Tembo ni kikundi ambacho kilikuwa kikijihusisha na mambo mengi ndani ya ulimwengu usioonekana,moja ya kazi kubwa ilikuwa ni Smuggling(kuingiza bidhaa mbalimbali kimagendo),Kuuza ngada,na kusafirisha meno ya tembo lakini pia kundi hili kama yalivyokuwa makundi mengine , lilikuwa likitumiwa na viongozi wa juu wa kisiasa na wafanya biashara katika kazi haramu , kama kuua , kuteka na mengineo yanayofanana na hayo.
Katika ulimwengu usioonekana mambo ambayo mengi si ya kihalali kwa kipimio cha haki na sheria katika ulimwengu unaonekana mambo hayo yote ni halali.
Katika ulimwengu usionekana kanuni kubwa ni ‘survive for fittest’yaani ndani ya ulimwengu huo unaishi kutokana na uwezo na nguvu zako za kumtawala mwingine , sasa basi baina ya hizi pande zote mbili , mara nyingi zinaenda sambamba , unaweza usielewe ila viongozi wakubwa duniani pamoja na wafanya biashara wanaelewa sana umuhimu wa huu ulimwengu usionekana.
Hivyo wafanyabiashara na wanasiasa siku zote wanahakikisha kuna uwiano sahihi kati ya hizi pande zote mbili, sasa kwa hapa bongo pia kuna sehemu ya ulimwengu huu usioonekana na raia wake tunaishi nao.
Ushawahi kukutana na mtu hana kazi maalumu mjini , ila yeye anavaa anakula na kutanua maisha kuliko wewe ambaye unahangaika kila siku , basi jua huyo mtu huenda anacheo kikubwa katika ulimwengu huo usionekana , unaweza kuupa majina utakayo , unaweza kuita ulimwengu wa kiza , ila wazungu wanapenda kuita ‘Underworld’ yaani the world of criminals(ulimwengu wa wahalifu) sasa usishangae sana ukaona mwanasiasa anatoka hadharani na anakemea matendo mabaya yanayofanyika ndani ya ulimwengu wa kiza lakini yeye akawa ni moja ya wahusika wa wahalifu hao, hii ndio sababu inayofanya ulimwengu huu kuja kudumu milele na inaweza ikafikia siku ule uwiano ukavunjika na ulimwengu huu ukawa na nguvu na hapa ndipo utaona mambo mengi ya kihalifu yakifanyika katika dunia,wewe ishi ila kuna mambo mengi yanafanyika eneo unaloishi na ni ya kutisha na usifahamu, na hautofahamu kwakuwa wewe upo kwenye unaishi kwa kutazama uhalisia unaonekana lakini yapo mengi yanayofanyika nyuma ya huo uhalisia. Unaouona.
Sasa kundi la Tembo , Black Mamba ndio makundi makubwa yaliokuwa yakifanya kazi ndani ya jiji hili la Dar Es Salaam , yapo makundi mengi ila hayo ndio yenye nguvu huku mmiliki wa kundi la Tembo akiwa ni Rose na mmiliki wa Black Mamba akiwa ni Marehemu Karimu.
“Huyu The Don ni nani haswa Rose?”Aliuliza Roma
“Hata mimi si mtambui , ila ndio mwenye nguvu kubwa sana hapa nchini , hafamiki kwa jina ila inasemakana ni mwanasiasa mkubwa na mfanyabiashara na mimi kabla ya kuweka makazi yangu hapa Dar nilipitia hatua za kuomba ruhusa kwa The Don”Aliongea Rose.
“Hebu niambie kwanza uliwezaje kuweka kundi lako hapa Dar?”
“Ni stori ndefu Roma ila ukweli ni kwamba ,damu nyingi zilimwagika mpaka kupata koloni hili na baadae kuingia mkataba na Black Mamba”aliongea Rose na Roma alielewa anachomaanisha na hakutaka maelezo mengi kwani muda umeenda , Rose alienda kuandaa chai na Roma alijiandaa vizuri na kunywa chai , na baada ya k ushiba , alitoka na kuingia kwenye gari yake.
“Hapa niende moja kwa moja kazini”Aliwaza Roma wakati akipita maeneo ya Rangi tatu sokoni.
*****
Juma alishangaa sana kumuona Najma baada ya kumfungulia Geti , bwana huyu alionekana kuwa na wasiwasi sana wakati wote ambao Najma alikuwa ameshikiliwa.
“Najma uko salama?”Aliuliza Juma , lakini Najma hakuongea kitu Zaidi ya kupita na kuingia chumbani kwake na kujirusha kitandanni huku akianza kulia kwa kwikwi , akiwa amejikunyata.
Jjuma yeye hakuweza kuingia kwenye chumba cha dada yake hivyo aliona jambo pekee ni kutulia , lakini kwa hali aliomuona nayo Najma aliamini kabisa kuna jambo ambalo limemkuta Roma.
“kwa hali aliokuwa nayo Najma lazima Roma hatupo nae tena Duniani na mpango wangu utakuwa umeenda kama nilivyokuwa nimepanga”Aliwaza Juma huku akionekana kutabasamu na kujiona mshindi.
“Ila yale maneno ya Mganga yatakuwa ya uongo yale”Alifikiia Juma maneno alioambiwa siku kadhaa zilizopita na mganga huko Chanika.
Ilikuwa hivi baada ya siku ile Roma kuondoka , swala lile lilimuuma sana Juma , yaani sio kidogo na kilichomuuma yeye lilikuwa ni swala la mafanikio ya Roma , katika maisha yake ashajiwekea kuwa Roma siku zote atakuwa masikini na yeye atakuwa tajiri , lakini mabadiliko yaliotokea ghafla yalimsononesha mno na alikuwa hana Amani hata kidogo katika moyo wake na ndio maana baada ya siku mili zilivyopita alienda kwa mganga chanika.
Mganga Maluweluwe alikuwa akisifika sana upande huu wa Chanika kwa tiba zake zake za kuaminika , watu wengi walienda kwake kwa ajili ya kutatua matatizo yao , sio viongozi wa kisiasa sio wafanya biashara walikuwa wakienda kwa Maluweluwe kwa ajili ya kutatua shida zao.
Sasa na Juma aliaminni swala lake linaweza kutatuliwa na mganga huyu na ndio maana alifunga safari kutoka Rangi tatu na kwenda kwa Maluweluwe .
Ilikuwa asubuhi Juma alifika mtaa huu wa Maluweluwe na kwenda moja kwa moja kwa mganga , Mganga huyu alikuwa yuko vyema sana kiuchumi, kwani katika eneo hilo nyumba yake ndio ilikuwa kubwa tena ya Ghorofa mbili kwenda juu huku ikiwa imezungushiwa ukuta mkubwa, na mafanikio ya Maluweluwe ni kutokana na tiba yake hio ya kienyeji ambayo alikuwa akiwafanyia watu.
Juma alikaribishwa pale na wasaidizi wa Maluweluwe , huku akishangaa baadhi ya magari yaliokuwa hapo ndani ya watu waliokuja kufata Tiba , hali hio ilimfanya Juma moyo wake unyong`onyee na kujiona ni mwanaume mwenye laana , kwani ukilinganisha na watu waliokuwa wapo hapo ndani na yeye , alijiona yeye pekee ndie ambae alikuwa masikini, sasa cha kushangaza Zaidi ni kwamba alikuwa hapo ndani kwa ajili ya kumroga mwenzake ili afanane nae.
Baada ya foleni hii kuisha hatimae Juma ilikuwa zamu yake , Maluweluwe alikuwa Profesheno kwenye kazi yake , kwani alikuwa na mhasibu kabisa na ukishalipia kwa mhasibu unaingia kwenye chumba ambacho juu kabisa kuna kibao kimeandikwa ‘Chumba cha Daktari’.
Ukweli licha ya Juma kumsikia sana sifa za Maluweluwe hakuwahi kumuona , lakini leo hii ndio amemuona na katika akili yake alikuwa akidhania kuwa anaenda kukutana na mzee mwenye mvi , ila Maluweluwe alikuwa kijana ambae kwa haraka haraka ungemkadiria umri wake kuwa miaka therethini kwenda juu.
“Karibu kijana”Aliongea mganga huyu ambae hakuwa na utofauti sana kimuonekano wa kimavazi na mitindo kama wale waganga unaowaona kwenye Bongo muvi , au kama wewe ushawahi kwenda kwa mganga basi utakuwa unajua muonekano wa Maluweluwe.
Basi kama kawaida ya waganga alianza mbwembwe za hapa na pale , na kupandisha mashetai ya kimchongo na kisha alimruhusu Juma kueleza shida yake kwa kina.
“Kuna rafiki yangu juzi juzi hapa kapata mke tajiri , jambo ambalo halijanifurahisha , kwani maisha yake yamebadilika sana, hivyo nimekuja umfanyizie aachwe na azidi kuwa masikini”.Mganga huyu alimwangalia Juma na ujasiri wake na kisha alianza kupandisha mashetani.
“Leta jinaaaa… Leta jinaaaa”Aliongea mganga huyu kwa sauti nzito na kumfanya Juma moyo wake utabasamu kuona yes hapa kafika mahali penyewe maana sio kwa mashetani hayo.
“Anaitwa Roma,, yes Roma Ramoni anaitwa”.Mganga baada ya kufanya mbwembwe zake pale aliita jini lake la utambuzi ili kumpa taarifa zinazomuhsu Roma na ndani ya dakika chache mganga huyu alionekana kutoa jasho.
“Kijana mtu unaetaka kumroga hashikiki ,,,, nasema haogekii , harogekii”
“Unamaanisha nini Maluweluwe?”
“Majini yamekataa kujihusisha na mtu huyo unaweza kuondoka”
“Maluweluwe nishalipia hela yangu , nataka tiba”Juma alijifanya haelewe na kumkazia mganga.
“Tiba sahihi kijana ni kukaa mbali na Roma , ni Zaidi ya mchawi na simuwezi na majini yamekataa kutoa tiba”
HIvyo ndivyo ilivyokuwa huko kwa mganga na maneno hayo yalikuwa yakimfikirisha Juma kwa siku nzima mpaka pale alipokuja kupata jambo jipya.
Juma siku ya pili yake akiwa kazini baada ya kutoka kwa mganga , alifuatwa na bwana mmoja hivi mwenye kijitambi cha pesa, na ni baada ya bwana huyu kuulizia ulizia ndani ya soko hili la Mbagala na ndipo alipokuja kumpata Juma aliekuwa bize kuhamisha magunia ya yeboyebo kwenda kuyahifadhi na muda huo ulikuwa jioni saa moja.
“Sikia nitakulipa mara mbili ya hela unayopata kwa kusukuma hayo magunia”Aliongea bwana huyu ili aweze kupata nafasi ya kuongea na Juma , na kutokana na ofa hio Juma hakukataa na kukubali na kuingia kwenye Gari ya Verosa nyeusi na bwana huyu mwenye kitambi na gari hii ilikuja kusimamishwa mtaa wa Zakiem kwenye mgahawa mmoja hivi pembeni ya barabara inayoenda Kijichi.
“Naitwa Ahmedi ni Meneja mauzo kampuni ya Tigo mkoa huu na nimekuomba kuongea na wewe juu ya mdogo wako Najma”Juma alishangaa ila alitaka bwana huyo aendelee kuongea.
“Sikia Juma nimetokea kumpenda sana Najma na nipo tayari hata kumuoa , lakini dada yako nimejaribu kila mbinu kumpata ila amekuwa mgumu na hio ndio sababu inayonifanya tuwe na haya maongezi , nataka unisaidie kumpata Najma maana kaniambia ana mtu anampenda , lakini anaonekana kunidanganya”.Juma kwanza alishangaaa , lakini alitabasamu moyoni kwa wakati mmoja, kwa bwana kama huyu mwenye pesa zake kumpenda dada yake , Juma mtu aliekuwa mbele yake sio mtu pekee anaempenda dada yake ila aliona fursa Adhimu sana.
“Bro nimekuelewa sana , pia nimefurahishwa na nia yako ya kutaka kumuoa Najma”Jamaa alitabasamu.
“Sasa unanisaidiaje kumpata Najma au ni kweli ana mtu kama alivyosema?”
“Ndio kuna jamaa mmoja hivi anampenda , ila mimi naamini sio upendo ila ni ujinga wa dada yangu tu kwani hajawahi kuingia kwenye mapenzi”Jamaa alitoa tabasamu la ushindi.
“Huyo mtu ni nani na anafanya kazi gani?”
“Huyo jamaa, alikuwa ni mbeba mizigo kama mimi anaitwa Roma , lakini kwa sasa ameoa na haishi maeneo haya..Broo tusiongee mengi mimi nimekukubali bro na Najma ni wako”Aliongea Abuu , lakini wakati wanaendelea kupiga Stori mara aliingia jamaa flani ambae alikuwa na nywele za kisomali hakuwa mweusi na pia hakuwa mweupe sana.
“Karim umejuaje niko hapa?”Aliongea bwana huyu Ahmed akimchangamkia Karim na walionekana walikuwa wakifahamiana.
“Kuna mtu nia miadi nae maeneo haya , ila naona tumekutana”Aliongea huku Juma akimwangalia Karim maana alikuwa akimjua vyema na hakuna ambae hakuwa akimjua Karim ndani ya meneo hayo ya mbagala maana alikuwa akimiliki biashara nyingi.
“Huyu ni kaka yake Najma”Aliongea Ahmedi na Karimu alimwangalia Juma na kisha akatingisha kichwa na wakati huo huo alifika bwana mmoja hivi alievalia kibishoo na kusogea meza waliokuwa wamekaa Juma .
“Vipi Zonga ni taarifa gani unayo , ambayo umesema ni muhimu”Aliongea Karim mara baada ya Zonga kufika .
“Bro huyo jamaa ndio anatoka na Rose”Aliongea Zonga huku akimkabidhi Karim picha , ambayo Juma baada ya kuiona tu aliitambua maana alikuwa amekaa karibu na Karim.
“Huyu Fala anaitwa nani na anakazi gani hapa mjini?”.
“Hana mishe yoyote ya kueleweka ila kwasasa anamke”Aliongea Zonga.
Ahmedi na Juma waliendelea na mazungumzo yao huku wakiacha kumfatilia Karim, lakini wakati wakiendelea kuongea simu ya Ahmedi iliita na baada ya kuona jina la mpigaji alijikuta akikunja sura yake na kunyanyuka na kutoa waleti yake na kumpa Juma nyekundu tatu huku akimpa simu ndogo aandike namba zake za simu.
“Sasa sikia Juma tutawasiliana , Karim ninadharula ngoja kuna mishe niwahi nitakutafuta mida basi”
“Okey poa”Alijibu Karim huku akiendelea kumsikiliza Zonga na Juma alinyanyuka na kutoka nje ya Mgahawa huo na zilipita dakika chache tu Zonga alitoka na kuondoka na baadae kidogo akatoka Karim na kuiendea gari yake.
“Broo”Karim aligeuka na kuangalia mtu anaemwita na alimwona ni kaka yake Najma.
“Vipi?”Aliuliza karim maana hakutaka stori sana maana alimuona Juma wakawaida sana kuongea nae , na bwana huyu alikuwa akijisikia mno na alikuwa akichagua wakuongea nae.
“Namjua huyo Roma , jamaa aliekuonyesha picha na najua namna ya kumpata”Aliongea juma haraka haraka na hapa karim alimwangalia Juma na kuvutiwa na mongezi.
“Ingia kwenye gari”Juma aliingia.
“Unamjua vipi Roma?”
Juma alianza kueleza namna alivyokuja kumjua Roma sikuyakwanza na mpaka Roma alivyopata mke .
“Sasa ni namna gani ya kumpata Roma?”.
“Roma anampenda sana Najma Sana , hivyo kama tutamtumia dada yangu itakuwa rahisi”Karimu aliona wazo zuri kwani alikumbuka maneno ya Zonga kuwa Roma alikuwa akimnyandua Rose mwanamke anaempenda na kumhangaikia kila siku , ila huyo fala anaeitwa Roma anakula bila ya kufanya juhudi yoyote moyo wake uliuma na aliapia kwenye moyo wake kumpoteza Roma Duniani na kubaki na Rose wake lakini alikuwa hajui namna ya kumpata Roma, sasa baada ya Juma kujieleza aliona yes , mpango wake unakwenda kukamilika kirahisi.
“Sasa sikia tutamteka Najma baada ya kumteka tutampigia Roma aje kumuokoa Najma maana umesema anampenda na una uhakika atakuja na hapo tutamkamata Roma”.
“Yes huo ndio mpango wangu bro”Karim alimuona Juma ni asset kumtumia kwenye mpango wake na siku moja mbele mpango ulikamilishwa ,Majambazi yalikuja ndani ya nyumba ya Juma na kumbeba Najma , huku Juma akiahidiwa kuwa Najma atakuwa salama , mpango huo Ahmed hakujua , Juma alitaka kupiga ndege wawili kwa jiwe moja , yaani kwanza Najma ashuhudie Roma akifa mbele yake , pili baada ya Roma kufa itakuwa rahisi kumshawishi Najma kuolewa na Ahmedi na yeye atakuwa na shemeji mwenye pesa na ukali wa maisha utapungua na aliwaza kabisa angemuomba shemeji yake mtaji aanzishe biashara.
Sasa baada ya mpango wenyewe kutekelezwa na Najma kupelekwa Vikindu na Karimu kwa mara ya kwanza kukutana na Najma mwanamke ambaye alikuwa akisikia taarifa zake kwa Ahmed , Karim alishangazwa na uzuri wa Najma kiasi kwamba pepo la ngono lilimvaa hapo na alipanga lazima alalale na Najma baada ya kutekeleza nia yake ya kumuua Roma , hakutaka kujali ahadi yake na Juma kwani alimuona kama kapuku tu , lakini pia hakutaka kmfikiria Ahmedi kwanza alijua uyo mwanamke hampendi hivyo hakuwa na hasara kufanya yeye.
Comments