Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

Baada ya Roma na Donyi kurudi  tu nchi kavu , mara vijana waliokuwa wamevalia Suti walikuja na kumzunguka Donyi , kitendo ambacho kilimuuzi sana Donyi kwani hakupenda walinzi  ambao walikuwa wameajiriwa na baba yake kwa aili ya kumilinda.

Alimgeukia Roma huku walinzi wale wakimwangalia  Roma kwa macho ya utahadhari , lakini kwa upande wa Roma kwanza hakushangaa sana , maana baada ya kukumbuka kwamba msichana huyo alimwambia kuwa anasoma chuo cha Yale , chuo ambacho licha ya ada yake kuwa kubwa  lakini pia sio wanafunzi wote kutoka mataifa ya  Afrika wanaweza kusoma ndani ya chuo hiko na hilo kwa Roma ilikuwa ishara tosha kwamba Donyi familia yake haikuwa ya kawaida ndani ya taifa hili la Tanzania.

“Siku nyingine Mungu akitukutanisha nitatimiza  ahadi yangu”Aliongea Donyi na Roma alitabasamu na wakagana , ukweli ni kwamba Roma hakuwa na mpango wa kulala na  mrembo huyo   hakuelewa ni kwanini lakini hakuwa na msukumo wa  aina yoyote wa kufanya nae mapenzi.

Muda umekuwa umeenda na Roma hakuwa na mpango wa kukaa sana nje ya nyumbani kwa siku ya leo , aliwaza kwenda  nyumbani akapumzike.

Masaa machache tu alikuwa ashafika na kuingiza gari yake ndani, lakini aliona gari mpya ndani ya eneo la kuegesha magari kwa muda  na aliona  lazima kutakuwa na ugeni , lakini bado alijiuliza ni nani kafika nyumbani kwake muda huu  wa  jioni  ya saa  kumi na mbili.

Kama alivyohisia kuwa kuna  mgeni , ni kweli aliona mwanaume ambaye hakuwa akimjua akiwa ameketi kwenye  masofa  , uwepo wa huyu mwanaume haukumchanganya sana wala kumshangaza ,  kilichomshangaza ni kwamba Edna alionekana kucheka kweli mbele ya huyu mwanaume  na alijiuliza ni ukaribu gani  mwanaume huyu anao  na mke wake.

Roma karoho ka wivu kalianza kumuingia  , kwani  licha ya kwamba zilikuwa ni siku chache tokea aanza kuishi na Edna  hakuwahi kumuona mwanadada huyo akifurahia namna hio.

“My Beutifull wife nimerudi”Aliongea Roma na kisha alienda moja kwa moja upande ambao alikuwa amekaa Edna na kisha akambusu shavuni  , Edna alitamani amkwepe Roma lakini alishindwa kufanya hivyo kwani kulikuwa na mgeni.

“Mke wangu hujanitambulisha kwa mgeni na wala haujaniambia kuwa tunatembelewa leo”.

“Elvice huyu ni  mume wangu , anaitwa Roma , Roma huyu ni  Rafiki yangu  wa utotoni mpaka ukubwani anaitwa Elvice ni  mwanajeshi   lakini pia ni rubani”Aliongea Edna kwa kuchangamka , lakini muda wote bwana huyu mgeni mwenye sura ya kihandsome , anaejipenda kutokana  na mavazi yake  , alionekana muda wote kumuangalia Roma  pasipo kummaliza, ni kama alikuwa akimlinganisha  na  Edna na kujiuliza  imekuwaje Edna akaolewa na mtu wa kawaida kama Roma.

“Nafurahi  kukufahamu  Elvice ,japo sijapenda  uzuru wa usiku usiku nyumbani kwangu”Aliongea Roma na Edna aliekuwa karibu na Roma kwenye sofa alimfinya, ila Roma hakujitingisha wala kuonesha dalili za maumivu.

“Nafurahi na mimi kukutana na  wewe Roma , nimekuwa ni wakujiuliza ni mwanaume wa aina gani   kaweza kuutingisha moyo wa Edna, nadhani  sasa nina majibu”Aliongea Elvice .

“Roma Elvice alikuwa akinisimulia habari za Jeshini , hapa nimejikuta nikicheka hatari , zinachekesha kwakweli ,Elvice hebu tuendelee  na hio stori basi”Aliongea Edna  huku  leo akionekana ni mwenye kuchangamka sana kuliko siku zote.

Elvice aliendelea  na stori  huku Roma akiwa pembeni  akisikiliza hio stori ambayo imemfanya  mke waka afurahi , lakini kadri Elvice alivyokuwa akiendelea kusimulia , Roma aliona ni uongo mtupu.

“Acha kumdanganya mke wangu”Aliongea  Roma huku akionesha hasira sana.

“Unamaanisha nini  nadanganya , ushawahi kufika jeshi wewe,Nikuambie tu Mr Roma ukkama ungepewa kikosi kama nilichopewa mimi   ukiongoze  na ukakutana na kipigo ungejikojolea”Aliongea Elvice lakini kwa Roma maneno yale yalionekana kama kejeli.

“Unaongea upumbavu , unaongea mambo ambayo hayana uhalisia hata kidogo  na ole wako uendelee kumdanganya mke wangu uone”Aliongea Roma kwa  msisitizo lakini Elvis alionekana kuendelea , swala hilo lililimfanya Roma  ahisi kichwa kuuma sana  na  kuanza kuona pichapicha  za miili ya watu ikiwa imekufa ikiwa imemzunguka  huku yeye mikono yote akiwa na damu. Ni kama  vile muvi ilikuwa ikipelekwa mbele kwa  namna ambavyo Roma alianza kuona mapicha picha hayo  , maumivu ya kichwa yalikuwa makali kiasi kwamba aling`ata meno  na kuinama  , lakini Elvice aliendelea kusimulia , kila neno ambalo Elvice alikuwa akiongea ni kama  lilikuwa live kwenye kichwa cha Roma .

Elvic na Edna hawakujua kinachoendelea   kwani Roma macho yalikuwa yashabadilika Rangi na kuwa  ya kijani huku yakiwa yametengeneza aina flani ya mishirizi ya damu.. lilikuw ni picha ya lutisha

Ilikuwa ni kitendo  cha haraka sana Elvice alijikuta akining`inia hewani huku akianza kukohoa mfuliulizo , huku Roma akiwa amemshikilia kwa mkono mmoja.

“Nikikuambia acha acha  , kwangu onyo ni mara moja tu”Ni sauti kama ya Roboti iliokuwa ikisikika Sebuleni hapa  na kumfanya Edna atetemeke , alimuona kabisa Roma akiwa amebadilika macho , na leo hii  kwake ni kama ilikuwa mara ya kwanza  kumshuhudia Roma rangi ya  mboni za macho yake kuwa za kijani , mrembo huyu alitetemeka , lakini kwa Elvice alionekana ni kama mtu aliekuwa akinyongwa na Kamba kwenye shingo kwani alikuwa akitapatapa  kwa kurusha miguu kukata roho huku Roma akionesha hana ishara kabisa ya kumuachoa na alionekana alikuwa akishindwa kuutawala mwili wake kabisa , kwani muda hio alionekana kama mnyama ambae mbele yake kulikuwa na kitoeo

Ilikuwa ni  kitendo cha kijasiri sana alichokifanya Edna , alimsogelea Roma kwa nyuma  na kumkumbatia  akipitisha mikono kwa mbele..

“Roma Please Stop….”Aliongea Edna huku  akitoa machozi  na ni kama  vile Roma alichomwa na sindano  kwani  alimwachia Elvice  akadondoka chini  na kisha akageuka nyuma na kumwangalia Edna anavyolia  na  ilichukua sekunde chache tu  Roma alidondoka chini  na kuzimia.

“Romaaa… Romaa !!!”Ilikuwa ni kama ndoto iliokuwa ikiendelea katika kichwa cha Roma , kwani  alijiona akiwa yupo  katikati ya msitu mnene  huku akimwangalia mwanamke aambaye alikuwa amefanana kwa kila kitu kama Edna  akimkimbilia huku akiliita  nina lake ,  na hii yote ni baada ya Roma kupigwa risasi ambazo zilitua kwenye kifua chake,Risasi ambazo zilimpiga mfululizo , lakini wakati mwanamke yule  akimkimbilia , mara aliona watu wale wale waliompiga  risasi  wakiwa wamevalia mavazi yao meusi na mahelmet usoni  , wakimpiga mwanamke yule anaefanana kwa kila kitu na Edna risasi za mgongoni na mwanamke yule mrembo alievalia mavazi kama  ya wakorea(robes) , alidondoka chini huku akiendelea kuliita jina la Roma huku Roma na yeye akijitahidi kutamka  neno.

“Seven … ntee..n !!” Roma alijikuta akizinduka ghafla  , na kujikuta akiwa kwenye masofa huku mke wake akiwa pembeni yake akiwa anamwita kwa wasiwasi huku machozi yakiwa yamejilenga katika mboni za macho yake  , aligeuka na kuangalia pembeni na kumuona Bi Wema.

“Nini kimetokea  mke wangu?”Aliongea Roma huku akionekana ni mwenye kusahau jambo ambalo amelifanya  dakika chache  nyuma  za kutaka kumuua  Elvice.

“Roma .. haukumbuki kilichotokea?”aliuliza bi Wema huku akionekana ni mwenye wasiwasi sana , ila Roma  hakuwa akikumbuka amefanya nini dakika chache nyuma. ,Edna na yeye haikueleweka ni nini kilichompata  ghafla kwani  alionekana kutoa machozi mfululizo huku akimwangalia Roma pasipo kusema neno , aliishia kunyanyuka mwanadada huyu na kukimbilia chumbani kwake , akimuacha Roma katika hali ya mshangao.

“Ndio nakumbuka kulikuwa na mwanaume hapa akipiga stori na  Edna  na nikamtahadharisha kwa kumwambia aache  kuongea maswala ya vita , lakini hakuacha na sikumbuki kilichotokea baada ya  hapo”Aliongea Roma   huku akimwangalia Bi Wema.

“Usijiumize sana kichwa Roma nenda ndani kapumzike”Aliongea Bi wema na kumuacha Roma aende chumbani kwake akapumzike.

Roma baada ya kuingia  chumbani kwake alionekana kuwa mwenye wasiwasi  sana .. kwa tukio alilolifanya muda mchache uliopita.

“Inawezekana ugongwa wangu unanirudia”Aliongea huku akisogelea begi lake  alilitoka nalo Mbagala Rangi tatu baada ya kuhamia hapo na kuanza kutoa nguo kwa pupa na alionekana  ni mwenye kutafuta kitu Fulani kwenye begi hilo na alikipata baada ya dakika chache za kuchanguza.

Kilikuwa ni kichupa  kidogo mfano wa babycare , lakini kilichokuwa na nembo ya  fuvu  na X katikati , Roma baada ya kupata Kichupa hiki alionekana ni mwenye kuvuta pumzi  ya ahueni.

“Angalau  hizi dawa zipo nadhani zinaweza kunisadia kwa muda , tatizo  hili likiwa kubwa ni hatari kwa binadamu waliopo karibu yangu”Aliongea Roma  huku akifungua kikopo hiko  na kutoa vidonge vyeusi tii kama mkaa na kuviweka kiganjani mwake.

“Lakini nilifanikiwa vipi kurudi kwenye hali yangu ya kawaida  gafla sana?”Alijiuliza swali hilo pasipo kujua ni vipi aliweza  kurudi kwenye hali yake ya kawaida ghafla , alikuwa hajui kama Edna alimkumbatia kwa nyuma na kumsihi aache ndio wakati alipoacha kweli na macho yake kurudi katika hali ya kawaida na kuzimia.

Roma baada ya kufikiria kwa muda , alisogelea tarakishi iliokuwa hapo ndani na kisha aliunganisha na internet  baada ya kumaliza alifungua VPN  na akaandika maneno flani  hivi ya kodi  zilizokuwa na mchanganyiko wa XQ na sifuri  na nukta nyingi nyingi  halafu akabonyeza ‘Enter’ na hapo hapo ikaonekana picha ya Tai  mkubwa mwenye rangi nyeusi na nyeupe , ni kama vile unavyofungua Facebook ile picha ya F Inayoonekana  ndio kilichoonekana kwenye tarakishi hii.

Baada ya picha  ile kutokea , ilikuja sehemu ya kujaza  jina , na Roma aliandika neno PLUTO  na kisha akaweka  password yake yenye herufi Zaidi ya ishirini ambazo hazikuwa kwenye mfumo wa mpangiloio yaani kulikuwa na ‘Cvbnmejdikeydndyodds’Ilikuwa ni nywira ya aina hio ambayo hata kama unawezo wa kukariri vipi usingeweza kuikariri hio nywira , baada ya kuandika alibonyeza kitufe cha ‘Enter’ na hapo hapo  yule mwewe kwa mfumo wa 'animation' alipeperuka na ikatokea video iliokuwa ikimuonesha mwanaume mmoja mwenye ndevu nyingi kama za wataliban lakini mzungu.

“Rìgh Pluto Tha còrr air sia mìosan bhon a rinn sinn conaltradh mu dheireadh”

“Mfalme Pluto ni Zaidi ya miaka sita sasa tokea tulipowasiliana”. Aliongea yule mzee alieonekana kwenye tarakishi hio akiwa na midevu mingi ya kutisha.

“Ndio Sauron , habari za hapo makao makuu ya The Eagles?”Alijibu Roma kwa lufha hio hio

“Hapa ni kwema  Pluto , hakuna mabadiliko makubwa tokea ulivyotuacha na kurudi kwenye nchi yako kuitafuta familia yako”

“Ni vyema kusikia hivyo Sauron , nimefanya mawasiliano na wewe siku  ya leo kwakuwa nahitaji msaada kutoka kwako”

“Mfalme Pluto hauna haja ya kuomba msaada kutoka kwangu , toa amri nifanye kile unachotaka ,The Eagles ni mtandao wako wa kijasusi uliouanzisha na pesa zako , kwanini  uombe msaada kutoka kwangu mimi ni mtumishi wako”Aliongea mwanaume mwenye  ndevu ambaye tunamjua kwa jina la Sauron na Roma aliona ni kweli  hapaswi kuomba  Zaidi ya kutoa  oda ,  alijikuta akitabasamu na kuona kuishi kwa miezi sita ndani ya Taifa la Tanzania kumembadilisha kwani aliwajua wabongo hata kama  jambo ni haki yao ya msingi walikuwa wakiomba tofauti na Wakenya  na mataifa mengine ambao walikuwa wakihirai sio kuomba..

“Kuna mambo makuu mawili nataka uyafanyie kazi  Sauron , jambo la kwanza nataka uangalie  The Zeros  kuna jambo gani la siri lineandelea”

“Mfalme  wangu Pluto samahani kama nitakuwa nimevuka mpaka ila naomba ni kuulize kama The Zeros wamefika Tanzania?”

“Ndio Sauron , leo  walinifanyia mashambulizi  ya kushitukiza na walionekana walikuwa na nia ya kuniua kabisa , jambo ambalo limenishangaza, kwanini waanze kunifatilia baada ya kuwa  kimya miaka yote hio   wakati nilitoka  kwenye   kundi lao kiamani kabisa na kuunda kundi langu”Aliongea Roma  na kumfanya mwanaume aliekuwa akionekana kwenye Tarakishi hio ashangae.

’Nitafanya hivyo  Mheshimiwa Pluto , nitatuma afisa vipenyo wetu wenye uwezo wa hali ya juu kufatilia nini kinaendelea ndani ya The Zeros , naomba uniambie ni jambo  lipi lingine napaswa kufanya”

“Nahitaji Mercenary(Masenari)  wasiozidi kumi uwatume Tanzania, wakiwa katika mgawanyo sawia wa kimajukumu”Aliongea Roma kwa kilugha na kama ungemsikia ungeshangaa na ukajiuliza huyu jamaa ni nani , kwani aliongea kama anavyoongea Kiswahili.

“Hakuna shida The Great Pluto  , unataka  waje na siraha za aina gani , vifaruu, ndege za kivita au meli?”Roma alijikuta akicheka na kuona Sauron utani wake haujaisha.

“Nataka waingie nchini kama watalii wakiwa na silaha za ukimya(silent Weapons) ili wasije wakashikwa kwenye rada za wanausalama wa taifa la Tanzania”

“Sawa  mfalme Pluto nitazingania hilo na nitafanya arrangement mapema na nitakupa ripoti kesho”.

“Nitakutafuta Mimi Sauroni muda wa mchana”

“Sawa Mtukufu mfalme Pluto nitahakikisha maombi yako yanafanyika na kujibiwa kwa wakati , naamini huko nchini Tanzania ni  usiku , nikutakie usiku kwema”

“Na wewe nikutakie asubuhi njema Sauron , wasalimie Watoto wako na mkeo mary”Baada ya maongezi hayo Roma  a.k.a Pluto a.k.a Hades alikata simu na kisha kurudi kitandani kukaa chini.

“Sina jinsi The Zeros ni ‘Assasination  group’ ambalo kama wakiamua jambo lao la kimauji lazima  lifanikiwe , mimi  ni uzao wao na nimeishi ndani ya uhatari wao na nisipochukua tahadhari mapema Edna  anaweza akaingia  matatizoni kwa sababu yangu”Aliwaza Roma huku akijiandaa kuingia bafuni kuoga maana  mwili wake ulikuwa na maji ya chumvi ya baharini.

Upande wa Edna  alionekana ni mwenye mawazo  sana , kwanza kabisa alikuwa akijiuliza kwanini moyo ulimuuma sana mara baada ya Roma kubadilika na kuwa kama  kiumbe ambacho hakina ubinadamu  ndani yake , alijiuliza kwanini moyo wake ulikuwa ukimuuma sana mara baada ya Roma kudondoka chini , lakini pia alijiuliza kwanini alivyomkubatia Roma ghafla tu  Roma  macho yake yalibadilika na kurudi  kawaida, lakini pia alijiuliza kwanini alijihisi kitu cha ajabu katika mwili wake baada ya kumkubatia Roma  hayo ndio maswali aliokuwa akijiuliza mwanadada huyu nakukosa majibu.

 Kama kuna kipande kimefutwa au hukioni acha comment hapo chini

Previoua