Wakati Roma anatoa gari kwenye Geti kuna hisia flani zilimfanya aangalie nyuma kwenye kioo , kwani alihisi kuna gari ambayo ilikuwa ikiwafatilia, hakujua ni watu gani ila hakutaka kujali sana kwani alijiamini mno .
“Nimeona ile habari kwenye gazeti Roma na nikutahadharishe tu achana na yule mwanamke atakuingiza kwenye matatizo”Aliongea Edna wakati wakiwa wanakaribia ndani ya Lango la ikulu wakisubiria kufunguliwa.
“Hilo lisikupe shida mke wangu”.Edna hakuongeza Zaidi mpaka wanaegesha gari na kushuka chini , huku wakwanza kutoka ni Roma na akakimbilia upande wa kushoto na kumfungulia Edna mlango huku Edna akiweka tabasamu bandia mbele ya watu waliokuwa ndani ya eneo hilo wakiwa wapo kwa ajili ya kuwapokea.
“Fatma kutana na mume wangu anaitwa Roma , Roma huyu ni katibu muhtasi wa ikulu anafahamika kwa Fatuma Adinani”Aliongea Edna kwa tabasamu akimtambulisha Roma mbele ya fatuma ambae alikuwa yupo eneo hilo kwa ajili ya kuwapokea .
Fatuma alikuwa ni mwanamke ambaye kwa haraka haraka umri wake haukua mkubwa sana ni kati ya miaka therathini kupanda , lakini alionekana kuwa na cheo kikubwa ikulu.
“Nafurahi kufahamiana na wewe Fatma”Aliongea Roma na kisha walitangulizana na Fatma kuelekea sehemu maalumu ndani ya eneo hili la ikulu.
Upande wa Roma hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuingia ndani ya eneo hili la Ikulu , lakini alionekana kama mtu ambae alikuwa mzoefu kwani hakuonesha uoga wa aina yoyote ile na hata walivyokuwa njiani pale alipoambiwa kuwa safari hio ni ya kwenda ikulu ni swala ambalo halikumshangaza sana kwani aliamini mke wake ni mtu mkubwa hivyo ni swala la kawaida kwa yeye kualikwa na mheshimiwa kumtembelea Ikulu.
Wafanya kazi wa hii ikulu walionekana kuwa katika kazi zao , huku ulinzi ukiwa umeimarishwa kila kona , jambo ambalo kwa Roma lilimfurahisha.
“Angalau wanajitahidi , licha ya mapungufu mengi”Aliongea Roma baada ya kuongekana kukagua eneo hilo pamoja na ulinzi wake wote.
Chakula cha usiku kiliandaliwa baina ya familia ya mheshimiwa Raisi na mualiko huo hakukuwa wa kikazi ulikuwa ni kama wa kifamilia , kwani hata waandishi hawakuwepo , swala ambalo pia lilimshangaza Roma kuona mke wake kuwa na ukaribu sana na familia ya mheshimiwa Rais.
“Edna karibu mwanangu”Alionekana mwanamke mmoja mrembo wa makamo akiwasogelea wakina Roma , huyu hakuwa mwingine bali mke wa mheshimiwa Raisi Senga afahamikae kwa jina la Damasi Senga.
“Asante Mama”.
“Huyu ni mume wako Doris , jamani unatabia mbaya , umefunga ndoa hata kuniambia mama yako”Doris aliona aibu kidogo.
“Nisamehe sana Mama ila ukweli swala hili lilitokea ghafla sana na ni makubaliano yangu na mme wangu , tumefunga ndoa lakini hata sherehe hatujafanya”.
“Nimekuelewa Doris wala hata usijisikie vibaya , Karibu sana Mr Roma Doris ni kama mwanangu maana mama yake alikuwa rafiki yangu sana tulisoma wote”Aliongea Mama huyu kwa ukarimu wa hali ya juu na kumfanya Roma atabasamu.
“Nashukuru sana kwa kunikaribisha kwa ukarimu”
“Dorisi twendenii tulikuwa tunawasubiri ninyi tu mfike”Aliongea mama huyu na kisha aliongoza njia na kuingia kwenye chumba kilichokuwa kushoto kilichokuwa kimetanganishwa na mlango mkubwa.
Baada ya kuingia hapa ndani ndipo Roma aliposhangazwa na ufahari wa hili eneo , kulikuwa na mpangilio mzuri sana wa samani zilizokuwepo hapa ndani , huku katikati kukia na meza kubwa ambayo ilikuwa imezungukwa na watu watatu wawili mwanaume na mmoja mwanamke.
“Oh!Doris karibuni sana ,tulikuwa tukiwasubiri nyie tu”Aliongea mzee huyu ambaye anafahamika kama raisi kwa waanzania ,lakini ndani ya eneo hili alionekana kama baba wa familia.
“Asante sana Mheshimiwa” huku wakisalimiana .
“Karibu sana Roma jisikie huru kabisa”Aliongea mheshimiwa huyu na kumfanya Roma atabasamu huku akiangaliana na mheshimiwa kiume.
“Ashley kumbe umerudi , sina taarifa zako”.
“Ndio Doris nina siku nne tu tokea niingie nchini”Aliongea huyu mwanamke mrembo huku macho yake yote yakimwangalia Roma , na alionekana ni mtu ambaye hakufurahishwa na uwepo wa Roma hapo ndani na Roma mwanzoni hakumuona Ashley baada ya kukutanisha macho yao ni kama waliwasiliana kwa macho na Roma aliketi karibu na mke wake.
“Ushamaliza masomo yako ya PhD?”
“Ndio nishamaliza”
“Hongera sana ni hatua kubwa umefikia”Aliongea Doris na kumgeukia kijana ambaye muda wote alikuwa kimya akiwa pembeni.
“Denis mbona huwachangamkii wageni kama hujawaona”Denisi alikuwa ni kijana ambaye umri wake hakuonekana kuwa mkubwa sana , alikuwa na rika la miaka 22 hivi na alikuwa chuo mwaka wa mwisho huko nchini Norway.
Denis alimwangalia Edna na kisha aliweka tabasamu feki usoni na kisha akamsalimia Edna na Roma , ila kwa upande wa Roma kuna ambo ambalo aliligundua katika macho ya Denis ila hakutaka kufikiria sana , aliweka kapuni swala hilo.
Basi Roma alitambulishwa kwa mheshimiwa Senga kama mume halali wa Edna na chakula kilifana sana kwani kilienda na stori nyingi za hapa na pale huku pongezi zikielekezwa kwa Edna kwa kupata mume kwani lilikuwa ni jambo la kipekee sana katika maisha ya mwanamke na hakuka aliekuwa anajua kuwa wawili hao walikuwa na ndoa ya mkataba na yote waliokuwa wakifanya ni maigizo..
Mheshimiwa Raisi muda wote alikuwa akimwangalia Roma kama mtu ambaye alikuwa na maswali mengi juu yake , ukweli ni kwamba mheshimiwa Raisi licha ya kutumia ushawishi wake na mamlaka yake kupata taarifa zilizokuwa zikimuhusu Roma lakini hakuambulia chochote .
“Mheshimiwa Taarifa zinazomuhusu Roma zinaonekana kuwa nyeti sana ndani ya shirkika la CIA na wamegoma kutuatia taarifa yake”.Aliongea Kabwe baada ya kuwasilisha utafiti wake aliokuwa ameufanya juu ya Roma.
“ kwa hio unamaanisha kuna taarifa inayomuhusu Roma ambazo CIA hawataki kuzitoa?”.
“Ndio mheshimiwa ni Top Confidential na hata baadhi ya viongozi wa CIA hawana uwezo kuangalia taarifa yake ni baadhi ya viongozi wakubwa tu ndio wenye uwezo huo”Aliongea Kabwe na kumfanya mheshimiwa ashangae Zaidi na kuzidi kujiuliza maswali ya Roma ni nani kiasi cha taarifa zake kufichwa na CIA.
Baada ya kuona swala lake limegonga mwamba aliona njia pekee ni kumkaribisha Edna ikulu kwenye chakula cha jioni ili aweze kuoanana na Roma aweze kumfahamu hata kwakumuangalia.
Ukweli licha ya Senga kumkaribisha Roma ikulu lakini alikuwa akikumbuka vyema kwa kitendo cha Roma kumuita babu, hivyo hakuwa akimpenda kwa dhati.
Baada ya chakula mheshimiwa alimwita Edna kwenye ofisi yake kwa maongozi Zaidi akimuacha Roma akiongea na wanafamilia.
Edna mara baada ya kufika kwenye ofisi ya mheshimiwa , Senga aliingiza mkono kwenye mfuko wa suruali yake na kisha alitoa Flash disk na kumkabidhi Edna.
“Hii inahusu nini mheshimiwa?”
“Ukifika nyumbani chukua muda wako kuangalia kilichomo humo ndani kila kitu kinajieleza ni wakati wako kujua swala hili”Aliongea Mhesimiwa na kumfanya Edna ashangae lakini hakujiuliza maswali mengi aliichukua na kuiweka kwenye mkoba wake.
“Umekutana kutana vipi na Roma mpaka kufikia hatua ya kufunga ndoa?”.
“Ni stori ndefu mheshimiwa, ila naweza kusema ni mwanaume wangu wa kwanza katika maisha yangu na atakuwa wa mwisho vilevile”Snga alishangazwa na jibu hilo la Edna na kisha akatabasamu.
“Unamwamini?”Edna alishangazwa na swali hilo , ila hapo hapo akakumbuka kuwa Roma alionekana kuwa na mwanamke mwingine kwenye mitandao hivyo alijua hueana mheshimiwa atakuwa na taarifa hizo ,ila asichokijua Edna ni kwamba Senga anajua pia uhusiano wa Roma na Edna.
“Kusema ukweli kuhusu kumuamini bado , ila moyo wangu unamuhitai Zaidi kuwa karibu yake”Alijibu Edna.
Mheshimiwa alishangazwa na maneno hayo na kujiuliza Roma ni mwanaume wa aina gani kiasi cha kuliliwa na kila mwanamke.
Huku upande wa Roma muda wote alikuwa akimangalia Ashley kwakumuibia ibia na kwa Ashley alikuwa akimwangalia Roma kwa kuibiaibia.
Roma aliomba kuoneshwa sehemu ya maliwato na alielekezwa na mfanya kazi na hio ni kama ikawa nafasi kwa Ashley kwani na yeye alinyanyuka na kuelekea upande huo huo, huku Denis aliekuwa akionga na mama yake wasielewe kitu baina ya hao wawili.
“Naona ushakuwa mume wa mtu tayari?”Ilikuwa ni sauti iliosikika nyuma ya Roma aliekuwa akikojoa na kumfanya atabasamu kifedhuli.
“Wewe unamuonaje mke wangu chombo kile”.
“Mwanaume unaroho mbaya sana wewe , hivi unajua ni kiasi gani mimi na Profesa Clark tulivyoteseka na tunavyoendelea kuteseka juu yako?”.
“Juu ya Clark , mimi na wewe ni swala ambalo lilikoma nilivyoamua kurudi Tanzania na nadhani itakuwa jambo jema mkiendelea kuheshimu uamuzi niliochukua , sasa hivi nishaoa na nitaishi kumlinda mke wangu na kuishi maisha ya kawaida”.
“Unajidanganya Ramoni Edna sio Seventeen licha ya wao kufanana kila kitu ,Seventeen ashakufa Ramoni”
“Ashley nadhani unakosea sehemu moja , hakuna sehemu ambayo nimesema Edna ni Seventeen , kwangu yule mwanamke ashakufa alivyojirusha baharini kipindi kile na nishaacha kumfikiria katika maisha yangu , Edna ni Edna na nimeamua kuishi naye maisha ya kawaida”Aliongea Roma na kisha kumpita Ashley kurudi alikowaacha wenzake.
“Clark kashapata dawa ya kukutibu Ramoni”Aliongea Ashley na Roma hakusimama alimsikia vyema , lakini aliongeza mwendo na kurudi alikotoka.
Baada ya madakika kadhaa mheshimiwa Senga aliomba kuongea na Roma na Edna bila shida alikubali na Roma aliitwa ofisini.
“Karibu sana Mr Roma”
“Asante sana mheshimiwa , nimeitikia wito”
“Nimekuita hapa tuongee kidogo maana Edna kwangu ni kama mtoto wangu wa kumzaa , na mama yake nafahamiana nae vizuri tu”Roma alitingisha kichwa kukubaliana nae.
“Japo sikufahamu vyema ulikotoka na wapi umezaliwa , ila nataka unihakikishe kwamba Edna atakuwa salama na hataumizwa na matendo yako”.
“Mheshimiwa unaonekana umetafuta taarifa zinazonihusu mimi tayari”aliongeaRoma.
“Ni kweli nimejaribu na inaonekana wewe sio wa kawaida na ndio maana nataka kukupa onyo . lolote likimtokea Edna basi jua mimi na wewe tutakuwa maadui”.
“Mheshimiwa Edna ni mke wangu na swala la kumlinda pia litakuwa juu yangu kama mume hivyo naomba swala hili lisikuumize kichwa , lakini pia unachojaribu kutafuta kuhusu mimi naomba uache na uendelee kuwaongoza watanzania wazidi kupata mema ya nchi”Aliongea Roma na kumfanya Senga aone kweli anaongea na mtu ambae hakuwa wa kawaida , kwani Roma hakuonesha hofu yoyote ile ya woga mbele yake na alikuwa mtu wa kunyoosha maneno tofauti na viongozi wengi walio chini yake.
“Okey ni hayo tu bwana Roma”
“Hakuna shida mheshimiwa naamini na wewe pia utaacha kufukunyua taarifa zinazonihusu” Mheshimiwa Senga aliitikia kwa kichwa na Roma alitoka.
“Fii***ck huyu Roma ni nani kwanini anajiamini hivi?” Mheshimiwa alionekana kuwa mwenye hasira kwa kutokumjua Roma ni nani.
Mheshimiwa alikuwa akitweta kwa hasira kwani katika maisha yake aliamini kama atakuwa raisi basi atakuwa na uwezo wa kuogopwa na kila mtu ndani ya taifa hili , lakini jambo hilo likawa rofauti kwani mpaka sasa amekuwa na watu wawili ambao hawakuwa wakimuogopa , wa kwanza alikuwa ni The Doni na wa pili ni Roma aliejitokeza.
Uliongea nini na mheshimiwa?” Aliuliza Edna baada ya kutoka nje ya geti hili la ikulu baada ya hafla yao kuisha .
“Hehe mke wangu nadhani ushajua alichoniambia”
“Sijui ndio maana nimekuuliza”
“Aliniambia ohh yeye na wewe ni kama mwana na baba hivyo nisije kukuumiza”
“Kama ni hivyo walausijali maana mkataba wetu wa ndoa uko pale pale , baada ya miezi sita kuisha kila mtu atafanya mambo yake”
“Hata usijali”Aliongea Roma huku akiendelea kuendesha gari kwa umakini na ndani ya madakika kadhaa alikuwa mbele ya geti la nyumba , lakini kabla hajaingiza gari ,wakai huo geti likiwa limefunguliwa , mara simu yake ilianza kuita mfululizo na kumfanya Roma aangalie na kuona mpigaji ni Juma , alishangazwa na upigaji huo , kwani tokea siku alivyoagana na Najma hakuwasiliana na Juma
“Juma kuna nini?”.
“Roma Wamemteka Najma ?Ilikuwa ni sauti ya wasiwasi ambayo aliisikia Roma na alijua kuna tatizo.
“Edna naomba ushuke kwenye gari?”
“Nini?”
“Nimekuambia shuka kwenye gari kuna sehemu naenda”
“Yaani uende kwa hawara wako na gari yangu”Roma hakutaka kumsikiliza , alirudisha gari nyuma kwa spidi akitaka kugeuza kitendo ambacho kiliwafanya hata walinzi kushangaa.
“Sawa ngoa nishuke”Aliongea Edna na kuhcukua mkoba wake na ile anashuka tu gari ya Roma ilitokomea kama mshale kiasi cha kumfanya atumbue macho kwa spidi aliotoka nayo Roma.
*****
“Erick umepata taarifa gani inayomuhusu?”Aliuliza mheshimiwa Kigombola mara baada ya Erick kuingia ndani ya ofisi ndogo ya mstaafu ndani ya Village G.
“Mheshimiwa kwa taarifa niliopata inamuonesha Roma ni mbeba mizigo kutoka soko la Kariakoo mpaka siku chache zilizopita”
“Unamaanisha nini mpaka siku chache zilizopita?”
“Roma sikuchache zilizopita alifunga ndao na CEO Edna”
“Niniii!” Mheshimiwa alijikura akishangazwa na swala hilo.
“Ndio mheshimiwa Edna na Roma ni wanandoa”
“Nadhani kuna taarifa nyingine Zaidi ya hio Erick inawezekanaje mbeba mizigo amuoe mtu mkubwa kama Edna bila ya sababu”.
“Mkuu kuhusu hilo sijui , ila taarifa nyingine ambayo imenishangaza inaonesha Roma ni mhitimu kutoka chuo cha Harvard amemaliza masoko katika uongozi wa biashara , lakini pia katika CV yake aliowasilisha ndani ya kampuni yetu , inaonekana anauwezo wa kuzungumza lugha ishirini na mbili”
“Lugha ishirini na mbili , hilo sio jambo la kawaida kwa mtu wa kawaida Erick , watu wa nmna hio huenda wakawa majasusi wanaofanya kazi kwa siri au ni Assasinators”.
“Ndio muheshimiwa nimejaribu kufatilia taarifa Zaidi kuhusu mahali anapotokea na alipozaliwa inaonekana hakuna taarifa hizo”Mheshimiwa huyu alimwangalia Erick kwa muda na kisha akafikiria jambo.
“kazi nzuri Erick unapaswa kwenda sasa , mpaka hapo nitaendelea mwenyewe”
“Sawa mheshimiwa”
Baada ya Erick kutoka Kigombola alitafuta namba ya simu yenye kodi ya nje ya nchi na kisha kupiga simu.
“Mr kigombola it`s pleasure to hear from you after long while”
“It s true mr Keneddy and am so sorry thar I did not contact you for this long but you are one of people that have special place in my life”
“It`s good you realise that , but I presume this call has request you want to ask me”.
“Its true kenneddy , I need all informations regarding someone who graduated at harvad”
“Just give me the name and I will look for it in minutes”
“He is Roma Ramoni he is now living here in Tanzania”
“Okey wait a second I will get back to you”
Mheshimiwa alikata simu akisubiria taarifa hio na alichokuwa anawapendea wazungu nikwamba ukiwaomba jambo hawanaga maswali mengi ,ingekuwa ni wabongo angekuwa ashakuuliza maswali kibao kwa mfano unataka taarifa zake za nini na ilichukuwa dakika chache tu taarifa simu yake ilianza kuita.
“ Yes Kennedy”
“I got info.. about him , it seems odd but it is true there is information regarding him graduating at havard business School”.
“What is odd Kennedy?”
“He was adopted with one of Michigan tycoon in business Mr Robert Eglon from when he was fourteen”.
“So what is Odd”
“There is no information regarding where he lived before being adopted”
“You mean there is no info .. like he was from Tanzania or anything like that?”
“Yes!, that which looks Odds Kigombola”.
Huyu Roma ni nani” Ni swali pekee ambalo liliibuka kwenye kichwa chake maada ya kupataa maelezo hayo kutoka kwa Kennedy , aliemwambia kuwa ni kweli Roma anaonekana kumaliza chuo Harvad lakini pia anaonesha kulelewa na familia ya mfanyabiashara mkubwa huko Michigan Marekani lakini jambo ambalo linaonekana sio kawaida ni kwamba haikuelleweka Roma aliishi wapi kwa miaka kumi na tatu nyuma kwani alianza kulelewa akiwa na miaka kumi na nne.
“Nadhani swala pekee ni kuagiza vijana wangu wamteke ili tumuhoji nadhani ndio njia rahisi”Aliwaza mheshimiwa
Comments