TANZANIA 2013 -JULY
Ilikuwa ni mwezi July ndani ya jiji la Dar pilika pilika zilikuwa za hali ya juu ndani ya jiji hili , si kwa wanausalama ,sio kwa majeshi , sio kwa wananchi , kwa mara ya kwanza jiji la Dar linaonekana kuwa safi kuliko siku zote.lakini haikuwa kwa swala la usafi tu , lakini pia ulinzi ulikuwa umeimarishwa kila kona ya jiji hili, huku makachero wa kizungu pia wakionekana kulandalanda huku na huko kuhakikisha hali ya usalama.
Naam hii yote nikutokana na ujio wa Raisi wa taifa kubwa duniani , taifa lenye ushawishi kila kona ya dunia , taifa ambalo lina uchumi mkuwa duniani , taifa ambalo linaongoza kwa teknolojia kubwa duniani,Raisi ambaye kwa mara ya kwanza anazuru ndani ya taifa la Tanzania na kufanya dunia isimame na kushangaa tukio hili la kipekee kabisa kutokea ndani ya taifa hili.
Ni baada ya masaa kadhaa ya ndege kubwa ya Raisi kutua ndani ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na mheshimiwa Raisi Kigombola raisi wa Tanzania akiongozana na viongozi wakubwa wa Tanzania walionekana kuwa katika hali ya furaha maa baada ya kumpokea raisi Barrack Mabo.
Mheshimiwa Raisi Kigombola alijisikia fahari sana , na katika Maisha yake ya uongozi alijihisi ni jambo kubwa sana ambalo amelitimiza , kwa kumtoa raisi wa dunia ambaye alikuwa na majukumu mengi duniani na kuja kutembelea taifa dogo la Tanzania.
“Ndoto zangu zimetimia nina uhakika maadui zangu ndani ya taifa hili wataelewa uwenzo na nguvu niliokuwa nao.,kumleta raisi wa Dunia Tanzania sio jambo dogo”Aliwaza mheshimiwa huyu wakati wimbo wa Taifa ukiendelea , licha ya kwamba mzee huyu alikuwa akiimba wimbo huu lakini akili yake iilikuwa ikiwaza maadui zake na mipango yake.
“Tanzania itakuwa yangu milele na milele ,m nitaacha mizizi ambayo hakuna kiumbe yoyote ambaye ataweza kuingoa”Aliendelea kuwaza.
Baada ya shamra shamra za aina yake hatimae safari ya kuelekea ikulu ilianza huku asilimia tisini ya ulinzi wa raisi huyu ulikuwa ukiratibiwa na vikosi vyake ambavyo vilikwisha kutangulia nchini kuhakikisha hali ya usalama.
“Karibu sana Rafiki yangu ndani ya Tanzania”Aliongea mheshimiwa Kigombola .
“Asante sana Kigombola , nimefurahi na mapokezi ya watanzania”aliongea na kumfanya mheshimiwa Kigombola aendelee kujiona yeye ndio yeye na ndio Raisi wa Tanzania ambaye ana akili nyingi kuliko raisi yoyote yule.
Baada ya chakula mheshimiwa Bamo alipewa ofisi yake kwa ajili ya kuendelea na majukumu ya kazi , kwani bwana huyu hakuwa ni mwenye kupumzika kabisa , muda wote alikuwa macho akifanya kazi , alikuwa ni raisi wa Taifa la Marekani , lakini alikuwa akitoa maamuzi na maelekezo yanayoenda kutekelezwa na maraisi wa mataifa mengine na hii yote inaifanya kazi yake kuwa ngumu sana na kumfanya kuwa bize.
Wakati akiendelea na kazi ndani ya ikulu ya Tanzania aliingia bwana mmoja alievalia mavazi ya kikachero yenye nembo ya taifa la Marekani, bwana huyu alionekana kuwa kijana mdogo , lakini alikuwa na nafasi kubwa katika kikosi cha ulinzi cha mheshimiwa huyu.
“Nipe Ripoti Chriss?”Aliongea mheshimiwa huyu na kisha akampatia mheshiwa Bahasha aliokuwa ameishikilia mkononi na Raisi huyu aliifungua na kuangalia kilichomo ndani , na alikuta ni picha, alizitoa na kuanza kuziangalia na bwana huyu macho yalimtoka.
“Wanafanana kwa asiliamia kubwa na Agent no 17, Umefuatilia ni nani baba wa mtoto huyu?”
“Mheshimiwa tumekusanya ripoti kadri tulivyoweza , huyo mwanadada anaitwa Edna ni mtoto wa Rahel na Adebayo wanafamilia wanaomiliki kampuni changa ya VEXTO”.
“Lakiini imekuwaje huyu Edna akafanana kwa asilimia mia moja na Agent 17?”.
“Hilo ndio swali lililofanya tuendelee kufatilia kwa ukaribu kama kuna muunganiko wowte kati ya 17 na Edna na katika uchunguzi tuliofanya tulibaini watu waliohusika kumfanyia matibabu Rahel kipindi cha ujauzito wake , wote walifariki vifo visivyoleweka lakini swala hilo halikuweza kutukwamisha kupata taarifa na kutokana na uwepovyanzo vingi vya taarifa tulivyovipandikiza hapa nchini tumegundua Agent 17 na Edna walizaliwa mapacha wa kufanana”.
“Nini, unahakika na hio taarifa Chriss”
“Ndio mheshimiwa”.
“Sawa Chriss , kazi nzuri kaendelee na majukumu yako mengine , ila hili swala kwa sasa nitampatia mtu mwingine ashughulike nalo , kwasasa hatupaswi kufanya jambo lolote lile”Aliongea Mheshimiwa naChriss alitoka ndani ya ofisi.
Baada ya Chriss kutoka mheshimiwa alirudia kuangalia zile picha mezani kwake kwa umakini mkubwa huku akionekana kuwaza sana.
“Hapana kwa namna yoyote ile siwezi kuruhusu tundu lolote ambalo litafanya Operation LADO kufichuka, Uwepo wa Edna duniani utamfanya Agent 13 na 17 kutaka kufahamu ukweli uliotokea katika Maisha yao ya nyuma kama watabahatika kumuona Edna na suluhisho la haya yote ni Edna kufa”Aliwaza mheshimiwa huyu huku akiangalia picha hizo.
Baada ya lisaa kukaa kwenye ofisi yake hatimae mheshimiwa Kigombola aliingia ndani ya ofisi hio na kukaa kwa ajili ya mazungumzo na mheshimiwa , swala la kwanza ni juu ya mipango yao , ambayo imemfanya bwana huyu mwenye madaraka makubwa duniani kufika ndani ya taifa , lakini pia swala la pili ni jambo binafsi alilokuwa akitaka kuomba msaada kwa Kigombola .
“Kigombola , kuna jambo la ziada unapaswa kunisadia”Alianzisha maongezi.
“Jambo gani hilo mheshimiwa wewe ni Rafiki yangu na nipo tayari kukusaidia jambo lolote hata kama unataka kasehemu ndani ya hii nchi naweza kukupatia”.Alitabasamu na kisha akatoa picha na kumpa Kigombola.
“She need to die and you as my friend utanisaidia katika hili”Aliongea Bamo na kumfanya Raisi wa watanzania ashangae nini tatizo.
“Mheshimiwa kuna haja gani ya mtoto kama huyu kufa?”.
“Kigombola fanya kama ninavyokuambia huyu msichana lazima afe la sivyo mafanikio yangu ambayo nimeyajenga kwa miaka na miaka yanaweza kuwa hatarini na uwepo wa huyu msichana”Aliongea na kumfanya Kigombola kumwangalia mheshimiwa mwenzake na kutingisha kichwa kwamba jambo hilo atalifanyia kazi.
Wakati hayo yakiendelea upande wa pili nchini Rwanda Jeremy anapokea taarifa kutoka kwa shushu wake ikulu iliokuwa kwa mfumo wa ujumbe wa sauti.
“Edna yupo hatarini kubaki nchini Tanzania”
“Nilitegemea swala hilo , ngoja niwasiliane na upande wa pili wa mpango wetu”Alijibu na simu ilikatwa.
“Fu**ck you Amerika , I must pay for what you Did , nitachimba na kuujua ukweli wote”Aliongea kwa hasira Jeremy.
****
Edna kama kawaida yake alikuwa amekaa chumba chake cha kujisomea akiwa anafanya baadhi ya kazi za hapa na pale kama ilivyokuwa kawaida ya mwanadada huyu kutokupumzika , lakini ufanyaji kazi wake wa leo mwanadada huyu haukuwa kama wa siku zote , alikuwa ni mwenye kuwaza mambo kadha wa kadha lakini kubwa lililokuw andani ya kichwa chake ni juu ya Roma.
Aliinua simu yake na kisha kuangalia picha zilizotumwa na Suzzane zikimuonesha Roma akiwa na Doris siku kadhaa nyuma wakionekana wameshikana viuno , lakini pia picha ya pili ilikuwa ikimuonesha Roma akitoka ndani ya nyumba ya Rose , lakini picha nyingine ikimuonesha Roma akiwa amekumbatiwa na mwanadada ambaye sura yake haikuonekana , lakini pia picha nyingine Roma akibusiana na Nasra kwenye gari , lakini pia picha nyingine Roma akiingia ndani ya chumba cha hoteli na Neema luwazo , Picha zote hizi zilitumwa na mwanadada Suzzane mlinzi wa siri wa Edna.
“Suzzane anafanya mambo ambayo sijamwagiza , haikuwa na haja ya kumfatilia Roma , ni mume wangu ndio lakini sio kwa mapenzi ila kwa mkataba na ukiisha tunaachana , sitaki kuyaingilia sana Maisha yake” Aliwaza
Licha ya kuona picha hizo lakini kwa Edna hakuonyesha kukasirika alichukulia kawaida tu lakini alionekana kuna kitu hakipo sawa , aliona licha ya Roma kuwa mume wake kisheria ,, lakini hakuwa akiishi kama mume wake ,vitendo ambavyo aliona Roma anafanya vitamletea shida kama watu watagundua kuwa Roma ana mahawala wengi
Wakati akiendelea kufikiria mala mlango wake uligongwa na alinyanyuka na kwenda kuufungua na uso kwa uso na Roma.
“Honey Darling Chakula tayari , twende tukale”Aliongea Roma huku akiwa ametabasamu na Edna alimwangalia Roma na hakummaliza.
“Sijisikii kula” Aliongea na kisha akafunga mlango kwa hasira , ila Roma hakuondoka alisimama na kugonga tena na awamu hii mlango ukafunguliwa tena na mwanadaa huyu huku akionekana ni mwenye kuwa na hasira.
“Hivi Roma nini , si nimekuambia sijisikii kula , unaweza kwenda kuendelea”
“Namimi siwezi kula peke yangu, na nitaendelea kugonga mlango mpaka ushuke tukale” Edna alimwangalia Roma na kwa alivyokuwa ana muona Roma aliamini bwana huyu alichokiongea alikuwa anaaanisha.
“Kale na Bi Wema , kama huwezi kula peke yako”
“Bi wema kasema hajisikii vizuri atakula baadae,Mke wangu mbona huna heshima kwa mumeo twende basi”
“Yaani Roma wewe sijui ni mwanaume wa aina gani huelewi”Aliongea Edna huku akitoka na kufunga mlango na kuelekea chini akitangulia huku Roma akimwangalia kwa nyuma na kuishia kutabasamu.
Bi Wema aliekuwa akiingia kutoka nje alijikuta akitabasamu na moyo wake kuwa wa moto mara baada ya kuona Roma na Edna wakiwa kwenye meza wakila chakula , ilikuwa ni picha ambayo ilimvutia sana, kwake na alitamani iwe kila siku kuona wanandoa hao wanafanya mambo kwa pamoja , hakupenda namna Maisha ambayo Edna alikuwa akiyaishi , alikuwa akiamini mwanamke hawezi kukamilika pasipo ya kuwa na mume na pia Mume hawezi kukamilika pasipo ya kuwa na Mke.
“Roma ..!!!”Aliita Edna na Roma alimwangalia Edna.
“Ndio mke wangu”
“Kwanini haupo kama wanaume wengine”.
“Unamaanisha nini mke wangu , usiniambie ushaanza kunifananisha na wanauame wengine?”
“Sio kukufananisha na wanaume wengine , lakini wewe upo tofauti kabisa , haupo siriasi na Maisha , kazi umepata lakini unaishai kucheza gemu na kufanya uzinzi”Aliongea Edna huku akionesha yupo siriasi ila Roma hakujali kwanza alitabasamu.
“Mke wangu nitakuwaje siriasi na pesa zote hizo ulizonazo , nani wakuzitumbua, wote tukiwa na pesa hainogi bebi , mmoja akiwa tajiri mwingine asiwe na pesa ili kuwe na mtu wa kutumbua pesa na kula bata ,Bebi Edna tuseme wewe umeolewa na mimi na ukanikuta na mipesa kama hii yako, kwanini uanze kujihangaisha na Maisha badala ya kula bata”
“Kwa hio wewe kazi yako ni kutumbua pesa zangu ?”
“Halafu mke wangu sio pesa zako ni za kwetu , ushasahau sisi ni mwili mmoja”Edna alimwangalia Roma kwa hasira kali mno , alishindwa kuelewa Roma ni mtu wa aina gani yeye yupo siriasi kumwambia mambo ya maana lakini anaanza kuongea ujinga juu ya maswala ya kutumbua hela.
“Kama unawaza kutumbua pesa zangu sahau , usipo tafuta zako hutipata chochote kutoka kwangu”
“Mke wangu kama hutaki nikitumia pesa zako nani atazitumia ...Halafu mke wangu mbona kama unampango wako kichwani wa sisi kutafuta mtoto halafu huniambii nijiandae”Edna alimwangalia Roma huku akishangazwa na uroppokaji wake , ‘Neno mtoto ‘ ni swala ambalo hakuwahi kulifikiria hapo kabla .
“Nani mimi … Mtoto ,, hata kama nitake mtoto siwezi kuzaa na mwanaume asiye siriasi na maisha Watoto wataiga nini”.
“Bebi kama hutaki kuzaa na mimi mumeo unataka uzae nje ya ndoa ?”Edna baada ya kuona topic ambayo hakuwa akiipenda Roma kaikomalia , alinyanyuka na kupandisha Ngazi kuelekea chumbani kwake huku Roma akiwa ni mwenye kutabasamu.
“Huyu mwanaume muda wote anafikiria ujinga tu , nifanye nini ili angalau kumbadilisha ili hata niwe na kujiamini nikimtambulisha mbele za watu”Aliwaza Edna huku akiwa amesimama kwenye dirisha chumbani kwake.
Ukweli ni kwamba kuna muda Edna alitamani kumuona Roma abadilishe mfumo wake wa kimaisha , alitamani awe kama wanaume wengine ambao wako bize na kutafuta Maisha na kuongoza biashara hatimae aweze kujivunia kuwa na mume mwenye mafanikio , lakini haikuwa hivyo , Roma alikuwa Roma kama alivyomtoa kule kwenye kazi yake ya ubeba mizigo , hakuwa amebadilika hata kidogo ,tabia yake ilikuwa vilevile
Edna wakati akiendelea kufikiria akiwa anaangalia eno la Nje alimuona mwamba Roma akaitoka tena awamu hii akiwa amepigilia miwani ya jua kabisa na haikueleweka katioa wapi , alimwangalia namna ambavyo anaingia kwenye gari yake na kuwasha na mpaka lilipotokomea nje ya geti.
“Lazima anaenda kutafuta mwanamke pale”Aliwaza Edna huku akirudi kitandani na kukaa.
Comments