Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA SABA

★★★★★★★★★★★★★


Lakini nikatuliza zaidi akili na kuanza kuona mawazo ya namna hiyo kuwa ya kipuuzi. Ikiwa mwanaume huyo alikuwa na lengo la kunidhuru eti kisa nimetoka na mwanamke wake, basi ningehakikisha naanguka chini pamoja naye akifanya jambo lolote kuniangusha. Hii ni njia ya kumaanisha kwamba nilikuwa na ujasiri wa kupokea lolote lile ambalo angelileta upande wangu, kwa hiyo nikaamua kuendelea kutulia na kutazama mechi.

Bobo akaanza kumsemesha Tesha kirafiki kuhusiana na mechi iliyokuwa inaendelea, na kijana akawa anazungumza naye pia. Ni mimi pamoja na yule "mwenye Masai" ndiyo pekee ambao hatukuongea, na kila mara nilipovuta chupa ya bia ili kunywa, ningekuta ananitazama usoni, nami ningeonyesha kutojali kabisa alichowaza kunielekea kwa kurudisha umakini wangu kwenye TV. 

Lakini nadhani alikuwa anajaribu kunisoma, hasa shauri ya mimi kuwa mgeni hapa. Alitaka kuona shobo zangu zimekaa vipi, na mimi kiukweli sikuwa mtu wa shobo, kwa hiyo aidha nilimpa ama sikumpa kile alichotarajia; angejua mwenyewe.

Dakika si nyingi sana kupita na wahudumu wawili wakawa wamekuja. Yule aliyetuletea bia mwanzoni pamoja na kengine kafupi na keupe kenye mwili namba nane, mmoja akiwa amebeba kontena lenye bia na mwingine sahani yenye mishikaki ya nyama za mbuzi kama miti 20 hivi. Bila shaka zilikuwa zinapelekwa kwa "boss," navyo vikawekwa kwenye meza yao na vinywaji kufunguliwa. 

Sikujishughulisha nao kabisa. Bobo alikuwa ameanza kuongea na huyo jamaa kuelekea mechi pia, nami nikawa namsikia akitoa maoni yake kuhusu uchezaji wa Simba. Alikuwa na sauti nzito lakini iliyotulia, akionekana kuwa na aina fulani hivi ya mridhiko. 

Nilipovuta bia tena, nikamwona anamsemesha mhudumu mmoja huku akinyooshea kidole chake upande wangu, naye Tesha akaniangalia kwa yale macho yenye kumaanisha aliona jambo hilo, nasi tukaendelea tu kutulia mpaka wahudumu hao walipotoka ndani hapo. 

Bobo akanisemesha kwa kunikaribisha nichukue mshkaki, mimi pamoja na Tesha, nami nilipomwangalia bosi mkuu, akanionyesha ishara kwa kiganja chake kwamba nichukue kweli. Ilikuwa kwa njia tulivu tu, nami nikatikisa kichwa kukubali. 

Tesha akaanza kuchukua huku akitabasamu kiasi, nami pia nikabeba mmoja na kuanza kutafuna. Sikuwa nimesahau kuhusu bastola ya jamaa huko nyuma ya kiuno, na kama hili lilikuwa jaribio lake kwangu ama basi tu aliamua kufanya haya kwa nia zozote, mimi ningeendelea kutulia tu mpaka mechi iishe, kisha niamshe na Tesha. Basi. 

Si dakika nyingi sana kupita nao Simba wakawa wamefunga bao moja. Tukashangilia pamoja, na Bobo, yule baunsa, pamoja na Tesha ndiyo ambao walikuwa na kelele za ushabiki kutokana na furaha waliyopata, ila mimi na jamaa mkuu, ilionekana kama tulikuwa tunavutiana manati vile halafu mawe hatuyaachii. Utulivu niliokuwa nao na yeye ndiyo alikuwa nao hivyo hivyo, tukijiweka kama watu fulani maalumu kweli sehemu hiyo. Na nafikiri alipendezwa na hilo. 

Wale wahudumu wakawa wamerudi tena, wakiwa na makontena yenye bia za Serengeti Lite 20. Zikawekwa mezani kwetu mimi na Tesha, kumi kwangu, kumi kwake. Tesha akamwambia mwanaume huyo anashukuru sana, ikiwa wazi ni huyo jamaa ndiye aliyekuwa ametununulia, na Tesha akasema hapo angezipiga zote kusherehekea ushindi wa Simba ambao bila shaka ungeletwa kwa magoli mengine zaidi. 

Lakini mimi hata sikutoa shukrani. Nikaendelea tu kutulia, nikinywa taratibu tu, nikitoka kwenda kukojoa na kurudi tena kukaa, na mara kwa mara tulipoangaliana na jamaa, angenitikisia kichwa kidogo kuonyesha uwana, nami ningemrudishia kutikisa kichwa kidogo na kuendelea na mambo mengine. 

★★

Tukaendelea kukaa humo mpaka kufikia kipindi cha pili cha mechi, Simba wakiongeza magoli mengine mawili bila kurudishiwa hata moja, na ndiyo kwenye dakika za mwishoni akawa amefika Joy ndani hapo. Mwanamke huyo alikuwa amependeza sana pamoja na wanawake wengine wanne alioingia nao. 

Alivalia blauzi nyepesi kama kaushi, iliyoacha sehemu kubwa ya kifua chake ionekane wazi, fupi kuonyesha kitovu chake, pamoja na pensi ya skinny nyeusi iliyovutwa juu kufikia kiunoni na kumchora vizuri sana pale kati. Mapaja yake yalikuwa wazi, miguuni akivaa ndala za manyoya, na kichwani alikuwa amesuka kwa mtindo mwingine leo hii wa nywele laini kama za wazungu, huku usoni akijidodeka mapodozi na kope fupi za bandia machoni. 

Wenzake pia walikuwa wamevaa blauzi laini, suruali zenye kubana, vikaptura, misuko ya aina mbalimbali na mawigi, wakionekana kuwa na lengo la kuja kufanya umalaya tu sehemu hiyo; kunywa na kutafuta pesa kwa wanaume yaani. 

Joy alipoingia na macho yetu kukutana, akaachia tu tabasamu la kirafiki kutuelekea sisi wote ndani hapo, huku Bobo akianza kumsemesha na yeye kuongea naye. Akamsalimia Tesha kwa kumshika kiganja, kisha akaja kwangu pia na kukishika cha kwangu kisalamu. 

Tulipokuwa tumeviunganisha viganja vyetu, nikahisi kucha ya kidole chake kilichokunjwa ikinisugua katikati ya kiganja kwa makusudi kabisa, nami nikakitoa changu kwake na kuendelea kupokea salamu za wenziye. 

Akanipita na kwenda mpaka kwa bwana wake, naye akakaa karibu naye na kuanza kuzungumza. Wale wanawake wengine wakawa wamekaa kwenye masofa pia, mmoja mwenye mwili mnene kiasi akiwa karibu nami zaidi, naye Bobo akatoka nje kidogo. 

Nilikuwa nimeshakunywa bia nne hivi, Tesha kama sita, nami nikamwona huyo jamaa anamwonyesha Joy ishara ya kidole kunielekea. Nisingeweza kujua kilichoongelewa, lakini nilikuwa tayari kwa lolote. Walilete tu, nami ningewaonyesha nini maana ya jina langu! 

Mechi ya Simba ikaisha, na jamaa akaanza kupiga makofi kufurahia ushindi wa magoli matatu kwa bila. Wengine pia wakaanza kumsindikiza kwa makofi na wanawake waliomo humo kusimama ili kuanza kucheza muziki uliowekwa na Bobo. Jamaa ndiyo alikuwa amerudi tu pamoja na wahudumu walioleta vinywaji zaidi, bila shaka kwa ajili ya Joy na wenzake. 

Nikawa nimeingia chupa ya tano, vibe likiwa limeshaniingia kitambo, nami nikamwangalia Tesha na kumwona alivyojiburudisha kwa kuongea na mwanamke mmoja kati ya wale wanawake walioingia na kumshika-shika mapajani. Ni wazi alikuwa amelewa, na bila shaka angeendelea kunywa tu. Kwa hiyo ningetakiwa kunywa kistaarabu sana ili kuhakikisha usalama wa huyu kijana pia, hasa ukitegemea dada yake alijua tuko pamoja.

Wahudumu walikuwa wamemletea kiongozi vinywaji kama Konyagi, K-Vant, na Valeur, glasi kadhaa pamoja na soda, bila shaka za kuchanganyia na bia hizo kali. Na wakaanza kuzichanganya kweli. Wale wanawake wakawa wanakunywa na kucheza taratibu muziki ulioendelea, naye Bobo akaniletea michanganyiko hiyo ya pombe ili nami ninywe pia. 

Lakini nikakataa, nikisema zingenifanya nijihisi vibaya, naye akampelekea Tesha. Kijana akatae? Nadhani alikuwa ameshaanza kuufurahia huu upendo wa "maVIP" kutoka kwa bosi wa Masai, lakini mimi bado nilikuwa na mashaka yangu. Nikawa nakunywa kwa kutegea tu, huku mwanamke yule pembeni yangu akinishika hapa na pale na mimi kuitoa mikono yake kwangu. 

Nilikuwa nimeweka umakini wangu mzuri kujitahidi kuendelea kuwa macho maana haya mambo ya kunyooshewa-nyooshewa vidole sikuyapenda kabisa, na kufikia mida ya saa nne usiku ikawa wazi kwamba wengine humo ndani walikuwa wamelewa vibaya mno. Ni mimi na Joy tu ndiyo ambao tulitegea kunywa sana, mimi nikiwa nazijua sababu zangu, lakini nisiweze kuzijua za kwake. Hata ile michanganyiko hakuinywa japo mtu wake alimsisitizia sana. 

Bobo, Tesha na baunsa walikuwa wanaongea kweli, wakicheza na wale wanawake kwa mitindo ya kimahaba, huku bosi mkuu, Joy na mimi pekee ndiyo tukiwa tumekaa tu. Hadi nilikuwa nasogezewa makalio na mwanamke mmoja humo karibu na uso wangu na kitikiswa! Si basi tu? Bangi!

Tesha alipoanza kupasua mpaka na chupa, nikaona hiyo ilitosha sasa. Ningehitaji kumrudisha kijana huyu kwao na nije kujitahidi kutoweka mazoea mengi ya kuwa natoka naye kulewa, maana kufanya hivyo kila siku kungeleta picha mbaya pale kwao. 

Nikaimalizia chupa yangu ya tano na kusimama, nisijali kuhusu zingine, nami nikamfata Tesha na kumsihi tuondoke. Akawa ananiambia bado mapema, na nadhani kwa kuniona kuwa nataka kuondoka, yule jamaa akaniponda na kisoda ili avute umakini wangu kwake. 

Nikamwangalia, naye akaniita kwa ishara ya kiganja chake. Hata Bobo akanionyeshea ishara kwa kidole kuwa niende hapo, huku kichwa chake kikiyumba, nami nikamwacha Tesha na kwenda kwa jamaa. Serious. 

Joy si alikuwa amekaa karibu yake? Jamaa akamwambia asogee pembeni kwenye sofa hilo ili mimi nije kukaa katikati yao, na mwanamke akatii. Wakati mwafaka wa kuijua akili yake kunielekea ndiyo ulikuwa umewadia, nami nikakaa karibu naye. 

Akapitisha mkono wake begani kwangu, kirafiki eti, mimi nikiona wazi jinsi pombe ilivyomkonga nyoyoni, hivyo nikaweka umakini zaidi ili nisikie alichotaka kusema.

"Uko poa?" akaniuliza.

Wakati akiwa ananiuliza hivyo, nilianza kuhisi vidole vyake Joy vikinishika pajani na kuanza mipapaso na kunibonyeza sehemu yangu ya siri. Nikajikausha tu.

"Fresh tu," nikamjibu jamaa.

"Kijana uko vizuri sana. Yaani vizuri sana. Na wewe mwanasimba, au siyo?" akaniuliza hivyo.

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Penyewe hapo! Unajua nini? Unanijua mimi?"

"Hapana. Ndiyo nakuona leo," nikamwambia.

"Aaa... mimi ndiyo Charles Gonga. Ulizia Chalii Gonga hapa Masai kila kona nafahamika... huwezi kunikosa..." akasema.

Nikatikisa kichwa kukubali, huku kero za Joy bado zikiendelea kunisumbua.

"We' unaitwa nani?" Gonga akaniuliza.

"JC."

"Aaa... kama JC Penney?" akauliza na kucheka.

Nikatabasamu kidogo tu, nikihisi huyu jamaa alikuwa amesoma sana, ama ni utashi tu wa kujua mambo.

"Sasa ngoja nikwambie kitu JC. Unajua kwa nini nimesema uko vizuri sana?" akaniuliza.

Nikatikisa kichwa kukataa.

"Wewe dogo... hauna show za kishamba. Sijui unanielewa? Nimekuangalia hapo... haushoboki kifala yaani. Napenda sana watu wa hivyo. Wewe ni mgeni si ndiyo? Huku Masai?"

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Hata mimi nimeona. Wa huku washamba sana. Napenda watu wa level yako. Sijui umenisoma? Yaani... ngoja nikwambie kitu... hapa hivi... wanawake hawa wote hawa... wanakutaka. Sijui umenielewa? Wote. Hadi huyu... Joy... ila hawezi akamwambia maana niko hapa anafikiri nitazingua. Lakini wewe ni mwanaume bwana au siyo? Unajua sisi hatuingizagi miguu yote, uwongo dogo langu?" akaniambia hayo.

"Hamna. Ni kweli kabisa," nikamjibu hivyo, nami nikakishika kiganja chake Joy na kukikandamizia kwenye sofa bila kumgeukia.

"Eee... asa'... nimekuangalia. Haupapariki na wanawake. Wewe kwa mwonekano wako... mimi kwa mwonekano wangu... hivi vitu unajua ni vya kuchezea tu, au siyo? Ukitaka naweza kukupeleka sehemu yenye wanawake, tena nikisema wanawake ni wanawake kweli... huku pamekaa kisenge, Joy ndo' anafunika. Haya yanachojali ni pesa, pombe na kuzaa tu... lakini nataka nije nikutoe... nikupeleke sehemu ambayo utakutana na warembo kaka... wanaojua mikakati na wananyonya mpaka unakufwa ganzi! Sijui unanielewa?" 

Kauli hiyo ya mwishoni ikanifanya nicheke kidogo kwa pumzi, nikiwa nimeshaelewa kwamba mwanaume huyo alipenda sana wanawake, na ilieleweka kwa nini hasa kwa sababu alijihusisha na biashara za wanawake kama nilivyoambiwa.

Nikamwambia, "Fresh. Me nimekuelewa."

"Kama vipi tutoke sa'hivi? Bado mapema..." akaniambia.

"Aa... kwa sa'hivi siwezi, kuna ishu nataka kufanya. Labda siku nyingine," nikamwambia.

"Aaa... kwani umeoa? Mapema hii, twende nikuonyeshe mambo mingi wewe! Hizo bia mbili nilizokuwekea hapo? Ndogo sana. Twende upige bia na watoto wa ukweli. Huwezi kuresist..." akanishawishi.

Nadhani alikuwa anataka kunitumia ili kujionyeshea kwa watu fulani, ama labda anihusishe kwenye ishu zake batili, ama huenda hata kuniumiza. Alitoa viashiria fulani vya mtu wa magendo sana, na mimi nilijua jinsi ya kushughulika naye.

Nikamwambia, "Usikonde brother, tutaenda tu. Leo kuna mambo tu nilipanga kufanya mapema kwo' ratiba haitaruhusu. Siku nyingine."

"Au siyo?"

"Yeah," nikamwambia kwa uhakika.

Akanipiga begani kidogo huku akitabasamu, kisha akatoa wallet yake mfukoni na kunipa shilingi elfu kumi. Nikaipokea huku nikimtazama kimaswali.

"Hiyo weka. Nauli. Nitakapokuita usije kusingizia hauna nauli. Ushan'soma? Nipe namba yako..." akaniambia hivyo.

Nikacheka kidogo na kutikisa kichwa kwa kutoamini mambo haya, naye akanipa simu yake ili niandike namba. Nikakiachia kiganja cha Joy ambacho mpaka sasa nilikuwa nimekikandamiza bado, nami nikamwandikia namba upesi na kisha kuitunza kwenye kitabu cha majina cha simu. 

"Huyu ni ndugu yako?" Gonga akaniuliza hivyo.

Alimaanisha Tesha, nami nikamwambia, "Ni rafiki yangu."

"Aaa... anapenda kuparty ila hana hela. Tembea kwenye njia moja na mimi JC... utafurahia sana," akaniambia hivyo kilevi.

Kazi nilikuwa nayo! Hili suala la kutengeneza marafiki mpaka wale wanaotembea na bastola liliikereketa sana akili yangu, lakini nikamkubalia tu jamaa na kwenda upande wa choo ili nikojoe kwanza. 

Kwa kiasi kikubwa, sikutaka kujenga ukaribu na huyo Chalii Gonga. Yeye ndiyo alikuwa analazimisha, maana aliona simshobokei kama wengine walivyofanya, na hivyo akafikiri nina kitu fulani cha pekee sana cha kumfaidisha nacho. Sijui ikiwa ilikuwa ni sura na mwonekano wangu tu, au labda Joy alimwambia vitu fulani, lakini kwa muda huu sikutaka kujali sana. 

Nikamaliza haja na kutoka, na Gonga akanitikisia kichwa kunionyesha namna anavyonikubali pale nilipompita. Nikiwa makini tu, nikamfata Tesha na kumwambia twende, akiwa ameshadata na mpenzi wake mpya wa kulipwa. 

Tukatoka, ikiwa ni saa tano sasa, naye Tesha akaniambia kulikuwa na geti lingine la kutokea nyuma ya jengo hilo kwa hiyo tuitumie njia hiyo kuondoka badala ya kupita kule mbele, nami nikaridhia.

Tukaanza kwenda, mwenzangu akiwa amelewa kweli lakini akijitahidi kutembea kwa mhimili mzuri, na ile tumekaribia kutoka getini, nikaitwa.

"JC..."

Kugeuka? Ni Joy. Agh! Pozi likaniisha. Nilitaka tuendelee tu kwenda maana sikuona haja ya kubaki kumsikiliza mwanamke huyo, nami nikamwambia Tesha tuondoke. 

Joy akaongeza kasi ya kuja na kusema, "JC, subiri basi..."

"Oyo... mtoto huyo..." Tesha akaniambia hivyo kilevi.

"Ah... twende bana..." nikasema hivyo.

"J... naomba unisikilize..." Joy akasema hivyo baada ya kutufikia.

"Tulia... me nawasubiri hapo nje... ah... nakusubiri hapo nje..." Tesha akaniambia hivyo.

Akatoka nje ya geti na kutuacha hapo, naye Joy akajisogeza karibu yangu zaidi na kunishika kiunoni. Nikawa namwangalia tu kwa mkazo.

"JC... nimekumiss..." akaniambia hivyo.

Nikaendelea tu kutulia.

"Unajua... jana penzi lako lilikuwa tamu sana. Sijakojoa muda mrefu kweli, yaani sijui una nini tu kilichofanya nilegee kama jana..." 

Aisee! Nilimwangalia kwa njia isiyoonyesha hisia kabisa, nisiwe na chochote cha kusema maana yote aliyoniambia hayakunipa athari yoyote ile.

"Najua nilikwambia naitaka kwa jana tu, ila leo nimekaa siku nzima nakuwaza mpenzi. Nataka niwe ndani ya mikono yako tena. Nataka unipe... na mimi nikupe mahaba matamu JC..."

Nikaangalia pembeni kiufupi, kisha nikamtazama tena.

"Sema kitu basi..." akaniambia.

"Kitu," nikamjibu.

Akacheka kwa madaha kidogo na kusema, "Nimekupenda sana JC. Ulivyo yaani... ni tofauti na wanaume wengine."

"Na Chalii je?" nikamuuliza.

"Ah, Chalii... unaweza kuchukulia hiyo kama biashara tu. Haniridhishi. Naridhika kwako wewe tu," akaniambia hivyo huku akisugua kiuno changu kwa makucha yake.

"Mbona yeye anakupenda? Ukiwa naye hata kama unapata kidogo si unapaswa kuridhika?"

"Ndiyo haniridhishi sasa!"

"Si umwambie? Amekukazimisha uwe naye?"

"Nitamwambia, ila..."

"Siku ukimwambia, mkaachana, ndiyo tutakuwa pamoja. Umenielewa?" 

"JC... jamani..."

"Nini? Si Umesema hakuridhishi? Mwambie, mwachane, ndiyo tutakuwa wote. Sawa? Mimi mambo ya kushare siwezi. Ila nakuomba kitu kimoja..." nikamwambia.

"Kitu gani?"

"Itoe mikono yako kiunoni kwangu," nikasema hivyo.

"JC... usinifanyie hivi...." 

Kuna watu wakawa wanakuja upande wetu, nami nikaitoa mikono yake kwangu na kuondoka hapo. Alaa! 

Nilikuwa nimejitahidi sana kumwonyesha ustaarabu ili aelewe, hii ikiwa mara ya pili. Nadhani alifikiri kwamba ningelegeza tu tena kama jana, lakini alikuwa amekosea. Sasa hivi ndiyo angeuona uchuma wangu uko wapi; tena yeye pamoja na bwana wake mbeba vyuma. 

Nikamkuta Tesha akiwa anatembea mdogo mdogo tu kuelekea nyumbani, nami nikajiunga naye mpaka tulipofika getini kwao. Akanishauri kwamba niende tu pale kwa Ankia nikapumzike, akinipa sifa kwa kuwa rafiki mwenye kujali mpaka kuhakikisha nimemfikisha kwao salama, nami nikaona nimkubalie tu. 

Nikamwacha na kwenda upande wetu, na gari la Miryam lilionekana mule ndani kwao nilipopatazama kupitia matobo ya uzio, kuonyesha dada mtu alikuwepo tayari. Nikaelekea uani kwanza kukojoa maana ulikuwa umeshanibana tena, kisha ndiyo nikaelekea ndani. 

Eh! Tokea tulipoondoka na Tesha ile mchana ndiyo mpaka sasa hivi nilikuwa naingia ndani hapo, nami nikamkuta Ankia akiwa ameketi kwenye sofa huku akiangalia TV. 

Wakati huu alikuwa amevaa T-shirt nyeupe yenye mikono mifupi, nyepesi kuonyesha michoro ya sidiria aliyovalia kwa ndani, pamoja na khanga iliyofunika umbo lake la chini mpaka kufikia miguuni. Alikuwa amekaa kwa njia ya kushika tama huku akiniangalia sasa baada ya mimi kuingia, akitarajia nimpe salamu bila shaka, lakini nikaufunga tu mlango na kisha kumpita bila kumsemesha hata kidogo. 

Nikaingia chumbani kwangu, nami nikavua nguo zote na kisha kuvaa pensi nyepesi na kaushi ili niende kujimwagia maji kisha nirudi kupumzika. Ingawa pombe ilikuwa inazunguka kichwani, niliweza kutambua kwamba chumba hicho kilitoa harufu ya mbali ya dawa za mbu, kitu kilichoonyesha kwamba Ankia alikuwa amenifanyia wepesi wa kuchoma dawa humo ili kuniondolea kero za mbu. 

Nikajikuta natabasamu tu kwa mbali, nami nikaweka taulo begani na kubeba sabuni kisha kutoka. Nikakuta Ankia akiwa upande wa jikoni akionekana kupakua chakula, naye akaniangalia, lakini mimi nikapita zangu tu na kwenda bafuni. Yeyote angeyaita haya niliyofanya kuwa maringo lakini nilikuwa na maana yangu. 

Nikaoga vizuri, joto la mwili likapungua, nami nikarudi ndani tena. Nikakuta Ankia akiwa amekaa kwenye sofa tena, huku mezani kukiwa na sahani ya udongo iliyofunikwa kwa sahani nyingine ya udongo; bila shaka kukiwa na chakula alichopakua. Mimi nikapita zangu tu kama vile sielewi somo, na kabla sijaufikia mlango wa chumba changu, akaniita.

"JC..."

Nikasimama na kumgeukia, nikiona wazi jinsi alivyonionyesha hisia za msisitizo wa kitu fulani kwa namna alivyoniangalia.

"Chakula... uje ule..." akaniambia hivyo kwa sauti ya upole.

Nikakitazama chakula hicho mezani, kisha nikaingia tu chumbani bila kutoa jibu lolote. 

Nilielewa jinsi gani ya kushughulika na huyu mwanamke, na mpaka kufikia hapo ilikuwa wazi kwamba alitaka kunionyesha ananijali. Sikumlipa kwa haya yote aliyokuwa ananifanyia, lakini ikiwa kuna sehemu yoyote ndani ya fikira zake iliyotegemea nimlipe fadhila alizonionyesha kwa njia YOYOTE ile, basi nilitakiwa kuhakikisha anafuta mawazo hayo. Nilikumbuka vizuri sana yote ambayo Tesha alinieleza kuhusu Ankia, kwa hiyo hili suala ningelikamilisha muda huu huu; ndiyo mambo mengine yafate. 

Nikajipaka mafuta yangu na kuzitengeneza nywele vyema, nikiwa na lengo la kutaka kwenda tena sebuleni ili nizungumze na Ankia kikubwa, lakini mlango wa chumba ukagongwa. Nikijua wazi huyo ni nani, sikutoa itikio lolote na kuendelea kurudishia vitu vyangu sehemu yake ili nikaufungue, ila nadhani kwa kufikiri sikutaka kumfungulia, Ankia akaufungua mwenyewe na kuingia taratibu. 

Nikamwangalia. Mikononi aliibeba ile sahani yenye chakula, naye alikuwa ananiangalia kwa macho yenye kutia huruma sana. Yaani ilikuwa kama vile mtu ambaye amefanya kosa kubwa na sasa anatafuta njia za kupata msamaha, na mimi kiukweli sikufurahishwa na hali ya namna hiyo kutokana na kunipa hisia ya kujiona mwonevu.

Akasema, "JC... nimekuletea chakula."

Sikumjibu. Nikaendelea tu kutulia.

"JC nakuomba tu upokee... ule hata kama umekunywa. Nimekupikia chakula kizuri," akaniambia hivyo.

Nikakaa kimya.

"Nijibu basi. Mbona unakuwa hivyo?"

"Uliniambia nisikusemeshe," nikamjibu hatimaye.

"JC... nisamehe. Naomba tuyasahau hayo... niliongea tu kwa hasira. Nisamehe..."

"Kwa nini unahitaji sana nikusamehe, Ankia?" nikamuuliza.

Akabaki kunitazama tu.

"Njoo. Kiweke chakula hapo..." nikamwambia hivyo.

Nikakaa kitandani, naye akakipeleka chakula kwenye meza na kukiweka kwenye nafasi ndogo iliyoachwa, kisha akaja usawa wangu na kusimama. Nikaushika mkono wake na kumvuta ili akae kitandani kabisa, naye akakaa. Alikuwa ananiangalia kwa macho yenye hisia sana, nami nikawa namwangalia kwa umakini.

"Sijalewa sana, kwa hiyo yote nitakayokwambia ujue nayamaanisha. Umenielewa?" nikamsemesha.

Akatikisa kichwa kukubali.

"Sisi ni binadamu, sawa? Kila mtu ana mapungufu... unajua hilo. Ukiona mtu anafanya jambo usilokubaliana nalo na ukahitaji kuzungumza naye, jitahidi tu kuwa msikilizaji mzuri pia. Huwezi kujua mambo yako vipi kwa upande wake mpaka na yeye uwe umemsikiliza. Hiyo ni kitu ambayo sisi sote tunatakiwa kuwa nayo, na wengi kuikosa ndiyo kunafanya migogoro iwepo. Ukipanick na kuzungumza tu kwa hasira bila kusikiliza... ndiyo mambo kama haya hutokea. Sasa... mimi nakuweka wazi kwa jambo moja. Huwa sipendi kuhukumiwa vibaya hasa na mtu ambaye hanijui vizuri. Wewe ni mwanamke. Nimekukuta hapa. Hatufahamiani vizuri. Ikiwa kuna mambo hupendi nifanye hapa kwako, hasa, ukiwa kama mwanamke, unaniambia, na ninayafata. Ikitokea nimekiuka sheria za hapa, ongea nami, nisikilize pia... kwamba aa, hapa kweli Ankia nimekosea, basi tuangalie hili lisijitokeze tena. Lakini ukianza tu kunirushia maneno... unajiweka position mbaya mpaka nami naanza kutenda vibaya... sipendi hivyo..." nikamwambia hayo kwa upole.

"Ndiyo maana nimekuomba msamaha. Sipendi unikasirikie JC... muda ule nilikuwa najihisi vibaya tu ila..."

"Ankia... nisikilize. Mimi, ama mtu mwingine yeyote yule, kamwe... narudia, kamwe, hapaswi kukufanya uogope kuongoza maisha yako kwa njia unayotaka. Sijui unanielewa?" nikamwambia hivyo.

Akatikisa kichwa kuonyesha uelewa.

"Nimekukuta hapa, una style ya maisha yako, nami nina style ya maisha yangu. Tunapoishi pamoja ndiyo tunajikuta tunafaana ama kutoendana kwa mambo mengi, lakini usiwe mtu wa kuyumbishwa kutoka kwenye misimamo yako eti kisa unaogopa nitakukasirikia kwa sababu nina ya kwangu. Mimi ni nani? Si nimekuja juzi tu? Haukuwa unaendesha maisha kivyako kabla sijaja?"

Akatikisa kichwa kukanusha hilo.

"Sasa? Kwa nini uwe hivyo? Ankia wewe bado ni kijana. Mtu mzima kijana. Sasa hivi mambo siyo kama yalivyokuwa zamani. Usipende kushikilia sana vitu ambavyo vimepita, hautabadili chochote kwenye maisha na utu wako. Hebu jiachie. Kuwa mtu bora unayeweza kuwa badala ya kubaki kujiona kama mnyonge kwa mambo ambayo yameshapita..."

Akawa ananiangalia kwa macho makini zaidi, akionekana kuivuta maana ya maneno yangu kwa kina.

"Mimi Ankia nakwambia ukweli. Nimekuja huku kupumzika tu. Kuishi maisha mengine. Sijaja kuwa kiongozi wa maisha ya mtu. Sijaja kuwa mume wako Ankia. Usinione mimi kama mume wako. Mimi ni rafiki yako. Ukitaka sukari, nakupa kama ninayo. Nikikuomba kitu kizuri ukakataa kunipa kwa sababu zako, me ni nani nikulazimishe?"

"Me siwezi kukunyima..."

"Umeona? Ni WEWE. Ni maamuzi yako. Haya mambo tunayofanya kufurahishana, ni ya kawaida tu. Usiwe unayashikilia sana cause at the end of the day, mwenzako akija kuachia, anayebaki kuumia ni wewe..." nikamwambia hivyo kwa upole.

Akatazama chini na kusema, "Natakiwa kujiachia. Niishi kwa uhuru zaidi."

"Eeeh. Usijali yaani just... ishi. Free kabisa," nikasema.

Akaniangalia na kusema, "Je kama nikisema nakupenda? Utaishi nami kwa kujiachia namna hiyo hiyo hata tukifanya mahusiano?"

"Hilo neno naambiwa sana Ankia kiasi kwamba lilishagakuwa la kawaida mno. Nakwambia hivi kwa sababu nakuona wewe ni rafiki... mimi maisha ya kupendana mpaka kuishi wote, sijui, mume na mke... siwezi. Ukinikubali nikakuelewa, tunatoka. Nikiona unazingua, ninang'oka. Ndivyo nilivyo. Masuala ya kufatiliana sana... a-ah. Nikikwambia nakupenda kama rafiki, elewa iko hivyo tu. Lakini hata kama nikitaka tulale wote na tukalala, hiyo haimaanishi ndiyo nimekupa kibali cha kuning'ang'ania. Hivyo ndivyo JC alivyo... nadhani umeelewa..."

Aliniangalia kwa macho yenye hisia sana, lakini kama vile hisia za kuvunjika moyo, naye akatikisa kichwa kuonyesha uelewa.

"Me nakuelewa sana Ankia. Wewe mwenye nyumba wangu, una moyo mzuri, ndiyo maana nakuweka wazi kwa haya mambo. Usiwe mtu wa kuweka matarajio mengi sana kwenye mambo mengi ili yasije kukuachia maumivu pale yakienda kinyume na ulivyodhania. Umeelewa?" nikamwambia hivyo.

"Ndiyo. Nimeelewa."

"Wala hata hukuwa na haja ya kuomba samahani kwa sababu jana kiukweli... nilikosea. Joy alilazimu tu mambo ila nakuahidi haitatokea tena. Hii ni nyumba yako, na hiki ni chumba chako pia. Sawa?" nikasema.

Akatikisa kichwa kukubali.

"Halafu ulikuwa unapiga hodi ya nini wakati hadi dudu langu ushashika?" nikamuuliza hivyo kiutani.

Akaniangalia na kucheka kwa haya kiasi, nami nikatabasamu pia.

"Umepika nini?" nikamuuliza.

"Ubwabwa, nyama, mchicha. Nikupe ule?" akaniuliza pia.

Nikamshika kiunoni kichokozi na kumwambia, "Vipi ukinipa hiyo tamu nyingine kwanza?"

Akacheka kwa aibu na kufunika uso wake kwa kiganja.

Nikamwambia, "Nakutania tu. Singependa u..."

"Hapana JC... nataka. Nimekuelewa vizuri, usijali. Sitakuwa namna hiyo tena. Ila nakuhitaji sana. Toka juzi ulivyokuja... ninawashwa mno kwa ajili yako..." akaniambia hivyo.

"Wee! Sikujua una maneno ya namna hiyo..."

"Haujui mengi kunihusu mimi pia... na ndo' nataka nikuonyeshe..."

"Wacha we!"

Akacheka kidogo.

"Em' nionyeshe basi..." nikamwambia.

"Nitakuonyesha kesho. Sa'hivi kula, me naenda kulala. Sawa?" akaniambia.

"Aaaa... kwa nini siyo sa'hivi?"

"Ahahah... umelewa wewe..."

"Sijalewa bwana..."

"Hata kama... me nataka unipe ukiwa fresh..."

"Au siyo?" 

"Ndiyo." 

"Ahahah... fresh. Naona umeanza kujiachia kweli, na ninafurahi tu kujua umenielewa. Ngoja nile msosi wako ili kesho kweli niyaonje hayo mahanjumati yako," nikamwambia hivyo na kumbonyeza pajani.

Akacheka kidogo na kisha kusimama. 

Nikawa namwangalia tu kiunoni, naye akanishika shavuni na kisha kunibusu kwenye paji la uso wangu kama wazungu eti, kisha akaanza kuondoka. Nikashusha pumzi ya utulivu na kuinamisha uso wangu. Nilikuwa nimeamua kumwonyesha Ankia upande wa utu wangu ambao sikuufurahia sana; sababu nikizijua mimi mwenyewe. 

Nilihitaji atambue kuwa mimi nisingeweza kuwa kile alichodhani ningekuwa katika maisha yake, na nilipanga kumfanya awe mtu wa kuona mambo kwa njia nyepesi zaidi badala ya kuruhusu mapito tu ndiyo yamwogopeshe kuishi maisha mengine. Kama angeona hayo hayafai, basi sawa tungeishi kawaida tu. Lakini kama alitaka kujichanganya na mimi, basi chochote ambacho ningempa ingekuwa kwa njia ya kirafiki tu. Si ndiyo kazi ya marafiki? Kusaidiana. 

Lakini sikuwa nimekuja hapa kutengeneza maisha pamoja na mwanamke huyu, na kama hilo alilielewa kweli basi tungeendesha maisha vyema, nami ningemwonyesha namna ya kuishi maisha mengine ya kujifurahisha bila kushikilia sana vitu mpaka impe wakati mgumu kuviachia. Maisha ndiyo yalivyo siku hizi, na inaonekana yeye aliyataka yale ya akina Dev na Ottoman, lakini hii ni Bongo, kwa hiyo angetakiwa kuishi kama mbongo kweli. 

Mimi nikavuta tu chakula chake baada ya hayo na kula kiasi, kikiwa kitamu kweli, na baada ya kushiba nikarudisha sahani mezani na kisha kwenda kuzima taa; huyoo kitandani kuutafuta usingizi. Bila shaka kesho ingekuwa na mambo kama yote yenye kusisimua, nami nikajiachia zaidi kitandani hapo ili usingizi uje kunibabua vizuri.


★★★


Nilikuja kuamka kukiwa kumeshakucha vyema, nami nikawa nasikia sauti za mbali kiasi za mtu akifoka kutokea huko nje. Ah sikuzijali sana na kuchukulia kuwa mambo ya waswahili tu, nami nikajinyoosha-nyoosha wee mpaka nilipoamua kunyanyuka kutoka kitandani. 

Bado nilikuwa na wenge la usingizi, nami nikafikicha macho na kuvuta simu yangu. Muda ukiwa ni saa nne asubuhi, kukiwa na jumbe kadhaa kutoka kwa marafiki na missed call pia. Nikajibu nilizoziona kuwa muhimu, na ya mtu mmoja ikanifanya nitabasamu. 

Ilikuwa ni ujumbe kutoka kwa Soraya, mwanamke mweupe aliyefanya kazi dukani kwa bibie Miryam, naye alikuwa amenitumia jumbe za salamu na kuniambia niamke maana ilionekana nilipenda sana kulala. Nikamjibu kuwa ndiyo nimeamka sasa hivi na kuuliza kama alikuwa poa. 

Nikiwa nasubiri jibu, nikaweka umakini zaidi juu ya hiyo sauti iliyokuwa ikiongea kwa njia ya kufoka huko nje, au kulalamika, sikujua. Ilikuwa ya mwanaume, akizungumza kwa hasira, lakini maneno yake hayakufikia vyema masikio yangu. 

Kwa kuona Soraya amekawia kujibu, ikabidi niweke simu pembeni na kisha kuvaa pensi na T-shirt ili kwanza nikaonane na mama mwenye nyumba wangu. Bila shaka nilitarajia mambo mazuri kutoka kwake kwa asubuhi hii, na nilipotoka chumbani kwangu kuelekea sebuleni, hakukuwa na mtu. 

Usafi na mpangilio mzuri wa vitu ulionekana vyema kumaanisha Ankia alikuwa amekwishaamka, lakini hakuwepo hapo. Sauti ya mwanaume huyo huko nje iliendelea kutoa maneno kwa njia ya kulalamika, ikiwa kama ugomvi, nami nikagonga mlango wa chumba cha Ankia na kumwita, lakini hakuitika. Nikaamua nitoke ndani. 

Nilipofika hapo nje, yaani siyo kule nje ya geti kabisa, niliweza kuona kupitia yale matobo kwenye ukuta uliotenganisha nyumba yetu na ya kina Tesha watu wakiwa wamesimama usawa wa geti, na japo sikuwaona vyema sana lakini niliwatambua wawili kuwa Tesha mwenyewe pamoja na mama mkubwa mweusi. Sauti ya mwanaume huyo ilitokea nje ya geti lao, na kwa hapo sikuweza kumwona. 

Nilipoangalia upande wa geti letu kuelekea nje, ningeweza kuona kwamba idadi ya watu waliokuwa wamekusanyika huko ilikuwa kubwa, kama kuonyesha wanashuhudia tukio fulani, nami nikawa nasikia malalamiko ya mwanaume huyo.

"...umekalia ujinga tu! Watoto hawa? Mtoto huyu? Unamwendekeza tu... nazipata habari zake ZOTE! Anarudi usiku amelewa, unamwangalia tu! Ndiyo matunzo bora hayo? Eti wanajamii, hivyo ndiyo tunalea watoto siku hizi? Jitu zima limekaa kubebwa tu... na wewe ni mpumbavu sana! Unawaleaje? Eh? Kwa misingi ipi? Unajionyesha una msimamo sana wakati huwezi hata kusimamia vyote vilivyoachwa na kubaki umejibweteka tu...."

Mh? Huyu mtu alikuwa nani? Alikuwa akiongea na nani?

Nikasikia sauti ya Zawadi mweupe ikisema, "Joshu... hebu acha! Unatudhalilisha hivi kisa nini? Eh? Umeshindwa kuingia ndani mpaka..."

"Niingie ndani kufanyaje? Nataka watu wote wajue na kuziona rangi za huyu mpumbavu leo... ataelewa tu!" mwanaume huyo akasema.

"Joshu!" sauti ya Zawadi mweupe ikanena hivyo. 

Hapo kulikuwa na jambo zito lililokuwa likiendelea, nami nikawaza kuwa bila shaka Ankia angekuwa huko nje. Ni nini kingine ambacho kingesisimua zaidi kwa asubuhi hii kama siyo kujua familia ya Miryam ilikumbwa na nini? Ningehitaji kujua. 

 


★★★★★★★★★

 ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Previoua Next