Mage kwanza kabisa alishangazwa na urembo wa Najma kiasi kwamba alijiulizaje huyu Jambazi akapata pisi kama hio kwenye Maisha yake , lakini hakukuwa na majibu sahihi yaliopatikanan katika halmashari ya kichwa chake.
“Najma usilie tena .. kaka yako alipatwa na matatizo na kwasasa yupo kalazwa anapatiwa matibabu , mimi naenda na hawa polisi kuna jambo la kuweka sawa , hakikisha kaka yako anapatiwa matibabu sawa?”Aliongea Roma kama mwanaume na mwanadada huyu aliekuwa ametokewa na machozi kutingisha kichwa kwa kukubaliana nae , lakini licha ya kumuuelewa alionekana hakuwa tayari kumuachia Roma.
“Eti kuna jambo la kuweka sawa .. yaani huna aibu unamuongopea mwanamke mrembo kama huuyu hahaha.. wewe mwambie unaenda jela na atafute bwana mwingine”aliongea Mage kwa kebehi na kumfanya Nama amwangalie mwanadada huyo kwa hasira.
“Wewe dada wa kitrafiki , mimi namjua Roma sio Jambazi na hayo maneno yote unayoongea hayakai kwenye Maisha ya Roma”Aliongea Najma na kumfanya Roma amwangalie mwanamke huyu na kutabasamu.
“Hilo litajulikana mrembo eh na Ushahidi tulionao , hakuna mengi ya kuzungumza na nitahakikisha hili Jambazi halirudi mtaani kuwarubuni Watoto wakike kama wewe , Mrembo wewe ni mhanga huyu jamaa kakubuhu hivyo shukuru ninamtoa kwenye Maisha yako , nakwambia utanishukuru baadae”
Aliongea Mage na baada ya kumaliza tu Difenda ya polisi iliingia hapo ndani na Mage aliwaamrisha polisi wengine waendeshe gari ya Roma na Mage akapanda kwenye pikipiki yake huku wakimwacha Najma anaetokwa na machozi.
“Najma nitarudi baadae sawa , usiwe na wasiwasi . hakikisha kaka yako anapatiwa matibabu”aliongea Roma na kufanya watu waliokuwa eneo hili la hospitali washangazwe na Roma maana maneno yake yalikuwa na nguvu sana kwenye mioyo ya watu hawa.
Ni baada ya lisaa limoja tokea Roma aingizwe ndani ya kituo kikubwa cha polisi wilaya ya Temeke alionekana mwanamke mmoa mrembo sana maarufu sana hapa nchini akiingia akiwa ameshikilia mkoba wake , huyu mwanadada alikuwa mrembo sio kawaida , ila licha ya urembo wake wote hakuwa akimfikia mrembo Edna.
Mwanadada huyu hakuwa mwingine bali alifahamika kwa jina la Nadia Alfonso , lakini nchini na duniani wengi walikuwa wakimuita kwa jina la ‘Goddes of law’ umaarufu wa jina hili mwanamke huyu hakupewa tu , ila yote hayo ni kutokana na heshima aliojijengea katika ulingo wa kutafsiri sheria, usomi wa mwanadada huyu pamoja na kipaji chake kilichangia pakubwa heshima aliokuwa nayo .
Nsdia Alfonso ni mwanasheria aliemaliza masomo yake ndani ya chou kikuu cha Harvard kuanzia digrii yake ya kwanza mpaka ngazi ya juu yabisa ya PhD , unaweza ukajiuliza inakuwaje mwanamke mdogo kama huyu kuwa na mafanikio makubwa kama hayo , lakini yote hayo ni kutokana na juhudi binafsi za mwanadada huyu tokea alipkuwa mdogo , lakini pia ukijumlisha na uwezo mkubwa wa akili Mungu aliombariki nao.
Umaarufu wake unakuja mara baada ya kusimamia kesi ya Raisi mstaafu wa Korea kusini , kesi ambayo ilikuwa ni gumzo sana duniani , kesi ambayo ilikuwa ikimtuhumu raisi huyo kwa ufisadi , lakini kwa uwezo mkubwa wa Nadia raisi huyo alipata haki yake na Dunia ikatambua kuwa raisi huyo sio kama walivyomdhania kwani alisafisha jina lake , lakini kufanikiwa huko kunazua gumzo baada ya Raisi huyo kutoa hotuba ya shukrani mbele ya waandishi wa habari na kumshukuru Nadia Alfonso kama mwanasheria mkuu alisimama kidete katika kufanikisha kwake kupata haki yake kisheria , lakini pia kusafishika kwa kile alichokiita kusingiziwa kesi ya ufisadi , kwanzia siku hio ndipo jina la Nadia liliposambaa duniani ,umahiri wake uliotukuka aliounesha katika kesi hio , kwanzia kukusanya Ushahidi ulimpa heshima kubwa sana., umaarufu ulimfanya mwanadada huyu kutafutwa na watu wengi maarufu duniani kwa ajili ya kusimamia kesi zao hayo ni machache kuhusu Nadia A.k.a Goddes of Law.
Polisi waliokuwa wakimjua mwanadada huyu ambaye alikuwa akipewa heshima kubwa na Taifa kwakuwa mtanzania wa kwanza kung`ara katika fani ya sheria , walihaha , walikuwa wakijiuliza imekuwaje mwanasheria huyu akaja kwenye kituo chao , na si hao tu , hata Mage aliekuwa yupo kituoni hapo kuhakikisha Roma hachomoki alishangazwa sana.
Kwanza kabisa Nadia kwake alikuwa ni Role Model , kwani katika Maisha yake Mage alikuwa akipenda sana sheria na alipigania sana ndoto yake hio kuja kuwa mwanasheria huku nguvu kubwa ya kimsukumo ikitoka kwa Nadia ambaye watu wengi katika sheria walimuita ‘Chain Breaker’ yaani mkata minyororo au kwa tafsiri ya haraka haraka yaa maana hi ni kwamba mtu ambaye ameshinda vizuizi vyote yeye kama mwanamke na kuudhihirishia ulimwengu kama mshindi , sasa wewe jaribu kuwaza mtu ambaye ulimhudusu kwenye Maisha yako yote akatokea mbele yako ghafla tu , basi hio ndio namna ambavyo Mage alishituka na hakuwa akiamini kwamba mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni ‘Goddes of law’ mwanamke aliekuwa akimpenda na kumpenda Zaidi ya neno lenyewe.
Mage machozi yalianza kumtoka , alikumbuka miaka kadhaa nyuma alivyokuwa akipambania kusoma sheria , lakini kutokanana na kile alichokiita mweyewe uwezo wake mdogo kiakili alikuwa akifeli kila mara na kumpelekea kukata tamaa na kuachana na sheria na kujiunga na jeshi la polisi huku akiamini kwamba polisi na wanasheria wanafanana kwa vitu vingi ,aliamini licha ya kufeli kuwa mwanasheria kuwa polisi sio mbali sana na ndoto zake.
Mkuu wa kituo cha polisi ndio wa kwanza kutoka kwa ajili ya kuonana na Nadia ili kumpa heshima zote kubwa , kwani mwanadada huyo hakuwa mdogo kabisa ndani ya taifa hili, lakini licha ya hivyo polisi wengine wote walijipanga mstari kwa ajili ya kutoa heshima kwa Goddes of law.
“Karibu sana mheshimiwa ,, Ini furaha kwangu kufamiana na mrembo kama wewe na mtu mkubwa sana duniani karibu kituoni kwetu”.
“Asante sana , lakini sijaja hapa kimatembezi nipo hapa kama mwanasheria na nina mteja wangu hapa”Aliongea Nadia kwa sauti yake tamu na kuwafanya polisi wote washangae , anachozungumza Nadia , kwanza hapo polisi hakukuwa na mtuhumiwa mwenye hadhi ya juu kama anavyoongea mwanadada huyu , kwani hakuwa na taarifa ya mtu wa hadhi alieshikiliwa na kituo chake Zaidi ya vikapuku tu waliowafunga.
“Mheshimiwa Labda umekosea , hapa hatuna mtu tuliemshikilia ambaye ni wa hadhi kuhudumiwa na wewe kisheria”
“Kwangu kila mtu anaehitaji sheria anapaswa kuhudumiwa na mimi na sijawahi kubagua watu kutokana na nafasi zao katika jamii”Baada ya kuongea hivyo alimpita mkuu huyu wa kituo .
“Pumbavu nimeongea ujinga”Aliwaza mkuu huyu wakituo huku akifatisha nyuma na waliingia kwenye ofisi ya kuonana na wageni.
“Nipo hapa kwa ajili ya mteja wangu anaefahamika kwa jina la Roma Ramoni”Aliongea na kumfanya Mheshimiwa ashituke na kujiuliza Roma ni nani mpaka mtu mkubwa duniani kama huyu aje kumtoa.
“Mheshimiwa mtu unayemzungumzia ni jambazi ambalo tulikuwa tukilitafuta kwa muda mrefu sana na leo tumemkamata hatuwezi kumuachia kirahisi” Aliongea Mkuu wa kituo na hakuwa tayari kumuachia Roma kizembe hivyo , kwani alishuhudia yale maburungutu ya pesa na alikuwa ashayapigia plani kabisa wa kulipa deni ambalo alikuwa akidaiwa na anaemdai kumkalia kooni , lakini pia alikuwa akipanga kulipa kodi ya nyumba anayoishi maana hakuwa akiishi kwenye nyumba za polisi maaruufu kama kota , lakini pia alikuwa akisumbuliwa na mchepuko wake juu ya hela ya mtaji na alikuwa amenyimwa kitumbua na mchepuko huyo kwa muda wa mwezi mmoja , pia mke wake alikuwa akidaiwa vikoba sasa kwa matatizo hayo yote aliona kwa pesa hizo zilizofika kwenye ofisi yake , aliona ni Mungu ndio kaleta fursa , sasa hakuwa mzembe kiasi hicho licha ya kwamba mtu aliekuwa mbele yake alikuwa mkubwa tu katika sheria, tamaa ya pesa ikisukumwa na matatizo aliokuwa nayo aliona asimamie msimambo wake
“Nishatangulia kusema sipo hapa kaa mtu maarufu , ila nimekuja kwa ajili ya mteja wangu na nina Ushahidi wa kutosha ambao unamfanya mteja wangu kutokuwa na makosa”
Aliongea mwanadada huyu kwa upole na kujiamnini kisha akatoa Ushahidi wake na kwa namna ambavyo mwanadada huyu alielezea na kuoonyesha uhahidi Mkuu wa kituo alijisemea moyoni yes hapa kakutana na profesheno mwenyewe.
“Naomba kwanza kuonana na mteja wangu”Aliongea Nadia na mkuu wa kituo hakuwa na sababu ya kumzuia .
Huku upande wa nje Mage alikuwa kwenye mshangao mara baada ya kusikia kuwa Mrembo Nadia amekuja kwa ajili ya Roma , alishangaa sana sana , inakuwaje choko kama Roma kuja kupata huduma ya kisheria kutoka kwa mwanasheria nguli duniani na hapo hapo swali la Roma ni nani lilianza kuibuka kwenye kichwa chake.
“Pluto!” Aliita Nadia na kumfanya Roma anyanyuie uso wake na kuangalia sauti tamu inayomwita kwa jina ambalo hajalisikia muda mrefu.
“Haha.. Nadia unafanya nini hapa?”Roma alishangaa sana na alionekana alikuwa akimfahamu vyema Nadia na mrembo huyu aliachia tabasamu ambalo ungekuwa mwanaume rijali kama Roma ungekuwa hoi.
“Za siku nyingi The Great Pluto nimefurahi sana kukuona tena , hujui tu nilivyokuwa nikitamani kupata nafasi ya sisi kuonana tena tokea tulivyo achana nchini Korea Kusini”
“Nadia hayo mambo tuache kuyaongelea sasa hivi , nataka uniambie unafanya nini hapa”Aliongea Roma kwa usiriasi na mwanadada huyu alimwangalia na kuonekana kama hajafurahia , kwani alitamani kumuona Roma akiwa kwenye mshangao na furaha ya wao kukutana tena baada ya miaka mingi.
“Nipo hapa kama mwanasheria mpya wa kampuni unayofanyia kazi, na nipo kukutoa”Aliongea mwanadada huyu na kumfanya Roma ashangae.
“Okey! Basi fanya hima nitoke hapa maana nina njaa sio poa”Aliongea Roma huku akijigusa tumbo , yaani kwa Roma alionekana hakuwa akimchukulia kabisa Nadia kama mtu mkubwa vile tofauti na wengi walivyokuwa wakimchukulia , kwani Nadia alikuwa akipewa heshima ya jiuu mpaka na maraisi wa Afrika , lakini kwa Roma alimuona Nadia kama wa kawaida.
“Tayari mpaka sasa upo huru”Aliongea Nadia na mlango ulifunguliwa na akaingia mkuu wa kituo akiwa ni mwenye kutoa jasho jingi usoni.
“Mheshimiwa mteja wako yupo huru”Aliongea mkuu huyu huku akionekana ni mwenye kuhema , sijui nini kimemtokea maana ujasiri aliokuwa nao umeisha wote.
“Daah ! Afadhali maana sio kwa njaa hii ,Nadia uko vizuri sana kwenye kazi yako”Aliongea Roma huku akiamka wa kwanza na kutangulia mlangoni akimuacha Nadia aliekuwa akimwangalia mwanaume huyo kwa hali ya hudhuni inaonekana alitarajia kitu kikubwa Zaidi kutoka kwa Roma.
“Niletewe begi langu lenye pesa niondoke nina njaa ”Aliongea Roma huku akimwangalia Mage aliekuwa akimwangalia bwana huyu pasipo kummaliza na alionekana ni mwenye maswali mengi sana katika kichwa chake.
“Boss begi lako hili hapa”Aliongea Afande mmoja kwa heshima na kumpatia Roma begi lake na Roma alilibeba lakini akasita.
“Huu uzito ni tofauti , kuna kiasi cha pesa kimepungua”Aliongea Roma na kuwafanya mapolisi hawa wote waangaliane kama kondoo.
“Rudisheni pesa zote zilizokuwa humu ndani , najua kiasi kamili cha hizi pesa , mkigoma nitakaa hapa nakuhesabu zote na hakuna mtu kuondoka nikihakikisha hela ni pungufu nitawasachi wote”
“Rudisheni pesa , acheni kuvunja sheria la sivyo swala hili sitoliacha lipite hivi hivi”Aliongea Nadia baada ya kumuona Roma anaongea na Polisi wote walitoa jasho akiwemo mkuu wa kituo.
“Huyu jamaa mahela yote hayo kajuaje nimepunguza vibunda viwili”Aliwaza mkuu wa kituo huku akikumbuka vibunda alivyoficha ofisini kwake,wakati akiendelea kutoa jasho simu yake iliingia ujumbe na kufungua na kuangalia meseji ilitoka kwa jina la ‘Mke Wangu’
“BABA LEAH MWENYE NYUMBA ANAKUSUBIRI NA ANASEMA HAONDOKI MPAKA UTOE PESA YAKE , HALAFU GESI IMEISHA MPAKA SASA HATUJUI TUNAPIKA NA NINI” ilikuwa ni meseji kutoka kwa mke wake iliandikwa kwa herufi kubwa kabisa kuonesha msisitizo , mzee huyu jasho lilizidi .
“Hapana sitoi zile pesa nitakuwa mjinga wa karne” Uasiri uliongezeka.
“Narudia nataka pesa zangu zote ili niondoke”Aliongea Roma akianza kuwangalia polisi mmoja mmoja na baada ya macho yake kutua kwa mkuu wa kituo , aliona jambo na kumsogelea.
“Nataka pesa zangu” Aliongea Roma huku akiwa amemkaribia mkuu wa kituo karibu kabisa.
“Sijachukua pesa mimi , siwezi kuiba , mimi ni mkuu wa kituo na nachukia wezi” Aliongea kwa kujiamini na muda huo huo Simu yake iliingia ujumbe mwingine na aliinua simu yake na kuangalia ujumbe huo ulitoka kwa jina la “Fundi cherehani’
“ WEWE MWANAUME VIPI MBONA HUTUMI HIO HELA , AU ULIKUWA UNAJIGAMBA BURE UMEPATA PESA NYINGI LEO , KAMA HUNA HELA USEME UACHE KUNISUMBUA MIMI KUNA WANAUME WENZIO WANAWEZA KUNIHUDUMIA , NITUMIE HIO HELA NIKANUNUE WIGI”
Baada ya mkuu huyu wa kituo kuona meseji hio alikunja ngumi na kusema liwalo na liwe pesa sitoi.
Roma baada ya kuona mkuu wa kituo anakataa , alimsukuma na kisha alimpita na kuingia kwenye ofisi yake , baada ya kuingia tu , alivuta mtoto wa Meza na kuibuka na mabuda mawili ya pesa na kutoka.
“Mimi siibiwi kizembe ohoo..”Aliongea huku mkuu wa kituo akimtukana moyoni na kuona mkeka umechanika.
“Hawa ndio majambazi ambao unatakiwa kuwakamata kama unajali sana sheria , sio raia wema kama sisi mrembo eh” Aliongea Roma wakati akiwa amemsogelea Mage karibu kabisa na Mage hakuwa na la kuongea kwani wakati huo alionekana kuwa kwenye mawazo mengi sana kwa wakati mmoja.
Roma baada ya kutoka alifanya mawasiliano na Nasr ana kumuuliza yuko wapi na mwanadada huyo alimjibu bado yupo ofisni , Roma alishangaa kwani muda ulikuwa umeenda sana , lakini alijua huenda mwanadada huyo kabanwa na majukumu mengi Zaidi.
Ndani ya masaa machache Roma alikuwa ashafika ndani ya kampuni , haikueleweka waliachana vipi na mrembo Nadia ila Roma alikuwa ni aina flani ya wanaume ambao hawakujali sana baadhi ya mambo na ilionekana anahistoria kubwa san ana mwanadada huyo.
******
MASAA MACHACHE NYUMA
Kitendo cha Roma kufanikisha kazi ya kurudisha feza kutoka PANZ Security kilimfurahisha sana Edna, na kwa mara ya kwanza alijihisi kweli ana mume.
“Nitampikia chakula leo ,ananidharau sana sijui kupika ananiona sistahili kuwa mke ”Aliwaza mrembo huyu wakati akiwa ndani ya ofisi yake
“Bosi Miss Nadia amefika?” ilikuwa ni sauti ya Monica akitoa taarifa kwa bosi wake.
“Okey mruhusu aingie”
“Wow! You are beutifull Edna as the rumors”
“Asante sana Nadia , na wewe pia umrembo”
Wawili hawa walikaribishana na kuanza mazungumzo ya kibiashara.
“Nimekubali ombi la kuwa mwanasheria wa Kampuni yako”Edna alishangaa maana haikuwa kazi rahisi kumfanya mwanasheria mkubwa duniani kuwa mwanasheria wa kampuni change kama Vexto maana Nadia alikuwa akifanya kazi na makampuni makubwa kama Sumsung
“Nashukuru sana Nadia kwa kuchagua kufanya kazi na kampuni yangu na niseme tu nitahakikisha unafurahia kufanya kazi na sisi”.
Nadia alitabasamu huku akihusudu urembo aliokuwa nao Edna , alikiri kuwa hakuwa akiingia kwa urembo wa mwanadada huyo hata kidogo.
Basi wawili hawa walikutana kwa ajili ya kusaini mkataba wa Nadia kusimamia kampuni ya Edna kisheria yaani VExto.
Wakati wakiagana mara simu ya CEO Edna iliita na alipoangalia jina aliona ni ‘Mbakaji’ na bahati mbaya ni kwamba simu ilikuwa mezani hivyo Nadia aliona jia hilo na kujiuta akishangaa.
“Hello!”
“Bebi nimekamatwa tena na polisi”Ilikuwa ni sauti ya Roma na Edna alishangaa.
“Ilikuwaje “
“Nina kesi ya utakatishaji fedha , nimedharau sharia za nchi”Aliongea Roma na Edna hakuongea chochote .
“Bebi mbona huongei , usiniambie mapenzi siku hizi yamepungua kiasi cha kutaka mumeo nikae jela”Edna alimwangalia Nadia.
“Natuma mwanasheria aje kukutoa” Baada ya kukata simu Edna alivuta pumzi.
“Nitaenda mimi” Aliongea mwanadada Nadia. Nadna alishangaa
“Lakini..”
“Usiwe na wasiwasi , najua unachofikiria lakini nitaenda mimi iweke kama kazi yangu ya kwanza kwa kampuni”Baada ya kuongea maneno hayo Nadia alichukua mkoba wake na kushuka hadi kwenye maegesho ya gari na kuingia .
“Evans nipe taarifa?” Aliongea mwanadada huyu na kupewa taarifa na mtu anaefahamika kwa jina la Evans.
“Okey ! nikusanyie ushahidi wote na tukutane”
“Sawa madam” ilisikika sauti upande wa pili wa simu .
Baada ya smu hio kukatwa mwanadada huyu alifatufa jina lingine na kupiga .
“ Ndio boss nishasaini mkataba, anaonekana kufurahia sana kwa mimi kufanya kazi ndani ya kamupini”
“Hongera sana Nadia ni mwanzo mzuri nadhani ni wakati sasa wa kuendelea mipango yetu” ilisikika sauti nyingine kwenye simu , sauti nzito.
Comments