Siku;tatu zilikuwa zimepita pasipo ya Roma kuonana na Najma , jambo ambalo halikumshangaza kwani alikuwa akikumbuka vyema kuwa Najma alimuona mwanamke kahaba alielala nae siku mbili zilizopita , hivyo alijua fika kuwa mrembo huyo atakuwa na hasira kali sana juu yake , kwani alikuwa akijua sana kwamba alikuwa akimpenda , hivyo hata yeye hakutaka kujishugulisha sana juu ya Najma , kwanza aliona ni jambo zuri kwani angejiweka mbali na Najma.
Upande wa Juma pia jambo hilo lilimfurahisha sana , kwani aliamini kwa jambo ambalo Roma amefanya litamfanya dada yake kutomfikiria kabisa Roma na kuendelea na maisha yake huku akimtafutia mpango wa kueoelwa na mwanamke mwenye pesa zake na ili kuhakikisha Najma hafikiriii kabisa kuendelea kumpenda Roma alifanya kila njia kuhakikisha taarifa za Roma kulala na kahaba mpaka asubuhi zinasambaa ndani ya wapangaji pamoja na majirani.
“Mh! Roma kabisa … siku zote nilikuwa namuona kama anamatatizo flani hivi kumbe anaonekana na yeye anapenda wanawake . lakini alishindwa nini kumchuku Najma mwanamke mrembo mpaka kwenda kuchukua mwanamke kahaba mtaani”
“Heheee… huenda Najma kuna kitu anakosa katika mwili wake ambacho hakimvutii Roma” Hao walikuwa ni wapangaji waliokuwa wakiongea kishambenga wakiwa wanasukana , na yote hio ilikuwa ni kumuumiza Najma ambae alikuwa akiingia kutoka kazini , na Najma aliwasikia vizuri tu na kuzidi kumchukia Roma kwa kitendo cha kuleta kahaba kwenye nyumba yao.
Najma alionekana ni mwenye mawazo , mengi mno , lakini licha ya hayo yote ambayo yalikuwa yakiendlea kwa wapangaji , moyo wake ni kama umegawanyika vipande viwili , kwani kuna upande ulikuwa bado ukimpenda sana Roma na hakuwa tayari kumuacha , lakini pia kuna upande ambao ulikuwa ukimchukia sana Roma, Pande zote mbili zilionekana kushindana vikali sana , huku upande unaompenda Roma ukichukua ushindi kila baada ya pambano., baada ya upande huo kushinda kila mara , hamu ya kutaka kumuona Roma ilizidi kujaa katika moyo wake , alikuwa amemkumbuka sana na alipanga usiku wa leo kumuona kwa namna yoyote ile.
Muda nao haukukawia sana kwani ulienda kwa haraka haraka , kwani ile Najma anakuja kushituka kutoka usingizini ilikuwa ni saa kumi na mbili , alinyanyuka haraka haraka na kisha alielekea gengeni kununua mboga za usiku , na siku hio alipanga kupika wali na Choroko , hivyo alinunua choroki na kuzichemsha na kuanza kuandaa chakula cha usiku.
“Noja leo nipike kingi , nitamuwekea Roma wangu katika chumba Chake akirudi ale”Alijiongelesha mwenyewe wakati huo akichambua mchele.
“Vipi mwenzetu mbona leo unaonekana ni mwenye furaha hivyo”Aliuliza mama Debora moja ya wapangaji , huku akimwangalia Najma usoni, Mama Debora ndio mpangaji pekee ambaye hakuwa na umbea mwingi na alikuwa ni Mlokole katika kanisa flani lililokuwa mita chache kutoka nyumbani kwa Najma na pia ndio mpangaji pekee aliekaa kwa muda mrefu mno , kwani yeye pamoja na mume wake walianza kupanga hapo kwao tokea wakianza kuona na mpaka sasa ambapo walikuwa na mtoto mkubwa tuambaye alikuwa chekechea anaefahamika kwa jina la Debora ,Mama Debora hakuwa mtu wa Nyumbani sana kwani alikuwa akifundisha shule ya msingi Ikwiriri , sehemu ambayo ilikuwa mbali na kumfanya kudamka sana asubhi na kurudi jioni , hivyo hakuwa akijua maswala yoyote yaliokuwa yakimuhusu Roma kuingiza kahaba.
“Hakuna jipya mama Debo , ni ile tu leo nimejikuta kuwa ni mwenye furaha”Aliongea Najma na kumfanya Mama Debo atabasamu.
“Hehehe .. acha kunificha Roma kakutamkia anakupenda nini?” Najma aliona aibu kwa sentensi hio na kuzidisha tabasamu .
“Nilijua tu , unaonekana kumpenda sana Roma Najma”
“Hhaha .. ndio”
“Muone sasa anavyoona aibu … nimekuja kuweka umeme mimi”Aliongea Mama Debo huku akimpita Najma na kuingia ndani kwa ajili ya kuweka umeme kwani Luku ilikuwa kwa ndani.
Najma alidumu sebuleni kwao kwa muda mrefu sana huku akiwasubiria kaka yake na Roma kurudi kazini licha ya kwamba alikuwa na usingizi mzito uliokuwa ukimnyemelea , lakini hamu yake ya kutaka kumuna Roma iliushinda usingizi na kuendelea kusubiri , siku hii ya leo si kama siku zingine kwani walichelewa kurudi mno , kwani mpaka inafika saa tano na nusu kaka yake hakuwa amerudi , baada ya kusubiri kwa takribani dakika ishirini hatimae mlango uligongwa na Najma haraka haraka alikwenda kufungua mlango.
“Najma hujalala tu , leo mbona umekua kunifungulia wewe”Aliongea Juma huku akiwa ni mwenye kumshangaa dada yake ,kwani siku mbili za nyuma alionekana sio mwenye kujali kuwafungulia yeye na Roma.Kwa Najma licha ya swali hilo , hakujali kabisa kwani alichokuwa akitaka kuona ni Roma Tu , lakini kilichomshangaza ni kwamba siku hio alimuona kaka yake pekee jambo ambalo lilimshangaza.
“Roma yuko wapi kaka , mbona haingii”
“Nilijua tu unataka kumuona Roma”Aliongea Juma huku akiweka uso wa hasira na kumpita baada ya kufunga mlango , lakini Najma hakuridhika alifungua mlango na kuangalia nje lakini Roma hakuonekana , jambo ambalo lilimfanya kuwa katika hali ya maswali , alifunga mlango na kukimbilia ndani.
“Kaka Roma yuko wapi , mbona hujaja nae”.
“Bwana eeh usiniulize maswali yako mimi , kwani umeona natembea nae mfukoni”Aliongea Juma na alikerwa sana na maswali ya mdogo wake , na aliona kabisa si kama alivyofikiria kuwa Najma alikuwa ashaachana na Roma baada ya kumuingiza kahaba geto kwake, alikula chakula alichowekewa na mdogo wake huku akitabasamu kwa kuona kuwa mdogo wake anajua kupika na baada ya kushiba aliignia kwenye chumba chake na kujilaza.
“Najma akiolewa na mimi naoa , nyumba yote inakuwa yangu na ili hili litimie sitaki Najma aolewe na Roma maana nina uhakika kwa maisha ya Roma atataka aishi na Najma hapa hapa”Alijiongelesha huku akiwa amejilaza na kukodolea macho taa mpaka pale alipopitiwa na usingizi pasipo ya kuzima taa.
Upande wa Najma yeye hakuweza kupata usingizi kabisa , muda wote masikio yake yalikuwa kwenye geti tu , ili asikie geti likigongwa ili akamfungulie Roma , lakini muda ulizidi kwenda , lakini alichokuwa akitegemea hakikuweza kutokea kabisa, baada ya kuona atasinzia alienda kusbiria Sebleni mpaka pale alipokuja kupotelea usingizini , na alikuja kushituka kukiwa kumekucha kabisa na hii ni baada ya kaka yake kumkuta Najma akiwa Sebleni, alijikuta hasira zikimpanda baada ya kuona dada yake kalala hapo sebleni na kung`atwa na mbu huku akimsubiria fukara Roma arudi.
“Huyu mpuuzi akirudi leo na mfukuza akapange kwingine , kwa hali hii Najma hawezi kuoelewa”Aliongea Juma na kisha alitoka mpaka vyumba vya nje vya wapangaji na kwenda kwenye chumba cha Roma na kukifungua na kuingia , ndani na kitu cha kwanza alichoona ni mabakuri mawili makubwa ambayo alikuwa akiyafahamu yakiwa kwenye kijimeza , aliyasogelea na kisha kufungua bakuli la kwanza na hapo nipo alipotoa macho huku sura yake ikianza kujikunja.
“Yaani huyu mpuuzi anamuwekea Roma mapaja ya kuku halafu mimi kaka yake ananiwekea wali na Choroko, hii haiwezi kuendelea hivi”Aliongea Juma kwa hasira huku akinyanyua yale mabakuli na kutoka nayo nje huku akipishana na Najma ambaye alimkata jicho , baada ya dakika chache Juma alitoka akiwa na kufuri lingine na kisha alifunga mlango wa Roma na kisha kurudi ndani na kupasha kiporo kile na kula.
Wakati yote hayo yakiendelea Najma ambaye alikuwa kwenye hali ya wasiwasi , alikuwa akimwangalia kaka yake tu , huku akiogopa hata ya kumuuliza chochote kuhusu Roma alipo , baada ya kusimama nje kwa dakika kadhaa , Juma alitoka nje huku akionekana safari ya kwenda kazini kwake ikiw aimewaidia.
“Kaka najua umekasirika lakini naomba uniambie Roma yuko wapi”.
“Usiniulize maswali ya kupuuzi na , kwa upendo wako wa kijinga jinga Roma kwanzia leo akirudi anaenda kutafuta chumba kwingine na nisikie fyoko fyoko uone”Aliongea Juma huku akiweka kibakrashia chake vizuri na kutoka huku mlango wa geti ukiipigiza kwa nguvu.
“Halafu huyu Mpuuzi kaenda wapi , tokea jana mchana sijamuona tena alipofuatwa na yule mtu mwenye suti”
****
JANA YAKE SAA SABA MCHANA
Roma mpaka kufikia muda wa Saa saba mchana alikuwa amepiga kazi kubwa sana ya kuteremsha mizigo ya Cement , kwenye Duka kubwa la vifaa vya ujenzi la Bozi , yeye pamoja na wenzake walikuwa wamechafuka mno kiasi kwamba hawakuwa wakitamanika , lakini wala hawakujali sana , kwani kwao pesa ilikuwa ndio kila kitu.
Njaa nayo haikuwaacha salama , na baada ya kupewa ujira wao , Juma aliwaongoza wenzake kuelekea upande wa pili wa barabara ili kwenda kujipatia chakula cha mchana kwa Mama Joshua. Kama ilivyokuwa desturi yao.
Baada ya dakika kadhaa tu Roma alikuwa ndio alikuwa mtu wa mwisho kunawa mikono , alianza kunawa uso ili kutoa vumbi la Cement na kisha alimalizia mikono , lakini ile anamaliza tu mita kadhaa kwenye barabara kuu , ilisimama gari aina ya V8 nyeupe , gari ambayo iliwafanya baadhi ya watu kuikodolea macho .
Baada ya gari hii kusimama , alitoka mwanadada mmoja aliekuwa amevalia suti ya rangi ya bluu na viatu vya rangi ya Pink , mwanadada huyu alitoa picha kwenye mkoba wake na kisha aliangaza kulia na kushoto huku akitoa simu yake iliokuwa ikiita na kisha kuiweka sikio mara baada ya kuipokea na baada ya maongezi machache alikodolea upande wa kimgahawa cha Mama Joshua huku akikagua mtu mmoja mmoja na baada ya kuona kile alichokuwa akitafuta alisogea kuelekea upande huo wa mgahawa ,. Huku baadhi ya watu wakishangazwa na urembo na shepu ya mwanamke huyo , lakini hakuna aliekuwa ni mwenye kujali.
“Habari yako kaka”Aliongea mwanamke huyu kwa sauti ya kujiamini kabisa na kuwafanya wakina Juma na wenzake kushangazwa na kitendo hicho , kwani mtu aliekuwa akisalimiwa alikuwa ni Roma.
“Salama”Aliitikia Roma pasipo kujali uzuri wa mwanamke aliekuwa mbele yake na kusogelea meza ya plastiki ya rangi ya bluu na kuketi kwenye kiti huku mrembo huyu kuonesha kuchukizwa na kitendo cha Roma kutokumuangalia usoni , licha ya kumsemesha , kwake alitafsiri kama dharau kubwa ambayo ameonyeshwa kwa mwaka huo , yaani katika maisha yake na urembo wake , hakuwahi kudharauiwa na mwanaume wa aina yoyote ile , lakini kwa Roma ilikuwa tofauti na hio aliingiza katika Top Ten ya dharau alizowahi kuonyeshwa katika maisha yake, lakini licha ya hivyo , mwanadada huyu bado alionekana kuwa ni mwenye shida ya kuongea na Roma kwani alisogea mpaka kwenye meza aliokuwa amekaa Roma na kumwangalia kwa kumshusha kwa mavazi yake ya kimasikini na uchafu uliomjaa.
“Mama Joshua nipe ugali mkubwa na Samaki “Aliongea Roma na kuwafanya marafiki zake wazidi kumshangaa Roma kwa kitendo hicho cha kutokujali , licha ya kuongeleshwa na mwanamke mrembo kama huyo ambaye kwao , ilikuwa ni kama ndoto kupata bahati ya kuongeleshwa na mrembo kama huyo.
“kaka nimekusalimia”
“Ooh !,, sorry sister , nilikuwa bize kidogo , kumbe ulikuwa ukiniongelesha mimi”.
“Ulifikiri na muongelesha nani , au dharau tu kaka yangu , sio vizuri”Aliongea mwanadada huyu kwa sauti yake ya kuvutia huku akionekana amekereka kweli kwa kitendo cha Roma kujifanya hakumsikia wakati wote huo aliokuwa anamsalimia , na kilichomkera Zaidi mwanadada huyu ni kutokana na watu waliokuwa wakimwangalia , alichokuwa ametegemea mwanamke huyu ni Roma kumnyenyekea , lakini swala hilo likawa nje ya mategemeo yake na kumfanya yeye ndio aonekane mwanamke mwenye shobo na katika baadhi ya watu waliamini huenda huyo mwanadada alikuwa ni demu wake.
“Ulikuwa unasemaje sista”.
“Wewe si ndio Roma”
“Ndio ni mimi”
“Basi naomba utangulizane na mimi kuna mtu muhimu sana anataka kuonana na wewe”Aliongea mwanadada huyu na kuwafanya watu wote waliokuwa hapo mgahawani kushangazwa na maneno hayo , ila kwa Roma hakuonekana ni mwenye kushangaa sana , kwani alipokea chakula chake na kuanza kula.
“Sister naomba ukae , kwanza unisubirie nimalize nipige msosi ndio tuongee maswala ya mtu Muhimu .. maana hii ni moja ya starehe yangu na mara nyingi ni kila sipendaki kusumbuliwa”Aliongea Roma kwa kujiamini huku akianza kumega bonge la tonge na kulichovya kwenye mchuzi na kisha kulimeza lote , kitendo ambacho kilimshangaza sana huyu mrembo , na kumkera kwa wakati mmoja.
“Nitasubiri kwenye gari , ukimaliza naomba tufutatishane kama nilivyokuambia”Aliongea ule mwanadada pasipo kusubiri jibu , na kisha kuondoka .
“Halafu we Ms**nge unapenda kuifanyisha matawi ya juu , mtoto mkali kama yule anakuongelesha unajifanya unaongea kama hutaki kama vile Mondi , vile au unatuoshea tu washikaji zako hapa”Aliongea Yusuph huku akiungwa mkono na wenzake.
“Ila jamaa nimemkubali sana , ile pia ni heshima”:Aliongea jamaa mmoja ambaye yeye hakuwa muongeaji sana , ila siku hio alionekana kuchangia.
“Hahaha .. Mhando hata wewe leo umechangia mada , inaonekana pia umeguswa sana na jambo hili”Aliongea Juma na kuwafanya wengine wacheke maana ni kwa mara ya kwanza kwa Mhando kuchangia mada , yeye alikuwa ni mkimya wa hali ya juu
Baada ya Zaidi ya nusu saa ya Roma kumaliza msosi wake , alipiga maji kwenye kikombe , na kisha alijishika tumbo lake na kujiona kushiba vyema na kutoka mgahawani na moja kwa moja alielekea kweye gari , na kugonga mlango wa kioo ulioshushwa.
“Ingia kwenye gari”Aliongea mwanadada huyu kwa sauti iliojaa machukizo na kwa Roma wala hakujali , baada ya kuingia kwenye gari , ilitolewa nduki kuelekea upande wa Kongonwe na kuja kugeuzwa na kurudi upande wa kuelekea kariakoo.
“Unanipeleka wapi Mrembo”Aliongea Roma lakini hakujibiwa , Zaidi ya kusonywa na Roma aliamua kutulia kwenye kiti chake , huku akifurahia kiyoyozi kilichokuwa kwenye gari hilo, na kutokana na uchomvu aliokuwa nao , alipitiwa na usingizi na hata pale alipokuja kushituka alijishangaa akiwa mbele ya jengo refu mno maeneo ya Mawasiliano Sehemu ambayo alijua haraka kwani alikuwa ni mwenyeji wa maeneo hayo , baada gari hii kusimama kwenye jengo hili Geti lilifunguliwa na gari ile iliingizwa mpaka ndani na kuegeshwa na kisha mwanamke yule mrembo alishuka .
“Karibuni Grand palace hoteli wateja wetu”Ilisikika sauti ya muhudumu iliowakaribisha kwa tabasamu na ucheshi wa hali ya juu ,Roma alimwagalia mwanamke huyo aliekuwa amevalia sare ya hoteli hio na kisha alimkonyeza kitendo ambacho yule mwanadada aliekuja na Roma kukiona na kubetua midomo , lakini kwa muhudumu alirudisha kwa tabasamu la kuita.
“Watu wenye pesa wanakula maisha sio poa”Aliongea Roma baada ya kuingia kwenye lift huku akiwa si mwenye kuacha kumkonyeza mrembo huyu ambaye amenuna kama muuza sumu.
Baada ya lift kufunguka katika Floor namba kumi na nane , Roma alifuata nyuma nyuma mpaka walipofika kwenye mlango wa chumba namba 708 na kisha huyu mrembo aligonga mlango na ndani ya dakika kadhaa mlango ulifunguliwa na mwanaume alievalia suti.
“Karibu Suzzane”Aliongea mwanaume huyu alievalia suti huku akiwa ni mwenye tabasamu lakini pia macho yake hayakuwa mbali na uso wa mwanaume aliekuwa nyuma ya Suzzane , mwanaume ambaye kwa macho ya haraka haraka alionekana kama Fukara.
“Bossi nisharudi na nimemleta”Aliongea mrembo Suzzane kikakamavu huku akimwangalia mwanamke aliegeukia dirishani , akionekana kuangalia nje akiwa amewapa watu wote katika chumba hiko mgongo.
Mwanamke huyu alikuwa amependeza mno kwa vazi lake la suti alilokuwa amevaa ,suti ya rangi nyeupe
“Asante Suzzane , mnaweza kuondoka m
paka pale nitakapowaita”
“Boss!!”Aliongea Suzzane kwa hali ya wasiwasi .
“Fanya kama nilivyosema Suzzane”Aliongea mwanadada huyo kwa sauti ya Amri na kumfanya Suzzane amkate jicho Roma ambaye alikuwa akikagua uzuri na ufahari wa chumba hiko.
Licha ya Roma kushangazwa na ufahari wa chumba hicho , lakini pia sauti ya mwanadada aliekuwa mita kadhaa mbele yake aliempa mgongo ilikuwa ikimsisimua mno , ilionekana kama inamkumbusha mbali sana.
Baada ya Suzzane na mwanaume yule kutoka nje , mwanadada yule aligeuka na kumwangalia Roma , kitendo ambacho kilimfanya Roma atoe mshangao na kutamka:
“Kahabaaa…!!!”
Comments