Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

Abubakari Hamadi  ni mtoto alielewa ndani ya familia ya tajiri maalufu ndani ya Tanzania afahamike kwa jina la Alex Kaoneka tokea akiwa mdogo ,Mzee Alex kaonekana alimchukua Abuu  ndani ya  kituo cha kulelea watoto yatima ndani ya wilaya ya lushoto miaka ya nyuma wakati akiwa moja ya wafadhili wakuu wa  kituo hicho.

Moja ya sababu kubwa ya Mzee Alex kuvutiwa na  Abuu  ni kutokana na uwezo wake wa akili, kwani katika watoto  wote waliokuwa ndani ya kituo hiki Abuu  peke  yake ndie aliekuwa akionesha uwezo wa kipekee sana wa akili kuwashinda wenzake wote.Sababu ya pili ya mzee Alex kumchukua Abuu ni kutokana na Mzee huyu   kubahatka kupata watoto wa kike tu katika familia yake.

Miaka ya nyuma Mzee Alex wakati anamuona Abuu   alikumbuka  ugonjwa aliokuwa nao ambao  aliupata na kumpelekea kupoteza uwezo wake wa kumpa mimba  mwanamke, na kupitia ugonjwa huo alikuwa akiishi sana kwa mawazo , kwani aliona licha ya kuwa na  mali nyingi , lakini alikosa mtu ambaye anakuja kumrithi na tumaini lake lilikuja kufufuka tena mara baada ya kumpata Abuu.

Mke wake Bi Anna alipinga vikali  swala hilo , ila kwa mzee huyu alikuwa na tabia moja tu , akishafanya maamuzi hakuna mtu wa kumzuia , hivyo  mke wake hakuwa na nguvu tena ya kumshawishi na hivyo kukubaliana nae na wakamchukua Abuu katika familia yake.

Sifa kuu ya Mzee Alex katika maisha yake ni ubaguzi wa kijinsia , bwana huyu alisifika sana kwa kudharau wanawake na katika maisha yake aliamini kwamba wanawake  hawawezi kufanya vitu ambavyo vilikuwa vikifanywa na wanaume na kwa kasumba hio iliokuwa imejaa ndani ya akili yake hakuwahi kufikiria kuwarithisha kabisa watoto wake makampuni  yake na chaguo sahihi kwake ilikuwa ni Abuu.

Abuu alikulia kama mtoto kabisa  wa Mzee Alex kwa kupokea  matunzo  na upendo wote ambao kama mtoto ni moja ya mahitai yake   makuu , alilelewa kitajiri , alisoma katika mashule makubwa ya hela nyingi, maisha ya Alex yalibadilika kabisa na hakuwa yatima tena bali alikuwa mtoto mwenye  familia ambayo ilikuwa ikimjali , lakini licha ya hivyo Abuu hakuwahi kuwaza kubadili dini yake kutoka uislamu kwenda kwenye ukristo na mzee Alex pia hakuwa na shida juu ya hilo kwani kwanza hakuwa  mpenzi wala mfatiliaji sana wa Imani za kidini , kwake  Imani yake kubwa ilikuwa ni Pesa , alikuwa akiabudu pesa kama Mungu wake, na alikuwa yupo tayari kufanya lolote  juu ya pesa na aliamini matatizo yote yanaweza kutatuliwa na pesa.

“Kama matatizo yote ninaweza kuyatatua  kwa kutumia pesa kuna haja gani ya mimi kuwa na dini inayomhusisha mtu asieonekana , mimi naamini vitu vinavyonekana kama pesa”Ni siku moja  mzee huyu alipokuwa akihojiwa na kituo kimoa cha Redio.

Kama alivyopanga mzee huyu baada ya Abuu kumaliza masomo yake  ya chuo kikuu kutoka Princeton Marekani alirudi Rasmi nchini kwa ajili ya kufanya kazi katika makampuni ya baba yake , mwanzo wa kufanya kazi katika makampuni haya ndio mwanzo uliomfanya  kijana huyu kumfahamu mwanamke mrembo CEO ,afahamikae kwa jina la Edna Adebayo.

Mara yao ya kwanza kukutana na mwanadada huyu ni kipindi ambacho alikutana na mwanadada huyo kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara juu ya bidhaa mpya ambayo ilikuwa ikifanywa kimkataba baina ya kampuni mbili yaani Vexto na JR , kipindi hiki Abuu alikuwa ni Assistant CEO na kwa mrembo Edna alikuwa pia Ni Assistant CEO.

“Abuu  Nadhani umemuona Edna?”

“Ndio baba”

“Mzuri Eh?”Aliuliza mzee huyu wakati wakiwa ndani ya kampuni hii ndani ya ofisi ya Mzee Alex.

“Nimzuri sijawahi ona baba, nimemkubali”

“Haahaha.. ndio maana nimekupatia dili hili la kibiashara ulifanyie kazi”Abuu alishangaa huku Mzee Alex akitabasamu huku akinywa   wine iliokuwa kwenye glass kidogo na kurudisha  kwenye meza.

“Unajua katika familia ya  Adebayoo , wanawake ndio wanaongoza familia na ndio maana mpaka sasa unaona kampuni karibia yote imejaa wanawake , Mzee Adebayoo mwenyewe hana nguvu kwa mke wake na yeye ni mmiliki wa kampuni pekee alizoanzisha yeye , lakini za kifamilia  hana nguvu yoyote”Abuu alishangaa lakini mzee huyu aliendelea

“Mzee Adebayoo mtoto pekee aliekuwa naye ni Edna   na kwa maana hio ni Dhahiri miaka ijayo mrithi mkuu  wa makampuni yote ya Vexto yatakuwa chini yake  baada ya mama yake kuachia uongozi na ndio maana unamuona Edna sasa hivi yupo kwenye nafasi kama yako”

Abuu alionekana kumuelewa  baba yake huyo mlezi  anakoelekea.

“Labda nikuambie tu kampuni ya Vexto  ni kampuni yenye nguvu kubwa kwa ukanda wetu huu wa Afika mashariki na Kati , nguvu yake ni kubwa mno  na hakuna kampuni yoyote  inayoweza kuipita likija swala la nguvu , kampuni inayofuatia ni ya kwangu , lakini bado sijaridhika na nafasi ya pili , nataka kampuni yangu miaka ijayo ichukue nafasi ya Vexto  na hii ndio misheni yangu kubwa mabayo nataka kuitimiza kabla ya kuingia kaburini , hivyo  njia pekee ya mimi kukumiliskisha makampuni yangu na kuyaongoza ni  kuhakikisha unampata Edna anakuwa mkeo , akishakuwa mkeo  automatically kampuni itakuwa yako  na hapo  utaifanya kampuni ya Vexto kuwa sehemu ya JR  na kampuni yetu itakuwa na nguvu kubwa mno kiasi cha kampuni yoyote ile kuifikia”

Abuu alielewa sasa  maelezo ya baba yake na ndoto aliokuwa nayo , maana katika maisha yake alikuwa akiwaza ni namna gani anaweza kumfurahisha baba yake huyo wa kambo ili amuaachie nafasi katika makampuni yake , lakini siku hio ndio alipopata kujua  ni nini ndoto  ya baba yake.

Kwanzia siku hio Abuu alianza kuweka ukaribu na Edna , alijaribu kumtongoza mara kwa mara apatapo nafasi , kumjali na kujipendeza kwake , lakini kwa Edna  hakuambulia chochote , kwani mwanamke huyo alikuwa mgumu kama chuma , lakini licha ya hivyo Abuu hakuwahi kukata tamaa , aliamini Edna ni mwanamke na wanawake wameumbiwa kuwa wadhaifu kuliko wanaume  hivyo aliamini ipo njia ya kumpata.

Miaka miwili mbele ya Abuu  kuhangaika , mama yake Edna alifariki  kwa ugonjwa wa kisukari na  hapo ndipo  Edna aliporithishwa uongozi wa juu wa kampuni ya Vexto na kuwa CEO na mmiliki halali wa makampuni hayo , jambo ambalo baba yake Edna alilipinga vikali , lakini kwakua sheria ilikuwa ikimlinda Edna basi baba yake Edna  hakufua dafu mbele ya sheria .

Mzee huyu baada yakuona amekwama kabisa  juu ya mpango wa yeye kumiliki kampuni ambazo zilikuwa zikimilikiiwa na mke wake  na hatimae kuangukia kwenye mikono ya  mtoto wake , mipango aliokuwa nayo miaka mingi ya kumiliki mali za familia na hapo ndipo alipokuja kutafuta mbinu mbadala , katika kutafuta kwake mbinu mbadala ndipo alipomuaomba ushauri rafiki yake mkubwa Alex kaoneka , sababu za mzee huyu kumuomba ushauri ni kutokana na kwamba mzee huyu alikuwa akijua kuwa kijana wa Alex alikuwa akimpenda  Edna.

“Mimi  naona njia pekee ya wewe  kumshinda Edna ni kumfanya aolewe na Abuu kijana wangu , Edna akishaingia kwenye mikono ya Edna  kihalali jina lake litabadilika kutoka kuwa Adebayoo mpaka kuja kuwa jina la Familia yangu na hapo mwanafamulia pekee ambaye utabaki kuwa na uhalali kwa kumiliki makampuni ya familia  ni wewe”Aliongea Mzee alex na kumfanya Adebayoo kutabasamu , aliona hilo lilikuwa ni wazo zuri mno.

Baada ya ushauri huo kutoka kwa rafiki yake moja kwa moja  alianza harakati  za kumlazimisha Edna kuolewa na Abuu , jambo ambalo  Edna alilipinga vikali , kwanza alikuwa na sababu nyingi sana za kumkataa  Abuu , sababu ya kwanza ni kwamba hakuwa amempenda na katika maisha yake alipanga kama atakuja kuolewa basi lazima aolewe  na mwanaume ambae anampenda, sababu ya pili  Edna alikuwa akikumbuka wosia wa  mama yake kabla ya kufa.

“Mwanangu hakisha unalinda kampuni hii kwa namna yoyote ile,epuka wanaume ambao watakulaghai na kukupokonya sehemu yako ndani ya kampuni” huo ni moja ya wosia  aliopatiwa na  mama yake na kwake ulikuwa ni kama Imani na kwa wosia huo alimuona kabisa  Abuu kama mmoja ya watu ambao ni maadui dhidi ya kampuni na ndio maana hakutaka ukaribu kabisa.

Kwa upande wa Abuu yeye licha ya kwamba alikuwa amepewa  misheni ya kumuweka mikononi Edna ila ndani ya moyo wake alikuwa akimpenda kwa mapenzi kabisa ya dhati , kiufupi alikuwa amekufa ameoza kwa mwanamke huyo , alikuwa haambiwi chochote juu ya Edna , alikuwa yupo radhi kufanya chochote kwa ajili ya kumpata mrembo huyo.

Baada ya kuona  swala lake linazidi kuwa gumu la kuutingisha moyo wa Edna kwa njia za kiushawishi aliona atumie nguvu  na njia pekee ya kutumia nguvu alipanga kumuhusisha baba yake Edna katika mapambano na hapo ndipo alipoharibu Zaidi kwani Edna alizidi kukaa nae mbali.

Baada ya Abuu kuona  ameshindwa kwa njia zote kumpata  Edna, huku  akipata presha kubwa kutoka kwa baba yake  ndipo alipoanza kupanga mbinu za kumnasa mrembo huyo , lakini katika mbinu zote  alizopanga hakuweza kufanikiwa  hata mara moja na hii yote ni kutokana na uwezo mkubwa wa kiakili wa Edna.

Edna alikuwa  na akili sana na ndio maana kwa kipindi kifupi tokea apewe uongozi wa makamouni ya kifamilia , aliweza kuleta mafanikio makubwa sana ,Edna alikuwa ni msomi kutoka chuo kikuu cha Oford uingereza  alikochukua masomo yake ya kibiashara kwa ngazi ya  Degree na Mastaers na katika kipindi chote cha masomo Edna aliweza  kufanya vizuri sana kuliko wanafunzi wote , sifa ya  Edna chuoni ilikuwa ni Mrembo Mgumu’ kwani Edna licha ya kubarikiwa kuwa na uzuri wa Ajabu , lakini hakuwahi kujihusisha na aina yoyote ile ya  mahusiano , alikuwa na marafiki wachache ambayo alikuwa nao kwa sababu moja tu ya kimasomo na hii ndio sabau iliompelekea kuzidi kung`ara kwenye masomo.

Hata aliporudi nchini Edna tabia yake ya chuo haikuwa imbevadilika kwanza alikuwa mwanamke  mkimya sana  na mpole , hakuwa muongeaji sana  na hii ilimfanya kuwa na mzunguko mdogo wa watu anaofahamiana nao nje ya kazi, ukimya wake uliongezeka baada ya  mama yake kipnezi kufariki.

Edna kwake ndugu pekee aliekuwa  akimpenda alikuwa  ni Bi Wema , kwake mwanamke huyo licha ya kwamba hawakuwa ndugu  wa damu lakini alimchukulia  kama mzazi wake mwingine baada ya  mama yake ,Edna na baba yake hawakuwa na mapenzi  ya kuwafanya  waonane kama ndugu , uhusiano wake ulikuwa kwenye damu tu na kwenye jina lakini ule ukaribu wa kibaba na mwana haukuwepo kabisa na hii yote ni kutokana na kwamba mzee Adebayoo hajawahi hata siku moja kumchukulia Edna kama mwanae na hakuwa akimpenda kabisa.

Siku moja  baada ya miaka kadhaa na Abuu kuwa CEO wa makampuni ya  JR , alipanga mpango wa  mwisho kabambe wa kumpata Edna , katika mpango wake jambo la kwanza aliloloifanya ni kuhakikisha kuwa  yeye na Edna wanaonana mara kwa mara na njia pekee ya kufanikisha wao kuonana mara kwa mara ni kwa maswala ya kibiashara , kwani Abuu alikuwa akimjua vyema Edna kuwa  likija swala la biashara  hana upinzani na kutokana na hivyo , aliingia dili nono na kampuni  ya Edna na hii ni mara baada ya tawi la kampuni ya JR kupata zabuni ya ujenzi wa barabara  ya mwendokasi iliokuwa ikianzia maeneo ya  Rangi tatu mpaka Chamazi , katika zabuni hio kampuni ya JR ilikuwa ikihitaji  malighafi nyingi kutoka nje kwa ajili ya kukamilisha ujenzi na  hapa ndipo Abuu alipokuja na wazo la kuwapa tenda Vexto kuwa kampuni pekee itakayowasaidia katika manunuzi na usafirishaji wa ‘material’ kutoka nje ya nchi na dili hili lilipowekwa mezani kwa CEO Edna hakutaka kufikiria sana , alikubali moja kwa moja kwani aliamini kupitia dili hilo  atakuwa amepiga hatua kubwa.

Mpango wa kwanza wa Abuu ukawa umefanikiwa wa kumuweka  Edna  karibu na alipanga dili hilo la kibiashara angelifanya yeye mwenyewe  na mpango wa pili aliupanga siku ya  kusaini makubaliano baina ya kampuni hizi mbili.

Siku ya kusaini mkataba ilifika na  Abuu aliwasiliana na Edna kumpa eneo husika ambalo makubaliano hayo yatafanyika na  eneo alilolichagua  Abuu ilikuwa ni ndani ya hoteli yao ya kitalii ya nyota tano iliokuwa  ipo maeneo ya Maji matitu Mbagala(JR Hotel) huku muda ukiwa ni saa   mbili za jioni kwani walipanga tukio hilo lifanyike wakati wa chakula cha usiku.

Edna na yeye bila ya kufikiria mara mbili alikubali  na muda wa saa moja na nusu ndio aliingia ndani ya  hoteli hii , akiwa mwenyewe bila ya mlinzi wake Suzzane.

Baada ya kufika alionyeshwa sehemu sahihi ya kuketi  na akaletewa juisi na mhudumu  baada ya kuagiza kwani hakutaka kunywa kilevi chochote huku akiwa anamsubiria Abuu , Edna hakuwa na wasiwasi , kwanza alikuwa akimuamini Abuu  na sababu kubwa iliomfanya amuamini ni kutokana na kwamba alijua fika kwamba Abuu alikuwa akimpenda kwa mapenzi ya dhati ni vile tu yeye hakuwa na hisia nae na pia  hata kama angekuwa na hisia nae  asingekubali kuolewa nae kwani aliogopa nguvu kubwa iliokuwa nyuma yake.

Ilimchukua dakika kadhaa tu baada ya kunywa  juisi ile na kupotelea usingizini kabla hata ya Abuu kuonekana , kwa upande wa Abuu yeye alikuwa  ashapanga vijana wake kwa ajili ya kazi hio, baada ya vijana wa  Abuu kuona mpango umeenda kama ulivyopangwa  walichukua chupa za  bia na kuziweka katika meza ya Edna ili kuonyesha kwamba mrembo huyu alikuwa amelewa na pombe , lakini Jose na mwenzake walishangazwa na kitendo cha bosi wao kuchelewa na hata pale walipo mpigia simu  hakuwa hewani , Zaidi ya masaa manne yalipita ndipo bosi wao alipoingia kwa pupa  na kwenda moja kwenye meza  waliokuwa  wamekaa vijana wake.

“Mmeshadaa chumba , nataka kila nitakachofanya kiwe kinarekodiwa sitaki uzembe katika hili”Aliongea  Abuu mara baada ya kuambia vijana wake kwamba alipata tatizo la kikampuni ndio maana alichelewa.

Wakati akiongea  na vijana wake ndio wakati ambao mwamba Roma aliingia na kujibebea mzigo akimdhania mwanamke huyo kama kahaba , kwanza walishindwa kuchukua maamuzi hapo kwa hapo kwani hawakua wakimjua mwanamme huyo na mpaka Roma anatokomea nje ya mlango  ndio   Abuu alipotoa  amri ya vijana wake wakamdhibiti Roma , lakini wakaishia kumkosa na mpango ukawa umefeli.

Upande wa Edna baada ya kuamka na kujikuta akiwa kwenye Godoro  , kwanza alishangaa  ni vipi alivyofika hapo ,  lakini alipojiangalia na kujiona alikuwa uchi huku akihisi maumivu  sehemu zake za uzazi ndipo alipojua mwanaume aliekuwa mbele yake  ashaitoa bikra yake bila ya ridhaa yake.

Alikumbuka kila kitu tokea akiwa hotelini , lakini baada ya kupotelea usingizini hakujua ni kipi kiliendelea .

Baada ya kurudi nyumbani na kujichua na maji ya moto kupunguza maumivu hapo hapo ndipo alipo mpa kazi Suzzane kufatilia kilichotokea , lakini kwa bahati mbaya Abuu alikuwa na akili kwani alifuta hatua zote, kwani kwanza hoteli ile ilikuwa ni ya kwao hivyo  mpango wake ulihusisha kuzimwa kwa Camera, hivyo Suzzane alivyofika kwenye hoteli kwa ajili ya kuomba  picha ya matukio ya jana yake ,  aliambiwaCamera hazikuwa zikifanya kazi.

Baada ya Suzzane kutoa jibu hilo kwa Edna  alimwambia kuwa  afanye uchunguzoi wa taarifa  za mwanaume alielala nae na katika kutafuta taarifa hizo ndipo alipopata taarifa kamili ya kilichotokea  kwani Suzzane alirudisha taarifa inayoonyesha  Roma alikuwa  ni mbeba mizigo  ndani ya soko Rangi tatu , Suzzane pia aliweza kupata  eneo na Muda wa eneo  alilokuwepo Roma kwanzia anarudi kazini na kwenda Club B   na hapo ndipo  Edna alipojua Roma  hakufanya kitendo kile makusudi  bali alimdhania  yeye kama kahaba na hii yote ni baada ya kukumbuka  wakati akiondoka  ndani ya chumba can Roma kwani mwanaume yule alitaka kumpatia  pesa yake.

“Yaani kulala na kuamka  nimekuwa kahaba”Aliwaza Edna kwa uchungu mkubwa  sana moyoni mwake , lakini kwa upande mwingine alishukuru  kwani aliamini    huenda mambo ambayo yangemkuta yangekuwa makubwa Zaidi  kuliko yaliomtokea  kulala na Roma.

“Miss jitahidi utafute mwanaume , huwezi ukaishi hivi   milele itakuumiza na kukuathiri katika maisha yako , unahitaji mtu wa kukufariji katika nyakati ngumu , mimi  siwezi kufanya hivyo kila siku nishaanza kuzeeka na sijui hata kesho nitakuwepo kwa ajili yako”Aliongea Bi Wema baada ya kumuona Edna akiwa ni mwenye mawazo mengi baada ya kutokurudi nyumbani usiku mzima.

M aneno ya Bi Wema kwake yalikuwa na maana , lakini hakuwa tayari kuwa na mwanaume , hakuwa akiwaamini kabisa ,  siku ya kwanza ilipita , ikaja ya pili yake , wakati wa usiku akiwa anajisomea ndipo alipoweza kupata wazo la kufunga ndoa na mwanaume yoyote kwa mkataba ili mradi kujiweka mbali na baba yake anayemsumbua  kuoelewa na Abuu  mwanaume ambaye hakuwa tayari kueolewa nae.

“Lakini mwanaume huyo ni nani?” Aliiwazia kwani hakuona mwanaume sahihi kwa yeye kufunga nae ndoa kimkataba.

“Nataka mwanaume ambaye atanisikiliza kwa kila kitu ,  ambaye atakuwa tayari kufanya kile nitakachokua namuambia , mwanaume ambaye    nitaweza kumuendesha nitakavyo”Aliwaza kwa sifa hizo , lakini bado hakuona  mwanaume anaefiti ndani ya sifa hizo , kila mwanaume aliekuwa akimjua alikuwa mbabe na mwenye utawala na tamaa ya pesa hivyo wote anaowajua walikosa sifa , yeye alitaka mwanaume bwege  , lakini wanaume wote aliokuwa akiwajua  kazini kwake  wote hawakuwa na sifa za ubwege.

“Napata wapi manaume Bwege wa kufunga nae ndoa ya mkataba?”Aliwaza na kuwaza na kujiona swala hilo alipe kiporo , lakini ile  anajaribu kunyanyua mguu kupanda kitandani mara alijihisi maumivu kwenye  kitumbua chake  na hapo jina la Roma liliibuka katika kichwa chake.

“Ndio atanifaaa , japo simjui  ila naamini atakuwa ni wale wanaume mabwege  na hata kama sio bwege pesa zangu zitamfanya kuwa bwege na nitamuendesha ninavyotaka , ndio anafiti   kabisa , kwanza hana pesa  ni masikini na hii ndio sifa kubwa”Alijiongelesha na kutoa tabasamu la ushindi.

“Ila nitamshawishi vipi..? , ila atakubali tu kama nitamwambia  nitamlipa , lakini akikataa je..?, hawezi kukataa , nani anaweza kunikataa mrembo kama mimi kama nitamwambia  nampenda , wanaume wote ni wadhaifu juu ya wanawake warembo”

Alijiongelesha  na  akili yake ikawa na jibu sahihi  ,jibu aliloata ni kumfanya Roma mume BWEGE.

Previoua Next