Kwa jinsi Roma alivyokuwa anaendesha gari , kila mtu alishangazwa na uwezo huo , Roma alikuwa akikwepa magari kama chizi kitendo ambacho wengi walidhania ni kama Muvi , dakika chache mbele alikuwa akiingia Mbagala , Roma aliendesha ndani ya mtaa huu uliokuwa na baadhi ya viwanda na kampuni za usafirishaji , lakini ile anakaribia nyumba anayoishi Najma , Alimuona Juma akiwa nje , alisimamisha Gari na kushuka haraka haraka.
“Niambie nini kimetokea?”Aliongea Roma huku akiona baadhi ya watu wakiwasogelea na walionekana kujua nini kimetokea.
“Kuna majambazi ambayo siyafahamu , yamekuja na kunitishia na bunduki na kisha wakamkamata Najma na kuondoka nae , huku wakiniachia maagizo kuwa nikitaka kumpata dada yangu akiwa mzima , niwasiliane na wewe na uende sehemu watakayo niambia”
“Sasa wamekuambia ni sehemu gani?”.
“Hawajaniambia wamesema watapiga simu ndani ya lisaa limoja”Aliongea Juma aliekuwa na wasiwasi huku wapangaji wakiwa wamewazunguka , kuna waliokuwa wakimwangalia Roma kwa wasiwasi ili kuona kama atakuwa na njia ya kumuokoa Najma , ila kuna wale waliokuwa wakishangaa mabadiliko ya Roma.
Baaada ya lisaa ni kweli simu ya Juma iliita na alipokea haraka haraka huku akiweka Loudspeaker na hata Roma kusikia.
“Dogo nadhani ushamwambia muhusika?”
“Ndio yuko hapa”
“Mpatie simu”Ilisikika sauti na Roma aliinyakua kutoka kwenye mikono ya Juma na kuweka silence huku akiiingia kwenye Gari yake na kufunga mlango.
“Ongea”.
“Roma hakikisha unakuja mahali ambapo tunakuambia kwa sasa na uje peke yako , ukifanya ujinga wa aina yoyote kama kutaarifu polisi Najma atakufa kifo cha kikatili sana”Ilisikika sauti hio.
“Nipe simu kwanza niongee na Najma siwezi kuja kabla sijasikia sauti yake mimi sio mjinga kiasi hiko”Aliongea Roma na dakika chache sauti ilisikika kwenye masikio yake.
“Najma uko salama?”
“Roma usije watakuua , wana siraha usifanye wanach..”Alipokonywa simu.
“Sikia Roma eneo ni Vikindu , hakikisha unakuja peke yako”Ilisikika sauti na kumfanya Roma akasirike na hio ni baada ya simu ile kukatwa na Roma hakujiuliza sana alitoa gari eneo hilo kwa spidi kiasi cha kufanya watu watumbue macho.
Roma alikuwa na hasira mno , kwanza kilichomkasirisha ni kwamba watu hao wamemuambia kwenda Vikindu lakini hawakuwa wameeleza Vikindu sehemu gani.
Roma baada ya kuingia ndani ya barabara ya Kongowe , alizidi kuendesha gari hio kwa spidi na ilikuwa na spidi kweli kwani zilikuwa zile gari za gharama ya hali ya juu , alikuwa akiyapita magari kama mwehu kiasi kilichofanya kuwanyanyua polisi wa barabarani.
“Shi**t huyu mpuuzi ni nani huyu anaendesha gari kwa spidi hivi kama hii nchi ya baba yake?”Alionekana mwanamke trafiki akiwa amekasirika mara baada ya kuisimamisha gari ya Roma lakini ilimpita bila ya kusimama na kumuachia upepo tu.
“Huyu hanijui vizuri ngoja nitamkamata tu”Aliongea mwanadada huyu mrembo huku wenzake wakiwa ni wenye kushangazwa na spidi ya gari iliowapita ndani ya eneo hili la Kongowe.
“Mage unaenda wapi?”
“Namfukuzia yule mshenzi, wasiliana na Trafiki wa mbele yetu uwape taarifa juu ya hio gari waizuie “Aliongea mrembo huyu mwenye kalio kubwa huku akikimbilia Pikipiki yake kubwa ya kijapani Kawasaki Ninja H2/R hii ni moja ya pikipiku ya kifahari sana na ni chache sana Tanzania , inaupiga mwingi sana hii pikipiki kwenye spidi , ina Zaidi ya 322bhp na imeingia kwenye kumi bora ya pikipiki zenye spidi sana duniani , thamani yake sio chini ya milioni 100 za kitanzania. .
Haikueleweka ni kivipi mtembo huyu Trafiki anaimiliki vipi kwani ni ya bei kubwa mno.
“Unafikiri ataifikia ile gari?”Aliuliza Trafiki wa kiume mweupe.
“Hio pikipiki ina upiga mwingi sana hio anaweza kuifikia ila inategemea na uwezo wake wa kuendesha”Aliongea Trafiki maji ya kunde.
Ni dakika chache tu Roma alikuwa ashafika Vikindu na kusimamisha gari huku akijiuliza ni uelekeo gani aelekee, alikuwa akiangalia daladala zilizokuwa zikiingia ndani ya stendi , lakini ile anajiuliza simu yake ilianza kuita tena.
Simama kwenye bango kubwa la Tigo hapo Stendi na kuna mtu atakufuata hapo”Roma aliangalia mahali sahihi pakuweka gari yake na kulisimamisha na kisha alishuka na kwenda kusimama chini ya Bango kubwa la Tigo.
“Hey! Brazaaa mambo ni vipi , kuna wana wameniambia nije nikuchukue nadhani wewe ndio Roma”Roma aliitikia kwa kichwa huku akimwangalia huyu kijana ambaye anaonekana kuharibiwa na madawa ya kulevya.
Baada ya dakika chache za kukata kona hatimae walivuka kiwanda kimoja amacho Roma hakukitambua kilikuwa cha nini , walipita upande wa kushoto na kusimama kwenye geti kubwa jeusi na mlango ukafunguliwa na Roma akaingia na hapa ndipo alipojua eneo hili ni la kuhifadhia nondo , kwani zilikuwa nyingi upande wa kulia , ni kama ghala.
Alitembea kwa kuongozwa na kijana huyo huku akiangalia baadhi ya mabaunsa waliokuwa wameshikilia bunduki za SMG wakilinda eneo hili kitendo ambacho kilimshangaza Roma , inakuwaje nhi yenye Amani kama hii kuna watu wanamiliki Siraha kiholela ila hakutaka kujisumbua maaana sio kazi yake, aliingia ndani na hapa ndipo alipomshuhudia Najma aliekuwa amefungwa kwenye nguzo, na kitambaa mdomoni , alionekana kuchoka kweli kweli alikuwa akitoa jasho kiasi kwamba baadhi ya Sehemu za Hijabu yake zimeloana.
Roma alimuonea huruma mrembo huyo kwa mateso aliokuwa akipitia , aligeuza macho na kuangalia mabaunsa haya Zaidi ya matano yakiwa na bastora na kisha aligeuka upande mwingine akimuangalia jamaa ambae alionekana kuwa ndio bosi kwani yeye hakushika siraha yoyote na alikuwa amekaa kwenye kiti na sigara yake mkononi.
“Roma unaonekana sana kumjali huyu mrembo, cheupe dawa mpaka ukajileta mwenyewe”Aliongea jamaa hili huku likionekana kutafuna bablishi.
“Nishafika mfungulieni Najma aondoke , ili tuongee shida yenu na mimi”Aliongea Roma kwa hasira.
“Acha upuuzi wewe , yaani unaniona mimi joka la kibisa , nimlete mrembo kama huyu ndani ya hili eneo halafu nimuache bila hata ya kumuonja”Aliongea Jambazi huyu huku akimshia kidevu Najma na kumuangalia kisha akaanza kumnusa usoni na shingoni.
“Kananukia vizuri na vijdomo vyake vidogo nadhani hata ka ‘K’ kake ni kadogo”Aliongea huyu jambazi mkuu na kumfanya Roma azidi kupandwa na hasira , ila hakutaka kufanya jambo lolote la kijinga kwani alihofia usalama wa Najma kwani watu hawa walikuwa wengi na wote walikuwa na siraha,Najma muda wote alikuwa mwenye kutokwa na machozi , alishindwa kuongea ila alionekana kumhurumia Roma kwani walikuwa wamemziba na matambala.
“Mfungeni kwanza , nataka nimfanye demu wake mbele yake”Aliamrisha na Roma alifungwa na yeye kwenye nguzo .
“Unajua kwanini nina shida na wewe fala?”.
“Wewe ndio umeniita hapa , naona unaanza kuuliza maswali ya kipuuzi”Aliongea Roma lakini alijikuta akianza kupigwa ngumi za Tumbo nyingi za haraka haraka na kisha akamaliziwa na Teke, kiasi cha kukohoa na kutema damu.
“Ulifanya kosa kubwa sana kulala na Rose,Mwanamke ambaye nimemhangaikia tokea anaingia ndani ya hili jiji , na wewe na hako kamashine kako ukajiona kidume, sasa leo nitahakikisha namto**mba huyu demu mbele yako , halafu nitahakikisha hautoki na hiko kibolo chako hapa ndani”Aliongea bwana huyu huku akionekana hakuwa ni mwenye utani kabisa.
“Hahaha .. sasa kama umemhangaikia ulishindwa nini kumpata , acha kuudhihirisha ubwege wako kwangu bwana , wewe ni fala tu”Aliongea Roma kwa hasira na kumfanya bwana huyo awaambie vijana wake wamsulubu Roma , kitendo ambacho kwa Najma kilimuumiza mno kwani ni kama alikuwa akipigwa yeye.
Roma alitema damu kwa mara nyingine na bwana huyu aliridhshwa na kipondo hiko na sasa kazi iliokuwa inafuata ni kukamilisha jambo lake kwa Najma.
“Ukimgusa huyo mwanamke nakuhakikisha nitakufanya kitu ambacho hutokisahau katika maisha yako”Aliongea Roma, kwani licha ya kupewa kichapo cha uhakika lakini alionekana kama hajapigwa vile.
“Ila lile jambazi kuu halikujali sana alimfungua Najma na kisha alimshika mkono kwa nguvu na akaanza kumvuta upande mwingine uliokuwa na maboksi.
“Kitendo kile kilimuuzi sana Roma kiasi kwamba mboni za macho yake zilianza kubadilika na kuwa za kijani na hata wale majambazi wengine walishuhudia hilo.
“Boss!”Aliita jambazi mmoja aliekuwa karibu na Roma , lakini kabla hajajibiwa alijikuta akiwa hewani na hakujua ni kwa namna gani , alipigwa na hapa Roma alikuwa amekata Kamba zote zilizokuwa zimemfunga .
“Mpige Risasi mbona mnamuangalia”Aliongea yule Jambazi kuu , lakini katika hali ambayo hata yeye hakujua imetokea vipi , aliskia sauti ‘Shwaa.. Shwaaa tiii …Aiii, Shwaa… Aiii..’ na mabodigai wote walikuwa chini huku wakiugulia maumivu.
Jambazi kuu alishangazwa na uwezo huo wa Roma na kuanza kutetemeka kwa woga , lakini sio yeye hata Najma alishangaa .
Wakati Jambazi hili kuu likiwa linashangaa , lilijikuta limefikiwa na Roma na kishikwa shingoni na kuning`inizwa hewani kwa mkono mmoja kitendo ambacho Najma ni kama alikuwa akiangalia Muvi za kihindi zile zenye uongo mwingi , yaani unakuta steringi kabeba gari na mkono mmoja.
“Sipendagi kutishiwa kwenye maisha yangu , pili Onyo mara moja ukirudia ni kifo, tatu sipendi watu wanaotumia watu wangu wa karibu kupambana na mimi Sababu hizo tatu zinanipa uhalali wa kukuondoa duniani maana wewe ni takataka”Ilikuwa sauti nzito kama ya Roboti.
“Najma Fumba macho mpaka nikwambie fumbua ”Aliongea Roma kwa sauti nzito na Najma alifumba kweli na ndani ya dakika mbili alimwambia fumbua na hapo ndipo Najma alipopigwa na mshangao , kwani majambazi yote manne yalikuwa yamelala chini huku yakiwa yamefunikwa na maboksi kwenye uso huku Roma akilipapasa lile jambazi kuu , lakini hakuambulia cha maana Zaidi ya pakiti ya sigara za SM na kuzichukua na kuweka mfukoni.
“Hawa wote ni maiti , ndugu zao watakuja kuchukua miili na sijui kama wanasafirisha au wanazika hapa hapa”Aliongea Roma bila wasiwasi na kumsogelea Najma ili amshike mkono , lakini Najma alirudi nyuma kwani alikuwa ni mwenye kutetemeka mno na alimuogopa Roma , hakumuona kama yule Roma aliekuwa akimjua na kumpenda ila huyu ni Roma mwinginekabisa mkatili na muuaji.
“Nifuate nyuma kama unaiogopa”Aliongea Roma na kuanza kupiga hatua na Najma japo alikuwa akimuogopa Roma ila alimkimbilia kwani aliogopa kukaa na maiti na isitoshe ilikuwa ni usiku.
Roma baada ya kukatiza kona ya chumba hiki alimwambia Asubiri kwa dakika chache lakini Najma hakusubiri , aitoka na kuangalia nje na hapo ndipo aliposhuhudia kwani alimuona Roma akitembea kama upepo flani hivi ulioambatana na kivuli cha mtu , na alichoweza kusikia ni ‘Crak shwaa..Aiii, Crak .. Shwaa ..Aii Crak.. Aiii Crak Crack;’.
Majambazi yote yalikuwa chini Roma akiwa ashayavunja shingo , yaani ni kitendo cha dakika moja tu , Roma ashamaliza kazi na aligeuka nyuma na kumuona Najma na kumuita kwa ishara ila Najma alizidi kumuogopa Roma.
“Najma nisamehe sana kwa kufanya mambo haya mbele yako , ila sikuwa na jinsi , sahau kabisa kilichotokea leo na nitahakikisha hakuna mtu anaekugusa tena”Aliongea Roma ila Najma hakujibu kitu aliishia kutoa machozi tu na kutangulia mbele.
Roma na yeye hakutaka kumuongelesha , alijuwa mwanake huyo atakuwa kwenye mshituko mkubwa sana , hivyo aliona muda pekee ndio utakao weza kumuweka sawa.
Baada ya kutembea kwa dakika kadhaa hatimae , walifika barabarani, alimuona kijana ambaye alikuja kumchukua akiendelea na upiga debe na Roma hakumjali sana , lakini ile anakaribia gari lake , aliona matrafiki wawili watatu wameegamia gari yake wawili wakiwa wanawake na mwingine akiwa ni mwanaume.
Na wakati huu macho yake yalikuwa yasharudi kwenye hali yake ya kawaida , na alikuwa Roma ambaye Najma alikuwa amemzoea , sio yule muaaji wa kutisha.
“Jamani habari zenu “Alisalimia Roma kama kawaida yake huku akitabasamu na Mage polisi aliekuwa akimfukuzia , aligeuza macho yake na kumwangalia Roma juu hadi chini, kwa muonekano wa Roma hakuonesha kuweza kumiliki ndinga kama hio na ndio maana baada ya kumuangalia kwa sekunde aligeuka na kuendelea kupiga stori na trafiki mwenzake wa kike huku akimuacha trafiki wa kiume akidili na Roma.
“Jamani mmesimama kwenye gari yangu nataka nikampumzishe huyu mrembo si , mnaona jinsi alivyochoka na pia giza kali hili”Hapo ndipo Mage aligeuka tena na kumwangalia Roma.
“Wewe ndio mwenye hii gari?”
“Ndio mrembo”
“Uko chini ya ulinzi kwanzia sasa , kwa kukiuka sheria za barabarani lakini pia kwa kuidharau serikali”.Aliongea Mage huku akiweka uso wa usiriasi.
“Mrembo nilikuwa na dharula ndio maana”
“Mpuuzi sana wewe , hata kama unadharula gani hii nchi sio ya baba yako kuendesha gari kama kichaa , unataka kusababisha ajali na usiku huu na mipombe yako”Aliongea Mage kwa hasira.
Roma aliona hana cha kujitetea , alimwangalia Najma alivyokuwa amechoka na kumuonea huruma.
“Utaenda na sisi mpaka polisi , usituletee shida kisa unaendesha gari la kuazima, Edwin endesha gari yake mpaka kituoni”Aliongea Mage na kumuamrisha trafiki wa kiume achukue funguo kwa Roma.Trafiki yule alitabasamu meno yote nje .
“Leo naenda kuonja kuendesha huu mchuma , Mungu anipe nini mimi nikimfikisha kituoni hata nikifa nitakuwa na Amani”Alijiwazia huyu trafiki kichwani mwake baada ya kupokea ufunguo
Najma , Roma waliingia kwenye gari na safari ya kuelekea kituoni ikaanza
Comments