Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

Taarifa za mheshimiwa Jeremy kuzimia  zilikuwa ndani ya ikulu , hazikutoka hata kwa  baadhi ya mawaziri Zaidi ya kitengo cha usalama  ikulu  pamoja na baadhi ya wanafamilia wa  mheshimiwa  Jeremy.

“Nini kimempata mheshimiwa  Linda?”Aliuliza mke wa Raisi Jeremy huku akionekana ni mwenye wasiwasi sana ,  wakiwa nje  ya chumba cha matibabu ndani ya ikulu.

Lakini  Linda hakuwa na jibu  la kuongea na kusema hakuwa akijua  ni nini   kimemkuta mheshimiwa Jeremy Zaidi ya kumwambia First lady huyu  wasubiri majibu kutoka kwa daktari.

Baada  ya masaa kadhaa  ya  hatimae daktarin wa ikulu alitoka  katika chumba cha matibabu.

“Inaonekana mheshimiwa kapata mshituko”.

“Mshituko , unamaanisha nini mshituko dokta?”Aliuliza mama huyu kwa Jazba huku macho yake yakimgeukia Linda aliekuwa mlinzi wa karibu wa raisi na Linda jasho lilimtoka.

“Linda niambie ni  jambo gani baya mheshimiwa kakumbana nalo mpaka kupata mshituko?”

“Madam ! hata mimi najiuliza swali kama hilo , lakini sina majibu sahihi ,maana mheshimiwa nilimkuta akiwa  katika hali ya kupoteza fahamu”.

Bado haikuwa ikimwingia akilini mwanamama huyu mwenye PhD ya lugha , aliamini kuna jambo ambalo mme wake limemkuta na kumpelekea kupoteza fahamu.

Baada ya masaa mawili  kadhaa kupita hatimae mheshimiwa  Jeremy alirejewa na fahamu zake  na swali la kwanza baada ya kuamka lilitoka kwa mke wake aitaka amueleze nini kimemkuta mpaka kupoteza fahamu , lakini mheshimiwa licha ya kuonyesha hali ya wasiwasi  hakuwa tayari kuweka wazi ni jambo gani lilimkuta.

“Linda nipe taarifa ya kinachoendelea?”

“Mheshimiwa taarifa ni zile zile ni Zaidi ya masaa nane sasa  ndege haijapatikana kwenye Rada  na satelaiti , na wataalamu wa anga wanajaribu kuifatilia kwa ukaribu”Alijibu Linda  na kumfanya mheshimiwa chozi   la utu uzim limtoke.

“No .. no Lorraine  you are not dead”Mheshimiwa aliongea kwa uchungu kiasi kwamba Linda alitoa machozi na kumuonea huruma mheshimiwa.

****

WHITE HOUSE -USA 1998 MARCH 8.

Ndani ya ofisi ya kiserikali ya   Marekani  ,alionekana  mheshimiwa Raisi , mwenye jina maarufu  The First Black  akiwa ameketi kwenye kiti  chake huku akiwa ameshikilia faili  lililokuwa na nembo ya ‘Top Confidential’ ikimanaanisha Nyaraka ya Siri sana.

‘Life and Death Operation’(LADO)  ndio jina la kichwa cha karatasi  kilichokuwa kikisomeka juu kabisa ya karatasi alioshikilia mheshimiwa The First Black(TFB) huku akionekana ni mwenye umakini mkubwa sana kusoma karatasi hio ambayo imetoka kwenye faili lililokuwa mezani .

Ni ndani ya dakika kama kumi na moja tu  alizotumia Mheshimiwa huyu kusoma , simu yake ilianza kuita mfululizo kiasi cha kumfanya mheshimiwa huyu aichukue na kuipokea .

“Yes Rogan  whati is news?”

“Mr President  the plane has landed safely on Life and Death Island”Ilisikika sauti na bwana huyu alitabasamu.

“Very Good Rogan Activate Project LADO   and all Concealment  Protocol should be followed strictly, I will deal with the Rest”Baada ya kuongea maneno hayo simu ilikatwa na mheshimiwa huyu akachukua simu  na kupiga na muda huo huo mlango wa ofisi ya mheshimiwa ulifungulikiwa na akaingia  mwanadada wa kizungu  mwenye umri  kati  ya miaka therathini hivi kupanda alievalia suti  ya zambarau na blazia nyeupe na viatu vyenye kisigino kirefu ‘high heels’

“Christine nipe taarifa ya kinachoendelea huko ulimwenguni”

“Mheshimiwa hali sio shwari kwa sasa , mataifa mengi yanahitaji  msaada kutoka kwetu , juu ya upoteaji wa ndege ya Malaysia Airlines, ufupi ni kwamba mheshimiwa dunia imesimama kutokana na tukio hili”Mheshimiwa alisimama na  kutembea kwa kuzunguka kwenye hii ofisi.

“Endelea kutoa taarifa kwa kila anaepiga simu, na waambie serikali yetu  itafanya kila namna kuhakikisha ndege hio inapatikana”Aliongea mheshimiwa  na kisha  Christine alitoka   na kwenda kuendelea na kazi .

Huyo mwanadada alikuwa ndio msemaji mkuu  wa kurugenzi ya White House.

Baada ya  Christine kutoka . mheshimiwa alivuta faili lingine kwenye  droo ya meza , lililokuwa likifanna na lililopo mezani . utofauti wa faili hili  na lile ni kwamba juu ya karatasi iliokuwa ndani ya faili hilo ilisomeka  kwa jina la ‘The Agrement’ huku kukiwa na baadhi ya orodhesho la mashirika makubwa Duniani ya kijasusi na sahihi za wakurugenzi wakuu wa mashirika hayo.

The first Black aliangalia  sahihi hizo,  lakini kuna jambo moja ambalo lilionekana halikumridhisha.

“Shirika la Urusi  pekee la kijasusi ndio Saini yao hapa haipo ,Beijing wamenihakikishia kwamba watashughulika na swala hili , lakini bado nina wasiwasi”Aliwaza mheshimiwahuyu na kurudisha mafaili yote  kwenye Safe Box ndani ya ofisi yake.

****

DAR ES SALAAM ,TANZANIA 1998  -March 8.

Ni ndani ya familia moja ya kitajiri  maarufu ndani ya Masaki , walionekana wanafamilia hii wakiwa kwenye hali ya furaha sana , na hii yote ni baada ya  kiumbe kipya kuja duniani ndani ya familia hio.

Rahel pamoja na  Bi Salome  walionekana  furaha ilikuwa imewazidia  kiasi kwamba muda wote walikuwa wakipokezana  kubeba kitoto kichanga  kalikozaliwa.

“Rahel umemleta mtoto mzuri  sana duniani , anafanana kwa asilimia  mia moja na wewe na hili  limenifurahisha Zaidi , asante kwa kumlindia mwanangu Adebayo heshima yake”Aliongea mwanamama huyu huku akimwanglia mtoto aliekuwa kwenye mikono yake , muda huu ikiwa yapata saa  mbili za usiku.

Wakati wanawake hawa wanaendelea kufurahia kiumbe kilichokuja duniani  , alionekana kijana  wa makamo  umri wa Rahel akiingia ndani  hapa huku akiwa amelewa chakali , baada ya kuingia ni kama hakuwa akijali waliokuwa sebuleni kwani alipandisha ngazi moja kwa moja.

“Adebayo  utaacha nini kulewa hivyo wewe”

“Mama niache  maamuzi ulioyafanya  licha ya kwamba nimeyakubali ila ni yenye kuniumiza na njia pekee ya kujipoza  ni kunywa”Aliongea kijana huyu na kisha alijikokota na kuingia chumbani kwake huku nyuma akimuacha Raheli aliekuwa akimwangalia kwa huzuni.

“Tutampa jina la Edna”Aliongea huyu mama mtu mzima na Raheli alitabasamu.

“Ni jina zuri mama”.

Upande mwingine mkoani Ruvuma  manispaa ya Songea  katika familia ya bwana Senga  kulikuwa na majonzi makuu  , huku  mtu aliekuwa akilia kama mtoto alikuwa ni Senga, bwana huyu katika kilio chake alikuwa akitamka  neno ‘Mke wangu na mtoto wangu mmeniacha ‘ bwana huyu alionekana watu wake muhimu walikuwa wamapatwa na jambo baya sana.

“Yote ni mipango ya Mungu Senga huna budi kumshukuru Mungu”.

“Hapana Desmond , ndio kwanza naanza kuyaona mafanikio lakini mafanikio yangu  yanasababisha  mke wangu  na mtoto wangu Denis kufa , bora ningebakia maskini huenda wasingeweza kupanda ndege na haya yote yasingewatokea”

Senga alikuwa akilia sana , na katika kilio  chake ilionekana   yeye ni moja ya familia  nyingi duniani ambazo  ni wahanga wa upoteaji wa ndege ya Malaysia Airlines.

Hakuna alieweza kumfariji bwana huyu akapata unafuu , mapenzi yake kwa watu walipotea na ndege yalikuwa ni makubwa mno , kiasi kwamba hayakuweza kupimika kwa aina yoyote ile ya kipimio, alikumbuka safari ya kimaisha aliopitia na mke wake Blandina ya msoto hatimae kupata pesa   na utajiri na Mungu akawabariki mtoto wao wa kwanza , lakini Mugnu huyo huyo akawachukua  wote wawili na kumuacha Senga akiwa  katika majonzi na machungu makubwa ndani ya moyo wake , hakika maumivu yake hayakuwa ya kupimika hata kidogo na na waliokuwa karibu yake hawakuweza kufanya jambo lolote Zaidi ya kumuonea huruma.

Bwana huyu hakujali tena mali alizokuwa nazo , alikuwa radhi kutoa kila kitu alichokuwa nacho iwapo mtu yoyote atatokea na kusema kwamba anaweza kuwarejesha wapendwa wake  duniani , lakini bado jambo hilo halikuwa likiwezekana , na  tumaini hilo likabakia kuwa ndoto ya mchana.Na waswahili wanakazia kwa msemo wao , alieenda ameenda na waliobaki Maisha yanaendelea,

T

Previoua Next