Roma aliingia ndani ya jengo hili mapokezi na kumkuta mwanadada mmoja alievalia tisheti nyeusi na kofia ya Chepeo ya kampuni ya Nike na mkufu shingoni , mwanadada huyu hakuwa mrembo sana , kwani kwanza alionekana kama wale wanawake ‘matom boy’.
“Nipo hapa kwa aili ya kuonana na kiongozi mkuu wa kampuni ya PANZ”.Yule Dada alimwangalia Roma kwa kumsanifu.
“Wewe umetokea wapi?”.
“Nimetokea kampuni ya VEXTO na nipo hapa kwa ajili ya kuchukua marejesho ya mkopo”
“Okey nenda floor namba nne ndio ofisi ya Chief ilipo”Aliongea huyu mwanadada huku akitabasamu rohoni.
Wakati Roma akielekea juu , mwanadada huyu alipiga simu.
“Chifu leo kaja mwanaume kutoka VEXTO”.
“Mwache aje tumkate Ma**mbu”Yule mwanadada alijikuta akicheka kicheko cha furaha akionekana kufurahishwa na jambo hilo.
Roma baada ya kufika ndani ya hii ofisi kwanza alishangazwa na sauti alizokuwa akisikia , kulikuwa na mlio wa vimashine sio vimashine , ni kama mlio wa wadudu flani hivi.
“Ndio maana wakajiita mapanzi “Aliwaza Roma wakati akiingia ndani ya hili jengo.
Roma alishangazwa na muonekano wa Floor hii , kwanza kabisa hakukuwa na meza kama meza ambazo ungedhania kuwa humu ndani ni kampuni bali kulikuwa na vitanda vya Deka upande wa kulia vitatu , na vyote vikiwa na magodoro ambayo hayakuwa yametandikwa.
Chini kulikuwa na Zulia la rangi ya maua maua , huku wakionekana vijana watano waliokuwa wamekaa chini kwenye hili zulia na katikati yao kulikuwa na kijisturi na kwa haraka haraka Roma aligundua hii sio kampuni kama kampuni, jina hilo la kampuni walipewa ili kulinda kile kinachofanyika , ila hii sehemu aliweza kujua ni sehemu ya kupimia madawa ya kulevya , kwani kwa kutumia pua zake aliweza kuvuta hewa ambayo alikuwa akiitambua vyema ,harufu ya ‘Coccaine’.
“Hey! Jombaa , nadhani mabosi wako wameamua kukutoa kafara mpaka kukuagiza kuja hapa kutudai”Aliongea jamaa mmoja ambae alikuwa na mwili mkubwa sana uliojaa mazoezi na kuonesha dharau mbele ya Roma na wale wengine wakacheka.
“Kino huyu leo Chief atambadilisha jinsia”Aliongea jamaa mmoja mwenye midevu mwembamba aliekuwa akijikuna.
“Sikieni nyie wavuta bangi , nimekuja hapa kuonana na huyo chifu wenu anipe changu nisepe”Aliongea Roma na kuwafanya wale mabwana wamwangalie kwa ujasili wake , lakini waliishia kucheka tena, huku lile jitu lenye miraba mine lilichukua unga kidogo kwenye kucha na kunusa na alionekana kujibusti.
“Aiii .. traaaaa tatatata,,, traaaaa aiiii .. tiitiiii”Yule bwana alionekana kupagawisha na madawa yale na hapa Roma ndipo alipokuja kugundua kwanini alikuwa akisikia sauti kama za Panzi.
Lile jamaa linaloitwa Kino baada ya kuona ashabusti mwili alimwangalia Roma na kisha kumsogelea kwa njia ya kumpiga ngumi.
“Aaargh..”Kino alikuwa amepokea bao la uso lililompelekea damu kuanza kumvuja puani , alijishika puani huku akisikia maumivu yaa ajabu na kisha akagusa zile damu kwa mshangao na kuzilamba huku hasira zikiongezeka maradufu,wenzake walishangazwa na kitendo kile Roma alichofanya kwa Kino
Jamaa baada ya kuona kadhalilishwa na Roma , hasira ziliongeza na kurusha ngumi kwa pupa lakini Roma akaudaka ule mkono na kisha akauzungusha kwa nguvu kiasi cha kufanya Kino azunguke kama anachezeshwa Rumba na Roma alimpiga bonge la teke mgongoni na kwenda kutua kwenye ukuta huku akitanguliza pua ile iliopata majeraha dakika chache zilizopita.
“Maaa … maaa ..aiii”Jamaa alitoa ukulele kwani katika maisha yake haawahi kusukumwa na nguvu kama ile na kujigonga , maumivu yake yalikuwa sio ya kifani kabisa , aliona nyota nyota ,Roma hakumwacha vile vile aliendeleza kipigo na ndani ya dakika chache tu tu wale vijana wote walikuwa wamepiga magoti kwenye zulia hili ,huku kila mmoja akiwa na maumivu , kuna waliokuwa wakitokwa na damu puani , kuna waliokuwa wakitokwa na damu mdomoni , kuna ambaye alikuwa ameshika jicho lake.
“Chifu wenu yuko wapi?”Aliongea Roma huku akikagua madawa yaliokuwa kwenye kijisturi na akachukua unga kidogo na kuvuta.
“Mnavuta mabaki mabaki, halafu nimeuliza Chifu wenu yuko wapi hamjibu, au nianze”
“Chifu yuko chumba chake cha mapumziko m huku akinyoosha uelekeo wa chumba na Roma aliangalia na kuona mlango upande wa kushoto na kuufuata, lakini kabla ya kuufungua aligeuka nyuma.
“Ole wenu mtu yoyote akimbie”Na kisha akafungua na kuingia ndani.
Roma aliangalia chumba hiki na kukuta mwanaume mmoja mwenye mwili wa wastani , akiwa amemwinamisha mwanamke Mbuzi kagoma akisindilia mpini wake.
“Nyie mafala , acheni use***nge, kwani huo upupu niliowapa mtoe nyege zenu hautoshi”Aliongea mzee huyu pasipo kugeuka , alionekana alikuwa akikaribia mshindo na Roma aligundua hilo kwani alitembea na kupeleka mkono kwa nyuma na kushika Dudu kitendo kilichomfanya bwana yule ashituke.
“Uwiiii …. Arghhh.. unaniua wewe k*ma”Alipiga yowe huyu bwana baada ya Roma kuminya dudu yake huku bwana huyu akilala chali kwenye kitanda na mwanamke yule ambaye alionekana kuwa mmama alishangazwa na kitendo hiko cha ghafla.
Roma hakuwa hata na kinyaa licha ya dudu la bwana huyu kuwa na utelezi , baada ya kuona mateso hayo yamemridhisha alimuachia .
“Na wewe ondoka”Aliongea Roma huku akimfukuza yule mwanamke na alichukua nguo zake na kukimbilia uchi nje.
Roma baada ya kumwachia Chifu , alianza kukagua chumba hiki kikubwa kilichokuwa na kabati huku akimpa mgongo chifu ,Roma alifungua kabati moja na kutoa macho baada ya kukuta maburungutu ya hela yamepangwa kwenye kabati hili .
Chifu baada ya kuona Roma amempa kisogo na hakuwa na habari nae , alichukua chupa iliokuwakwenye kijimeza cha kitanda na kumsoglea Roma huku akiwa ni mwenye kujikaza kwa maumivu aliokuwa akisikia .
Ni kama Roma alikuwa anamsubiria kwani ile anamkaribia aligeuka kwa spidi na kumtwanga ngumi ya jicho na kumfanya bwana huyu aone nyota nyota huku akitoa ukulele.
Roma aliendelea na ukaguzi wake , na kuvuta Droo na kuona bastora , aliitoa na kuitoa magazine kwa kitendo cha haraka sana na kuona kuna Risasi.
“Barreta 582 ya 1984” Aliongea Roma aliikoki kwa haraka na kisha akamgeukia Chifu, na kumnyooshea na bwana yule alinwangalia kwa jicho moja na kuanza kutetemeka.
“Unadaiwa kiasi gani na VEXTO?”
“Tulikopa bilioni moja ila tulitakiwa kurudisha Bilioni mbili”
“Sasa kwanini hamjarudisha mpaka sasa?”Aliongea Roma huku akiwa amekalia kiti na bwana huyu akiwa amepiga magoti akimwangalia Roma kwa woga.
“Bossi alitupa maagizo tusirudishe”.
“Bosi wenu ni nani?”Jamaa alionekana kuwa na wasiwasi sana kutaa jina la Bosi na Roma alilijua hilo aliingiza kidole kwenye Triga.
“Naongea usiniue”
“Ongea sasa …”
“Bossi wetu ni Hassani”.
“Acha upuuzi mimi nitamjuaje Hassani , ongea vizuri Hassani ni nani , nataka melezo ambayo yatanifanya nimjue harakaharaka”.
“Ni kiongozi mpya wa kundi la Black Mamba”Aliongea huyu bwana na hapa ndipo alipomkumbuka Karim aliemuua siku mbili nyuma.
“Sasa hapo nimekupata , lakini hujamalizia , huyu Hassani yukoje na kwanini aliwazuia kutolipa hela za Kampini mlizokopa”.
“Sikupewa maagizo mengine , Zaidi ya kuambiwa nisirudishe”Aliongea kwa woga
“Hapa ndani mna kiasi gani cha pesa?”Jamaa kimya na Roma akanyanyika kumsogelea .
“Zipo .. zipo milioni mia nne”.
“Na kwenye akaunti kuna ngapi”Jamaa kimya na Roma alizunguka kwa nyuma yake na kuingiza mkono upande wa kushoto wa mbavu na kumfanya bwana huyu atoe yowe.
“Kwenye akaunti kuna ngapi?”
“Bilioni .. bilioni mbili”Roma alitabasamu na kisha alimwambia bwana huyu anyanyuke na waelekee kwenye ofisi yake ,baada ya kutoka Roma aliwakuta watu wake wakiwa wamekaa vile vile na kuona yes , dozi imewaingia na wamekuwa na Adabu.
Roma alitabasamu baada ya kuona kifaa kama simu cha kufanyia miamala cha Equit bank .
“Tuma pesa zote kwenye akaunti hizi nitakazokutajia sasa hivi?”Aliongea huku akimuonyesha Chifu kwa ishara akae kwenye kiti chake cha ofisi na bwana huyu , alitamani kufanya jambo ila aliogopa”
“Bossi ataniua nikifanya kama anavyotaka?”
“Endelea kufikiria ujinga wako tu , nitakuua mimi sina utani, eniwei labda unaona nafanya utani ngoja nikuonyeshe kama niko siriasi”Aliongea Roma na kisha kwa haraka sana alimshika yule bwana kiganya cha mkono wa kushoto na kilichosikika ni viungo vya Jointi na misuli ikipishana.
Chifu alitoa ukulele wa aina yake kiasi kwamba hata vijana wake wa kazi nje walisikia na kuzidi kumuogopa Roma.
Chifu hakuwa na jinsi , hakutaka kuvunjwa kiganja kingine cha mikono , na alitii haraka haraka na kufanya kama alievyoelekezwa na ndani ya dakika chache , akaunti yake ilisoma Dollara mia nne na akatuma kiasi cha Bilioni moja na mia sita kwenye akaunti ya VEXTO.
Baada ya zoezi hilo kuisha , Roma alimwamuru kijana mmoja aliekuwa na nafuu kidogo na kumwambia aweke hela zote zilizokuwa kwenye kabati kwenye begi na ndani ya dakika chache akawa ashakamilisha kazi yake.
Ila bado hakuwa ameridhika , alivuta faili moa lililokuwa kwenye Meza na kuangalia na hapa akatabasamu.
“Enhe Chifu tumalizie , haya Magari yanayoonekana hapa kwenye hizi karatasi yako wapi?”Aliuliza Roma na Chifu kama kondoo alimwangallia Roma.
“Kwenye Basementi chini”Aliongea na Roma akatabasamu .
“Ongoza njia”
Roma alitoka kwenye hii ofisi na kisha akafunga mlango kwa nje na funguo akiwafungia wale wengine na kisha wakazama kwenye lift na chifu , ndani ya dakika tu walikuwa eneo la chini kabisa ya jengo hili na kwa mtu wa kawaida usingejua kuwa chini kuna Basementi ,tena kubwa kabisa , jambo hili pia lilimshangaza Roma.
Aliona sehemu ambavyo ilikuwa kama Maabara na alijua kwa vyoyvyote hapo ni sehemu ya kutengenezea madawa.
Wakati akiendelea kumfatisha Chifu aliekuwa kwenye hali mbaya ya maumivu ya kiganja na jicho , alisikia sauti ya mguno alipopita kwenye Chumba kilichokuwa kikinekana kufungwa na mlango wa chuma , hisia za Roma hapo hapo zikamwambia kuwa hapo ndani kuna mtu.
“Humo ndani kuna nini,Hebu fungua”Aliongea Roma na Chifu alisogelea chumba hiko na kukifungua kwa funguo iliokuwa ipo upande wa kulia kwenye kiboksi na hapa ndipo Roma alipatwa na mshangao baada ya kumuona mtu aliekuwa hapo ndani akiwa hatamaniki kwa majeraha, alimsogelea mtu huyu aliefungwa kwa Kamba akining`inia , huku mwanga mdogo ukiwa unammulika , alimuinua kichwa chake kwa mikono yake na hapa ndipo aliposhangaa.
“Juma!!!”Aliongea Roma kwa mshangao na akajiuliza inakuwaje Juma akawa yupo mahali hapa , alimwangalia Chifu na kuonekana alikuwa akitaka maelezo.
“Nini kimetokea kwanini yupo hapa?”Hapa ndipo alipopewa mkasa wote na alikuja kugundua kumbe Juma alikuwa akihusika na kutekwa kwa Najma , alikasirika mno na alitamani kumpiga tena Juma , lakini kwa hali ya nusu uhai aliokuwa nayo Juma aliona aache.
“Juma alijichanganya sana kufanya kazi na Karim”Aliongea Roma huku akimkumbuka Najma , alijiuliza mwanadada huyo atakuwa kwenye hali gani, lakini pia alijiuliza kama atakuja kujua kuwa Juma anahusika na kutekwa kwake ingekuwaje.
Comments