Roma alishangaa kujua mke wake ndio CEO na mmiliki wa Makampuni ya Vexto ,Unajua Roma licha ya kujua Edna ana hela lakini hakuwahi kuwaza mke wake anaweza kuwa na pesa nyingi kiasi cha kumiliki mkampuni huu mkubwa ambao ulikuwa ukichangia asilimia mbili za uchumi wa Taifa , Makampuni ambayo yalikuwa na wafanya kazi Zaidi ya elfu hamsini , yaani kwa maneno marahisi ni kwamba maisha ya familia Zaidi ya Elfu hamsini zilikuwa zikimtegemea mke wake mrembo Edna.
“Bebi yaani nahangaika vyote hivyo na makaratasi na mausaili kumbe wewe ndio bosi”
“Roma chunga kauli yako , hapa ni kazini sio nyumbani mambo ya kuitana bebi siyataki mimi ni bosi wako”.
“My beutifull Edna , usiniambie kuwa tukiwa kazini mimi sio mumeo?” Edna hakujibu Zaidi ya kumwangalia Roma na kumtafakari ni mtu wa namna gani , yaani yale mawazo aliokuwa akiyawazia juu ya Roma yalikuwa ni Zaidi ya tofauti.
“Huyu baada ya miezi sita ya mkataba wetu kuisha nampa chake , siwezi kuishi na mwanaume asie na aibu kama huyu” Aliwaza Edna
Roma hakumjali Edna , alikuwa ashamjua ni mtu wa namna gani hivyo hakutaka kufanya kama alivyokuwa akitegemea yeye kufanya , alipanga kufanya mambo kinyume chake na hivyoo kumtania utani unaomkasirisha alikuwa akifanya makossa kabisa , lakini ni ukweli kabisa Roma hakuwa mtu mwenye aibu.
“Haya niambie My wife umeniitia nini , Au unataka unipe cheo kikubwa kikubwa” Edna alikunja ngumi maana alikuwa akichukiwa na neon ‘Wife’.
“Usomi wako hauendani na wewe kabisa , uliwezaje kumaliza ndani ya chui kikubwa duniani na tabia kama ulokuwa nayo”
“Hehe .. mke wangu hilo swali hata siwezi kujibu , mimi nilienda chuo kuchukua maarifa na ujuzi wala sikwenda kubadili tabia yangu”.
“Okey!, nimekuita hapa kukupa onyo mimi na wewe kuwa mke na mume ni nyumbani , mtu yoyote asijue sawa! , pili nakupongeza kwa kuwa mfanya kazi wetu , kampuni yetu inajali wafanya kazi , hivyo kama kuna jambo lolote usisite kuwasiliana na uongozi”
“My Edna siwezi kukubali onyo lako bila ya malipo”.
“Nishamaliza kuongea unaweza kwenda”Roma alitabasamu kifedhuli na kisha kusogelea ofisi ya sekretari na kumuita ndani ya ofisi.
“Mimi na bosi wako ni…”.
“Monica unaweza kwenda kuendelea na kazi”Aliongea Edna na Monicca alijikuta akishangaa , ila hakusema neno alitoka nje.
“Yaani wewe…Haya unataka nikulipe nini?” Roma alitabasamu na kwenda kukaa kwenye sofa na kukunja nne.
“Unaonaje ukinikiss”.
“Roma nipo kazini naomba ujichunge “Aliongea Edna kwa kukasirishwa.
“Haya mke wangu kipenzi usikasirike .. malipo yangu ni kwamba usije ukanifukuza kazini”.
“Hilo sina maamuzi nalo ukifanya mambo ambayo yataenda kinyume na maadili ya kampuni basi nitakufukuza”.
“Msimamo wangu ndio huo , wewe ndio boss , ukitaka nimtangazie kila mfanya kazi kama sisi ni wanandoa basi nifukuze kazini”Aliongea Roma na kutoka huku akimwacha Edna akizidi kumtafakari.
“Nimeingia cha kiume , huyu sio mwanaume bwege niliokuwa nikimtaka”Aliwaza Edna.
Baada ya Roma kutoka ndani ya ofisi ya CEO alienda moja kwa moja mpaka sehemu ambayo alikuwa akitakiwa kufanyia kazi , baada ya kuingia ndani ya ofisi kubwa iliokuwa na Tarakishi nyingi , huku kila meza ikionekana kuwa na mwanamke aliekuwa akifanya kazi , yaani Roma alishangazwa na warembo waliokuwa katika hii ofisi.
“Habari zenu Warembo mniite Roma Ramoni ni mfanyakazi mpya , ninafurahi kufanya kazi na warembo kama nyie na naamini tutashirikiana kwa ukaribu” Warembo wote walijikuta wakishangazwa na utambulisho huo.
“Karibu sana Roma , naitwa Benadetha , mimi ndio kiongozi wa idara hii ya Public Relation na kwa niaba ya wafanya kazi wa idara hii tunakukaribisha”Aliongea mrembo mmoja mwenye mwanya na kumfanya Roma atabasamu na kisha alionyeswa meza yake na tarakishi yake ya kufanyia kazi.
“Hivi hii kazi kwanza inahusiana na nini maana sina ninachojua mimi , wangeujua sijawahi hata kukanyaga ndani ya chuo cha Harvad wasingenipa hii kazi”Aliongea Roma baada ya kuona hana cha kufanya.
“Hey! Handsome , unaweza kuanza kazi kesho sio lazima leo”
“Nimeamua kuanza leo mrembo , ili tuzoeane mapema, unaitwa nani vile?”
“Niite Recho”Aliongea Recho huku akionekana ni wale wanawake waongeaji na wajana wajanja.
“nafurahi kufanya kazi karibu na mrembo kama wewe”Aliongea Roma huku akimkonyeza na Recho aliishia kutabasamu na kisha kuendelea na kazi.
“Huyu mwanaume anaonekana kuwa muhuni”Alijiwazia Recho.
Roma alifungua Tarakishi yake na kutafuta cha kufanya na alijikuta akiishia kwenye Gemu la Zuma lililokuwepo ndani ya tarakishi hio na kuanza kucheza kupoteza muda.
Wakati akiendelea kucheza mara aliingia mwanamke aliemfanyia usaili , kwanza mwanamke huyu hakumuona mpaka pale aliposhituliwa kwani muda wote alikuwa akicheza Gemu.
“yaani wewe wenzako wanafanya kazi wewe unacheza gemu…”
“Mrembo wa mapokezi ni wewe..!?”.
“Mimi sio mremnbo wa mapokezi niite Nasra, tabia ya kucheza gemu muda wa kazi ni kinyume na sheria za kampuni leo nitakusamehe ila siku nyingine nikikukuta unacheza gemu mshahara wako utakatwa nusu”.Huku akiondoka kwa hasira lakini Roma alimwita
“Eti Nasra, hakuna kazi nyingine tofauti na kukaa chini kukodolea Komputa , kazi kamaaa.. kubeba mizigo ya kampuni au kazi yote inayotumia nguvu mimi kazi kama hii sijaizoea”Aliongea Roma na Nasra alimshangaa na hakuongea neon aliondoka
Muda wa chakula ulifika Recho alimwambia Roma waongozane kwenda kantini ya Kampuni, Recho alikuwa na tabasamu muda wote , alifurahia uwepo wa Roma kwenye idara yao, kwani hakukuwa na mwanaume hata mmoja kitendo kilichompelekea kukosa kampani.
“Sasa mrembo sijabeba hela utanilipia basi”
“Usijali , kampuni hii ina wajali wafanya kazi hivyo kuna chakula cha bure”
“Kumbe..!!”
“Ndio” Walikuwa wakiongea huku wakitembea na ile wanafika kwenye lift walimkuta Nasra na waliingia huku Roma kama kawaida yake alimkonyeza Nasra na Nasra alietua mdomo ila Roma hakujali.
“Nasra unaonaje tukienda kukaa meza moja na Roma”Nasra alimwangalia Roma na Roma aliachia tabasamu.
“Umeongea pointi ya maana Recho, ni vizuri tukila pamoja au unasemaje mrembo Nasra..”
“Sawa.. ila punguza kuongea kama uko mtaani hapa ni kazini”.
“Ndio Tabia yangu unizoee na isitoshe sina nilipokosea ni kweli wewe ni mrembo”Recho na Nasra waliangaliana.
Baada ya sekune chache walifika chini kabisa ya Kantini na walichukua sahani zao , Roma alichukua sahanni mbili na kujaziwa zote huku akiwafanya wadada wamshangae , na walizidi kumshangaa Zaidi alivyoanza kula.
“Utakimaliza chote hiko Roma..?”
“Ndio mimi napenda sana kula”Aliongea na wakati huo mara waliingia warembo wawili , waliofanya hali ya hewa ya hapo kantini ibadilike , mrembo wa kwanza alikuwa ni Dorisi na wapili alikuwa ni Edna CEO.
Edna ndio wa kwanza kumuona Roma , alimwagalia namna alivyokuwa amezungukwa na wanawake huku akila bila wasiwasi na kujiwazia huyu mtu kawezaje kutengeneza marafiki ndani ya muda mfupi.
“Romaa..”Aliira Doris na Edna alishangaa na Roma alimkonyeza Dorisi na kumfanya acheke huku Edna akizidi kushangazwa na vitendo vya Roma na kuchukia zaidi.
*****
Abuu hakuwa tayari kumuacha Edna kizembe hivyo , alijua namna ambavyo alihangaika juu yake , aliona itakuwa ujinga sana kumwachia mtu kama Roma kumchukua mwanamke wake kizembe, lakini pia Abu alikuwa akitakiwa kuhakikisha anaingia kwenye kampuni ya Vexto ili kukamilisha mipango ya baba yake na pia kukamilisha mpango wa The City Master(Doni).
Unajua licha ya Abu kulazimishwa kukamilisha mpango wa kumuweka Edna kwenye mikono yake na kulazimishwa na baba yake kuhakikisha swala hilo linafanikiwa , hakuwa akimjua mtu anaeitwa The Done au The City Master.
Mara ya kwanza kusikia jina la mtu huyu ni kutoka kwa baba yake , miezi sita baada ya yeye kukabidhiwa kiti cha Uraisi wa makampuni ya JR.
“Sikia Abu sasa umekuwa CEO wa makampuni haya na najua fika una uwezo mkubwa wa kuyaongoza haya makampuni , na siku zote nilikuwa nikikufundisha kufanya kazi kwa kufuata sharia za nchi , lakini kuna jambo pekee ambalo sikuwa nimekueleza”Aliongea Mzee Alex siku moja akiwa na kijana wake Abuu kwenye kampuni alivyomtembelea.
“Katika ulimwengu wa kibiashara kuna vitu vingi unapaswa uvijue , vile vinavyoonekana na vile visivyoonekana”
“Unamaanisha nini mzee?”
“Kuna ulimwengu wa biashara unaonekana na kuna ulimwengu wa kiabiashara usio onekana , licha ya kuonekana ama kutokuonekana hivi vitu vyote vinaenda sambamba ,yaani biashara zisizo onekana unaweza kuziita zile ambazo si halali kisheria,nafikiri ushawahi kusikia Black Market?”
“Ndio nishawahi kusikia”
“Good! , basi kwa kukurahisishia kuelewa ni kwamba Black markert ni sehemu tu ya ulimwengu wa biashara zisizoonekana” Abuu alitingisha kichwa kuonesha alikuwa anamuelewa vyema baba yake mlezi.
“Hii kampuni usione imekuwa kubwa hivi kwa miongo kadhaa tokea kuanzishwa kwake , yote haya niliweza kuyafanikisha kwa kuhakikisha ninajiweka katika uwiano kati ya ulimwengu wa biashara unaonekana na ule usio onekana, na kwakuwa wewe ni mrithi niliekuchagua basi hili unapaswa ulielewe na ndicho kitu ninachokufundisha sasa”Abuu aliitkia kwa kichwa.
“Watu pekee wenye nguvu ndani ya ulimwengu huu usionekana hapa nchini ni The Doni au The Master , unaweza kumuita wewe mwenyewe kwa namna inayokupendeza”Abuu alishangaa .
“The Doni?”
“Nfdio huyu ni mtu pekee ambae hata mimi mwenyewe sijawahi kuua jina lake halisi , ila ninachojua huyu mtu katika ulimwengu unaonekana ni moja ya wanasiasa wakubwa sana ndan ya taifa hili , lakini katika ulimwengu usionekana ni mfanyabishara mkubwa”.
“Kwwanini unaniambia haya mzee??”
“Nakuambia haya kama nilivyokwisha kukuambia awali kwamba ukitaka kuendesha biashara kubwa kama hii na ifanikiwe unatakiwa kuwa na uwiano wa mambo yote mawili yaani ni nikimaanisha unatakiwa kujiweka kwenye usawa katika ya ulimwengu wa kibishara unaonekana na ule usio onekana , bila hivyo utaishia kuwa mfanya biashara mdogo na wakati , hivyo basi hakikisha swala la kwako na Edna linafanikiwa kwa asilimia mia moja kwani ni swala ambalo pia limepewa Baraka zote kutoka ulimwengu wa kibiashara usio onekana”.
Abuu alishangazwa na maneno hayo ya baba yake , aliona swala la yeye kumpata Edna ni swala ambalo ni Zaidi ya biashara za baba yake , kitendo cha kusema mpaka The Doni anataka swala hilo lifanikiwe na macho yote yapo kwake kufanikisha swala hilo lilimshangaza.
Hayo ndio yalikuwa mazungumzo ya Mzee Alex na Abuu miaka miaka kadhaa nyuma , abuu hakuwa akimjua The Doni na alichokuwa akijua kuwa mtu huyo alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa kwenye ulimwengu usiooonekana , lakini pia ni mwanasiasa mkubwa nchini katika ulimwengu unaonekana , mtu huyo ni nani?, kwanini tageti yao ni Edna na kampuni yake , kuna nguvu gani ipo ndani ya kampuni ya Edna ? yaliokuwa ndani ya kichwa cha Abu na kadri alivyokuwa akifkiria maswala hayo ndivyo alivyozidi kutaka kujua Zaidi aliokuwa hayajui.
“Hakikisha swala hili linafanikiwa kwa namna yoyote ile , kama utashindwa kumpata Edna chukua kampuni yake , mpango wako B unaonekana kuwa mzuri , lakini pia nataka ujiandae kwa mpango mwingine kama huo hautafanikiwa”
“Sawa baba”Abuu alikumbuka maneno ya mwisho wiki siku chache zilizopita baada ya kumueleza mpango B
“The instinct of person wanting to know what he/she doesn’t know its what makes a human” kwamba ile hali ya mtu kutaka kujua kile asichojua ndio kinamfanya mtu kuwa binadamu, na kwa upande wa Abu alitaka kujua hivyo kwenye moyo wake aliamini jambo pekee ambalo litamuwezesha kujua asichokijua ni kuhakikisha Edna anakuwa chini yake , alimchukulia Edna kama ‘Portal’ ya kuingia ulimwengu usioonekana.
Abu anaonekana akiwa ndani ya ofisi yake kubwa hii iliokuwa ikiwakilisha ukubwa wa makampuni ya JR kutokana na muonekano wake wa kifahari, wakati akiwa anaendelea na majukumu ya kazi aliingia Marasta ndani ya ofisi hii na kumfanya Abu amwangalie.
“Bosi tayari nishatafuta vijana watakaomaliza mpango B usiku wa leo”.
“Good , Sitaki uzembe kwenye mpango huu kabisa , nataka ufanikiwe kwa asilimia mia moja hivyo hakikisha wewe na wenzako mnakuwa makini”
“Sawa Boss”Aliitikia Marasta na kisha alitoka huku Abuu akiinuka na kulisogelea dirisha , baada ya kuangalia kwa madakika kadhaa nje ya jiji hili la Dar alitoa simu yake na kupiga namba.
“Kila kitu kipo tayari jiandae kwa ajili ya ukamilishaji wa Plan B”.Na kisha akakata simu.
Comments