Ni5 muda wa saa moja za jioni ndani ya soko la Mbagala Rangi tatu pilika pilika zilionekana kuwa nyingi sana kwa wafanya biashara , kwani muda huu kwa wafanya biashara wengi ndani ya soko hili ndio muda ambao walikuwa wakifunga biashara zao na kurudi majumbani , hususani wale waliokuwa wakifanya biashara za nguo na vyakula.
Kikawaida ndani ya hili soko wafanyabiashara wengi walikuwa wakihifadhi mizigo yao sehemu salama kwa wale ambao walikuwa na mizigo mikubwa ambayo hawakuwa na uwezo wa kurudi nayo nyumbani , ambao pia hawakuwa na maduka maalumu ya kufanyia biashara , hivyo mara nyingi hulazimika kuhamisha mizigo yao kutoka eneo wanalo fanyia biashara mpaka sehemu ya kuhifadhia.
Kazi hii ya uhamishaji wa mizigo ni kubwa kwa wafanyabiashara hivyo huomba msaada kwa waendesha mikokoteni na wabeba mizigo kuwasaidia kuhamisha huku wakiwalipa kwa kiasi cha mizigo wanayobeba.
“Roma njoo leo unisaidie kubeba mizigo yangu basi nikahifadhi muda umeenda sana” aliongea mwanamama mmoja hivi mweupe wa wastani mnene aliekuwa akifanya biashara ya kuuza madela , vijoli pamoja na viatu vya kike ndani ya soko hili la Rangi tatu.
“Mama Nasra wala hata usiwaze , nitakuhamishia haraka haraka maana nina kazi pia ya kuhamisha na mzee Saidi”.
“Haya mwanangu nashukuru sana”Aliongea mwananamama huyu huku akimuonesha Roma mizigo ya kuingiza kwenye mkokoteni wake kwa ajili ya kwenda kuhifadhi sehemu husika.
Ndani ya dakiika kadhaa tu Roma alikuwa ameshamaliza kazi ya kuhamisha mizigo yote ya kibiashara ya Mama Nasra na kulipwa buku lake na sasa alikuwa bize na kuhamisha mizigo ya Mzee Saidi , ambaye alikuwa ni muuza Viatu vya mtumba.
Uchapakazi na uaminifu wa Roma ulikuwa ukiwafurahisha sana wafanya biashara wengi sana wa soko hili kiasi cha kupelekea mara nyingi kumtaka Roma awasaidie kila linapokuja swala la kubeba mizigo kuitoa sehemu moja kwenda nyingine , alikuwa akifanya kazi kwa haraka sana , kiasi ambacho hata wenzake abao aliokuwa akifanya nao kazi hio hio walikuwa wakimshangaa kwa uwezo na nguvu alizokuwa nazo Roma .
“Kijana Asante sana kwa kuhamisha kwa haraka haraka maana nina dharula”
“Usijali mzee wangu” Aliongea Roma kwa kuweka tabasamu usoni mwake na kisha alipokea noti yake ya shilingi elfu mbili na kisha kuingiza mfukoni.
Mpaka kufikia muda wa saa nne za usiku Roma alikuwa amesomba bidhaa nyingi za wafanya biashara na kwenda kuzihifadhi na sasa alikuwa amekaa kwenye moja ya meza tupu iliokuwa haina kitu akihesabu hela zake.
“Hatimae nimeingiza Elfu kumi na tano , ni kiasi kikubwa sana hiki kwa leo , ngoja nikale ugali na nyama ya Mbuzi kwa mama Joshua nisepe home nikalale”Alijiongelesha Roma huku akinyanyuka mahali alipkuwa ameketi na kusogelea mkokoteni wake na kuuweka pembeni sehemu ambayo mara nyingi anauhifadhi yeye pamoja na wenzake mpaka siku inayofuata .
“Oy mwanaa , leo umepiga kazi sio poa”.
“Kawaida tu Juma , japo ni kweli siku ya leo haikuwa kama jana”Aliongea Roma akiongozana na rafiki yake Juma wakielekea uelekeo mmoja . Juma ni rafiki yake Roma wa muda na walikuwa wakifanya kazi pamoja , utofauti wa Juma na Roma ni kwamba Juma yeye alikuwa ni mwenyeji wa jiji hili la Dar es salaam , akiwa amezaliwa ndani ya jiji hili na Roma alikuwa na muda wa miezi sita tu tokea aingie ndani ya jiji hili la Dar es salaam kutokea mikoani na alikuja ndani ya jiji la Dar kama moja ya vijana wengi wanaokuja kwa kisingizio cha kutafuta maisha.
Roma alikuwa ni mrefu wa wastani , mwenye mwili uliokuwa umejengeka vyema kimazoezi , hakuwa handsome sana wala hakuwa mwenye sura mbaya , alikuwa ni wale wanaume ambao walikuwa wakionekana kawaida sana katika macho ya wengi na moja ya sababu kubwa iliompa Roma umaarufu ni kutokana na uchapaji kazi wake ndani ya soko hili la Rangi tatu.
Baada ya marafiki hawa kuvuka upande wa pili wa barabara hatimae walikuwa ndani ya mgahawa wa Mama Joshua kwa ajili ya kupata chakula cha usiku , waliungana na wenzao wengi waliokuwa ndani ya eneo hilo na kuagiza chakula huku wakiendelea kupiga stori za hapa na pale ili mradi kunogesha maongezi yao.
“Oya Wadau leo Club B kuna bonge la Party , leo ni full bia nusu bei”Aliongea jamaa mmoja mbeba mizigo aliekuwa maarufu sana ndani ye eneo hili la Rangi tatu aliekuwa akifahamika kwa jina la Yusuph.
“Tukitoka hapa lazima tukatembelee eneo hilo, ila hio parti inahusu nini?” aliuliza jamaaa mmoja mwembamba hivi.
“Mrembo Rose leo ni siku yake ya kuzaliwa na kuna bosi anaetoka nae hapa town ndio kaamua kumfanyia bonge la sherehe”.
“Kama ni hivyo hapo ni sawa kwa sisi kwenda kutembelea , au unaonaje Roma “ aliongea Juma akionekana ni mwenye kufurahia tukio hilo linalokwenda kutokea kwani alikuwa ni mwenye kupenda sana kunywa bia hasa zile za ofa.
“Nyie mtatangulia mimi nitarudi Getto kwanza nikaoge then nitaungana na ninyi”
“Ahaaa.. mzee unazingua , hapa hata sisi tutaenda kuoga kwanza ndio turudi kwenye Parti”aliongea Juma na kuwafanya wengine wote wamsapoti.
Naam ni muda wa lisaa limoja tu Juma akiwa ameongozana na Roma walikuwa mbele ya nyumba iliokuwa na geti jekundu Mbagala Biasi pembezoni kabisa na kilipokuwepo kituo cha Tanesko , taa kubwa za kituo hiki ziliwamulika na kufanya waonekane vyema kwa wapiti njia , kwani licha ya kwamba muda ulikuwa umeenda sana , lakini bado pilikapilika za watu wa eneo hili zilikuwa zikiendelea.
Baada ya kusimama kwa madakika kadhaa hatimae mlango mdogo wa geti hilo ulifunguliwa na mwanadada mmoja mrembo aliekuwa amevalia shungi na kuwakaribisha ndani.
“Najma vipi , ulikuwa umelala mbona umechelewa kfungua mlango?”.
“Hapana nilikuwa chumbani na hata sikusikia” aliongea mwanadada huyu kwa sauti yake iliokuwa ikisikika vyama na kisha alimwangalia Roma na kumsalimia.
“Roma mambo”
“Poa Naj , habari za siku nzima”.
“Safi tu”
“Oya Roma kajiandae chap tuondoke muda unakwenda wenzetu watatangulia kufika” aliongea Juma ilimradi tu akatishe maongezi yaliokuwa yakiendelea kati ya Roma na Najma .
Najma alikuwa ni mdogo wake Juma , alikuwa akiishi ndani ya nyumba hio ambayo ilikuwa ni yakwao walioachiwa ya urithi , ilikuwa ni nyumba kubwa tu ambayo ilikuwa wameigawa nusu wapangaji na nusu walikuwa wakiishi yeye pamoja na kaka yake.
Najma alikuwa akifundisha shule ya chekechea eneo moja lililokuwa likifahamika kwa jina la Kiramba, licha ya kwamba alikuwa akilipwa ujira mdogo , lakini alikuwa pia akionekana kuipenda kazi yake hio ya ufundishaji.
Tokea siku ambayo Roma anafika ndani ya nyumba yao na kupanga , Najma alitokea kumpenda Roma, Najma alikuwa si mwenye furaha asipomuona Roma , na kutokana na shughuli za kaka yake na Roma kuwa ni za kuwaruhusu kurudi usiku na kudamka asubuhi asubuhi , hivyo mara nyingi alikosa muda wa kuonana na Roma , hali ambayo ilimfanya kuhakikisha kila siku yeye ndio anaewafungulia mlango kila wanaporudi kutoka kazini.
Licha ya Najma kumpenda Roma kwa kaka yake ilikuwa ni tofauti , hakupenda kabisa Najma kujihusisha kimapenzi na Roma kabisa na hii yote ilisababishwa na hali ya kimaisha aliokuwa nayo Roma ,Juma alimuona Roma kama mtu ambaye hakuwa na malengo na maisha yake , hivyo aliona kitendo cha dada yake kuingia katika mapenzi na Roma dada yake asingefika mbali kimaisha na angeendelea kuishi katika hali ya maisha duni jambo ambalo hakuwa akitaka litokee kwani aliamini kwa uzuri aliokuwa nao dada yake , kama ni kupata mwanume mwenye pesa na kumuoa lisingekuwa jambo gumu , lakini asiliolijua Juma ni kwamba ni wanaume wengi sana walikuwa wakikataliwa na Najma licha ya kutaka kumhonga pesa nyingi na hata kumuahidi kumuoa ,mlimbwende huyu alikuwa amekufa na kuoza kwa mwanaume ambaye hakuwa na chochote cha kutishia jamii , mwanaume wa kawaida sana na maskinini mpangaji wao anaenda kwa jina la Roma.
Katika akili ya mwanadada huyu mrembo Najma aliamini siku moja Roma atamtamkia tu kuwa anampenda na yeye pia atamkubali na watayaanza maisha yao pamoja , hio ndio Imani aliokuwa nayo Najma juu ya Roma.
Kwa upande wa Roma alikuwa akijua fika kuwa Najma alikuwa akimpenda sana kimapenzi , lakini pia alikuwa akijua sana kwamba Juma hakuwa akitaka dada yake kutoka na yeye kimapanzi kutokana na hali yake ya kimaisha , hivyo licha ya yeye kumuona Najma kama mwanamke mrembo ambayey yeye kama mwanaume rijali anapaswa kuwa naye katika mahusiano , lakini alijitahidi sana kujizuia kumuonyeshea mapenzi mwanadada huyo , kwani hakuwa ni mtu mwenye kutaka ugomzi na rafiki yake Juma , kifupi alikuwa amependa sana chumba alichopanga ndani ya nyumba hii ya Roma na dada yake.
Basi baada ya Roma na Juma kujiandaa na kubadilisha nguo hatimae walitoka kwa kupitia geti dogo na kisha kutoka ndani ya nyumba hio na kuelekea uelekeo wa Club B , kutoka Bias mpaka ilipokuwa ikipatikana Club B hapakuwa mbali sana , Club hii ilikuwa ikipatikana Chalambe nyuma kidogo kabla haujafika sehemu iliokuwa ikifahamika kama Maji Matitu , ilikuwa ni moja ya Club kubwa sana na ya kuvutia iliokuwa ikipatikana ndani ya eneo hili , lakini pia ilikuwa maarufu sana kiasi kwamba ilikuwa ikitembelewa na watu waliokuwa wakiishi ndani ya mji huu pamoa ambao waliokuwa wakiishi nje ya eneo hili , ikiwemo Chamazi , Temeke , Kisemvule na baadhi ya meneo ya karibu.
“Wadau mmechelewa sana tena Sanaa yaaniii ….. bia ya tatu hii”Aliongea Yusph huku akigida bia yake kwa mbwembwe iliokuwa na chapa la Safari Lager .
“Usijali Yusuph tutakufikia tu “Aliongea Juma huku akiangaza macho huku na kule akikagua mandhari ya hapa ndani na hata kwa upande wa Roma hivyo hivyo.
“Siku hii ya leo watu walionekana kuwa wengi , kwani makelele yalikuwa mengi , huku harufu ya Pombe ikiwa imetapakaa kwa hali ya juu ndani ya eneo hili.
“Handsome Boys karibuni niwahudumie”Ilikuwa ni sauti moja nyororo iliosikika kwa vijana hawa na kuwafanya wamuangalie aliekuwa akiongea na hapo kila mmoa alitoa macho ya uchu baada ya kumuona mwanamke wa haja. Mrembo alievalia suruali ya kitambaa iliomchora vyema umbo lake namba nane , mwanamke huyu alikuwa ni mzuri kweli , si kujaliwa tu shepu lakini pia alikuwa amejaliwa sura nzuri yenye urembo wa asili ambao huwafanya wapenda ngono wengi kummezea mate.
“Aaaaa..hhh Sister Rose sjijatarajia kukuona leo ukihudumia bhana”Aliongea Juma kwa mshangao na kumfanya Rose kutabasamu huku macho yake yote akiwa ameyaelekeza kwa Roma ambaye alionekana kama mtu ambaye hakuwa na habari na mtu aliekuwa mbele yake kwani alikuwa ni mwenye kukagua kila mtu aliekuwepo ndani ye neo hilo kama jasusi anaetafuta adui.
“Mimi nipe Safari kama Broo wangu yusuph hapo , nipe ya baridiii”Aliongea Juma huku akikaa vizuri kwenye viti hivyo virefu huku akiwa amechia tabasamu pana usoni mwake.
“Na wewe Roma vipi leo” Aliongea huku akimwangalia Roma kwa madaha kiasi kwamba wenzake wote walikuwa wakimuonea wivu kwa kuangalia na mwanamke mrembo kama Rose kwa staili hio.
“Nataka ofa leo , nipe Heinken gharama ni juu yako”Aliongea Roma pasipo kupepesa macho na kumfanya Rose atabasamu na kisha kumwambia asijali anamletea na atalipia kwa kila kinywajia atakachokunywa kwa siko hio , jamboa mbalo liliwafanya marafiki zake waone ni upendeleo , lakini wala Rose hakuwajali.
“Oya mwanangu Roma huyu Manzi anakukubali sana kitambo tu , nashangaa mzee huchangamki , au unaogopa ni vya wakubwa”Aliongea jamaa mmoja aliekuwa pembenni ya yuspuh ,jamaa huyu alikuwa akifahamika kwa jina la Samia.
“Kweli kabisa Samia , Manzi anamkubali sana Mwamba hapa , lakini jamaa anazembea zembea , ningekuwa mimi ningekuwa nisharekebisha tayari na hapa ningekuwa nakunywa bia fulu fulu bureeee”Aliongeezea Yusuph na muda huo huo alikuja Rose na kuweka vinywaji huku akimpatia kinywaji Roma.
“ Bebi kuna ,mbuzi choma nikuleteee” wote waliangaliana kwa macho ya kimshangao na ya kutamani kile kilichosemwa , lakini hawakuambiwa wao , mtu aliekuwa amepewa ofa hio alikuwa ni Roma.
“Kweli mama leo umezaliwa upya , kama ni ofa mimi sina tatizo na nipo tayari kwa kila ofa inayopatikana”Alionea Roma .
“Ofa nyingine hautaweza , siku zote umekuwa ni wa kunikimbia” aliongea Rose kwa kumnong`oneza Roma na kumfanya atabasamu , kwani alikuwa akijua alichokuwa akimaanisha Mrembo huyu.
Huu usiku kama walivyotegemea vijana hawa ndio kile walichopata , kwani walilewa chakalii kwa bia za ofa ambazo zilikuwa zimetolewa na kibosile ambaye ilikuwa ikiaminika alikuwa akitoka kimapenzi na mwanadada Rose.
Baada ya masaa matatu baada ya ya keki kukatwa na sherehe kukaribia kumalizika , huku waliokuwa wakiendelea kula mziki na kunywa bia wakiendelea , alikuja jamaa mmoja aliekuwa mhudumu wa hii Club na kumpa kijimemo Roma, ambaye licha ya kunywa bia nyingi alionekana kuwa ngangari kuliko wenzake wote , baada ya kufungua kimemo hiki , alitabasamu na kisha alinyanyuka na kuoelekea nje , na kukata kushoto na ndani ya dakika chache alikuwa nje ya chumba na kugonga , na mlango ulifunguliwa na mrembo Rose aliekuwa amevaa khanga moja tu, alionekana alikuwa ametoka kuoga.
“Karibu Mpenzi”Aliongea Rose kwa namna ya kudeka huku akimvuta Roma ndani na kuzama mzima mzima .
Comments