Damiani ni kijana wa miaka ishirini na mbili, mhitimu wa chuo kikuu cha Tanzania Institute of Accountancy (TIA), akiwa amechukua kozi ya Finance and Accounting in Public Sector (kozi inayohusu masuala ya uhasibu). Mara baada ya Damiani kumaliza masomo yake, hakutaka kubaki ndani ya jiji la Dar es Salaam kwani hakuwa na kazi maalum ambayo ingemuwezesha kujiingizia kipato ndani ya jiji hilo. Pia, maisha ndani ya jiji hilo yalikuwa ghali sana na yalihitaji pesa ili kuweza kuishi.
Hivyo, mara baada tu ya kumaliza masomo yake, aliamua kurudi nyumbani kwao kijijini, mkoani Tanga, kwa ajili ya kusikilizia upepo wa ajira. Mwaka ambao alikuwa amemaliza masomo haukuwa kama miaka ya nyuma ambapo ukimaliza unasubiria matokeo na kupata ajira mara moja. Kinyume chake, ilimbidi asubiri matokeo yatoke, kisha kuomba ajira kwa makampuni yenye uhitaji ama serikali pale itakapotangaza nafasi za ajira. Wakati huo, kulikuwa na wimbi kubwa la vijana wahitimu wasio na ajira, hivyo kupata nafasi ilikuwa ngumu sana—ilikuwa kama bahati nasibu kwani waombaji wengi walikuwa na sifa zinazofanana.
Kijiji cha Mkuzi
Mkuzi ndicho kijiji alichotokea kijana Damiani. Kijiji hiki kilikuwa ndani ya Wilaya ya Lushoto, kilomita kadhaa kutoka Lushoto mjini. Safari kwa gari ilichukua dakika 30 hadi 40 kufika kijijini hapo. Mkuzi kilikuwa ni moja ya vijiji vilivyozungukwa na misitu na kuwa na mazingira ya kuvutia sana. Mazingira yake yalikuwa miongoni mwa vivutio vilivyowafanya watalii wengi wa mataifa ya nje na hata watalii wa ndani kupenda kutembelea eneo hilo, hasa kutokana na hali yake ya hewa safi na ya kuvutia.
Damiani alikulia kijijini hapo na kupata elimu yake ya msingi na sekondari. Alikuwa kijana mpole, mcheshi, mrefu, mwenye rangi ya maji ya kunde, na sura iliyochongoka vizuri. Mwili wake ulikuwa wa wastani, na alikuwa akiishi na mama yake pekee, kwani baba yake alifariki dunia akiwa na umri wa miaka kumi.
Kurudi kwa Damiani kijijini baada ya kumaliza masomo yake ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa mama yake. Alifurahi kumuona mwanae akirejea, kwani alimpenda sana.
"Karibu sana mwanangu!"
Mama yake alionyesha furaha yake kubwa kwa mwanae kumaliza masomo ya juu, akihisi kuwa amefanikiwa kulea mtoto wake vizuri. Kwa kijiji chao, si watoto wengi waliokuwa wakifanikiwa kufika kiwango hicho cha elimu.
"Asante mama, hatimaye nimemaliza chuo na nimerudi rasmi,"
aliongea Damiani huku akiachia tabasamu. Huko nje, watoto wengi walikuwa wakimwangalia na kumshangaa—hali iliyozoeleka sana vijijini kwa wale waliotokea mjini au kwa wageni.
Mama yake alimkaribisha vizuri Damiani katika nyumba yao ya vyumba vitatu iliyoezekwa kwa samora. Kwa kuwa alikuwa na chumba chake tangu akiwa shuleni, mama yake alipeleka begi lake huko na kufanya usafi.
Malengo ya Damiani
Maisha ya kijana Damiani ndani ya kijiji cha Mkuzi sasa yalianza rasmi. Pamoja na kuwa kijijini, alikuwa na mipango mikubwa sana kwa maisha yake ya baadaye. Alitamani kuwa mfanyabiashara mkubwa sana, ndicho kilikuwa kipaumbele chake, japo alikuwa na elimu na alitarajia kuajiriwa. Hata hivyo, ajira kwake haikuwa jambo la msingi sana. Lengo lake kubwa lilikuwa kupata mtaji wa kuanzisha biashara.
Alijua wazi kuwa safari yake ilikuwa ndefu, lakini hakutaka kukatishwa tamaa na mazingira aliyokulia. Alijiamini kuwa kwa bidii, juhudi, na malengo sahihi, angefanikiwa. Hakutaka hali ya maisha ya umasikini nyumbani kwao iwe kikwazo, bali aliamini kuwa mawazo chanya na kazi kwa bidii vilikuwa silaha muhimu za mafanikio.
Hatimaye, wiki, mwezi, na hata miezi ilikatika. Matokeo yake ya mwisho yalitoka, na alikuwa amefaulu kwa daraja la kwanza. Kwake na kwa mama yake, hilo lilikuwa jambo la faraja kubwa sana. Aliamini kuwa ufaulu wake mkubwa ungeweza kumrahisishia kupata kazi kwa urahisi zaidi.
Badala ya kusafiri mpaka Dar es Salaam kutafuta ajira, aliamua kutumia njia rahisi zaidi—kutuma maombi kwa makampuni yote yaliyotangaza nafasi za ajira kwa njia ya mtandao.
Kusubiri Ajira
Mwezi wa kwanza uliisha, lakini Damiani hakuwa amepata ajira. Alikuwa ameomba kazi kwenye makampuni zaidi ya matatu lakini hakuwa amepata hata wito wa mahojiano ya kazi (interview). Siku zilivyozidi kusonga mbele, alihisi kama anaanza kukata tamaa.
Hata hivyo, siku chache baadaye, moja ya makampuni aliyokuwa ameomba kazi ilimrudishia jibu la kuhudhuria interview. Kampuni hiyo ilikuwa ya usafirishaji, yenye makao makuu yake Posta, Dar es Salaam. Kwa Damiani, ilikuwa habari njema sana kwani alihisi kuwa tumaini la kupata ajira lilianza kurejea.
Alienda kumpa mama yake habari hizo, na mama yake alifurahia sana.
"Mwanangu, Mungu atakusaidia, utafanikiwa,"
alimwambia huku akimpa baraka zote kwa ajili ya safari yake ya kwenda kwenye mahojiano hayo.
Safari ya Dar es Salaam
Ilikuwa Jumatatu, siku ambayo Damiani alisafiri kwa basi kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya interview yake. Kabla ya safari, alifanya maombi kwa Mungu juu ya safari yake na kusudio lake la kazi.
Kutoka Lushoto hadi Dar es Salaam ni safari ya masaa sita hadi saba, hivyo alipofika jijini ilikuwa saa nane kamili mchana. Kwa kuwa hakuwa na ndugu wa kufikia jijini, aliamua kwenda kwa rafiki yake Elvis, ambaye alikuwa akiendelea na masomo chuoni.
Akiwa ndani ya basi, alifikiria kwa makini kuhusu kesho yake—siku muhimu ya mahojiano.
Baada ya kushuka kituo kikuu cha mabasi, alielekea kwenye daladala zinazoelekea Mbagala na kisha alishukia Mtongani, ambako rafiki yake Azizi Ally alikuwa akiishi.
Kumpata Elvis
Aliposhuka daladala, alielekea upande wa kushoto wa barabara, akapita vichochoro viwili au vitatu, kisha akafika mbele ya nyumba moja kubwa yenye ukuta. Alisimama nje ya geti akiwa kama mtu anayejishauri—agonge au la?
Baada ya sekunde chache, aliamua kugonga.
Mlango ulifunguliwa na msichana mmoja aliyekuwa amejifunga khanga moja, huku mikononi mwake ikiwa na mapovu ya sabuni—dalili kuwa alikuwa akifua nguo.
"Karibu,"
alisema kwa sauti nyororo.
Damiani alimwangalia kwa jicho la kudadisi—bidada huyo alikuwa mrefu wa wastani, mwenye rangi ya chocolate, uso wa duara, na umbo la kuvutia.
"Nimemkuta Elvis?"
aliiuliza.
"Katoka, lakini atarudi muda si mrefu. Wewe ndiye Damiani?"
"Ndiyo, ni mimi."
"Okey! Alinipa maelekezo kuwa nikukaribishe ndani."
Msichana huyo alimtangulia huku Damiani akimfuata nyuma…
Yaani acha tu, mzee! Toto la toto, na isitoshe limedata! Ndiyo limenifanya nihangaike siku ya leo."
"Unahangaishwa na nini sasa?"
"Hahaha! Lazima kuhangaika! Unajua jana ulivyonicheki unakuja ilikuwa ghafla sana, na sikutaka kukwambia kuwa naishi na mtoto wa kike. Kwa hiyo, unavyoniona hapa, kuna msela nimetoka kumpanga ili ukale mbonji kwake ukamilishe mambo yako. Maana hapa sikuwa na jinsi."
"Dah! Hapo ndiyo maana nakukubali, mshikaji wangu!"
"Hahaha! Usijali, mzee. Si unajua hata wewe umenisaidia mara kibao? Hata mavitu haya ni kama ulinipa tu kutokana na bei ile."
Basi, Damiani alichukuana na rafiki yake na kutoka eneo hilo kuelekea barabarani, kisha wakapanda magari yanayoelekea Rangi Tatu. Walipofika Mbagala Zakhem, walishuka na kuchukua upande wa kushoto wa barabara. Baada ya kutembea umbali wa mita kadhaa, hatimaye waliingia kwenye chochoro ambayo iliwatoa katika mtaa mwingine, na mwishowe wakajikuta mbele ya kanisa la KKKT. Hapo walipinda kushoto tena na kufika mbele ya nyumba moja kubwa yenye geti, ambapo kwa nje ilisomeka kwa maandishi ya "Lodge".
Elvis alisukuma mlango na kuingia ndani, huku Damiani akifatisha tu kuona mwisho wake, kwani kulikuwa na hisia zilizomwambia kuwa kaletwa lodge.
"Oyaa, mshikaji anakaa hapa! Siyo lodge tena japo ilikuwa lodge. Mwenye nyumba kaamua kuifanya nyumba ya kupangisha," aliongea Elvis, jambo lililomfanya Damiani aelewe.
Walipita kwenye vyumba kadhaa na hatimaye wakasimama nje ya mlango mmoja. Elvis aligonga, na baada ya nusu dakika, mlango ulifunguliwa na jamaa mmoja wa makamo, mfupi mwenye mwili mkubwa wa kibonge.
"Karibuni," aliongea jamaa huyo.
Waliingia ndani ya chumba hicho, ambacho kilikuwa kikubwa na kizuri sana. Pia, hata kitanda na samani (furniture) zilizokuwemo humo zilionesha kuwa jamaa anayeishi humo hakuwa mnyonge kipesa.
"Oyaa, huyu ni Joshua, rafiki yangu sana wa mwaka wa kwanza. Hivyo, utachill hapa kwake mpaka utakapo kamilisha mambo yako," alisema Elvis.
Joshua alimkaribisha Damiani, kisha Elvis aliaga na kuondoka.
Siku nyingine iliingia, ambayo ndiyo ilikuwa siku ya Damiani kuelekea mtaa wa Posta kwa ajili ya kufanya interview. Alivaa vizuri, akapendeza, maana kwenye nguo alikuwa nazo, na mkopo ulimsaidia sana kipindi akiwa chuo.
Alijisogeza mpaka barabarani ili kusubiria gari ya kwenda stesheni ya Posta apande. Ila, mara baada ya kufika nje kabisa ya supermarket iliyoandikwa jina "Kivoni", ghafla ilisimama gari moja aina ya Vanguard nyeusi.
Kioo kilishushwa, na akaonekana bwana mmoja wa makamo, makadirio ya miaka 30 kuendelea, mweusi, aliyekuwa amevalia shati jeupe, koti, na miwani.
Damiani, wakati huo gari hiyo iliposimama, alikuwa akiitazama, na hata yule jamaa aliposhusha kioo, macho yao yaligongana. Damiani alijikuta akishtuka, na hiyo ni baada ya jamaa huyo kumuonesha ishara ya kumuita.
Alijihakikishia kuwa ni yeye aliyekuwa akiitwa, ndipo alipopiga hatua kulisogelea gari hilo.
Comments