana Tristan, haiko hivyo," akasema kwa kubembeleza na kuniachia mkono wangu, kisha akaushika uso wangu kwa mikono yake yote.

"Boss usifanye hivi... unajiaibisha ujue? Kutoka na mke wa mtu ni kitu ambacho hakijawahi kuingia kwa akili yangu hata mara moja."

"Mimi siyo mke wa mtu Tristan," akasema kwa uhakika kabisa.

Nilitulia na kuendelea kumsikiliza maana hii ilikuwa habari mpya kwangu.

"Mimi na baba yake Sarah tulitalikiana miezi mingi nyuma kabla hata haujaajiriwa hapa," akasema kwa sauti yenye huzuni.

"Kwa nini mlitalikiana?" nikauliza.

"Nilikuja kugundua kuwa alikuwa anatoka kimapenzi na mdogo wangu. Lakini walikuwa wamedumisha mahusiano yao kwa karibia miaka mitatu bila mimi kujua, na nilikuja kujua baada ya mdogo wangu kuthibitisha ana ujauzito wake," akasema huku machozi yakimlenga.

Hiki ni kitu ambacho sikutarajia. Boss Ritha sasa alikuwa mpole kwa sababu alitaka muhogo wangu. Lakini nyuma ya pazia, kihalisi jambo hilo lilichochewa na mambo mengi yaliyotokea kwenye maisha yake ya kifamilia. Niliwahi kusikia kuwa mume wake huyo, kabla hata boss hajapewa uongozi wa hii kampuni, alikuwa ana tabia za kumpiga mara kwa mara. Ndiyo maana nilikuwa nikichukulia tabia za boss kuwa ni kutokana na stress za familia kutoka kwa mume wake. Ila sikujua kama walikuwa wameshatalikiana. Na alijitahidi sana kuficha jambo hilo kwa muda mrefu maana hata wambea hawakujua.

"Aam... pole sana," nikamwambia baada ya kuanza kumwonea huruma.

"Asante. Mimi... sikuwa hivi Tristan. Nilikuwa mtu mmoja mstaarabu sana. Nilimpenda sana Mike, na nilimvumilia kwa mengi kwa zaidi ya miaka 18. Niliwahi hata kumsikia akisema kwa rafiki yake kuwa alinioa kwa sababu tu nilimng'ang'ania na sisi kuwa na pesa. Alinifanya nipate depression kubwa sana kiasi kwamba nikaanza kutenda mambo mabaya tu. Na sasa nimeyazoea," akaeleza.

"Aisee! Hiyo siyo poa hata kidogo. Sikutambua ulipitia wakati mgumu sana. Lakini boss, kumbuka kuwa una maisha ambayo watu wengi hawana. Kuna watu wanateseka mitaani kutafuta hata shilingi elfu 2 tu na wanaikosa... wewe unapoteza mamilioni kisha unamlaumu mtu mwingine na kumwachisha kazi, huoni unafanya ubaya mkubwa sana?" nikamweleza.

"I know Tristan. Ila tu sijui nifanye nini ili nirudie hali ya kawaida. Sijui nani atanisaidia..."

"Hakuna atakayekusaidia ila wewe mwenyewe boss. Najua wewe ni mtu mzuri, na najua unaweza kubadilika. Just... do it," nikamtia moyo.

"I will. But Tristan, I really need you..."

"Boss...."

"Please Tristan. Umeamsha hisia ndani yangu ambazo zililala kwa muda mrefu sasa. Tokea tulipotalikiana na Mike, sijawa na mwanaume yeyote yule. Ndiyo sababu ya mimi kuanza kufanya masturbation tokea wakati huo. Leo... baada ya wewe kunishika, nimehangaika sana, na najua ni wewe tu ndiye unaweza kunituliza," akanibembeleza.

Nilimtazama machoni na kuona kweli alikuwa na uhitaji. Lakini bado moyo wangu haukuridhia kufanya kile alichotaka nifanye. Ni wakati huu ndipo nilihisi simu yangu iki-vibrate kwenye mfuko wa suruali. Nikaitoa huku nikiwa bado nimesimama karibu ya boss na kusoma ujumbe niliotumiwa. Sikuwa nimetambua kuwa muda ulikuwa umesonga.

"Aam... ni muda wa lunch. Nina... ninaenda na Justine kupata lunch, ananisubiri... kwa hiyo..."

"Please Tristan, I'm begging you... please.." boss akaendelea kuniomba.

Nilikuwa nimeshindwa nikatae vipi ili aelewe. Lakini kuna hisia nilizopata kumwelekea hasa baada ya kunisimulia kisa chake, zilizofanya nivutiwe zaidi na huu utu wake halisi ambao watu wengi hawakuujua. Nikashindwa hata niseme nini. Nilibaki kumtazama tu machoni huku nimeiinua simu yangu. Akaichukua taratibu na kuiweka mezani, kisha akanitazama na kunifata mdomoni kunipiga busu kwa mara ya kwanza.

Mwanzoni, sikujua niitikie vipi busu yake. Aliweka mkono wangu nyuma ya kiuno chake na yeye kujibana zaidi kwangu. Alinifanya nishindwe kuwaza la kufanya. Sikujua la kutarajia. Mapigo ya moyo wangu yalidunda haraka, nami ningeweza kuhisi yake yakidunda haraka pia. Nilianza kujitahidi kukazia fikra hisia nilizopata, badala ya kufikiria kile tulichokuwa tunakifanya. Kwa muda huu, niliamua tu kufanya kile ambacho moyo wangu uliridhia badala ya kuwa kama mtu ambaye anawaza tu watu wengine wangemwonaje.

Kisha, boss akajitoa mdomoni mwangu, naye akaongoza mambo mpaka tukajikuta tukipeana mapenzi ofisini hapo. Tulianzia mezani mpaka kwenye kochi, naye akaridhika baada ya saa zima kupita.

"Tristan..." akaita kivivu.

"Mmm," nikaitika.

"Thank you," akasema.

"Karibu," nikamwambia.

Akajinyanyua taratibu huku akiwa bado amenikalia na kunitazama usoni.

"Una nguvu sana we kijana," akanisifia.

"Kawaida tu," nikajibu.

"Mwili wako ni wa mazoezi pia. Una ratiba ya mazoezi magumu?" akauliza.

"Hapana. Niliwahi kufanya scout kipindi cha nyuma, hivyo niko fiti."

"Wapi?"

"Aam... ni mbali kidogo. Boss unajua hatupaswi kuendelea kukaa namna hii," nikamwambia baada ya kutambua lunch time iliisha na sasa kazi ziliendelea.

"Me nataka tukae humu humu mpaka jioni," akasema.

"Hicho ni kitu ambacho hakiwezekani."

"Kwa nini?"

"Kwa sababu umeniita me mwendawazimu muda mfupi uliopita," nikatania.

Akacheka kidogo kisha akasema, "Samahani. Nilikuwa... kama unavyosema, kiburi changu ndiyo nilikuwa natanguliza."

"Najua mimi ni mdogo kwako kukupa ushauri, lakini..."

"Hapana. Uko sahihi Tristan. Nahitaji kubadili mtazamo wangu kuhusiana na mambo mengi sana," akanikatisha.

"Kwa sababu tu nimetuliza hamu yako?" nikamuuliza kumtega.

"Ahahah... hapana. Kwa sababu ndiyo jambo sahihi kufanya. Nitamrudisha Magda kazini na kumwomba msamaha. Nimemfanyia vibaya sana yule dada."

"Nafurahi kujua umetambua hilo. Ndiyo jambo bora unalopaswa kufanya boss."

"Kuanzia leo, mimi kwako siyo boss tena, niite Ritha," akaniambia huku akianza kunisogelea mdomoni ili anipige busu.

"Unajua kuwa hatuwezi kuendelea hivi, siyo?" nikamuuliza kabla hajanibusu.

"Why? Kwa sababu mimi ni boss wako? Au kwa sababu nakuzidi umri? Nina miaka 42 tu, siko mbali kihivyo."

"No, ni kwa sababu nafikiri unastahili mtu mwingine ambaye atakupenda na kukujali jinsi utakavyo," nikamjibu.

"Na huyo siyo wewe?"

"Ahahah... hapana. Me ni kiazi tu."

"Nakutaka hivyo hivyo."

"Nisikilize boss. Utakachofanya kuhusu kubadili suala la Magda na mambo mengine, fanya kwa ajili yako, siyo kwa ajili yangu. Nathamini kujua kwamba utafanya mabadiliko siyo kwa sababu nilikutisha, ila kwa sababu unataka kutoka moyoni kuyafanya."

Akatabasamu kidogo na kusema, "Sikujua kuwa huwa unaongea vizuri hivi."

"Nina mazoezi ya speech," nikasema.

Akacheka kisha akasema, "We' ni mtundu sana. Napenda macho yako."

"Asante," nikamwambia huku nikiwa nimemwaza Salma baada ya yeye kusema hivyo.

Sikujua ikiwa macho yangu yalikuwa na athari fulani kwa wanawake hawa, ila kila walipoyasifia nilijisikia vizuri.

"Umependa nini kuhusu mimi?" akaniuliza.

"Nimelipenda kalio lako, tokea zamani sana," nikasema.

Akacheka kidogo kisha akaanza kunipiga busu.

"Boss nahitaji kurudia kazi zangu," nikamwambia huku namwonyesha nataka kunyanyuka.

"Kwa hiyo, hii inamaanisha hatutakuwa pamoja tena?" akauliza huku sura yake ikionyesha kukwazika.

"Hapana... siyo lazima iwe hivyo. Tuta... tutaonana tena, wakati mwingine," nikamwambia ili kumtuliza.

Nilifata shati na suruali yangu na kuanza kuivaa. Nikachukua viatu na kuvaa pia huku nikimwacha yeye amekaa kwenye sofa akinitazama tu. Nilipomaliza, nilichukua funguo zilizokuwa mezani na kumwonyeshea huku nikizitingisha hewani ili ajue kuwa nilikuwa naenda kufungua mlango; kama kumuaga.

Alinyanyuka na kuanza kunifata taratibu na viatu vyake virefu, akiwa kama alivyozaliwa, na kunikumbatia. Mwili wake ulikuwa wa moto na hilo lilifanya nisisimke. Aliniachia na kunipiga busu kwenye shavu, kisha akaniangalia na kutabasamu. Nilitabasamu pia na kwenda kufungua mlango.

Nilichungulia kama kuna mtu hapo karibu, na kisha nikatoka baada ya kuridhika hakukuwa na mtu yeyote. Kwa kuwa nilijua baadhi ya watu wangeshangaa kuniona nashuka kutoka ofisini kwa boss, nilihitaji kutoka pale bila kuonekana. Nilipoangalia simu, nilikuta ni saa nane na nusu na sasa nilikuwa nimebakiza muda mfupi kabla ya kazi kuisha. Nilisema maneno yale ambayo sikuwa nimeyasema kwa kitambo kifupi sasa.

"Aóratos."

Kisha nikashuka moja kwa moja hadi kwenye vyoo vya wanaume na kuyasema tena maneno hayo ili nianze kuonekana. Nilirudi mezani kwangu na kuketi ili nianze kazi, na kushtushwa na Justine aliyenichoma kwa peni mgongoni.

"We fala ulikuwa wapi?" akauliza.

"Dah, mbona kuchomana tena bro? Nilikuwepo mbona muda wote," nikamwambia.

"Haukuwepo wewe tokea muda ule ulivyopanda juu. Na sikukuona ukirudi chini."

"Macho yako tu."

"Uliuona ujumbe wangu? Yaani umepitwa mwana nilienda lunch na Juliet na Lydia hapo. Tumepiga mazaga kama yote. Umeukosa utamu," akaniambia huku akiwa hana habari mimi nilikula utamu zaidi yake.

"Pole mwana, nilikuwa chooni," nikamwambia.

"Hivi huko chooni huwa unafanya nini bro? Yaani we' huwa ni chooni tu! Huwa unakaa kuhesabu makapi ya watu huko ama?"

"Iih... hivi nilikuwa sijakwambia kwani?" nikamtania.

"Tutaonana kesho," akasema na kuanza kuondoka.

Nilicheka sana na kuanza kuangalia kazi zilizokuwepo. Nikajitahidi kukazia fikra kazi lakini akilini mwangu bado boss Ritha alizunguka. Nilijua kujizuia ilikuwa uamuzi mzuri, lakini bado niliendelea kuuwazia mwili wake ule, midomo yake, kalio hilo, na tamu tamu sweet eti. Nilijisikia fahari kuwa niliweza kumsaidia kubadili maoni yake na kutuliza hamu yake; angalau kwa leo. Nilipata text kwenye simu yangu muda mfupi baadae na kuichukua ili nisome.

'umekula?' ilisomeka. Alikuwa ni boss Ritha.

'hapana.. namalizia kazi nitakula baadae,' nikamjibu.

'nimeagiza mtu akuletee chakula'

'boss, sidhani kama hiyo ilikuwa ni busara maana huu ni muda wa kazi. Watu watashangaa kwa nini umeniruhusu nile'

'usiwaze kuhusu hilo my Tristan. Be free kabisa'

Duh! Nimeshakuwa "my Tristan" wa boss sasa! Nilicheka kidogo na kutambua kuwa, kama kuniganda, basi ataniganda sana. Muda mfupi baadaye, nililetewa chakula pale nilipoketi, na nilitambua watu walinitazama sana wasielewe nimetolea wapi ujasiri wa kuleta msosi muda wa kazi. Niliwapotezea na kuanza kukamua taratibu huku naendelea na kazi.

★★

Baada ya saa za kazi kuisha, nilimfata Justine ili tuongozane kuondoka. Alikuwa anamalizia baadhi ya mambo yake, pale nilipomwona boss upande wa juu wa ngazi akiwa amesimama akiniangalia. Alitoa ishara kwa kidole kuwa nimfate, kisha akarudi juu ofisini. Nilijua fika kuwa alifanya hivyo makusudi, kwa sababu kama alitaka kuniita kawaida, angeweza kunitumia ujumbe, lakini alifanya hivyo kusudi baadhi ya watu wamwone ili nisiweze kukataa kwenda.

"Umeona? Nilikwambia fala wewe, ukajifanya mjanja. Unapenda mno kulala chooni. Nenda kalambwe nyekundu sasa hivi," akaniambia Justine.

Alikuwa anamaanisha suala la mimi kuleta chakula muda wa kazi, akifikiri boss alikuwa ananiita ili anifokee au kunipa adhabu fulani kwa kukiuka utaratibu. Ilibidi niigize tu kwamba sikuwa na jinsi; nikapanda ngazi mpaka ofisini kwake. Kwa kuwa nilikuta mlango uko wazi, niliingia moja kwa moja na ndipo nikahisi mkono wangu ukivutwa na kugeuka nyuma.

Ilikuwa ni boss aliyenivuta hivyo na kunipeleka kinywani mwake pale pale, akinibusu kwa fujo. Kwa kuwa hakuonekana kujali kwamba mlango ulikuwa wazi, nilianza kumsogeza taratibu kwa kutembea kuuelekea mlango huku bado akiung'ang'ania mdomo wangu, kisha nikaufunga kwa nyuma yake na kumkandamizia mlangoni kwa mgongo. Alishika sehemu yangu ya siri, nami nikajua alichokuwa anataka, lakini kwa wakati huu mimi sikutaka kukifanya. Nikaushika mkono wake na kuutoa juu ya suruali yangu. Aliachisha busu yake na kunitazama.

"Boss..."

"Nilikwambiaje kuhusu kuniita hivyo?" akanikatisha.

"Aam... Ritha, najua unachotaka. Lakini now's not a good time," nikamwambia.

"Nooouh... I want right now!" akasema kwa sauti ya kudeka.

"Tupange wakati mwingine tafadhali... nimechoka kidogo," nikajifanya kama nimechoka kweli.

"Okay. Kesho basi... kwa kuwa hautakuja kazini, tuonane," akaniambia.

"Oh... kesho Jumapili? Ah sikutambua jinsi siku zinaenda. Sawa basi, ikiwa itawezekana nitakupanga," nikamwambia.

"No. Mimi ndo' nitakupanga. Nataka twende sehemu moja nzuri sana."

"Wapi?"

"Utaona tu. Na sitaki masuala ya kusema 'ikiwa itawezekana,' fanya juu chini iwezekane," akasema huku amenikazia macho.

Mambo yalikuwa yamejijenga haraka sana kufikia hatua hii. Nilipendezwa na boss, lakini siwezi sema nilijihisi huru sana kuwa naye. Nilimheshimu, na sasa alikuwa anataka jambo lingine zaidi ya heshima kutoka kwangu ambalo nilimpatia kwa muda mfupi saa zile. Nilikuwa mtu mmoja ambaye sikupenda kukwaza watu, lakini kama matendo yao yangepita kiasi, nisingesita kuyakataa au kuyazuia. Kwa upande wa boss, nikaona tu nikubali ili auridhishie moyo wake furaha aliyoitaka kwa wakati huu. Lakini nilijua ipo siku nilitakiwa kuvunja muungano wangu pamoja naye.

Alinipiga busu tena kisha nikaondoka. Nilimkuta Justine na wengine wakinisubiri kuniuliza alichoniitia boss, nami nikawaambia tu alinikanya nisirudie tena kula ndani ya ofisi. Ilionekana kuwa vyepesi zaidi kusema hivyo tu.

★★

Baada ya kuondoka na kufika nyumbani, nilimkuta Salma akiwa ameketi chini ya mlango wa kuingilia chumbani kwangu. Kwa kiasi fulani, moyo wangu ulifurahi sana kumwona. Lakini akili yangu ilijua kuwa lazima kutakuwa na jambo zito alilotaka kuniambia hadi achukue hatua hii. Aliponiona, alinyanyuka na kunitazama kwa macho yaliyoonyesha wasiwasi.

"Tristan," akaita.

"Salma," nikaitika.

Alinifata haraka na kunikumbatia kwa wororo sana. Alikuwa akisugua kichwa chake kwenye bega langu taratibu (purring), nami nikamzungushia mikono mgongoni mwake taratibu.

"Nimeku-miss sana mpenzi wangu," akasema kwa sauti ambayo ilisikika kama analia.

Nilimwachia na kumtazama. Alionyesha huzuni usoni lakini hakutoa machozi.

"Kwa nini uko hapa? Vipi wazazi wako wakikuona?" nikamuuliza.

"Hawapo... wametoka" akajibu.

"Sawa. Nime... nimeku-miss pia. Nini kinaendelea?" nikamuuliza kama vile sifahamu.

"Tuingie basi ndani ili tuongee," akasema.

Nilitii kisha kufungua mlango na sote tukaingia. Aliketi kitandani, nami nikaketi pembeni yake.

"Sijui... nisemeje," akasema.

"Sema tu," nikamsihi.

"Nimetafutiwa mchumba."

"Okay. Umetafutiwa mchumba na nani?"

"Wazazi wangu."

"Kwa hiyo... umeafiki?"

"Aam... yaani... mimi sitaki kuolewa naye," akasema huku akiangalia chini.

"Kwa nini usiwaambie wazazi wako hilo?"

"Wanajua. Lakini wananilazimisha... hasa baba. Imefikia pindi nikakosa amani kabisa. Huyo kaka ni mtu mzuri tu, lakini sijampenda," akaeleza.

"Pole Salma. Kwa hiyo... umemkataa?" nikamjaribu.

"Sikuwa na jinsi Tristan. Imebidi nikubali kwa sababu ya..."

Nikamshika mabegani na kumtazama kwa ukaribu. "Usijali. Mimi na wewe... ilikuwa perfect yaani. Lakini ikiwa suala hili unaona liko nje ya uwezo wako na inakubidi ukubali, basi fanya unachoona kuwa sahihi. Na mimi nitaheshimu hilo," nikamwambia kwa upole.

"Lakini Tristan, mimi nakupenda wewe," akasema huku machozi yakianza kumtoka.

Nilimfuta machozi yake na kumwambia, "Najua. Lakini pia najua kwa hali yetu, dini, na mambo mengi, haitakuwa rahisi kwetu kuendelea kuwa pamoja. Na kama huyo kijana ni mtu mzuri, mpatie nafasi. Mjue vizuri zaidi ili ujenge connection naye itakayowaunganisha," nikasema kwa hisia.

Alianza kutokwa tena na machozi huku akitikisa kichwa chake zaidi kama anakataa. Nilimkumbatia naye akaendelea kulia. Ni kama dakika mbili zilipita ndipo tukasikia mlango ukigongwa. Nilimwachia taratibu Salma naye akaanza kujifuta machozi.

"Nani?" nikauliza kwa sauti.

"Ni Zaina," akajibu.

"Unasemaje Zai?" akauliza Salma.

"Wako njiani kurudi," akajibu nje ya mlango.

"Haya nakuja," akajibu Salma.

"Zaina alikuwa anajua uko huku?" nikamuuliza Salma.

"Ndiyo. Anajua kuhusu mimi na wewe. Nilimwambia ninakupenda," akajibu.

"Nani mwingine anajua kuhusu sisi?"

'Ni yeye tu na wale rafiki zangu. Lakini Tristan, nakuahidi, hata kama nitaolewa na mtu mwingine, sitoacha kukupenda kamwe," akasema.

Niliona maneno haya kuwa kama moja ya ahadi ambazo watu fulani hupeana lakini baada ya muda zinasahaulika. Nilijua binti huyu alipendezwa nami sana, lakini hakujua kwa undani jinsi gani niliyaona mahusiano ya kimapenzi. Hakujua sababu iliyofanya nikae single kwa muda mrefu vile. Na pia nilijua alikuwa na rundo la hisia zilizovurugika kutokana na haya yote, hivyo nikamwitikia vizuri ili aridhike moyoni mwake.

Nilimbusu kwenye shavu, kisha akaondoka haraka. Alikuwa akificha machozi yake zaidi ili nisiione huzuni yake. Nikashusha pumzi na kuwaza kwa kweli, kazi ninayo. Mara huko boss, mara huku Salma, mara kule Enrique, mambo mengi nilihitaji kushughulika nayo kwa akili. Lakini kwa kuwa kesho ilikuwa mapumziko, niliwaza tu kukiachia kichwa changu kutokana na stress na kufanya mambo ambayo yangeniletea ahueni.

Simu yangu ilianza kuita muda mfupi baadae nami nikakuta ni Magda. Nilikuwa nimepanga kumpigia baada ya kula lakini akawa ameniwahi. Alinieleza kuwa boss Ritha alimpigia na kumwomba samahani kwa jinsi alivyomtendea, na kwamba alimuomba arudi kazini Jumatatu. Aliniuliza niliwezaje kumshawishi boss mpaka akawa mpole namna hiyo, nami nikamwambia ilikuwa rahisi kama maji ya kunywa tu. Alinishukuru sana, nami nikamwambia ikiwa atahitaji lolote lile, niko pamoja naye.

Kwa upande huo mambo yalikwenda vizuri, na baada ya hapo nilipiga story kidogo na Justine kisha nikaenda kulala.


★★★


Nilikuwa nimepanga kulala mpaka saa sita mchana wa siku mpya, lakini haikuwa mbaya baada ya siku kukucha na kukuta ni saa tatu ndiyo nimeamka. Nikafanya usafi kama kawaida yangu na kunywa chai. Nilikuta 'missed call' mbili na meseji chache kutoka kwa boss baada ya kuangalia simu yangu. Aliniambia nimtafute haraka ili tuongee na kunifanya nicheke. Bado alikuwa na mwelekeo wake wa kulazimisha mambo, lakini angalau kwa sasa nilikuwa napendezwa naye, hasa baada ya yeye kuonyesha kweli ameanza kubadilika baada ya kumwomba radhi Magda.

Nikampigia simu mara tatu, lakini hakupokea. Nilihisi labda anafanya mambo yake, hivyo nikamwacha ili akija kuziona missed call zangu anipigie mwenyewe. Baada ya kuangalia baadhi ya vitu vilivyoisha ndani, niliamua nitoke kwenda kununua bidhaa mbalimbali sokoni na kurudi haraka. Wakati natoka, nilimpita mama yake Salma pamoja na Salma wakiwa wameketi nje pale na kuwasalimu. Salma alinitazama kama alitaka nimpe ishara fulani, lakini mimi nikapita zangu tu getini na kuosha.

Nilikuwa nakaribia maeneo ya soko kubwa la bidhaa pale nilipomwona mwanamke fulani mrembo sana. Yaani alikuwa mzuri kiasi kwamba nilishindwa kujizuia kumtazama sana. Alikuwa amevaa T-shirt nyeupe iliyobana yenye mikono mifupi, na suruali ya 'jeans' ya blue iliyobana hips zake vyema na kufanya kalio lake kubwa kiasi lionekane vyema kwa nyuma. Alikuwa na ngozi nyeupe sana; kitu ambacho kwangu mimi sikuzote kilinipendeza kwa mwanamke ni ngozi nyeupe. Alikuwa na nywele ndefu kufikia mabega yake na nafikiri zililazwa kwa dawa na kufanya zing'ae.

Lakini, haikuwa uzuri wake tu ndiyo ulionifanya nimkazie fikra sana. Ilikuwa ni kama namfahamu, na jambo hilo lilinitia wazo la kuwa lazima angekuwa na umuhimu fulani kwangu. Sikujua ni kitu gani tu, lakini kitu hiki kilinisukuma nimfatilie kuona alielekea wapi. Nililivuka soko na kuanza kumfata taratibu. Alikuwa upande wa pili wa barabara, hivyo nilitaka kumsogelea karibu zaidi, lakini kwa njia ambayo hangetambua namfatilia.

Nilifika kwenye kona moja na kujibanza, na baada ya kuhakikisha hakukuwa na mtu, nikasema, "Aóratos," kisha nikarudi barabarani ili niendelee kumfata. Kuna wakati nilikuwa najiona kama mpuuzi kufanya jambo hili, lakini bado nilisukumwa na moyo wangu kuamini kuwa nilikuwa nina maana yangu. Nilivuka barabara, bila mtu yeyote kuniona, na sasa nilikuwa usawa wake kwa nyuma nikimfata taratibu huku najihadhari nisigongane na mtu kimakosa. Alitembea kwa maringo fulani huku nikiwaona baadhi ya wasela wakimtolea macho kwa matamanio. Mimi pia nilikuwa mmoja wao, lakini sikuonekana!

Tulifika maeneo fulani yaliyokuwa na uwazi mpana sana, na upande wa pili wa barabara niliweza kuiona shule fulani kubwa ya international ya watoto. Alifika kwenye duka fulani mbele kidogo na kusimama kisha kuanza kuzungumza na muuzaji nafikiri. Kwa jinsi walivyoongea, Ilionekana walijuana maana alikuwa akicheka sana. Nilikuwa nimesimama kwa umbali kidogo, na baadhi ya watu wangepita na kunipamia bila kuniona, hivyo nikajibanza kwenye ukuta mfupi ambao ulikuwa kama fensi la nyumba kubwa iliyokuwa na maduka upande huu wa mbele.

Nilimtazama dada huyu, alinichanganya sana. Sikujua nimewahi kumwonea wapi, lakini nilihisi kuwa na ukaribu naye ambao sikuweza kutambua ni nini. Niliangalia tabasamu lake na mwili wake uliopendeza sana. Nikawaza bila shaka aliyekula hapo lazima alikuwa ameenda shule.

Nilipokuwa nikiendelea kumtazama mrembo huyu, nilishtushwa na sauti nyuma yangu ikisema, "Wewe usijali... kila kitu kitakwenda kama tulivyopanga."

Niligeuka nyuma na kukuta ni mwanaume fulani aliyekuwa amevalia kitanashati; suti nyeusi na miwani yenye kuonyesha macho, kama vile ni kwa ajili ya macho. Hakuwa akinitazama, kitu ambacho kilinipa ahueni kwa kuwa bado nilikuwa sionekani. Nilishusha pumzi taratibu na kuangalia huku na kule kama kuhakikisha bado sionekani.

Nilipomtazama tena, nikatambua alikuwa ameweka simu sikioni, na hiyo ikaniambia kuwa alikuwa akiongea na mtu fulani kwenye simu. Alikuwa amesimama kando yangu, bila kuniona kabisa, na akaendelea kuongea na mtu wake upande wa pili wa simu. Niliona nimpotezee kwa kuwa hakuwa na jambo lolote kunielekea mimi, na kurudi zangu kuendelea kumtazama mrembo wangu.

Baada ya kuwa nimegeuka kurudi kumwangalia mrembo yule, nilivunjika moyo sana pale ambapo sikumwona tena sehemu ile. Niliangalia huku na kule lakini sikuweza kumpata mbele ya macho yangu, huku nikiwa sina wazo angekuwa ameelekea wapi. Nilihisi huzuni moyoni, lakini pia hisia za kukerwa, kwa kuwa huyu boya nyuma yangu ndiye aliyesababisha nikengeuke na kufanya ndege wangu apeperuke.

Nilisikia hasira ya kutaka hata nigeuke nimkoe kichwani yule jamaa, pindi nilipogeuka kukuta ameshikilia bastola ndogo mikononi mwake. Nilishtuka kiasi lakini sikujongea hata kidogo. Alikuwa akiikoki mikononi mwake, kama kujiandaa, na kisha akaiweka nyuma ya kiuno chake na kuifunika kwa koti juu yake ili isionekane. Nilipomtazama usoni, sikuona dalili yoyote ya ugaidi, alikuwa na uso uliotulia na hilo lilionyesha kuwa kwa jambo lolote alilokuwa anataka kufanya, alijiamini. Nikawaza kuwa huenda ni askari na alikuwa kwenye masuala ya upelelezi eneo lile.

Sikutaka kutia bidii sana kutaka kujua mengi kuhusu jamaa huyo, hivyo nikaona nitulie tu mpaka aondoke na mimi niende kivyangu. Alianza kutembea kuelekea barabara na kuivuka. Ijapokuwa nilikuwa nataka kuondoka, udadisi ulinifanya niendelee kumtazama ili kuona angeelekea wapi.

Nilishangaa sana kuona akiingia getini mwa shule ile ya international ya watoto. Niliwaza huyu mtu angehitaji nini kutoka kwenye shule ya watoto wadogo, ambacho kingemfanya aikoki bastola namna ile huku pia akiwa ametoka kuongea na mtu fulani kwenye simu kumhakikishia "mpango" wao utaenda vizuri.

Kwa kuwa bado nilikuwa sionekani, wazo likanijia kichwani kuwa ingekuwa jambo lenye kuburudisha ikiwa ningepata kujua kilichoendelea shuleni hapo. Nikaanza kutembea kuelekea geti la shule ile huku akilini nikikumbukia michezo tuliyofanya utotoni ya polisi na jambazi. Eti sasa na mimi nikaanza kujifanya nimeingia kwenye movie fulani hivi; naenda kufichua jambo zito.

Nilipofika karibu na geti la shule ile, niliona kuwa mlango mdogo wa getini ulikuwa wazi. Nilipenya na kuingia ndani pale. Upande wangu wa kushoto kulikuwa na jengo dogo ambalo ndani yake kulikuwa na wanaume wawili; wakiwa wamevaa sare za rangi ya samawati (blue). Nikatambua kuwa hawa walikuwa ni walinzi, lakini hawakuweza kuniona kwa kuwa waliendelea kupiga story.

Nilisogea mbele kidogo na kuitazama shule ile. Bila shaka watoto wengi waliosoma pale walikuwa na wazazi wenye pesa kwa jinsi ilivyokuwa imepangiliwa kwa umaridadi. Niliweza kuona sehemu yenye uwanja mkubwa uliokuwa na bembea za watoto na kiwanja kidogo cha mpira wa miguu. Upande mwingine ulikuwa na magari yaliyoegeshwa; mabasi ya shule na gari zingine ndogondogo, huenda za walimu na wafanyakazi wa pale.

Jengo lile la shule lilikuwa kubwa; likiwa na ghorofa tatu ambazo zilikuwa na madarasa mengi. Nilitazama huku na kule kama ningeweza kumwona yule mwanaume lakini sikuweza. Nilifikiria atakuwa ameingia ndani ya jengo lile, lakini nisingeweza kujua amekwenda wapi kihususa. Nilianza kuona kama kitu nilichokuwa nakifanya wakati huu kilikuwa cha kipuuzi na kitoto. Nikaona bora tu niondoke, kwenda kwenye mambo muhimu zaidi; kama boss Ritha.

Ni wakati huo nilipokuwa nafikiria kuondoka, pale nilipomwona yule jamaa akishuka kutoka kule juu, huku akiongozana na mvulana mdogo. Mvulana huyu alikuwa mweupe na alivaa miwani machoni; nikahisi ni miwani ya macho. Mwanaume yule alikuwa ameweka mkono mmoja kwenye bega la mvulana huyo huku ikionekana kama alikuwa anamwongoza kwenda sehemu. Walifika mpaka kwenye sehemu ya maegesho na kuingia ndani ya gari dogo jeusi; aina ya Suzuki, kwenye siti za nyuma.

Nilishindwa kuelewa. Nilikuwa nina uhakika kwamba nilimuona mwanaume huyo akiingia shuleni humo huku akitembea. Gari aliloingia pamoja na mtoto yule lilitoka wapi? Na kuona kwamba waliingia siti za nyuma ilimaanisha kulikuwa na mtu siti ya mbele kama dereva; ikimaanisha tayari alikuwa pale akiwasubiria watoke.

Haingepatana na akili kufikiri kwamba labda yule jamaa alikuwa baba yake; baba gani anamfata mtoto shuleni akiwa na bastola, tena kuikoki kabla ya kuingia? Nikiwa bado najiuliza-ulizamaswali, gari lile lilianza kuja upande wa getini ili litoke nje. Kwa kuwa sikuwa mbali sana na geti, nilirudi nyuma kidogo na kusimama pembeni karibu na kale kajengo walikokaa walinzi. Gari lilipofika usawa huo, likasimama kwa kuwa ilihitajika mlinzi afungue geti.

"Aaah William mwanangu vipi?" akasema mlinzi mmoja baada ya kusogea karibu na kioo cha mbele cha gari.

Lakini hakuwa akimtazama dereva, bali alitazama kuelekea siti za nyuma. Nilisogea mpaka nyuma ya gari lile, na kufanya kama nimejibanza kwa upande ule aliosimama mlinzi huku naangalia.

"William anaumwa leo, ndiyo tumekuja kumchukua kumpeleka hospitali," akasema dereva mbele.

Niliona mlinzi akimtazama dereva kwa makini kisha akamuuliza, "Nani amewatuma mje kumchukua?"

"Baba yake," akajibu yule dereva.

Niliona mlinzi akitazama tena nyuma kisha akauliza, "Unaumwa nini dogo langu?"

Bila shaka alikuwa anamuuliza mvulana huyo swali hilo, lakini hakujibu.

"Ana homa kali sana," akajibu yule mwanaume aliyekaa nyuma.

"Lakini mbona ameletwa hapa leo asubuhi akiwa mzima kabisa?" mlinzi akauliza.

"Alianza kuzidiwa muda mfupi baadae, ndiyo tukapigiwa simu na baba yake tuje kumchukua aende hospitali," akajibu.

Nilizunguka upande wa pili wa gari hilo ili nimwangalie huyo mtoto. Niliona kupitia kioo alikuwa amebanwa na mkono wa huyo jamaa, kama kamkumbatia, huku uso wake ukionyesha jambo moja lililonitia mashaka; alikuwa anaogopa. Sasa nilitambua kuwa hawa watu hawakuwa wazuri na huenda wangemdhuru mtoto huyu.

Nikiwa najiuliza jambo la kufanya, sauti za geti lililokuwa likifunguliwa zikapiga masikio yangu. Sasa gari lingeondoka na kwenda mahali ambako sikujua. Hakukuwa na muda wa kuita polisi au kujitokeza kujaribu kujifanya shujaa. Niliichezesha akili haraka sana na kuomba kwa Mungu kuwa nilichotaka kufanya kingefanikiwa. Nilirudi nyuma ya gari haraka na kushika kifungulio cha mlango wa nyuma kabisa ya gari, ule wenye tairi la ziada, kisha kuuvuta kwa nguvu nikiwa na matumaini utafunguka. Sala yangu ilijibiwa na papo hapo ukafunguka; taratibu ukipanda juu.

Kutoka niliposimama, baada ya mlango kuwa umefika juu na kutulia, nilikutana uso kwa uso na jamaa akiwa anashangaa baada ya kuona mlango unapanda juu. Hakuniona, kwa kuwa aligeuka na kutazama mbele ya gari kisha kusema, "Oya, ulikuwa hauja-lock buti ya nyuma... imefunguka."

Yule dereva alishuka ili aje kuufunga mlango ule. Pale pale nikaingia faster, kwa umakini, na kujilaza pale nyuma. Niliona tu mlango ule ukishuka chini na kubamizwa kwa nguvu, kisha ukasikika uki-lock kwa funguo. Alirudi ndani ya gari na kuanza kuendesha kutoka getini, bila kujua kulikuwa na abiria asiyeonekana akiwa amejilaza nyuma ya gari.

Lazima niseme kuwa kile kilikuwa kitu chenye kusisimua sana ambacho sikuwahi fanya kabla. Mapigo ya moyo yalidunda kwa uharaka hivyo nikajitahidi kupumua kwa utulivu. Sasa nilikuwa nimejiingiza kwenye ishu ambayo sikujua ingenipeleka na kuniacha wapi.

"Dah... umeona jinsi palivyokuwa tight pale? Ndiyo maana ilikuwa vizuri kama tungeingia kwa pamoja," akasema yule dereva.

"Wala hata hawangezingua hao mabwege," akajibu jamaa wa nyuma.

"We ndo' unazingua. Ulitakiwa uwahi ili tuingie wote kwa hiyo hata wakati wa kutoka wasingekuwa na udadisi sana."

"Kama wangeleta zengwe ningewalamba mbili za kichwani tu. Uzuri dogo anajua kuigiza huyu."

Nilikuwa nyuma nikiwasikia wakiongea namna hiyo. Nilinyanyua kichwa changu ili niweze kuangalia nyuma pale na nikaona yule jamaa akiwa ameketi huku ameshikilia bastola yake mkono mmoja na mwingine ameuweka juu ya siti kumzunguka mtoto. William, huyo mvulana mdogo, aliendelea kuketi kwa utulivu sana.

Ghafla, gari likaweweseka na kunifanya niangukie upande wa nyuma; bila kutoa kishindo kikubwa. Lilikatisha mwendo baada ya dereva kufunga breki ghafla sana.

"We vipi?" aliuliza jamaa aliyeketi na William.

"Kuna mtu huko nyuma yako!" akajibu dereva.

Macho yangu yalitanuka kwa kupatwa na mshtuko. Nilijua wazi kuwa alimaanisha mimi. Lakini aliwezaje kuniona?


★★★★★★★★★

 ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Previoua Next