Saa kumi na mbili na nusu Roma alinyanyuka na kujivuta kisha akashuka chini kwenye chumba cha mazoezi kwa ajili ya kupasha mwili joto , wakati akiendelea kuchukua mazoezi , alikuwa akikumbuka vyEma usiku wa jana alivyoumaliza na yule mwanamke ambaye hakuwa akimjua hata jina Zaidi ya kumnyandua.
“Nadhani hatutaonana tena”Aliwaza Roma
Saa moja kamili Roma alikuwa ashamaliza kila kitu na alikuwa mezani akinywa chai yeye pamoja na Edna kwa ajili ya kuelekea kazini.
“Wife mbona unaniangalia hivyo”
“Hivi Roma tokea uanze kazi umefanya nini ndani ya kampuni?”
“Sina nilichofanya Zaidi ya kucheza gemu mke wangu , sijui cha kufanya kama vipi nipe kazi hata ya ulinzi nifanye hio kuliko ya kukaa kwenye meza”Edna alishangaa ila hakuongea kitu , aliendelea kunywa chai na alimaliza wa kwanza akimuacha Roma.
“Usisahau leo kuna sehemu tunapaswa kwenda, nitamwagiza Suzzane akuletee nguo za kuvaa”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae.
“Mke wangu nguo si ninazo kuna ulazima gani wa nguo zingine?”
“Fanya kama nilivyokuambia ,acha maswali mengi”Edna hakutaka kuongea Zaidi na Roma alimuaga Bi Wema na kisha ndani ya Sekunde chache Roma alisikia mngurumo wa Gari ukipotelea nje ya geti.
Roma na yeye baada ya kumaliza kunywa chai , alitoka na kuingia kwenye gari yake kuelekea kazini.
“Nikifika nipakue mtandaoni Gemu lingine lile limenichosha sina ninachojua mimi kuhusu kazi za kukaa ofisini najua kurudha ngumi tu na kuua”Aliwaza Roma huku akikanyaga pedeli kuelekea kwenye kampuni.
Roma alifika na siku hii Recho alionekana kuchelewa kufika kazini kwani Roma hakumkuta,wakati Roma anawasha Tarakishi yake kwa ajili ya kupakua gemu , mara aliingia Doris akiwa ni mweye kununa , baada ya kumfikia bila hara ya salamu alimpa Roma Tablet alioishika mkononi na Roma aliichukua na kuangalia baadhi ya picha zake zikiwa mtandaoni.
“Huyu mwanamke kumbe alikuwa waziri , mbona mdogo hivi”Aliongea Roma kwa sauti na kumfanya Doris azidi kufura kwa hasira.
“Usiniambie huyu ni wewe kweli?”
“Bebi Doris ni mimi ndio, si unaniaona kabisa hapo kuna kipi cha kuficha sasa”Aliongea Roma na kumfanya Dorisi azidi kushangaa inakuwaje huyu mwanaume hata kujitetea hafanyi , maana kwa alivyokuwa anawajua wanaume lazima wangeanza kutoa sababu ila kwa Roma yeye alikiri.
“Bebi Doris huyu mwanamke alikuwa mrembo ila sikumdhania ni Mbunge”Doris alimwangalia Roma kwa hasira na kisha bila ya kusema neno aliondoka na Roma hakujali , aliendelea kupakua gemu lake kwa aili ya kuendelea kucheza.
Ndani ya ofisi ya CEO Dorisi aliingia na kumkuta Edna akiwa anaendelea na kama kawaida yake mwanamke huyu kwa uchapaji kazi , baada ya Dorisi kumfikia.
“Bosi umeona taarifa ya Roma inayozagaa mtandaoni?”
“Hapana sijaona”Aliongea Edna na Doris alimkabidhi Edna ile tablet na Edna aliangalia kwa muda huku uso wake ukijikunja kiasi.
“Kumbe alivyoniaga anatoka kidogo alienda kukutana na huyu kimada , mwanaume Malaya huyu”Alijiwazia Edna na kisha alimrudishia Doris Tablet yake.
“Hii sio nzuri kwa image ya kampuni Edna”
“Doris haya ni mambo binafsi ya Roma na wala hayahusu kampuni hivyo swala hili achana nalo na kaendelee na kazi”Aliongea Edna na Dorisi aliondoka huku akionekana ni mwenye hasira kweli .
Baada ya Dorisi kuondoka Edna alijikuta akivuta pumzi na kuangalia mlango aliotoka Edna.
“Maskini hata Dorisi kashaingia kwenye mtego wa huyu mwanaume”Aliwaza na kisha akanywa kahawa kidogo na kuendelea na kazi.
*****
Upande mwingine ndani ya mji wa Mheshimiwa Mstaafu sehemu iliokuwa ikifahamika kama Village G alionekana mheshimiwa Raisi mstaafu bwana Kigombola Hamisi Hamisi akiwa ameketi kwenye sofa za bei ya hali ya juu kwenye jumba lake hili la kifahari ndani ya kijiji hiki , muda huu ilikuw ni asubuhi ya saa nne akiangalia runinga huku akipata chai yake taratibu.
Wakati mzee huyu mwenye mvi zilizoacha uwararaza akiendelea kuangalia runinga mara aliingia moja ya Sekretari wake na kumsogelea.
“Mheshimiwa kuna taarifa hapa nataka kukutaarifu juu ya Madam Neema”
Mheshimiwa alichukua ile simu ya Iphone kiana huyu aliokuwa ameishikilia na kuanza kuangalia picha zilizokuwa zimetumwa kwa njia ya Watsapp , Moja ya picha hizo zilimuonesha Roma akiingia ndani ya chumba na Neema huku wakiwa wameshikana viuno.
Mzee huyu mara baada ya kuona picha hii alionekana kukunja sura kwa hasira kali na kisha alichukua kikombe kilichokuwa na chai mbele yake na kunywa kidogo na kisha alimgeukia huyu bwana.
“Erick nataka taarifa zote za huyu mwanaume kwenye hizi picha kabla ya saa saba mchana”
“Sawa mheshimiwa”
Neema Luwazo kwa wale wasio mfahamu ni kwamba mwanamke huyu ni moja ya wanawake maarufu sana ndani ya ulingo wa siasa , moja ya sifa kubwa iliomfanya mwanamke huyu kuwa maarufu ni uzuri wake aliokuwa nao.
Kabla ya neema kujiingiza katika siasa alikuwa ni msanii na mwigizaji mkubwa sana lakini pia ashawahi kushinda shindano la umiiss miaka kadhaa iliopita.
Kipindi cha uongozi wa mheshimiwa Kigombola ndio kipindi ambacho Neema kwa mara ya kwanza alipata uteuzi na kuwa mkuu wa wilaya ndani ya jiji la Dar es salaam , uteuzi ambao ulianza kufanya watu wahisi kuna kitu kinachoendelea kati ya mheshimiwa Kigombola na Neema.
Licha ya tetesi hizo zilizokuwa zikisambaa mtandaoni , hakukuwa na ushahidi wowote wa kuthibitisha taarifa hizo na hata pale Neema mwenyewe alivyoulizwa alisema.
“That is just Groundless Rumors na siwezi kuzungumza lolote kwani sipo kama watu wanavyonifkiiria , nimefikia hapa kutokana na juhudi zangu mwenywe”Hilo ndio jibu ambalo alilitoa Neema miaka kadhaa nyuma , lakini jibu hili pia lilionekana kuwa na mashiko kwani licha ya mwanadada huyu kuwa mkuu wa wilaya , lakini pia alisifika kwa kuwa na mali nyingi sana ambazo alirithi kutoka kwa wazazi wake miaka kadhaa baada ya wao kufariki katika ajali ya ndege.
Utajili wa Neema ulikuwa ni kiasi cha dola za kimarekani milioni 570 wakati akiwa anarithi mali zote za wazazi wake kama mtoto wa kipekee alieachwa duniani.
Baada ya miaka kadhaa ya kufanya kazi Neema alizidi kujizolea umaarufu mwingi kutokana na uchapakazi wake , lakini pia uzuri wake uliopitiliza lakini pia utajiri aliokuwa nao ambao ulizidi kuongezeka miaka hadi miaka.
Katika kipindi chote hiko cha kuwa mkuu wa wilaya ,Neema hakuwahi kuhusishwa na mwanaume yoyote yule kutoka nae kimapenzi jambo ambalo lilifanya mashilawadu wengi kila siku kuandika makisio yao ya hapa na pale , lakini tetesi hizo zilikuja kukoma mara baada ya Neema kubeba ujauzito na pale alipohojiwa juu ya baba wa mtoto ndipo alipoweka wazi kuwa baba wa mtoto ni mheshimiwa Kigombola na kipindi hiki mheshimiwa kigombola alikuwa kwenye muhula wa mwisho wa uongozi wake.
Kwanzia hapo , ndipo ilipofahamika Rasmi kuwa Neema ni chombo ya wakubwa na watu wengi walijiweka mbali na mwanamke huyo , hakuna mtu alieweza kumsogelea na kumtongoza Neema jambo ambalo lilimfanya mwanamke huyu kuwa mpweke kiana licha ya kuwa na mahusiano na mheshimiwa.
Baada ya uongozi wa Senga , Neema ndipo alipopata ubunge wa viti maalumu na kuteuliwa kuwa naibu waziri wa Sanaa na michezo , kipindi hiki mtoto wa Neema wa kike afahamikae kwa jina la maarufu la Donyi alikuwa na miaka minne tayari.
Upande wa mheshimiwa Kigombola alikuwa amekufa na kuoza juu ya Neema , alikuwa haambiwei chochocte kuhusu Neema na kutoka na mapenzi yake juu ya mwanamke huyo , alikuwa ameweka watu ambao walikuwa wakimchunguza mienendo yake kwa siri.
Upande wa Neema licha ya kuzaa na mheshimiwa , hakuwa na mapenzi yoyote kwake na kuna tukio ambalo lilimtokea Neema na kumfanya aombe msaada wa Mheshimiwa na hapo ndipo ulipoanza mwanzo wa kulala na mheshimiwa mpaka kupata mtoto Donyi na yeye alimchukulia Kigombola kama ‘stepping stone’ kwenye carear yake ya kisiasa.
Sasa hii ndio maana siku Roma wakati anamsogelea Neema watu wengi walikuwa wakimshangaa kwa ujasiri wake wa kutoogopa kuonekana na chakula ya wakubwa , ila kwa upande wa Roma hakuwa akimjua kabisa Neema kwani hakuwahi kukaa na kuanza kufatilia siasa za Taifa la Tanzania.
*****
Ni muda wa saa kumi na mbili na Nusu za jioni Roma alieonekana kupendeza sana kwa suti nyeusi ya bei ghali , iliochangamshwa na tai , huku chini akiwa na kiatu kikali cha kampuni ya Louis Vuitton pamoa na Saaa ya Rolex mkononi , hakika ungemuona Roma usingemdhania ni yule wa siku kadhaa zilizopita aliekuwa akibeba mizigo.
Dakika chache mbele za Roma kusubiri chini ya eneo hili la Sebuleni akiwa na Bi Wema mara hatua za viatu zilisikika zikishuka kutoka juju na hapo ndipo Roma alipogeuza macho yake na kumuona mwanamke mrembo kama malaika akishuka , huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni mrembo Edna.
Edna alikuwa akivutia haswa , muonekano wa mavazi yake jioni hii ulimfanya Roma kupagawa , bwana huyu alikuwa ameona wanawake warembo ila kwa Edna alikiri alikuwa mzuri tena Zaidi ya mzuri , kila kiungo cha mwanamke huyu katika mwili wake kilikuwa kimepangwa kimpangilio ili kuleta radha ,Edna alikuwa amevalia kigauni flani cheupe cha kampuni yake kilichokuwa na shingo ndefu na kumuacha shingo yake kama ya Kinyarwanda wazi na kumfanya apendezeshwe Zaidi na mkufu wa madini ya Almasi uliokuwa ukimeremeta shingoni kuonekana vyema , kigauni hiki kilikuwa sio kirefu sana na kumfanya miguu yake ya bia ilionona na kuwa na michirizi flani kuonekana vyema , kilichomfanya Edna kuzidi kuwa mzuri ni rangi ya sura yake iliokuwa sio nyeupe wala sio nyeusi , alikuwa na karangi flani hivi kiasi kwamba ukimwangalia baba yake na mama yake Edna kwenye picha ungejiuliza ilikuwaje wakawa na mtoto wa aina hio maana mzee Adebayo alikuwa ni mbaya wa sura
“This is God Masterpiece of creation which he ever did”Aliwaza Roma huku akitabasamu na kumeza mate kwa wakati mmoja akiwa anamwangalia mke wake.
“Mke wangu umzuri sana mpaka nayaonea wivu macho yangu”Aliongea Roma na kumfanya Bi Wema agune na kutabasamu na kwa Edna alionyesha hali ya aibu kwani macho ya Roma yalikuwa yakimtazama sana kwa matamanio.
“Twende tunachelewa”Aliongea Edna na kisha Roma alitangulia mbele kuelekea kwenye magari na kutoa V8 nyeusi ya bei ghari na kuisogeza mpaka katikati ya jumba hili na kisha akatoka na kumfungulia Edna mlango.
“Kuitwa mume wa Edna ni heshima Tosha hata kama haonekani kuwa na mpango wa kunipa kitumbua” Aliwaza Roma na kisha alitoa gari hio taratibu kuelekea ikulu.
Comments