Muda wa saa kumi na nusu Edna alifika nyumbani huku mwanadada huyu akionekana siku ya leo kuwa na furaha kuliko siku zote jambo ambalo Bi wema aliligundua , lakini hakuuliza Zaidi , kwake huyu mwanamke alitamani sana kumuona Edna akifurahi ndio iliokuwa ndoto yake kubwwa sana , alikuwa akiumizwa sana na tabia ya Edna muda wote kufanya kazi kiasi kwamba kwake hakuwa na siku ya kupumzika , Edna hakuwa kama wafanya biashara wengine ambao walikuwa wakipenda kula bata kila ifikapo wikiendi , Edna yeye alikuwa ni aina flani ya wanawake ambao alikuwa akirudi nyumbani ni kusomana kulala.
Ndani ya chumba cha Edna kulikuwa na mavitabu mengi sana na karibia vitabu vyote hivyo alikuwa amevisoma , kwa mtu wa kawaida unaweza kushangazwa na swala hilo lakini kwa Edna lilikuwa swala la kawaida sana , ndio Maisha yake ambayo alikuwa amezoea , kwake kusoma vitabu ndio ilikuwa starehe yake kuliko kujichanganya na marafiki.
Edna alikuwa ni mtu wa kutabasamu mara chache sana , muda wote alikuwa yupo siriasi kiasi ambacho kilifanya hata wafanya kazi wenzake wamuogope kumsogelea, lakini leo hii mwanadada huyu anaonekana kutabasamu mbele ya Bi Wema , mwanamama huyu aliekula chumvi nyingi alitamani kujua ni kipi kinamfanya mwanae huyu wa kambo kutabasamu , ila hautaka kuuliza.
“Bi Wema leo niachie jiko nitapika mimi” aliongea Edna na kumfanya Bi wema kutumbua macho lakini Edna hakujali sana , alikaa kwenye sofa huku mkononi akiwa ameshikilia kitabu cha mapishi.
“Sawa Miss , lakini haujawahi kuingia jikoni utapika nini?”
“Bi Wema hio ni siri , wewe utaona wakati wa kupakua”Bi Wema alijikuta akitabasamu na katika akili yake alikuwa ashajua kilichokuwa kikiendelea kwa Edna , aliamini kuna jambo ambalo lilikuwa limetokea kazini na kusababisha mabadiliko hayo .
Saa moja kamili za jioni Edna alikuwa bize na mapishi huku Bi Wema akiendelea kuangalia tamthilia, muda nao ulisonga lakini Roma bado hakuwa amerudi.
“Bi Wema Roma hajarudi bado?”Aliuliza mwanadada huyu aliekuwa amevalia Apron na kumfanya apendeze sana , kiasi kwamba wewe ndio ungekuwa mume wa Edna na ungemuana jinsi alivyovalia Apron ni hakika ungenenepa kabla hata ya kula chakula.
“Hajarudi bado na hajatoa hata taarifa kama atachelewa kurudi”Aliongea Bi Wema na kumfanya Edna kuonyesha hali ya kuhuzunika.
“Ukute na hangaika hapa yupo na mwanamke”Aliwaza Edna huku akirudi jikoni kuendelea na upishi akitegemea Roma atarudi.
Muda wa saa tatu na nusu alionekana Bi Wema akiwa ndani ya chumba cha maliwato akitapika huku akisukutua maji.
“Nimewahi kula chakula kibaya ila hiki cha leo ni kiboko , Chakula kama mavi ya mtoto mchanga khaa.. Edna ananitia aibu jamani”Aliongea Bi Wema huku akisukutua .
“Nimekula kumridhisha tu ilia aone na yeye mwanamke , ila kile sio chakula”.
Wakati Bi Wema akiendelea kutapika huko ,Edna alikuwa amekaa kwenye sofa akimsubiria mwamba Roma arudi huku Mabakuli ya chakula akiwa ameyapangilia kwenye Meza , na kwa jinsi yalivyopangwa moja kwa moja utaamini kuwa kuna bonge la pishi limefunikwa.
Upande Nasra alionekana akiwa nyumbani kwake jikoni akiwa bize na mapishi , alionekana kuwa mtaalamu kweli , kwani kwa namna ambavyo alikuwa akikata kitunguuu Ungejiambia mwenyewe ndio hapa yupo mwanamke.
Bebi Nasra unajua sana kupika” Aliongea Roma huku akiwa amejipumzisha na pensi la kike na haraka haraka ukimwangalia lazima ugundue hilo pensi ni la Nasra maana lilikuwa na Marinda Marinda chepete , ila Roma hakuwa na habari huyu bwana , yaani hakuwa na aibu hata kidogo.
Baada ya kula na kushiba , hakukuwa na kilichoendelea zaidi ya kuingia kwenye mtanange .
“Bebi hii Staili inaitwaje?”Aliuliza Nasra huku akionekana kukosa pumzi maana alikuwa amelemewa na utamu.
“Mh! Mimi hata sijui ila umekaa kipopo popo ,, itakuwa ndio Popo kanyea Mbingu”Aliongea Roma huku akiongeza spidi.
Muda wa saa kumi na mbili za Asubuhi Roma aliingiza gari yake nyumbani bila wasiwasi kabisa na baada ya kuliegesha aliingia ndani na kumkuta Bi Wema.
Bi wema kama kawaida , alikuwa mzungu wa Roho maana alimpokea Roma na kuitikia salamu kama hakujatokea kitu ila kiukweli moyoni alikuwa na huzuniko , kwani kwa mara ya kwanza anamuona Edna akiingia jikoni jambo ambalo kwake aliliona kama hatua ya kwanza ya Edna kuwa kama mwanamke aliekamilika , lakini Roma hakuonekana nyumbani , aliona kitendo hicho kimemnyong`onyesha Edna juhudi zake , kwani Edna kwa mara ya kwanza alimsubiria Roma kwa muda mrefu jambo ambalo sio kawaida.
“Roma jana ulikuwa wapi , hukutoa taarifa Miss alipika na akakusubiri lakini hukutokea”Aliongea Bi wema wakati Roma akianza kupandisha ngazi kuelekea chumbani kwake , lakini baada ya kusikia maneno hayo alijikuta akisimama na kushangaa.
“Bi Wema unamaanisha Edna jana kaingia jikoni kupika?”
“Ndio chakula bado kipo mezani”Aliongea Bi Wema na Roma hakuendela kwenda juu ,, alirudi chini na kwenda meza ya kulia chakula na kufunua mabakuli yaliopikwa.
“Bi Wema nitakula kama kiporo na chai”Aliongea Roma na kupanda ngazi kuelekea chumbani kwake na baada ya muda alishuka kwa aili ya Chai na Edna alikuwa amejaa mezani akinywa chai oamoja na Bi Wema.
“Wife hebu tuone leo ulichopika”Aliongea Roma na kisha alifunua mabakuli hayo huku Edna licha ya kwamba hakuwa akimwangalia Roma usoni lakini akili yake ilikuwa ni kusbiria nini ataongea Roma baada ya kula chakula chake.
Roma alipakuwa chakula na kisha alichota mtori hhuo na kupeleka kinywani na kula.
“Nilijua mtori kumbe ni tambi Looh! Hapa nina jipu sio mke”Roma aliwaza moyomi na kisha akachota kijiko kingine na kula , wakati huo Bi Wema alikuwa amekunja sura utadhani chakula kilikuwa kikiingia Tumboni kwake.
Roma alimwangalia Edna huku mrembo huyu akijifanyisha kunywa chai , lakini alikuwa akisubiri Roma atamke neno.
“Wife umejitahidi sana leo, ukiendelea hivi utakuwa mpishi mzuri”Aliongea Roma na kuendelea kula bila ya wasiwasi huku nia yake ni kutokumkatisha tamaa Edna na Bi wema alifurahishwa na maneno ya Roma na kule kukasirika kwa kutokurudi nyumbani kulipotea , lakini bado kuna kitu kilimshangaza , kwa jinsi chakula hiko kilivyokuwa na chumvi , alijiuliza Roma amewezaje kula.
“Okey ! ngoja nijipe adhabu ya kumaliza hiki chakula maana sio kwa huu utopolo”Aliwaza Roma , ila kwa Edna moyo wake ulitabasamu , licha ya kwamba hakuwa akionyesha usoni lakini alifurahia sifa hizo kutoka kwa Roma.
Roma baada ya kumaliza kunywa chai ya asubuhi alipandisha chumbani kwake kwa ajili ya kupumzika , siku hii ya leo aliona akae kidogo nyumbani , kwani tokea afike ndani ya familia hii hakuwahi kukaa nyumbani kwa muda mrefu , muda mwingi alikuwa misele ya hapa na pale.
Wakati akiwa amejilaza kwenye kitanda alijikuta akiachia tabasamu .
“Edna mambo yake ni kama ya Seventeen nakiri kwa asilimia kubwa wanafanana”Aliwaza Roma huku akiwa ni mwenye tabasamu.
****
1998- KIGALI RWANDA March 8
Ilikuwa ni ndani ya ofisi ya mheshimiwa Jeremy Paul (JP),walionekana watu wanne wakiwa wameketi ndani ya ofisi hii na ilionekana kuna kikao kilichokuwa kikiendelea kati ya mheshimiwa Jeremy na wanaume watatu kukamilisha idadi ya wanaume wane ndani ya ofisi hii.
Wanaiume watatu walikuwa ni watu maarufu sana waliokuwa wakifahamika ndani ya jiji la Kigali na moja ya sifa kubwa ambayo ilikuwa ikiwafanya watu hawa kufahamika ni kutokana na michango yao katika taifa hili dogo.
Mtu wa kwanza aliekuwa amekaa upande wa kushoto wa mheshimiwa Jrtrmy alifahamika kwa jina la Uwimana ,huyu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana ndani ya taifa hili la Rwanda na alikuwa akimiliki visima vingi vya Mafuta , pamoja na kampuni kubwa ya usafirishaji , Mwingine alikuwa ni Jean , Wengi ndani ya taifa hili wanapenda kumuita kwa jina la Profesa J , huyu nae licha ya kuwa mfanya biashara lakini pia alikuwa ni mkuu wa chuo kikuu cha Rwanda,Mtu wa tatu hakuwa akifahamika sana ndani ya taifa la Rwanda kama alivyokuwa akifahamika ndani ya taifa la Tanzania ,Alikuwa akifahamika kwa ina la Aziz Mohamed huyu alikuwa ni moja ya wafanya biashara wakubwa sana kutoka taifa la Tanzania , lakini pia alikuwa ni moja ya wawekezaji wakubwa ndani ya taifa la Rwanda na ndio maana mchango wake ulikuwa ukiheshimika ndani ya taifa hili.
“Ndoto yangu yangu kubwa ni kuona Rwanda ikiwa nchi kubwa sana kiuchumi ndani ya bara la Afrika , na haya yote hayawezi kufanikiwa bila ya uwepo wenu”Aliongea. Huku mabwana hawa wakionekana kutingisha vichwa kuashiria kuwa wako pamoja na mheshimiwa na muheshimiwa.
“Mheshimiwa sisi tupo tayari kukuunga mkono katika safari ya ndoto yako ya kuifanya Rwanda kuwa kubwa na tutakuwa ni wenye kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha kuinua uchumi wa taifa hili”Alingea Uwimana
Kikao hiki kilionesha dhahiri kilikuwa ni cha mipango juu ya kuifanya Rwanda kuwa nchi kubwa kwa miaka ishirini ijayo, mipango ambayo mheshimiwa Jeremy aliona watu pekee wakufanikisha nao swala hilo ni hao mabwana watatu , haikueleweka ni kwanii Mheshimiwa akamwinginza mtu mwingine kutoka taifa la nje yaani Azizi Mohamed.
Baada ya kikao hiki kuisha Mheshimiwa huyu alionekana kuwa na maongezi binafsi na Aziz kwani wale mabwana wengine walikuwa washatoka ndani ya ofisi hii.
“Asante sana Aziz kwa kufanikisha kurudisha sehemu ya damu yangu mikononi mwangu”.
“Jeremy sisi ni marafiki wa muda mrefu sana hupaswi kunishukuru , lakini nisingependa kuona katika Maisha yako unakosa furaha , umemkosa Rahel , lakini naamini zawadi aliokupatia ni kubwa na angalau itakufanya usiishi kwa kujuitia”Aliongea Azizi huku akimtaja Rahel na Jeremy alionekana kukosa furaha mara baada ya kusikia jina la Rahel.
“Ni kweli Aziz.. lakini Maisha yangu bado naona kama hayajakamilika kwa kumkosa Rahel , katika Maisha yangu niliamini kwa kuwa raisi hakuna kitu ambacho ninaweza kukosa na kunifanya nisiwe na furaha , lakini Rahel amenifanya nione sikuwa nikifikiria kwa usahihi”.
“Ni kweli Jeremy, lakini kwa sasa unatakiwa kumsahau Rahel , yule mwanamke ni mke wa mtu kwa sasa na ni maamuzi ambayo aliyafanye yeye mwenyewe na akakuacha wewe , angalau sasa wekeza nguvu zako katika kulea kichanga alichokuachia kama zawadi”Aliongea Aziz lakini muda huo huo aliingia mwanadada makamu hivi, hakuwa mrembo sana , ila alionekana kuwa mtanashati
“Mheshimiwa kuna taarifa mbaya?”
“Unamaanisha nini Linda , unamaanisha nini kuhusu taarifa mbaya?”
Mwanadada huyu aliefamika kwa jina la Linda alisogelea Rimoti ya Tv na kisha akawasha Runinga na kuweka chaneli ya BBC .
BREAKING NEWS: NDEGE YA MALAYSIA AIRLINE ILIOKUWA IKISAFIRI KUTOKA KUAL LAMPUR KUELEKEA BEIJING CHINA YAPOTEZA MAWASILIANO.
Taarifa hii ilionekana kumshitua sana mheshimiwa pamoja na Aziz waliouwa wakiangalia Runinga hio lakini kati ya watu hao aliekuwa kwenye hali mbaya Zaidi ni Jeremy.
“Linda wasiliana na shirika la ndege la Malaysia wakupe orodha ya majina ya watu waliopanda kwenye hii ndege”Aliongea Mheshimiwa Jeremy huku akiwa ni mwenye wasiwasi mwingi sana.
“Jeremy punguza presha naamini huenda kuna tatizo la kawaida tu ambalo limetokea”
“Aziz siwezi kutulia kabisa ,unafikiri nitaishije kama kitu kibaya kikimkuta Lorraine ,Nitamwabia nini Rahel , hapana nitaishi kwa majuto makuU kwenye Maisha yangu yote , naomba jambo baya lisitokee”Aliongea Mheshimiwa Jeremy huku akishikilia kifua chake.
Ni ndani ya dakika tano Linda alirudi na kuingia ndani ya ofisi , huku wasiwasi ukiwa umejaa kwenye macho yake.
“Mheshimiwa hii ndio orodha ya abiria”Aliongea lakini Azizi aliona wasiwasi uliokuwa kwenye macho ya Linda na kwakuwa alikuwa karibu nae alichukua ile karatasi na kuangalia majina hayo na bwana huyu alijikuta akitumbua macho na kumwangalia Rafiki yake Jeremy.
“Azizi usiniambie Lorraine ni sehemu ya abiria walikuwepo kwenye hio ndege?”
“Jeremy taarifa inasema ndege imepoteza mawasiliano , lakini sio kuanguka tusubirie taarifa kamili , Acha kufikiria mambo mabaya”Aliongea Azizi lakini baada ya kumaliza sentensi yake…
“Mheshimiwa..!!”Aliongea linda kwa sauti mara baada ya Mheshimiwa Jeremy kudondoka na kuzimia.
Comments