Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

Roma  aliona  ana bahati mbaya sana na Mage , kwani kila mara wanavyokuwa wanakutana inakuwa sio kwa heri bali ni kwa shari.

“Naomba ushuke kwenye gari  haraka?”Alimrisha Afande Mage kwa hasira , huku baadhi ya watu waliokuwa karibu na hili eneo wakishangaa , na kilichokuwa kikiwashangaza kwanza kabisa ni  gari aliokuwa akiendesha Roma, walikuwa wakijiuliza  inakuwaje mtu anaendesha gari kama hii halafu  anafanya makosa na kusimamishwa na polisi.

“Nipo na  mgonjwa na siwezi kushuka mpaka nimfikishe hospitalini”Alizidi kumpanisha Mage hasira.

“Unajifanya mjuaji sio,Shuka kwenye gari”Aliongea tena  na Roma alimwangalia Mage na kisha akafunga kioo jambo ambalo lilimkasirisha Zaidi Mage , wakati Mage akifikiria cha  kufanya alishangaa  Roma akitoa gari  kwa spidi  na kupelekea kumpushi Mage na kusogea pembeni.

Watu waliokuwa ndani ya hili eneo walishangilia kwa tukio hilo  kitendo ambacho kilimuongezea Zaidi Mage hasira.

Mage alianza kuifukuzia gari ile kwa miguu kwa  spidi  na kufanya mpododo wake utingishike  pwa pwaa.., lakini alikuwa amechelewa kwani gari ile ilikuwa ikipotelea kwenye macho yake , lakini hakukubali kushindwa , alikimbilia Pikipiki lake la kifahari na kisha kuanza kukimbiza ile gari , na kusahau kabisa kuwa alikuwa akiongoza magari wakati huo . watu waliokuwa pembeni walishangilia

“Sh**t huyu mpumbavu ama zake ama zangu leo lazima nimkamate”Aliongea Mage kwa hasira  huku akifunga helmeti.

Pikipiki hii ilitoa mlio wa ajabu kiasi kwamba iliwafanya watu waliokuwepo  stendi ya daladala hii eneo hili la misheni wapige mayowe ya shangwe  , maana ni tukio ambalo hawakuwahi kulishuhudia na nikama walikuwa wakiangalia muvi ya kimarekani.

“Sema yule mwamba anaendesha ile ndinga ni mwehu na  kakutana na kichaa mwenzake”Aliongea jamaa mmoja   aliekuwa akiuza Samaki.

“Unadhani atamkamata?”

“Athu mimi sidhani kama ataweza kumkamata ila ngoja tuone, kama atakamatwa lazima tutajua tu”Aliongea  bwana huyu huku wakiendelea na kazi zao.

Upande wa Roma alitumia dakika mbili na nusu tu na alikuwa akiingia ndani ya geti la mbele la hospitali hii ya Zakhiem , baada ya kuegesha gari hii  alikimbilia nyuma  na kufungua mlango na kumtoa  Juma na kumkimbiza eneo la Mapokezi  na haraka sana akapokewa na manesi hao na kuingizwa Wodini.

“Amefanya nini huyu?”Aliuliza Dockta lakini Roma hakuwa na majibu ya kueleweka na aliwataka watimtibu majeraha yake kwanza.

Madaktari hawa walishangazwa na alama  zilizokuwa kwenye mwili wa Juma  na kwa kuangalia tu waligundua kuwa  mtu huyo alifanyiwa  vitendo vya kikatili sana ila hawakutaka kulizungumza hili haraka , walichofanya ni kuanza kumuwekea Juma dripu ya maji wakichanganya na Dextrose  ili kumuongezea nguvu  , kwani alionekana kuwa mnyonge sana.

Baada ya Roma kuona ashakamilisha kumkabidhi Juma kwa madaktani , aliona atoke  arudi kwanza kazini ili kukabidhi hela alizokuwa nazo kwenye gari maana zilikuwa nyingi sana na hakutaka kuendelea kukaa nazo.

Lakini ile Roma anatoka tu , aliwekwa chini ya ulinzi na  afande wawili wa kiume pamoja na Mage.

“Upo chini ya Ulinzi  kwa makosa  mawili , la kwanza  ni kuendesha gari bila ya pleti namba , kosa lako la pili ni kuidharau  sheria  ya nchi hii”Roma alimwangalia mrembo huyu  huku akitabasamu na  kisha akafungwa pingu.

“Afande Sepengo  chukua  funguo tukague gari yake , huenda ameficha madawa huyu”Aliongea Mage  na Sepengo alifanya kama alivyoambiwa na  alichukua funguo na  kufungua milango wa ndinga hii,Sepengo baada ya kufungua mlango kwanza alianza kunusa nusa gari hii kama  mbwa.

“Ma**mae  hii gari  inanukia vizuri hii , humu hata ufanyie uzinzi au dhambi yoyote malaika wanaweza wakakukingia kifua  mbele ya Mungu”Aliwaza Sepengo  na huyu Afande alikuwa akifanana na jina lake , kwanza alikuwa na meno yaliopishana ila ya njano  , alikuwa ni kijana ila kutokana na uvutaji wa sigara anaonekana kuwa mzee.

Mage baada ya kuona Sepengo badala ya kukagua anashangaa uzuri wa gari aliona kazi hio aifanye mwenyewe , alilisogelea begi lililokuwa kwenye siti ya nyuma na kisha akalifungua na macho yalimtoka baada ya kuona maburungutu ya hela na Mage alitabasamu.

“Utakatishaji fedha kosa lingine”Mage aliwaza huku akitoa tabasamu la ushindi, lakini pia hakuishia hapo tu , aliendelea kufukunyua begi hilo , kwani kuna kitu kilimwambia kuna jambo la ziada atalipata na ni kweli ile anafungua  kajizipu kadogo , alikumbana na kajimfuko  ka unga unga kama wa chumvi.

Roma alijikuta akishangaa mara baada ya kumuona  Mage akitoka na kajimfuko kaunga na hapo hapo alijikuta akinywea na kuona wale mabwege huenda  walificha unga wao kwenye hilo begi na yeye hakulikagua vizuri.

“Nilijua tu  wewe ni Jambazi  ,Afande Marko huyu tunampeka moja kwa moja kituo kikubwa  cha wilaya Temeke kule”Aliongea Mage na kisha akatoa simu yake ya upepo.

“Naripoti kutoka  Mbagala Zakhem ,Jambazi kuu lipo chini ya ulinzi , Narudia jambazi kuu lipo chini ya ulinzi , tunahitahi usafiri haraka Ova”Aliongea Mage 

“Kwa kulikamata hili Jambazi  nadhani nitapongezwa sana na nitaweza kurudishwa kwenye kazi yangu ya upolisi,Mungu ni wa ajabu sana ,yaani huwa anajibu Maombi kwa namna ambavyo hata hutegemei”Aliwaza Mage huku akimwangalia Roma aliekuwa hana wasiwasi  akiwa amegamia gari.

“Mrembo hio gari inakuja saa ngapi? , nina njaa sio poa”Aliongea Roma na kumfanya Mage amwangalie kwa hasira.

Lakini wakati wakiwa wamesimama hapo ndani , huku baadhi ya watu wakishangaa  mara  alikuja mwanamke na kumkimbilia Roma  na kumkumbatia , ni kitendo ambacho hata Mage hakukiona kilivyofanyika, kwani Roma alikuwa amekumbatiwa na mwanamke mzuri mno.

“Najma … !,Unafanya nini hapa?”Aliongea Roma huku akimshangaa Najma aliekuwa amemkumbatia , kumbatio ambalo  lilimfanya   ahisi  kitu cha tofauti katika mwili wake.

“Roma  kaka .. kaka.. Jumaa kanitelekeza ..Roma.. hihiii hii….”Najma alikuwa akilia kama mtoto,alionekana ni mwenye huzuni kweli.

Unajua nini , Baada ya Juma kumfikisha Najma Hospitalini na yeye kuondoka siku mbili nyuma ,  baada ya vipimo kutoka Najma aligundulika kuwa na Malaria kali , kiasi kwamba ilibidi alazwe kwa ajili ya kupata  dawa kali  za Malaria .

Baada  ya masaa nane ya dozi ya kwanza kuisha  alipatwa na ahueni   kiasi cha kumpelekea kuinuka na kukaa kitako ndani ya wodi hii ya wanawake  ,muda nao ulizidi kusonga na Najma alijikuta akilala tena na kuja kushituliwa na  Mama Debora ambaye alikuja kumtembelea , akiwa amebeba chakula na hakuwa peke yake  alikuwa na mpangaji   aliemleta hospitalini  aliekua akifahamika kwa jina la Mama Bedo.

“Najma Juma alikuja? , nimejaribu kumpigia simu lakini hakuwa akipatikana”Aliongea  Mama Bedo  baada ya kupeana salamu za pole kwa mgonjwa na mama Debora.

“Mh! Hajaja , lakini labda atakuwa kazini kwake”.

“hata kama ndio azime mpaka simu  jamani huku mdogo wake anaumwa  , kukitokea shida  nani wa kuambiwa sasa , halafu pia aliondoka kabla hata vipimo vyako havijatoka”Aliongea Mama Bedo huku akionekana  kusikitishwa na matendo ya Juma.

Walijaribu kujipa sababu ambazo huenda Juma anazo ndio maana hakuwa ameonekana mpaka muda huo , kwa ajili ya kumuona  lakini  muda ulizidi kusonga Juma hakuonekana Mama Debora alienda nyumbani na kurudi tena kumletea Najma  chakula  lakini bado hakumuona .

“Hivi kweli kaka Juma anaweza kubanwa na kazi kiasi cha kutokuja kunitembelea mdogo wake jamani , mpaka muda huu?”Aliwaza  Najma huku akiwa ni mwenye kusikitishwa na  matendo ya kaka yake,Mwanadada huyu hakuwa akijua kuwa kaka yake alikuwa ametekwa na alichokuwa akijua ni kwamba kaka yake alikuwa akithamini mambo yake kuliko yeye  na ndio maana alionekana ni mwenye kulalamika.

Siku ya kwanza ilipita . huku Najma akiendelea na matibabu  na kuanza kupata nafuu , lakini bado mwanadada huyu hakuweza kumuona kaka yake , jambo ambalo lilizidi kumsononesha na kuona kaka yake hakuwa akimjali , aliumia sana moyoni  licha ya Mama Debora kumwambia kuwa kaka yake hakurudi nyumbani kabisa  kwa  Najma  bado aliona kaka yake  alikuwa bize na kazi na wala hakukuwa na jambo ambalo lilikuwa likimuweka bize kiasi cha kutofika hospitalini kumtembelea.

Ile hali  ya Najma kutokumuona kaka yake ilianza kuibua jina lingine katika akili yake na jina hilo halikuwa la mtu mwingine bali ni la mwanaume aliekuwa anampenda  kwa  mapenzi ya Dhati kabisa.

“Roma ndio mtu  pekee anaenijali,amekuja kuniokoa bila ya woga wowote  lakini kaka yangu kuja tu kunisalimia ameshindwa , sasa ndio najua nani ananijali kati ya kaka  yangu na Roma”Aliwaza Najma huku akisahau miaka yote iliopita nyuma  walivyoishi na kaka yake na alichokuwa akiwaza muda huo  ni kwamba Roma ndie anaemjali na kaka yake hakuwa akimjali.

“Lakini Roma  hafananii na nilivyokuwa nikimfahamu ,lakini hapana yote yale yalitokea kwasababu yangu , ananipenda sana na ndio maana alionekana kuuwa , ni hasira tu zile ,Roma sio muuaji  ,Roma sio Mkatili  yote ameyafanya kutokana na hasira , atakuwa ananipenda sana”Hayo ndio mawazo aliokuwa nayo Najma  siku ya pili  yake  baada ya kulazwa muda wa asubuhi.

Yale mapenzi   ambayo alidhania yalipotea katika moyo wake baada ya kumshuhudia Roma akiwa kikatili , yalirudi upya tena awamu hii yalionekana kuwa na nguvu kubwa sana , kiasi kwamba mwanadada huyu alitamani kumuona tena Roma , alikuwa  ni mwenye wasiwasi sana , kwani alikuwa akikumbuka mara ya mwisho Roma alimuacha kituo cha polisi

“Sijui alitoka jamani ?”Roho ya  Najma haikutulia tena  , alikuwa na mawazo mchanganyiko mazuri na mbaya kwa wakti mmoja , lakini mawazo yaliokuwa na nguvu kwa wakati huo ni yaliokuwa mazuri juu ya Roma , alitamani sana kujua  ni hali gani anayo Roma , wakati akiendelea kuwaza alikumbuka simu yake , lakini baada ya kukumbuka  hakuwa akifahamu ni mahali gani ameicha baada ya kutekwa na wale watekaji  alizidi kusononeka.

“Binti hali yako sasa imetengemaa na dozi yako ya  kwanza imekamilika na kwa sasa utatumia dawa za kumeza , hivyo haina haja ya kubakia hapa hospitalini , utaendelea nazo   ukiwa nyumbanni , lakini kama ukijisikia hali yoyote mbaya unaweza kurudi”Aliongea Daktari wa  raundi ya asubuhi na kumfanya Najma apatwe na furaha kwani alikuwa amechoka kukaa ndani ya hii wodi  kwani harufu yake haiukuwa ikimfurahisha  hata  kidogo.

Baada ya Najma kupewa taarifa hio , hakuwa na haraka ya kuondoka  lakini pia hakuwa amelipia  gharama za matibabu mpaka wakati huo na hakuwa na hela ya kutosha , baada  ya kukaa kwa  takribani lisaa akiwa na mawazo ya Roma  pamoja na namna ya kumaliza matibabu hatimae alikuja  Mama Bedo.

“Mama Bedo nisharuhusiwa  tayari , bado kulipia gharama tu za matibabu nirudi nyumbani , lakini hela niliokuwa nayo haitoshi na kaka Juma haonekani mpaka leo hii”Aliongea  Najma na mama Bedo alimhurumia   lakini pia alimlaani Juma kwa kutoonekana ,alimwangalia.

Mwanadada huyu mrembo , mwenye haiba  ya utoto alionekana kuwaza jambo na ghafla wazo lilimuingia kwenye kichwa chake.

“Mama Bedo umekuja na simu?”

“Ndio hii hapa Najma , tena ina salio , unataka kumpigia nani?”

“Rafiki yangu  mmoja  hivi” Aliongea huku akichukua simu  kwenye mikono ya mama Bedo kwa ajili ya kupiga.

“Hellow! “Sauti nyororo ilisikika  upande wa  pili.

“Twin  ni mimi Najma”.

“Haan..jamani shosti  mbona unapenda kunipa wasiwasi namna hio , nimekutafuta siku mbili zote  sikupati hewani”.

“Ni stori ndefu  pacha  na ndio maana nakupigia na simu nyingine , nipo  hospitalini nimelazwa   unaweza kuja  kuniona sasa hivi  , nina shida mpenzi”.

“Naja.. Shida nini  nisubiri  Najna muda si mrefu nisubiri..”Ilisikika sauti upande wa pili  ilionekana kuwa na wasiwasi.

Najma alivuta pumzi mara baada ya kufanya mawasiliano hayo na  kurudisha simu kwa Mama Bedo.

Ni ndani ya masaa mawili waliokuwa wamesubiri mara alionekana mwanamke mrembo sana akiingia ndani ya  hospitali hii na gari zuri sana aina ya  BMW M4 ya pink   na kufanya watu wamkodolee macho , kwani alikuwa mrembo haswa , na wanaume waliokuw a ndani ya eneo hili waliambizana.

“Sema mzee kuna  wanaume wanakojolea  pazuri aisee , yaani  hii pisi ikinipa raundi moja tu  Maisha yangu yatakuwa ya baraka sana”.

“Acha kuwaza sana Shaba , hivyo ni vya wakubwa , usione pisi kama hio inaendesha gari kali  na inapendeza  jua kuna mwamba  nyuma anafanya kazi  kwa  juhudi , Waswahili wanakuambia usione vya elea jua vimeundwa”.

“Ni kweli tupige kazi tu”Hawa walikuwa ni wafanyakazi wa usafi ndani ya  hospitali hii na muda wote walikuwa wakiangalia pisi hio ikipotelea mapokezi  na mabwana hawa waliokuwa wamevalia  glovusi na Mabuti makubwa , waliendelea na kazi yao ya kukusanya takataka.

Ndani ya wodi ya  wanawake aliingia mrembo huyu  huku akitembea kwa madaha kabisa na kusababisha harufu yake ya perfume kali ya  bei ya juu  isambae ndani ya eneo hili , mwanadada huyu alitembea na  baada ya kumuona mtu anaemtafuta  alikimbia  na kwenda kumkumbatia huku akianza kulia na waliambizana kulia hawa warembo wote.

Naam mrembo huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Nasra  Mhasibu mkuu wa  makampuni ya Vexto na inaonekana mwanadada huyu alivyomuacha Roma Mtongani hakuwa akija kuonana na mteja bali alikuwa akija kuonana na Najma.

Wagonjwa wlaiokuwa wamelazwa ndani ya hii wodi walishangazwa na mapenzi yaliokuwepo baina ya wadada hawa warembo , kitendo chao cha kulia hapa hospitalini kilimfanya  Mama Bedo na baadhi ya wagonjwa kuguswa na tukio hilo kiasi cha kuwafanya   watokwe na machozi.

“Nisamehe sana Najma , nisamehe mpenzi , sikujua ulikuwa  unaumwa hivi”Aliongea Nasra  huku akionekana alikuwa ni mwenye huzuni  mno na kuumizwa na kuumwa kwa Rafiki yake

Wawili hawa walionekana kufahamiana sana   sana  na ilionekana sio kufahamiana kwa siku chache  , bali urafiki wao ulionekana ni wa  muda.

Baada ya wawili hawa kubembelezana   hatimae  Najma alianza kumwambia  yaliokuwa yamemtokea  mpaka kupoteza simu.

“Kwa hio unamaanisha The chosen one  ndio alikuja kukuokoa?”Aliuliza  Nasra huku akimtaja Roma kama The Chosen one yaani kwa tafsri ya ‘Aliechaguliwa’ na Najma alitingisha  kichwa.

“How Romantic ….jamanii natamani na mimi initokee Twin”

“Wee ,, muangalie unavyofikiria ujinga sasa , nilikuwa nikiogopa balaa”.

“Hapo ndio penye point sasa Naj.. yaani unatekwa   unaogopa mpaka unataka kujikojolea  halafu pale unapojiona umekata tamaa , mara vuup .. bebi huyo anatoa kichapo  then anakuokoa kwenye mikono ya watekaji .. how Romantic.. haha .,Najma nikwambie tu hakuna  mwanamke ambaye  hapendi  hio Fantansy .. you know I cant  picture how things was ..but I know for sure it was real  amaizing scene .. I wish someday  jambo kama hilo linitokee Naj… Your love Experience is far more  exciting Twin, you should be happy”Mwanadada huyu mrembo alionekana kufurahishwa san ana tukio hilo na alisahau kabisa uhatari ambao ungemkuta  Najma kama tu Roma asingetokea kumuokoa ,Nasra aliegemea upande wa mazuri  yaliomtokea  Najma,

Maneno ya Nasra kwa Najma  ni kama yalilipua bomu la huba ndani ya moyo wa  Najma , mwanadada huyu alijona kama mjinga kwa wakati mmoja , siku zote alikuwa ni mwenye kujifunza kutoka kwa Rafiki yake huyu  , alichojilaumu ni pale kuegemea upande wa mambo ya kutisha yaliotokea katika tukio lile na kuacha yale mambo mazuri  maana ni kweli Roma alihatarisha Maisha yake  kwake.

“Twinie .. I have always been one to tell you to focus only to  good thing  that happn around  you .. I know you were frightened  at the moment but  the Ending was good .. ungewezaje kujua ni kiasi gani The Chosen anakupenda  ,, hii yote ni mipango ya Mungu Naj.. be happy” Maneno aliokuwa anaongea mwanadada huyu  yalionekana kumuingia vizuri  na alijikuta akianza  kumuwaza  Roma tena na kuona ule uuaji wa Roma ni Swaga  na sasa   zilikuwa zinausuuza moyo wake.

Wawili hawa walipiga stori za hapa na pale  , mpaka pale Nasra alivyopigiwa simu kurudi kazini haraka kuna  dharula inayomuhitaji  na kwakuwa alimuona Najma  alikuwa  amepona , wasiwasi wake ulipungua , alilipia gharama zote na kisha  akaaga huku akimwambia asiwe na wasiwasi kaka yake anamjali   na asimfikirie vibaya .

“Kila siku ninapopata shida   inayosumbua akili yangu , nikionana na  Nasra  huwa Napata kitu kipya na wasiwasi wote kuisha ,Nasra kabarikiwa kweli kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuingoza akili yake ,  tokea utoto wetu  nilipokutana na Nasra  nimekuwa mtu wa furaha sana kuwa na Rafiki kama yeye” Aliwaza mwanadada huyu  mrembo sana ambaye  hajawahi kuwa na mpenzi kwenye Maisha yake Zaidi ya kuwa na Roma ambaye alikuwa akimzingua .

Najma hakuwa amemueleza  Rafiki yake kama Roma alikuwa ameoa na ana mwanamke ambaye alikuw aamepotezana nae kwa miaka mingi nyuma  , lakini mwanadada huyu licha ya Roma kuwa na mwanamke mwingine lakini bado hakuwa ni mwenye kuacha kumpenda Roma , alimfikiria kila siku na aliamini kabisa Mungu wake hakufanya makosa kumkutanisha na Roma na kwamba siku moja  atakuja kuishi  na Roma kama mke na mume.

“Mpaka sassa nimejua ni kiasi gani Roma ananipenda , na nitaishi kwa kumpenda Maisha yangu yote na nitamlindia heshima na nafasi yake ndani ya moyo wangu”

Aliwaza huyu mwanamke mrembo  wakati akitoka  mapokezi  kwa ajili ya kuelekea  nyumbani kwani walikuwa washakamilisha taratibu zote , lakini ndipo  moyo wa Najma ulipopiga kwa nguvu mara baada ya kumuona  mwanaume  wa Maisha yake  na hakutaka kujiuliza mara mibili  aliona yes , hii ndio Chance  na lazima aitumie vizuri , hakujali Pingu alizokuwa nazo Roma , alichojali ni  kile kilichomjaa moyoni mwake .

Na kama muvi la  kuchi kuchi hotae hee , mrembo huyu  kwa spidi maridhawa kabisa , alikimbia , akakimbia na kwenda kutua kwa mwanaume  , mwambaaa Roma Ramoni .

Je unadhani  ndoto za mwanamke huyu zitatimia … Endelea kula mtori nyama zipo chini.

Previoua Next