Unaambiwa hakuna Trafiki aliekuwa akiwasumbua watu waliokuwa wakipita barabara ya Kongowe kama Mage, huyu Trafiki waendesha daladala na boda boda walikuwa wamembadilisha jina na kumuita ‘Mnaaa’, Mage alikuwa mzuri mno lakini hakuwa akifanania na usiriasi wake akiwa eneo lake la kazi , aliwanyoosha watu kisawasawa.
Mage anamiezi miwili tu tokea aanze kufanya kazi hii ya utrafiki na kilichomfanya kuwa trafiki ni adhabu aliokuwa amepewa , kwani Mage alikuwa ni Koplo polisi ndani ya kituo cha Osterbay jijini Dar es salaam , lakini kutokana na kumpiga mtuhumiwa mpaka kuzimia wakati akifanya nae mahojiano ndio kilichomfanya kupewa adhabu ya kufanya kazi kama Trafiki na kutolewa katika cheo chake.
Mwanzoni mkuu wa polisi alitaka amfukuze Mage lakini alishindwa kutokana na nguvu iliokuwa nyuma ya mrembo huyu , kwani inasemekana baba yake ni mtu mkubwa sana ndani ya ulingo wa siasa.
“Jina nani?”
“Roma Ramoni”
“Umri?”
“Miaka 24”
“Kabila”
“Mhehe”
“Uraia wako” Roma kimya .
“Jinsia yako?”
“Mwanamke”Jamaa yule wa kipolisi alimwangalia Roma kwa hasira na kisha kuendelea kuandika na baada ya dakika chache aliingia kwenye kijiofisi hiki afande mwingine.
“ Afande Dulla ,Mage amesema atadili mwenyewe na mtuhumiwa”Jamaa alionekana kukasirishwa sana jambo hili , kwani kwanza baada ya afande Dulla kuona gari kali ya Roma V8 aliamini huo ni mchongo Mungu amempatia usiku huo na aliona akiacha mchongo huo upite atakuwa fala.
“Huyu Mage ni mnoko sana tokea apangwe ukanda huu hakuna Amani na michongo imepungua”Aliongea Afande Dulla huku akitoka kwa hasira nje,hakuwa na cha kumfanya Mage kwani alikuwa akizijua tetesi kwamba Mage sio mtu wa kuwa nae adui.
Najma alikuwa asharudi nyumbani kwani hakuwa akihusika baada ya kutoa maelezo yake , aliekuwa amebaki kituoni alikuwa ni Roma , lakini jambo ambalo lililomkasirisha Roma ni kwamba Mage alichelewa sana , yaani alifika kituoni baada ya saa moja na Nusu.
“Kwanza huna leseni , pili nilivyokusimamisha ukajifanya mjuaji na kunipita , tatu spidi ya gari yako kwenye barabara hii yenye magari mengi ni kinyume na sheria , mpaka hapo una makossa matatu”Aliongea Mage , lakini wakati huu Roma alikuwa anamwangalia tu mrembo huyu huku akitafakari inakuwaje pisi kama hii ni Trafiki.
“Inakuwaje mrembo kama wewe ukawa polisi ,halafu unaonekana umeanza mzunguko wako wa mwezi jana”.Mage alizidi kukasirika.
“Huyu fala kajuaje nipo kwenye Period na nimeanza jana?”
“Wewe Nguruwe unadhani upo mtaani hapa, au kwasababu unaendesha V8 unataka kujiona upo kwenu hapa?”
“Hehe…Inaonekana nimepatia”Aliongea Roma na ilikuwa kitendo cha dakika tu alisikilizia maumivu kwenye mguu wake maana Mage alirusha buti yake yenye kisigino kirefu na kutua kwenye mguu wa Roma kiasi cha kumfanya Roma ainame huku akisikilizia maumivu.
Baada ya kupishana kwa muda hatimae Mage alimpa adhabu ya Roma kulipa faini milioni moja kwa makossa yake yote matatu.
*****
Ni usiku muda wa saa saba Edna hakuwa amelala, haikueleweka kwanini alikuwa hajalala , ila alionekana ameshikilia kitabu cha kingereza kilichokuwa na Title ‘HOW TO THINK POSITIVE akiwa anasoma , ni dakika chache pekee alizosoma alisikia simu yake ikiianza kuita mfululizo kiasi cha kuichukua haraka haraka ila alipoangalia jina ni ‘Mbakaji’Alikuta akiendelea kuangalia ikiendelea kuita.
Ilikatika na ikaita mara ya pili na hapa hakuwa na jinsi na kuipokea kisha akaweka sikioni.
“Unataka nini?”
“Bebi ,Usiniambie ulikuwa umelala mumeo sijarudi”
“Sema shida yako nina usingizi mimi?”.
“Kuna polisi mrembo hapa anataka kuongea na wewe”Aliongea Roma .
“Hellow! habari za Kiza kinene, nadhani huyu mlevi ni mumeo , basi hapa ni kituo cha polisi Chalambe tunamshikiria mumeo kwa kukiuka sheria za barabarani na kuidharau Mamlaka na atatoka iwapo atalipa kiasi cha milioni moja za kitanzania kama faini”.
“Sawa”Aliongea Edna na kukata simu.
Baada ya kukata simu ile alionekna ni mwenye kukasirishwa na jambo hilo , ila alifikiria kwa dakika na kuona ni jukumu lake kutatua matatizo ya ndoa , kwani licha ya wawili hao kutokuoana kwa mapenzi , ila walikuwa ni wanandoa kihalali na walikuwa na wajibu wa kusaidiana.
Edna alitafuta jina kwenye simu na kisha alipiga , japo muda ulikuwa umeenda sana , lakini simu hio iliopokelewa.
“Nataka aachiwe kwa sasa nadhani unakumbuka nilikusaidia kupandishwa cheo , sasa hivi ni usiku sana sitaki aendelee kuwa kituoni”Sentensi ya mwisho Edna alioongea na kisha akakata simu.
Upande wa huku Mbagala chalambe ,Mage alionekana kuwa ndani ya maliwato huku akiwa ameshusha jezi yake ya kitrafiki huku mkononi akiwa ameshikilia pedi , Alitoa ile aliokuwa amejifunga na kisha akachukua ile nyingine mpya na kuiweka vizuri na kisha akajivalisha vyema nguo yake ya ndani na kupandisha jezi yake hio nyeupe na akanawa mikono na kutupia ile pedi iliotumika kwenye dustibin.
“Hivi huyu choko kajuaje mimi niko kwenye period”Alijiongelesha huku akijigeuza geuza kwenye kioo kuangalia kama ana alama yoyote ya damu inayomuonesha yuko kwenye Period, alijikagua kwenye mpododo wake ambao ni ugonjwa wa wanaume wengi lakini hakuona kitu.
“Au hapa mbele pametuna sana ,Mh! Lakini panaonekana kawaida”Baada ya kumaliza alichukua mkoba wake na kutoka kwenye maliwato.
“Mage kuna simu yako kutoka kwa mkuu”Aliongea Edwin na Mage alipokea .
“Mkuu haiwezekani huyu ni muhalifu na sheria inapaswa kuchukua mkondo wake , kwanini tumuachie”
“Mage nakuambia muachie sasa hivi , huyo mtu uliemshikiria ana koneksheni na wenye nchi, sitaki kuhatarisha kibarua changu ninasomesha bado , muachie haraka , halafu acha ubishi mkuu wako wa kazi akikuambia achia , wewe achia ,nikikuambia jamba jikakamue jamba hio ndio maana ya mwanajeshi kutii amri Ala”Huku simu ikikatwa na Mage alitoa sonyo.
“Edwin mrudishie yule choko vitu vyake aondoke”Edwin alishangaa ila hakuwa na cha kuongea Zaidi ya kufanya hivyo.
“Hey!Mrembo usicheze na wenye nchi”Aliongea Roma ilimradi tu kumkasirisha Mage aliesimama karibu na barabara.
“Siku nyingine nikikukamata nakuapia lazima uozee jela”.
“Hehehe..Sawa bibie , ila naona ushabadilisha”
“Nishabadilisha nini?”Aliongea Mage kwa mshangao na Roma hakujibu aliingia kwenye gari lake na kuondoka kwa spidi huku Edwin akiliangalia gari kwa matamanio .
“Huyu choko ukute mchawi huyu kajuaje nimebadilisha pedi huyu”Alijiwazia Mage huku akijionea aibu , alikiri katika maisha yake ya kibabe kama mwanamke ashawahi kukutana na watu wengi ila hakuwahi kuyumbishwa kama alivyoyumbishwa usiku huo,alikasirika maradufu na alijiapiza siku atakayo mkamata Roma hata kama ana koneksheni atamtia kwanza ukilema na mengine yataendelea.
Ilikuwa ni asubuhi saa kumi na moja Roma alikuwa akikata kiuno huku mwanadada Rose akitoa miguno ya kimahaba ya kila aina , mwanadada huyu mrembo alikuwa mwekundu kama nyanya , kwani alikuwa anakunjwa , aligeuzwa geuzwa kama andazi linalokaangwa huku likirukaruka , alikuwa akibonyezwa bonyezwa kama embe huku ametoa ulimi kama anakata moto ni Zaidi ya dakika sabini zimepita Roma hajafunga goli hata moja huku yeye akipoteza hesabu ya idadi ya magoli aliokuwa ametupia.
“Roma tupumzike kwanza , kuna waka moto”.
“Tulia bebi namalizia chenga ya mwisho nitupie wavuni kama Mayele”Aliongea Roma na ndani ya dakika kumi alikuwa ametupia wavuni na kujitupa pembeni ya Rose.
“Bebi sidhani kama kuna mwanaume anajua kuto**mba kama wewe?”.
“Rose mpenzi usiniambie unawaza kufanya utafiti na ushapata idea”.
“Hahah.. yaani wewe , mimi nimeongea tu”Roma alitabasamu huku akimfinya Rose mashavu na muda huu wote wakiwa uchi.
“Halafu bebi ulitokea wapi jana , mbona ilikuwa usiku sana”.
“Halafu umenikumbusha , hebu kalete kwanza kiberiti nina sigara zangu kwenye suruali”Aliongea Roma na Rose alinyanyuka bila ya nguo na kwenda kuchukua kiberiti , alikuja nacho na kisha alipekua mfuko wa suruali ya Roma na kisha alitoa pakiti ya sigara na kuchomoa moja na kisha akampatia na kisha akawasha moto na kuunguza sigara ile na akaweka kiberiti pembeni na kurudi kwenye kitanda hiki kikubwa , huku Rose akiwa ameshikilia sahani flani ya udongo ,Roma alikuwa akivuta kidogo anaweka majivu kwenye ile sahani.
Ungemuona kitendo anachofanya Rose ungedhania ni wanawake wanaotumika kuwafurahisha wafalme kwenye majumba yao(maids) , hakuwa yule Rose ambae anaongoza kundi la Tembo na kuogopwa na walio chini yake.
“Kuna mpuuzi jana amemteka Najma , na kunitishia Amani huku akijinadi kwamba wewe ni wake na mimi nilikosea sana kulala na wewe”Rose alishangaa lakini pia aliwaza ni mtu gani mwenye uwezo wa kufanya jambo hilo na hapo hapo jibu alilipata.
“Unataka kuniambia Karimu ndio aliefanya hivyo?”
“Sitaki hata kumjua jina ni mpuuzi mmoja hivi mwenye nywele za kisomali”Huku akitoa moshi wa sigara na kufanya chumba kijae harufu ila Rose hakujali.
“Ni karimu bebi huyo , unakumbuka ile siku zile bia za ofa kwenye bethidei yangu , basi yeye ndioe alielipia gharama zote”Roma alielewa.
“Kwa hio ilikuwaje mpenzi?”
“Jibu unalo Rose”Alitoa macho.
“Unamaanisha..”
“Ndio nimemuua na vifaranga vyake vyote nadhani ndugu zake watakuwa wanaomboleza kwasasa kama wamepata taarifa”.
“Ila mpenzi ikijulikana wewe ndio umemuua inaweza ikakuletea shida , baba yake Karim ni meya , lakini pia ni mmiliki wa kundi la Black Mamba ni kundi kubwa sana kuliko la kwangu na linajihusisha na mambo mengi , kama kuuza viungo vya binadamu nje ya nchi , usafirishaji wa meno ya Tembo , Madawa na mengine mengi ambayo si halali katika ulimwengu unaonekana, na huyo Karimu ndio mkuu wa kundi hilo ila maagizo yote anapokea kwa baba yake , lakini pia inasemekana, baba yake Larim na The Doni wanaukaribu ambao unahisiwa kuwa ni undugu”Aliongea Rose kwa kirefu na kumshangaza Roma.
“The Doni?” Alishangaa Roma
Comments