Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Ysiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA TANO

★★★★★★★★★★★★★


Nilishangaa. Alihitaji kunyanyua miguu yake ili aweze kuizungushia vyema mikono yake mgongoni kwangu sababu ya mimi kuwa mrefu, na niliweza kuzihisi vyema sana pumzi zake laini shingoni kwangu. Yaani hata kama ningekuwa nimebarikiwa kuishi kwa karne mia moja, hiki ni kitu ambacho singetarajia kuja kukipata ndani ya muda huo wote. Kumbatio lake lilikuwa laini, yaani, hakuubana sana mwili wake kwangu, na mimi kutolirudisha upesi ndiyo kulifanya nisiuhisi vyema zaidi mwili wake mbele yangu. Kusudi la yeye kunikumbatia hivi lilikuwa nini?

"Asante."

Neno hilo lilisikika kutoka kwenye kinywa chake nyuma yangu, nami nikajipa tu ujasiri wa kurudisha kumbatio la mwanamke huyu kwa kuubana mwili wake kwa mikono yangu taratibu. Hata pombe haikuwa imenichanganya sana kunizuia nisielewe shukrani aliyotoa ilihusiana na nini. Alikuwa ananishukuru kwa kumsaidia mdogo wake, yaani Mariam, bila shaka akiwa ameambiwa yote yaliyotokea jioni ya siku iliyotangulia; maana hii ilikuwa mpya sasa. Kuubana mwili wa mwanamke huyu namna hii kulinipa hisia ya joto lenye kutuliza, siyo mwilini, ila moyoni. Sikuelewa ni kwa nini ila nilihisi amani yenye nguvu sana. Akaniachia taratibu na kurudi nyuma, nami nikawa namwangalia tu machoni. Mpaka kufikia hapo sikuwa nimetilia maanani kuwa alivaa 'night dress' laini na ndefu yenye rangi ya shaba iliyong'aa, ila ndiyo sasa nikawa nimeiona vizuri.

"Haya, usiku mwema. Nenda kalale," akaniambia hivyo huku akijifunika vizuri kwa nguo ya juu ya hiyo 'night dress.'

Kuna kitu kiliniambia kwamba alifanya hivyo akidhani nimelewa sana, kwa hiyo labda nisingekuja kukumbuka namna alivyonikumbatia ama shukrani yake ya moyoni aliyoitoa. Lakini niliithamini mno, na hilo ni jambo ambalo sidhani kama alifikiri nililichukulia kwa uzito.  Nikatazama upande wa mlangoni ambako tayari Tesha alikuwa ameshaingia ndani, nami nikamtazama machoni na kutikisa kichwa kidogo kuonyesha uelewa, kisha nikaelekea nje. Sauti za makomeo ya geti kufungwa zilisikika mpaka nilipofika upande wa pili wa ukuta uliotenganisha nyumba zetu, nami nikasimama kumtazama mwanamke huyo kupitia yale matobo ukutani. Alikuwa anaingiza viatu vya mdogo wake ndani, kisha akafunga geti dogo la mlangoni na mlango pia, akitokomea huko. 

Nikashusha pumzi kujipa utulivu maana angalau hali ya hapo ilikwenda vyema zaidi ya nilivyotazamia, nami nikaenda mpaka kule ndani ili nikawaangalie wale walimbwende. Sijui walikuwa wameshazimia huko? Nikafika ndani na kumkuta Joy sebuleni, akiwa amekaa kwenye sofa moja huku mkononi akishikilia bakuli la plastiki na kijiko. Alionekana kunywa mchuzi wa nyama pamoja na kutafuna nyama, nami nikasimama usawa wa meza.

"Ankia yuko wapi?" nikamuuliza kwa sauti ya chini.

"Ameingia kulala," akajibu.

"Na wewe?" 

"Nilikuwa nakusubiri uje."

"Sawa. Ngoja nikafunge geti kwanza. Sijui hata funguo huwa anaweka wapi..."

"Hapo juu ya mlango," akaniambia.

Nikageuka na kunyoosha mkono wangu mpaka juu ya mlango wa kuingilia, nami nikazichukua funguo.

"Siyo mara yako ya kwanza kuja hapa, eh?" nikamuuliza.

"Hamna, hapa ni nyumbani. Tushalala sana hapa," akaniambia.

Nikafungua tu mlango tena ili niende kule nje kulifunga geti.

"Utakuta nimekuwekea nyama, sawa?" akaniambia hivyo.

"A-ah... usiniwekee. Nikija ni kulala tu," nikamzuia namna hiyo na kisha kwenda nje.

Nikaenda na kuhakikisha nimelifunga vizuri geti letu dogo huko nje, na kiukweli bado pombe ilikuwa inazunguka kichwani lakini nilikuwa naweza kujiongoza vizuri sana. Nikarudi zangu ndani na kuifunga milango pia, na Joy alikuwa amekaa tu kwenye sofa bado huku bakuli akiwa ameshalishusha. Nikaweka funguo juu ya mlango, kisha nikamgeukia.

"Me naenda kulala. Nizime taa, au bado upo?" nikamuuliza.

"Hamna, zima tu. Twende tukalale," akaniambia hivyo na kusimama.

Ka!

"Tukalale wapi?" nikamuuliza.

"Chumbani kwako," akajibu.

"Aa wee... nenda kalale na mwenzako huko. Sitaki bughudhi," nikasema hivyo na kuzima taa.

Nikaanza kutembea na kumpita, lakini akakishika kiuno changu kutokea nyuma na kunifanya nimgeukie.

"JC..."

"Nini?"

"Me nataka tukalale wote," akaongea kwa sauti ya utongozi.

"Kwa nini?"

"Mhh... nakupenda..."

"Eh... Joy, naomba uniachie. Utanipenda siku nyingine, leo hapana," nikamwambia hivyo.

"Nisikilize JC..."

"A-ah..."

Nikaitoa mikono yake kwangu na kumwacha akiwa amesimama hapo, nikielekea tu chumbani. Si unajua tu huwa kuna kale kakitu kanakokusukuma ukifate kitanda baada ya kunywa pombe na kupiga usingizi bila kujali chochote? Ndiyo kalikokuwa kameniteka sasa hivi. Nilitaka kulala zaidi ya jambo lingine lolote. Nikaweka simu yangu chaji, nikavua kila kitu Isipokuwa boksa tu mwilini, nami nikakaa kwanza kitandani. Kahisia kazuri kanakotokana na kulewa kiasi nilikuwa nakasikilizia, huku nikijishauri sijui nishushe neti, sijui niache? Ah neti kwenda kule! Ningelala hivyo hivyo tu maana mbu wengi walikuwa wamenyamazishwa kwa dawa hata hivyo, kwa hiyo kilichokuwepo ilikuwa ni kuzima tu taa na kulala. Lakini kabla sijatoka kitandani kwenda kuizima, mlango ukafunguliwa. Nikaangalia hapo kwa umakini na kumwona Joy anaingia, naye akasimama hapo hapo mlangoni huku akinitazama kwa macho yaliyolegezwa na pombe.

"We... funga mlango bana, mbu wanaingia," nikamwambia hivyo.

Akaingia ndani na kuufunga mlango, na sasa nikaweza kumwona vyema zaidi. Wakati huu alikuwa ameshaitoa nguo yake aliyokuwa amevaa, akiwa amebaki na nguo za ndani nyeupe na laini zilizoficha sehemu za uanamke, ingawa ningeweza kuyaona mashavu manene kiasi ya mlima wake kwa nyuma. Akanigeukia na kunitazama kwa ujasiri, naye akaanza kuja mpaka kufikia nilipokaa na kusimama mbele yangu.

"Mbona umeufunga mkono bandeji? Umeumia?" akaniuliza.

"Nilikwambia ufunge mlango, sikukwambia uingie," nikamwambia hivyo.

"Acha mashauzi yako bwana..." akanisemesha kwa nyodo.

"Nani anajishaua?"

Akanishika usoni kwa viganja vyake, lakini nikavikwepa na kuitoa mikono yake karibu nami.

"Mbona unakuwa hivyo?" akaniuliza.

"Ni sehemu ipi ya maneno 'nataka kulala' ambayo huelewi?" nikamuuliza pia.

"Kulala tutalala... me nataka unifinye hata kidogo tu JC..."

"Sitaki, hata kama ni kikubwa. Nataka kulala. Naomba uondoke."

"Kwa nini unanifanyia hivyo? Kwamba me siyo mzuri sana kama Ankia wako, au?"

"Eee... utajua mwenyewe. Nenda."

"Amekupa nini ambacho mi' siwezi kukupa?"

"Ah, aisee!" nikasema hivyo kwa kuchoshwa na hali hii.

Akanishika mapajani na kupiga magoti chini, huku akiniangalia kwa macho yaliyoonyesha hamu nzito, naye akasema, "JC, nipe tu hata kidogo. Nina ugwadu mwenzio..."

"Nenda kachukue koleo, uukokoe. Utatoka tu," nikamwambia hivyo.

Akacheka kidogo huku akinipapasa kwa viganja vyake mapajani. "Una mwili mzuri... huwa unaenda gym?" akauliza kwa madaha.

"Joy nielewe basi..."

"Usinifanyie hivi JC... nipe tu kama kunisaidia. Sitakuomba tena."

"Kulikuwa na wanaume wengi Masai, ulikosa wa kumwomba akusaidie?"

"Ningeenda kwao, lakini we' si ukaniita?"

"Mimi nilikuita?"

"Ndiiiyo... ukaniambia nikae... na mimi naitaka yako, siyo ya hao wengine..." akaongea kwa deko eti.

"Unaitaka nini?" nikamuuliza.

"Hii hapa..." akasema hivyo na kuishika sehemu yangu ya siri.

Alikuwa amesababisha nipandishe hisia bila kupenda, nami nikautoa mkono wake hapo na kumwambia kwa umakini, "Joy naomba utoke. Nitakuzibua sasa hivi."

Nilimwambia hivyo huku nimemnyooshea kiganja kuashiria kumpiga kofi, naye akasema, "Nipige tu... lakini mi' siondoki."

"Hivi we'... saa tisa sa'hivi Joy, nina usingizi, mbona huelewi? Haya, basi nenda... nitakupa siku nyingine. Sawa? Nenda."

"Sitaki JC, nipe sasa hivi. Hata kimoja tu..."

"Kimoja changu, au chako?" nikamuuliza hivyo.

"Chako," akajibu kwa matumaini.

Nikashindwa kujizuia kutabasamu, kwa kuwa hali hii yote ilikera kwa kufurahisha sana. Nikamwona anaivuta-vuta midomo yake kwa tabasamu la haya.

"Mbona unang'ang'aniza sana? Unataka kuniambukiza eti?" nikamuuliza.

"Sina magonjwa mbona..."

"Nitajuaje?"

"Basi vaa mpira..."

Ai kudadeki! Wanawake!

"Situmiagi mipira mimi," nikamwambia.

"Hata me napenda peku, ila si unaogopa magonjwa?"

"Kwani ni lazima? Si ukafanye na mtu mwingine?" nikamuuliza kwa njia yenye hasira.

"Me nakutaka wewe..." akasisitiza.

Akaishika boksa yangu usawa wa kibofu na kuifunua.

Nikafumba macho na kukaza meno kwa hasira, nami nikamwambia, "Joy nakuomba kwa mara ya mwisho utoke. Nikinyanyuka!"

"Nipige tu... lakini humu sitoki..."

"Eee?"

"Eee..."

Alionekana kuwa mkaidi zaidi sasa hivi, mpaka nikahisi kama vile pombe imeniisha kichwani shauri ya hisia hizi mpya kuamka ndani yangu, hasira na mhemko, na zote alikuwa amezilazimisha yeye. Akaifunua nguo yangu kwa lazima, akipendezwa na uimara niliokuwa nao. Sikutaka hata kumshika maana alikuwa amenikera kwa kadiri fulani, lakini nikamwacha tu afanye kilichomridhisha. Akawa ananiongelesha kwa njia ya kilevi, akiniambia ningefurahia sana penzi lake maana alijua kupagawisha mwanaume, nami nikawa namwangalia tu. Alijiamini sana. 

Joy akawa amepata alichokitaka kutoka kwangu hasa kutokana na pombe kusindikiza hisia alizozilazimu zipande juu yake, na kiukweli nilimpa dozi kama namwonea vile. Ilikuwa kukaa, kusimama, nikamkaba, naye akafika kule milimani kwa mara tatu kabisa katikati ya usiku huo mzito mno. Nikaona nimtulize, yeye akiwa anapumua kama hajiwezi, hivyo nikamgeuzia kitandani na kisha kumwachia. Akakidondokea na kulalia tumbo huku mimi nikianza kujisafisha.

"Haya, imetosha. Nenda sasa," nikamwambia hivyo.

"Hhh... si twende nyingine tena..." 

"Wewe, em' nyanyuka. Halafu fata dekio ufute haya maji hapa chini," nikamwambia hivyo na kuanza kuvaa.

"Dekio huwa analiacha njee," akaniambia hivyo kwa deko.

"Kafate nguo yako ufute. Sitaki panuke mikojo humu."

Akakaa na kusema, "Lakini wewe... acha masihara basi..."

"Masihara? Naonekana kama nakutania?"

"Mh... haya bwana. Me napafuta."

"Harakisha, nataka kulala."

Akacheka kidogo kwa mguno, kisha akanyanyuka na kuanza kuvaa sidiria yake. Nikalitoa shuka maana lilikuwa limelowana kiasi, nami nikalikunja-kunja na kulirusha pembeni chini, kisha nikaenda kabatini kuchukua lingine.

"Sijui una tenki la maji humo? Utanipa kazi kuyafua mashuka ya Ankia..."

Nikasema hivyo, naye sasa akawa amemaliza kuvaa.

"Unaonekana mjeuri, ila penzi lako la kibabe sana. Siyo mzembe. Ankia lazima anafaidi," akaniambia hivyo.

"Sana tu. Sema una king'ang'anizi mno, ungenikuta vizuri ungepata raha hata zaidi," nikamwambia hivyo huku natandika shuka lingine.

"Nikiamua kumwambia tumefanya, je?" akaniuliza hivyo.

"Ish! Mwambie tu, kwani shida iko wapi? Hiki ni chumba chako? Aliyenifata huku nani? Nimekwambia kafate kitu uje ufute hapa, usijisahaulishe," nikamwambia hivyo.

Joy akacheka kidogo na kupiga kofi laini kiganjani mwake, naye akatoka ndani humo hatimaye. 

Nikamaliza kutandika shuka, nikiwa nahisi uchovu na kichwa kuanza kuuma kwa mbali, naye akarudi pamoja na dekio lililolowanishwa na kuanza kupafuta hapo chini. Akamaliza kupafuta, naye akaniambia nimpe namba yangu ili tuje kutafutana tena, lakini nikamwambia atazichukua kwa Ankia akishamwambia tuliyoyafanya. Akaanza kuniambia alikuwa anatania tu, nisifikiri yeye ni mbea, lakini nikamwambia sijali kabisa. Kwa kuwa alikuwa ameshapata zaidi hata ya kile alichotaka, nikamwambia aondoke na kuniacha mimi nilale. Nikaenda kuzima taa kabla hata hajatoka, naye akanisogelea na dekio lake na kunibusu shavuni, lakini nikausukuma taratibu mwili wake kuelekea nje ya chumba huku yeye akicheka, kisha nikafunga mlango. Mambo yalikuwa mengi! Nikakikimbilia tu kitanda na kujitupia kama mzigo mzito wa kuni, nikianza kuutafuta kwa bidii usingizi mtamu niliokuwa nauhitaji.

 

★★★

 

Nimekuja kuamka muda ukiwa umeenda sana. Macho pamoja kichwa kwa pamoja viliuma kiasi, nikihisi uzito kama vile dunia ilikuwa inanivuta chini. Nafikiri shauri ya kupitisha muda pia bila kuwa nimekunywa kama jana. Nikajitoa kitandani na kuchukua simu nitazame muda, kukuta ni saa saba mchana. Nilihisi kichefuchefu kwa mbali, nami nikaamua kuvaa T-shirt na bukta ili cha kwanza kwenda kufanya iwe ni kunywa maji baridi sana kupunguza uzito wa hali hiyo. Nilipotoka chumbani, nilimkuta Ankia akiwa amekaa kwenye sofa akitazama TV. Akaangalia upande wangu mara moja, kisha akaendelea kutazama runinga bila kunionyesha hisia yoyote. Nikasogea mpaka hapo na kumwangalia usoni. Alionekana kuudhika. Mimi nisijue sababu kuu ni ipi, makisio yakawa kwamba huenda alijua kilichotokea baina yangu na Joy usiku uliopita, kwa hiyo alikuwa amekasirika. Pamoja na hilo, nikajivisha utakatifu na kumpa salamu.

"Mambo vipi Ankia?" 

Hakujibu. Akaendelea tu kuangalia tamthilia yake, nami nikaona nimsemeshe tu tena.

"Joy yuko wapi?" nikamuuliza.

"Sijui, labda nikuulize wewe," akajibu hivyo bila kuniangalia.

Ohohoo! Msumari kwenye kidonda! 

Nikatabasamu kidogo na kusema, "Kinachokufanya unune nini sasa?"

Akabaki kimya.

"Sikiliza Ankia. Ishu ya jana na Joy ilikuwa...."

"Usiniambie mimi. Ukiamua kuanza kuwaleta na kuwaingiza mahawala kwenye hicho chumba ni juu yako. We' si ni mtu mzima? Jiamulie unachotaka..." akaniambia hivyo.

"Iih! Ankia unanisemesha namna hiyo?" nikamuuliza kwa sauti ya upole.

"Kwani nimeongea vibaya? Au umesahau kwamba mimi ni mwenye nyumba wako?" akasema hivyo na kuniangalia kwa mkazo.

"Sijasahau hilo."

"Sasa? Unawaingiza tu wanawake humo na...."

"Wanawake gani Ankia? Unajua kilichotokea jana... ama niseme leo. Unajua kilichotokea kikweli au?"

"Kwa hiyo nini, unataka kukataa? Kwamba mi' kipofu, au sisikii? Najua ulichofanya na Joy ulipomleta hapa...."

"Mimi ndiyo nilimleta Joy hapa? Si alikuja na wewe? Kama hukutaka aje ungemzuia toka tumeondoka Masai, halafu kwanza...."

"Agh, usinisemeshe bana! Utajua mwenyewe," akasema hivyo kwa kuudhika.

Eeh? Nisimsemeshe? Sawa. 

Nikapita zangu na kwenda nje, moja kwa moja mpaka uani. Nikashusha mzigo kwanza huku nikiwa nimepokea kero kama kitu cha kwanza tu baada ya kutoka kuamka. Kwa mambo mengi, Ankia alikuwa sahihi. Hapo palikuwa kwake, na mimi kutambua hilo ndiyo moja ya mambo yaliyofanya nisitake kutoa penzi kwa Joy usiku huo. Lakini king'ang'anizi cha yule mwanamke machachari kikanifanya nimpe tu alichotaka ili aniondolee kelele, ukitegemea nilikuwa nimechangamshwa na pombe pia. Sasa sijui lilikuwa limemwambia nini Ankia kilichofanya anikasirikie hivyo, si unajua wanawake kwa chumvi? Usikute hata lilimwambia mimi ndiyo nililipeleka chumbani! Yote kwa yote, sasa ningetakiwa kushughulika na hii hali kwa namna ambavyo mwenye nyumba wangu alitaka tuisongeshe mbele. Si alitaka nisimsemeshe? Hilo lilikuwa jambo rahisi sana kwangu kufanya. 

Nikamaliza haja zangu na kujisafisha, kisha nikarudi ndani. Nilimpita mwanamke huyo kama simwoni vile. Nikaenda na kuchukua hela kidogo ili nifate maji baridi sana dukani, nami nikaenda tena pale nje kuyafata. Safari moja tu na kurudi chumbani tena, kisha nikatulia humo humo. Sikutaka kujishughulisha sana na simu baada ya kuangalia mambo machache tu ya humo kutokana na kuhisi njaa, hivyo nikaamua kwenda kuoga kwanza halafu nitoke kutafuta msosi; labda kule kule tulipochukua chips jana na huyu mama mnunaji. Sikuzote endapo kama mtu angenipa bega la baridi, mimi ningemrudishia mgongo wa baridi zaidi. Eti uninunie au kunichunia halafu labda nihangaiiike, sikuwa na kitu kama hicho. Ikiwa Ankia alifikiri kwamba ningejipeleka kwake na kuanza kumbembeleza kwa kuwa tu mwanzoni tulikuwa tumeanza kuchokozana kimapenzi, basi alikuwa amekosea mno. Nikatoka zangu na kwenda bafuni kuoga, wakati huu yeye akiwa jikoni kuandaa chakula nafikiri. Nijali nini? Nikaoga, nikaingia ndani, nikavaa vizuri na kujitengeneza vyema, kisha nikatoka tena bila kuaga mtu. 


★★


Mwendo wa taratibu tu mpaka Mzinga kwenye shughuli nyingi za wapambanaji ukanifikisha sehemu ile tuliyonunua chakula jana. Nikaagiza tu chips kavu na mishikaki minne, Pepsi baridi, nami nikaenda kukaa kwenye kiti cha wazi na kusubiri huduma yangu. Chakula na kinywaji kikaletwa, nami nikala mpaka kumaliza. Nikatoka na kuanza kurudi mdogo mdogo kuelekea nyumbani kwake Ankia. Sikuzote kujua kwamba ninaangaliwa mno kulinipa aina fulani ya ujasiri, au kujiamini, lakini inaonekana kwa wengi nilionekana kuwa mtu mwenye kujisikia sana. Kwa hiyo mimi kama mimi kuwaacha watu wawe na mtazamo wowote kunielekea ndiyo lililokuwa jambo sahihi la kufanya, kwa sababu ni mimi tu ndiye niliyejijua kihalisi jinsi nilivyo. 

Hapa siongelei tu kutazamwa na watu kutokana na sura yangu, bali kuhukumiwa kwa tabia zangu na watu wanaofikiri wanajua sana kuhukumu. Inaeleweka namwongelea Ankia. Alionekana kuwa mwanamke mwenye kushikilia sana mambo, yaani hata ukimuudhi kwa jambo dogo, anaumia kiasi kwamba hawezi kuliachilia kiurahisi. Mtu kama huyo sikuzote inatakiwa kumwacha tu achukulie mambo jinsi anavyoona kuwa sahihi, kwa sababu huwezi kamwe kubadili mawazo ya binadamu kwa kulazimisha waone mambo jinsi wewe unavyoyaona. Hivyo hata kwa ishu hii iliyokuwa imezuka sasa, ningetakiwa kutulia tu. Nimpe anachotaka, maisha yaendelee. Namaanisha kutomsemesha.

Nikafika hapo nyumbani na kumkuta Tesha akiwa amefika. Nikaingiwa na furaha, hasa kwa sababu jamaa alinyanyuka na kunipa salamu iliyojaa uchangamfu, na bado midomo yake ilitoa harufu ya mbali ya pombe. Ankia alikuwa amekaa kwenye sofa lile dogo, nami nikaketi pamoja na rafiki yangu mpya kwenye sofa moja.

"Dah, kaka nimelala kichizi leo! Yan' sasa hivi tu ndiyo nimetoka kuoga, nimelala mpaka nikaamka kupumzika!" Tesha akaniambia hivyo.

"Ahahaha... me mwenyewe nimelala masaa yameenda kwa hiyo nikachelewa kuamka. Kweli ndiyo mida hii umeamka?" nikamuuliza.

"Sasa hivi tu yaani. Ila... kwenye asubuhi nilishtuka, nikakojoa, nikarudi tena kulala. Nimelala kaka!" akaniambia tena.

"Si joto la jana..." nikasema.

"Ah, usipime! Vibe lilinipanda kweli jana, sikutukana mbele ya sister kweli?" Tesha akaniuliza.

"Haukuwa umelewa kihivyo bwana, unazingua," nikamwambia hivyo.

Akacheka kidogo na kumwangalia Ankia. Mwanamke huyo alikuwa amekaa kwa utulivu tu sofani, miguu yake iliyopandishwa juu kwa pamoja ikiwa imefunikwa kwa khanga. Juu alivalia jezi nyeusi ya Yanga, huku akiwa kimya tu akitazama TV kwa umakini.

"Mwone huyo alivyotulia... hangover kali la asubuhi halijamtoka eti," Tesha akasema.

Nikatabasamu kidogo tu. Sikumwangalia Ankia hata kidogo, lakini macho si yana upana wake bwana? Nikaweza kuona kwamba alitutazama baada ya Tesha kusema hivyo.

"Ananiambia eti kichwa kinauma. Mama na bado! Leo tena tunaenda kuzimua," Tesha akasema hivyo akimwambia Ankia.

Ankia akacheka kwa pumzi, ile cheko ya mara moja huku ameikunja midomo kwa njia wafanyayo wanawake.

"Ulikuwa mbali mwanangu?" Tesha akaniuliza.

"Hamna, nilienda tu hapo Mzinga," nikamjibu.

"Ndo' umetokelezea hivi?" akaniuliza.

"Kawaida tu. Nilienda kupiga msosi," nikamwambia hivyo Tesha.

"Aaaa... Ankita, hujapika mamaa? Mbona unamtesa mwarabu wetu?" Tesha akamuuliza hivyo Ankia.

"Chakula kipo mbona? Hajataka tu kula," Ankia akasema hivyo huku ameangalia TV.

Tesha akanitazama usoni, nami nikamwangalia kwa ufupi, kisha nikatoa simu yangu mfukoni kuangalia ujumbe ulioingia. Nafikiri kijana huyo aliweza kusoma mchezo haraka kwamba hali baina yangu na Ankia haikuwa nzuri, kwa hiyo akaamua kuanzisha mada nyingine.

"Oy, kwa hiyo na leo tutaingia Masai, au siyo?" akaniuliza.

"Kuna ishu gani? Tusije tukatoka usiku mno tena, dada yako anaweza ku...."

"Sister siyo mzinguaji JC. Yuko peace sana. Hata yeye huwa tunaenda naye akiwa free. Muulize hata Ankia," Tesha akaniambia hivyo.

Nikamtazama Ankia machoni kwa ufupi, nami nikakuta ananiangalia pia. Nikakatisha utizami huo taratibu na kusema, "Fresh tu kaka, tutaenda."

"Ee... af' leo kuna game ya Simba saa moja, tutaicheki. Nataka tuingie VIP kule," Tesha akaniambia.

"Aaa sawa," nikasema hivyo.

"Unashabikia timu gani?" akaniuliza.

"Simba," nikamjibu.

"Aina hiyo kaka. Umeona chibonge? Wanaume halisi wako Simba! Unajiweka kwa hao vyura wa kijani kufanya nini?" Tesha akamwambia Ankia.

"E-eeh... niache. Yanga ndiyo timu yangu tokea wakati ambao haukujua kutamka neno 'Simba,'" Ankia akamwambia hivyo.

Tesha akacheka na kusema, "Unalo bibie!"

Ankia akasonya kidogo.

"Twende VIP wewee... acha unyonge," Tesha akamwambia.

"Akha! VIP yenyewe imekaa kama sebule yangu. Nendeni tu," Ankia akasema hivyo na maudhiko yake.

"Kwa hiyo tunatulia mpaka saa moja?" nikamuuliza jamaa ili kukwepa kisirani cha mwanamke huyo.

"Ee, ila, nilikuwa nimekuja kuangalia kama hauna mambo mengi sana, tutoke tukazurure Mbagala hapo," Tesha akaniambia.

"Hauna kazi za kufanya?" Ankia akamuuliza.

"Naongea na wewe kwani? Huyu amekuwaje?" Tesha akasema hivyo.

"Fresh tu kaka, twende hata sa'hivi," nikamwambia hivyo.

"Poa," akaitikia.

Sikutaka kujizungusha na mengi. Nikanyanyuka na kuelekea nje bila kujishughulisha na Ankia. Tukatoka baada ya jamaa kuvaa viatu vyake. Alikuwa amevalia T-shirt jeupe na pana, suruali-modo nyeusi, pamoja na kofia ya kumkinga na jua. Mimi nilikuwa nimetupia tu T-shirt jeusi la mikono mifupi pamoja na jeans, na miguuni masai zangu safi.

Tukiwa tunatembea taratibu tu kwa mitindo ya kujiamini, Tesha akaniambia, "Mwanangu inabidi uwe unavaa cap. Jua kali kinoma, litakubabua uwe mweusi."

"Unasema kweli. Halafu linaniumiza macho. Nataka nichukue kama hiyo yako tukifika Mbagala. Angalau kuzurura kama hivi kutanizoesha maeneo shuta," nikamwambia.

"Asilimia mia. Pamekaa nyuma kidogo siyo kama mitaa mikali mikali kama kule kwenu Sinza ama Kigamboni, ila pana janja zake. Wakati nimefika sikufikiri kuna chimbo hata moja, ila yapo!" akasema hivyo.

Nikatabasamu na kumuuliza, "Na we' unaendaga kwenye hayo machimbo?"

"Ah, ya huku hamna, wanawake wa kizee tu, ni mabaka! Ubungo, Sinza, ndiyo kuna pisi kalee!"

Nikacheka sana na kutikisa kichwa.

Akacheka kidogo na kusema, "Au nadanganya? We' mwenyewe najua ushapita sana huko."

"Hapana, sipitagi."

"Ah wewee! Unazingua..."

"Ih, unafikiri? Siendagi huko mimi. Kama kuja huwa wanakuja wenyewe tu, me mpaka kumfata hivi mwanamke Tesha... ujue nimemwelewa sana. Haya mambo ya gusa mara moja na kupokezana naonaga hayana faida. Sema me kwangu yakija kama yamenikuta vibaya, ndo' unakuta napiga. Ila sishobokei kivile kaka..."

"Au siyo?"

"Ndiyo hivyo."

"Dah, haya bana. Ndo' maana kumbe hata na jimama Ankia humtaki?" akaniuliza.

Nikacheka kidogo tu.

"Halafu mbona kama amevimba sana leo? Mmetibuana wapi?" akauliza.

"Ah... si ndo' mambo kama hayo?" nikamwambia.

"Imekuwaje?"

"Amenikasirikia kisa jana."

"Nini?"

"Nilimpiga Joy," nikamwambia.

Tesha akasimama na kunishika mkononi, naye akasema kwa sauti ya juu, "Weweee! Acha basi mwanangu, unasema kweli?"

"Kweli."

"Muda gani?"

"Muda ule nimekuacha kwenu, nilipofika ndani Joy akakitaka..."

"Kwo' ukamwingiza chumbani?" akauliza huku tukianza kutembea tena.

"Alikuja mwenyewe, kang'ang'ania kweli. Ikabidi nimpige tu aridhike, aondoke. Sasa ndiyo Ankia kanikasirikia, hataki nimsemeshe," nikamwambia hivyo.

Tesha akacheka kidogo na kusema, "Ah! We' noma! Ushakula hadi na Joy usiku wa kwanza mmekutana? Utamaliza wake wengi za watu sisi tunakuangalia tu."

"Kwani Joy ameolewa?"

"Hamna, ila yule mwanamke huwa anatoka na wanaume wenye pesa sana. Yaani hata pale Masai, nasikia huwa anapigwa miti na mwenye Masai, halafu huyo jamaa ana kahoteli kengine kakubwa huko Buza. Hapo hivi Joy huwa anawaleta mademu wakali wanaouza, si unaelewa? Yuko kama Kingpin wa kike yaani, halafu hizi ishu hakuna wengi wanaojua..."

"We' umejuaje?"

"Kuna jamaa hapo ndiyo meneja Masai anaitwa Bobo, sema jana hakuwepo, ni mshkaji wangu pia nitakuonyesha. Ndiyo huwa ananiambia vitu. Wale wana ishu nyingi sana halafu Joy anapitisha mambo mengi kona na kona, biashara zinaendelea. Si unajua mjini? Macho mengi yako kwa huyo demu maana anajiwekaga fresh sana. Halafu nasikia analindwa, kuwa mwangalifu asije akakutafutia balaa mapema," Tesha akaniambia.

"Mbona anaonekana wa kawaida sana?"

"Kwani mwanangu jambazi atakwambia yeye ni jambazi? Si mpaka aje agongwe risasi ndiyo unabaki kinywa wazi?" 

Nikacheka kidogo tu.

"Kwa hiyo mtoto akaililia?" akaniuliza.

"Ah, we' acha tu. Nilikuwa namwambia toka, hasikii. Akanikera mpaka nikampiga vya kukomesha!" nikasema hivyo.

Tesha akacheka na kusema, "Anaonekanaga mtamu kweli. Me mwenyewe nawakubali sana hawa wanawake, sema Masai hapo fitina nyingi, ndiyo maana naendaga zangu Ubungoo. Kwa hiyo Ankia akamaindi sana ulivyompiga Joy?"

"Sana. Na unajua ni kweli, kufanyia hivyo kwake siyo fresh. Si pombe tu jana na king'ang'anizi cha Joy? Ila sema Ankia ameniudhi, hataki kunisikiliza. Anasema nimeshaanza kuingiza mahawala..."

Tulikuwa tunaikaribia lami sasa, naye Tesha akanishika begani huku bado tukiwa tunatembea taratibu.

"Kinachomuuma ni kwamba umefanya mapenzi na mwanamke nyumbani kwake, au kwa sababu tu umefanya mapenzi na mwanamke mwingine bali si yeye?" akaniuliza hivyo.

"Inaonekana ni vyote... sijui sana," nikamwambia.

"Ahah... ngoja kwanza..."

Alisema maneno hayo na kunisimamisha kabisa ili nimsikie kwa umakini, nami kweli nikaweka umakini wangu kwake hata zaidi. 

"Nafikiri Ankia amekupenda. Tena siyo ile kupenda kama ya mwanamke wa aina ya Joy ya kutaka penzi tu kumridhisha, ila ile kupenda ya moyoni. Sasa kwa Ankia hiyo ni shida kwa sa'abu... huyo mwanamke amepitia magumu na mume wake. Unafahamu alikuwa ameolewa?"

"Ndiyo."

"Ee... alikuwa anakaa hapo na mumewe na mtoto wake wa kike, miaka kama sita hivi. Ila huyo mtoto akawa amekufa. Aliumwa sana. Ankia ye' hana wazazi, ndugu zake wengine sijui wako wapi huko, na hiyo nyumba aliachiwa na baba yake aliyekufa siyo muda mrefu sana baada ya Ankia kuolewa... ndiyo walikuwa wanaishi na familia yake hapo..."

Nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa.

"Asa' ile mtoto wake kufa vile, badala ya mume wake na ndugu zao kumfariji, wakawa wanamrushia lawama kwamba... hajui kutunza, hawezi malezi, kama vile kusema...."

"Yeye ndiyo alimuua."

"Eeeh kaka, imagine! Mume wake sijui walikuwa wa kabila gani huko, wajinga-wajinga tu, watu wake wakamshawishi aachane naye, halafu Ankia alikuwa anampenda kweli huyo jamaa. Biashara za baba'ake alimwachia msela aongoze, jamaa akawa anamletea dharau tu. Alipoamua kumwacha kabisa... Ankia alivurugika wewe! Sisi tumekaa naye hapo... alikuwa wa kulia tu, da' Miryam alijitoaga kweli kumsaidia mpaka akajikakamua tena. Angalau siku hizi kama unavyomwona, anajitahidi kuchangamka. Lakini hayo ndiyo mambo yaliyomfanya asitake mwanaume tena... kama mwaka sasa hivi sijamwona na mtu kabisa... amekuwa wa nyumbani tu."

Nikaangalia chini kiasi na kusema, "Hiyo siyo poa."

"Ee. Hakuwa hata na ile... nguvu ya kutaka kuendelea na kazi, agh akaamua tu kuuza-uza vitu vyao vingi na kurudisha biashara za baba'ake... ila sijui mengi sana kuhusu hayo. Umeona? Kwa hiyo... ni mtu ambaye tunamwelewa sana. Nadhani hata hii ya kupangisha mtu hapo kwake ilikuwa njia ya kujiingizia kapesa ili asogee-sogee kimaisha zaidi... na sasa wewe kuja ndiyo naona kumemchangamsha. Kuna kammama kamoja kanaitwa mama Chande kalikuwa kananiambia... kabla sijakufahamu... kwamba Ankia alikuwa anakutendea kama vile umemwoa tayari maana alifurahia mno kuwa na wewe hapo..."

"Dah, halafu huyo mama mbea..."

"Wee! Kumbe unamfahamu? Hata hujamuuliza kitu, tayari kashasambaza ubuyu! Masai kote wanamjua," Tesha akasema hivyo.

"Aisee! Kwa hiyo unasema kwamba Ankia kujua nimetoka na Joy kunaziumiza sana hisia zake za moyoni?"

"Ndiyo hivyo kaka. Anaweza akaanza kuwa kama kipindi kile."

"Lakini Tesha me nimekuja juzi tu. Hajui natoka wapi, nimeishi vipi... sawa, ni normal sana haya mambo ya kuvutiana na nini lakini mimi sijaja huku kwa misingi ya kuwa kitulizo cha moyo wake. Je kama nina mpenzi wangu mwingine? Ama labda kama ningekuwa nimeoa? Hatakiwi kuweka matarajio ya namna hiyo kwangu mimi kwa sababu bado hajanijua vizuri... haya mambo ya kufurahishana... yanabaki kuwa ya kufurahishana tu... ila kama ni kwenda kule anakotaka twende, sidhani kama nitaweza," nikamwambia ukweli.

Akanishika begani na kusema, "Ndiyo maana nimekwambia haya, ili uje kuongea naye. We' ni mwanaume, mwambie tu unamwelewa, na kama atataka mwende mpaka sehemu fulani, basi mweke wazi kabisa kwamba utaishia mahala fulani... ili asije kukuzoea mno ikawa shida. We' mwenyewe utajua cha kufanya mwanangu. Niliposema hatakagi kuguswa shauri ya kuogopa ngoma nilikuwa natania tu... hivyo ndiyo hali ilivyo kwake..." Tesha akanipa ushauri huo.

Nikatikisa kichwa kidogo kwa njia ya kusikitika kiasi, naye akaniambia tuvuke sasa barabara ili tukapande daladala za kuelekea Rangi Tatu. 

Sikufikiri Tesha angeyageuza mazungumzo hayo kuwa yenye kugusa namna hiyo, lakini ni kweli, yalinigusa sana. Tena hadi nikawa nimeingiwa na kale kahisia ka hatia kutokana na matendo yangu ya kuanza kumwonyesha uvutio wa kimapenzi mwanamke yule bila kuelewa vizuri zaidi hisia zake kwa ujumla. Ni kitu cha kawaida sana kwetu sisi wanaume kufanya, na Tesha kunielezea kisa cha maisha ya Ankia kukaanza kunipa mwanga kuona kwamba jambo hilo halikufaa. Hivyo, kutokea hapa ningetakiwa kushughulika na mwanamke huyo kwa njia ambayo isingemwachia maumivu niliyofikiri yangekuwa ya kawaida kwa sababu ya kuchuniana tu. Ningetakiwa kuzungumza na Ankia, anielewe, nimwelewe... tuelewane.

 

★★★★★★★★★★

 ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

Previoua Next