Roma baada ya kumaliza kumwangalia Juma alimwambia Chifu amuoneshe Magari yalipo na hapa chifu hakugoma maana ashakuwa mtumwa kwa Roma , na alifungua geti moja kwa Rimoti na hapa ndipo alipoona ndinga nyingi zikiwa ndani ya hili eneo , zilikuwa ni gari ambazo baada ya kuzihesabu haraka haraka zilikuwa kumi na zote zikiwa za kifahari na hazikuwa hata na pleti namba.
Roma aliangalia gari hizo na kisha akavutiwa na gari moja aina ya Aud Q7 toleo la 2021 .
“Bosi wako akija mwambie nimechukua hii Gari na akitaka malipo anifate”Aliongea Roma huku akimpa maelekezo Chifu atoe ufunguo , na funguo za magari yote alikuwa nazo mkononi kabla ya kushuka huku chini.
Dakika chache baadae Roma alitoka nje ya jengo hili la Zera akiwa na begi la hela pamoja na Juma aliempakia nyuma ambae hakuwa akijitambua .
Roma alipanga kumpleka Juma hospitali ya Mgagala Zakhiem ,watu waliokuwa barabarani walishangaa ndinga inayochanja mbuga , tena ikiwa haina hata Pleti namba.
“Kuna watu wana magari na kuna watu wanausafiri” Alisikika kijana mmoja aliekuwa akiuza Matikiti.
Roma ile anafika Misheni ,sehemu ambayo kulikuwa kuna mgawanyiko wa barabara iliokuwa inaelekea Kijichi , alipigwa mkono na Trafiki wa kike na Roma hakutaka kuleta ubishi awamu hii, Trafiki yule ni kama sura yake ilikuwa inakujakuja hivi na kupotea , lakini ile anakaribia ndipo Roma alipomtambua.
Alikuwa ni Mage mwanamke aliemletea shida siku kadhaa nyuma na alikuwa kazini , mzuri kama kawaida lakini kauzu ka ma anafanya kazi Mochwari.
Mwanamke yule aligonga kioo na Roma alishusha na kumwangalia mwanamke huyu kwa tabasamu,Mage alimwnagalia Roma na moyo wake ukalipukwa na furaha.
“Yess huyu choko nimemkamata Tena , gari haina pleti namba na anaendesha anavyotoka , leo hachomoki labda sio mimi Mage”Aliwaza Mage huku akimwangalia Roma kwa hasira .
Kiufupi Mage alikuwa ni mwingi wa hasira , kila siku alivyokuwa akidamka kwa ajili ya kuingia kazini , alikuwa akimuwaza Roma tu , moyo wake uliumkia , kwani katika maisha yake kwanza hakuwahi kudharauliwa , lakini pia hakuwa akipenda kushindwa , Mage alikuwa akiamua kufanya jambo mpaka alione linafikia mwisho wake na zote atahakikisha anashinda.
“Mungu baba naomba yule mtu afanye kosa lolote lile nimkamate , naamini kwa rehema zako baba hujali kile waja wako wanachokuomba , na mimi mja wako nimepiga magoti haya kukuombaili roho yangu inayoumia itulie naomba yule mtu afanye tena kosa na nimkamate mimi AMEN”
Hayo ndio maombi ya Mage ya siku mbili mfululizo kila anapoingia kazini anapiga magoti na kumuomba Mungu juu ya hitaji lake hilo na pia kila akirudi alimuomba Mungu.
Mage alikuwa akiishi Mikocheni kwa Warioba ndani ya Apartment za Ayo na alikuwa akiishi mwenyewe na hata mwanaume hakuwa nae , ila alikuwa na ‘Artificial Male Organ’Ambayo ilikuwa ikimridhisha.
Huyu mwanadada licha ya kuonekana mtu mwema na mpenda haki , ila alikuwa akifanya sana ‘Musterbation’ na viungo bandia na alikuwa ameathirika pakubwa , na ndio maana katika maisha yake hakuwahi kuonekana kuwa na mwanaume , na hata wazazi wake walimshangaa na baada ya kusumbuliwa sana , ndipo alipofanya shauri na kuhamia kwenye nyumba hizo ili apate uhuru wa kujiridhisha , hayo ndio yale ya ndani kabisa anayoyafanya Mage.
Lakini licha ya mambo hayo Maombi yake yakajibiwa kwa namna ambavyo hakutegemea maana ni ghafla sana
****
Mrembo Edna kama kawaida , alikuwa akipiga kazi kama vile hakuwa na pesa , kumbe mwanadada huyu alikuwa Tajiri mwenye pesa nyingi sana kiasi kwamba hata aamue kulala tu mpaka akizeeka hela zake haziishi.
Leo licha ya kuonekana kuwa na mengi ambayo alikuwa kiyafikiria , lakini bado mawazo hayo hayakumsbabishia kutoendelea na majukumu yake ya kazi.
Alionekana kuna karatasi aliokuwa akiisoma kwa umakini mkubwa kiasi kwamba kuna baadhi ya vitu alikuwa akivizungushia kwa wino , na ilionekana hakutaka kabisa kupitwa hata na nukta iliokuwa kwenye karatasi hio
Baada ya kusoma kwa muda kama wa nusu saa hivi , aliinua mkonga wake wa simu na kupiga .
“Doris njoo ofisini kwangu”
Aliongea Edna na kushusha mkonga wa simu hii ya mezani na ndani ya dakika chache Dorisi aliingia ndani ya ofisi hii , akiwa mrembo kama kawaida , huku leo hii akiwa amepigilia suti na miwani ya kimchongo na kumfanya azidi kupendeza.
“Naam Boss”.
“Natarajia kuingia dili nono na kampuni ya YAMAKUZA ya kijapani na leo hii nimepokea mkataba wa kibiashara kutoka kwao juu ya utengenezaji wa Malighafi mpya , ni dili nono sana na sifikirii hata mara moja kulikataa , kama malighafi hizi zikifanikiwa kuingia kwenye soko la ukanda huu wa Afrika, kampuni itakuwa imepiga hatua kubwa sana “Dorisi alishangaa na Edna akaendelea.
“Hili dili litafanyika baina ya kampuni mbili kwa hapa Nvhini yaani ya kwetu na JR , mkataba huu utasainiwa nchini Japani….”Lakini kabla hajaendelea kuongea mara mlango ulifunguliwa, na Nasra na kuingia na wote wakamgeukia Nasra alieingia kwa pupa.
“Nasra kuna nini?”Aliuliza Dorisi akimwangaia Nasra aliekuwa anahema kama mbwa anaekimbizwa.
“Zimeingia bosi..”
“Zimeingia nini Nasra ongea”Aliuliza Edna.
“Muamala wa Dola bilioni moja na nusu umesoma , na umetokea kwa PANZI Security”.
Aliongea Nasra huku akionesha ni mwenye kujawa na furaha mno , hakuamini kama Roma alikuwa amefanikisha jambo ambalo wao walikuwa wamelishindwa kwa kipindi kirefu.
Edna aliachia Tabasamu lakini kwa upande wa Doris hakuwa akielewa chochote , licha ya kujua kuwa Kampuni ya PANZI Security walikuwa wakiwadai kiasi kikubwa cha pesa na walikataa kulipa , lakini muda huo kusikia kwamba PANZI wamelipa alishangaa ilikuwaje na alitaka kuelezwa na hapo ndipo nafasi hio akaichukua mwanadada Nasra na kuanza kueleza .
“Unamaanisha Roma ndio kaenda kufuata hizo pesa?”
“Ndio Dori.. japo sio kiasi chote tunachowadai ukijumlisha na Riba , lakini hela tuliowakopesha imerudi”Aliongea
Doris alimwangalia Edna na kujiuliza kwanini mwanamke huyu alimchagua Roma kwenda sehemu ya hatari kama hio , lakini pia alijiuliza imekuwaje Roma akafanikisha swala hilo , kwani lilishidikana hata kwa sheria.
“Sawa Nasra , utamkabidhi Roma kiasi nilichokuambia kama sehemu ya bonasi ya kufanikisha hili, na unaweza kwenda kuendelea na kazi”Aliongea na kisha Nasra alitoka huku muda wote akimuwazia Roma .
“Mimi nitampa Pongezi kwa kumpa kitumbua changu afokonyoe mpaka achoke”Alijiwazia mrembo huyu wakati akiwa anatoka na tabasamu likiwa nje nje.
“Sasa Doris huu mkataba nataka ukausome , uelewe , lakini nikutahadharishe kwamba mkataba huu utahitaji uwekezaji mkubwa sana Zaidi ya asilimia themanini ya pesa yote nitaiwekeza hapa , hivyo swala hili liwe siri na utaniwakilisha katika kusaini mkataba huu Japani na Roma Atakusindikiza kama mkalimani wako.
Doris alitoa macho baada ya kuambiwa kuwa ataenda na Roma kwenye safari hio ya kuelekea japani kusaini mkataba huo unaohusu mapesa karibia yote ya kampuni.
****
Ni ndani ya makao makuu ya nchi , pembezoni kidogo ndani ya jijji hili mtaa mmoa uliokuwa ukifahamika kwa jina la Magufuli , sehemu ambayo majumba mengi yaliokuwa yakionekana ndani ya hili eneo kuwa ya kifahari ,katika moja ya jumba moja walionekana watu wakiwa wanaingia na kutoka na sio watu tu pia hata magari mbalimbali yalikuwa yakiingia ndani hapa na kutoka na karibia magari yote yalionekana kuwa ya kifahari.
Ndani ya uzio wa jumba hili kulionekana kukiwa na maturubai yaliokuwa yamepangwa kwa ustadi kukiwa na viti vingi vilivyokaliwa na watu ambao walikuwa na mavazi meusi wengi wao , wakiwa na nyuso za huzuni.
Jumba hili lilikuwa kubwa mno na lilionesha mtu anaemiliki hili jumba alikuwa na pesa nyingi .
“Pole sana Meya kwa kuondokewa na kijana wako”Aliongea mkuu wa mkoa wa Dodoma akimpa Meya pole kwa kuondokewa na kijana wake wa pekee.
“Asante sana Temba , inaniuma sana kwa kumpoteza kijana kama Karim , alikuwa nido mrithi wangu”Mzee huyu alionekana kuwa kwenye majonzi makubwa.
Wageni mbali mbali walifika ndani ya hili jumba kwa ajili ya kutoa salamu za rambirambi za msiba ,Mzee Bakari Meya wa hili jiji la Dodoma alionekana kupendwa sana , kwani watu waliokuwa hapa ndani hawakuwa wachache.
Pole zilikuwa nyingi sana na mzee huyu pamoja na mke wake na watoto wao wa kike , walionekana kuzipokea kwa moyo mkunjufu kabisa.
Baada ya dakika kadhaa kupita , aliingia ndani ya hili eneo Abubakari CEO wa JR na alionekana na yeye alikuwa mahali hapo kwa ajili ya kutoa salamu za Rambirambi.
Meya baada ya kumuona Abuu alijikuta akipatwa na hali flani ya tumaini kwenye uso wake , alisalimiana na Abu na kupokea pole kutoka kwa kijaa huyu.
“Washafika?”Aliuliza Abu
“Ndio wapo wote ndani hapa”
“Ni vyema tukianza hili swala kabla hatuaelekea makaburini kumpuzisha kijana maana taratibu za kiislamu za kuzika ni tofauti na za kikristo , hatutakiwi kuchelewesha mwili wa marehemu”Aliongea Abu na mzee huyu alitingisha kichwa na kisha aligeuka na kuangalia upande wa kushoto na kumuona kijana mweusi hivi mrefu alievalia suti mwenye ndevu nyingi kama mtalibani , ila amependeza maana zilikuwa ziking`aa sio kama zile za watalibani , bwana huyu mara baada ya kumuona Meya anamwangalia alisogea mpaka alipo.
“Hassan tuma ujumbe kwa wanabodi na tukutane ndani ya dakika tano ofisini kwangu”Aliongea mzee huyu na Hassani akaondoka .
Baada ya dakika chache Mashekhe walianza kusoma swala ya kuuombea mwili wa Marehemu , lakini ndani ya hili eneo Meya hakuonekana , ila hawakujali kwani waliendelea na shughuli hio.
Upande mwingine ndani ya jumba hili ndani ya chumba kikubwa walionekana watu sita wanaume, wakiwa wamezunguka meza kubwa sana , watu hawa wenye sura ambazo zilionekana kuwa na ukwasi mkubwa uliokuwa nyuma yao , maana siku zote umasikini haujifichi lakini pia utajiri vile vile haujifichi na mabwana hawa walionesha kabisa hali ya pesa katika maisha yao haikuwa ni ya kujificha.
Watu hawa walikuwa wakifahamika kwa majina yao , kwani wote walikuwa na nafasi nyeti serikalini , kuna waliokuwa ni wabunge na mawaziri , kuna waliokuwa ni wakuu wa mkoa na kuna waliokuwa wafanya biashara akiwemo Abubakari Hamad.
“Hili jambo limetuhudhunisha sana ,kuona kijana mchapa kazi kama Karim kufa kifo cha kikatili namna ile”Aliongea mkuu flani wa mkoa.
“Ni kweli kabisa na tupo mahali hapa kwa ajili ya kujadiliana tunafanya vipi ili kuhakikisha tunapoza machungu yetu kwa kulipiza kisasi”Aliongea wazri wa Wwizara Fulani.
“Karim alikuwa ndio nguvu ya Black Mamba mimi nimeumia sana na nipo tayari kufanya lolote”Aliongea mbunge wa jimbo Fulani.
“Nimewasikia vyema waheshimiwa na mimi niseme pia nipo na Zaidi ya uchungu , lakini pia sio mimi mwenyewe pamoja na nyie wote hapa na The Doni pia ameguswa na swala hili sana na yupo tayari kwa kuunga mkono mpango wowote tutakaoupanga juu ya kulipiza kisasi”Aliongea Meya.
“Nadhani uweke mpango wote wazi kwa sasa ili tuone kama unafaa au haufai na kama unafaa una mapungufu gani na ni michango gani tunapaswa kufanya katika kukamilisha huo mpango”Aliongea Mfanyakazi Fulani wa Ikulu na Meya alimangalia Abuu aweke mpango Mezani
“Yamakuza ,,…. Kusanyiko la wafanyabiashara nchini ………”Mpango huu mimi mwandishi wenu sikupata kuweza kupiga chabo ila nilichosikia ni kwamba huo mpango unahusu YAMAKUZA ,pamoja na kusanyiko la wafanyabiashara,Rejea kadi ya mwaliko ya Edna.
“Unahisi Edna hatagundua lolote juu ya hili?”Aliuliza Mkuu wa mkoa Fulani .
“Hawezi umesukwa huu mpango ukasukika na tutapiga ndege mmoja kwa jiwe moja , tutachukua kampuni na tutamuua Roma na kulipiza kisasi”Aliongea Abu na mabwana hawa wote waliridhishwa na maelezo hayo na kuubariki mpango huo kwa asilimia mia moja.
Je ni mpango gani ???”
Comments