Mfumo wa Mawakala
FasihiNet Agent System โ Jinsi unavyofanya kazi
Wakala wa FasihiNet ni washirika walioidhinishwa ambao hukusaidia kusimamia, kukuza na kuchapisha riwaya zako โ ili wewe uzingatie ubunifu wako.
Wakala ni Nani?
Wakala wa FasihiNet ni mtumiaji aliyeidhinishwa rasmi na jukwaa ambaye anaweza kusimamia riwaya za mwandishi kwa idhini yake. Wakala si mmiliki wa riwaya โ yeye ni msaidizi wa kitaalamu anayefanya kazi kwa niaba ya mwandishi.
Wakala anaweza kupewa majukumu maalum na mwandishi: kuchapisha simulizi, kuandika na kuchapisha sura, au kuunda rasimu tu. Mwandishi anabaki kuwa mmiliki kamili wa riwaya zake wakati wote.
Ili kuwa wakala wa FasihiNet, mtumiaji anapaswa kupata idhini ya msimamizi (admin) wa jukwaa. Kila wakala lazima azingatie Masharti na Sheria za FasihiNet pamoja na Sheria Maalum za Mawakala.
Faida za Kuwa na Wakala
Usimamizi wa Simulizi
Wakala hukusaidia mwandishi aliyetingwa na majukumu kushughulikia simulizi zake โ kuchapisha simulizi mpya na kurasa bila kukuwa ukisimamia kila hatua.
Kurekebisha Makosa
Wakala anaweza kukagua na kurekebisha makosa ya kiuandishi, sarufi, na muundo โ kuinua ubora wa simulizi kabla ya kuchapishwa.
Kutangaza & Kukuza Mapato
Wakala anaweza kutangaza simulizi ya mwandishi ndani ya jukwaa ili kuongeza wasomaji, kukuza mapato, na kupanua ufikiaji wa hadhira.
Ubunifu wa Simulizi Mpya
Wakala anaweza kuunda rasimu za simulizi mpya kwa niaba ya mwandishi, ambazo mwandishi anakagua na kuidhinisha kabla ya kuchapishwa.
Jinsi Mfumo Unavyofanya Kazi
Mwandishi Anamchagua Wakala
Mwandishi anaenda dashibodi yake โ kichupo "Wakala" โ anamtafuta wakala anayemtaka โ anabonyeza "Mpe Uwakala" na kuweka ruhusa maalum kwa kila riwaya.
Wakala Anakubali au Kukataa
Wakala anapokea arifa katika dashibodi yake. Kabla ya kukubali, anaona onyo kuhusu asilimia ya mapato na masharti ya jukumu. Anabonyeza "Kubali" au "Kataa".
Wakala Anafanya Kazi
Baada ya kukubali, wakala anapata ufikiaji wa kurasa za usimamizi wa riwaya. Anaweza kuchapisha sura, kurekebisha maudhui, au kuunda simulizi mpya โ kulingana na ruhusa alizopewa.
Mapato Yanagawanywa Kiotomatiki
Mapato yote kutoka riwaya inayosimamiwa na wakala yanagawanywa moja kwa moja: 84% kwa mwandishi, 16% kwa wakala. Hakuna malipo ya ziada ya mkono.
Aina za Ruhusa za Wakala
Mwandishi anaweza kuweka ruhusa tofauti kwa kila riwaya:
| Ruhusa | Maana | Kwa Nini |
|---|---|---|
| Simulizi: Chapisha moja kwa moja | Wakala anaweza kuchapisha riwaya mpya bila kukuuliza | Mwandishi aliyemwamini wakala wake kabisa |
| Simulizi: Draft tu | Wakala anaunda rasimu โ mwandishi lazima akubali kabla ya kuchapishwa | Msingi โ inashauriwa kwa usalama |
| Sura: Chapisha moja kwa moja | Wakala anaweza kuchapisha sura bila ukaguzi | Kuharakisha mtiririko wa maudhui |
| Sura: Draft tu | Wakala anaunda rasimu za sura โ mwandishi lazima azikubali | Mwandishi anahitaji kudhibiti ubora |
Mgawanyo wa Mapato
Mgawanyo huu unatumika moja kwa moja kwa mapato yote yanayotokana na riwaya inayosimamiwa na wakala โ ikiwemo malipo ya sura, pass za wasomaji, na bonasi. Hakuna malipo ya ziada.
Masharti na Wajibu wa Wakala
Wakala lazima azingatie vigezo vyote vilivyoainishwa katika Masharti na Sheria za FasihiNet na Sheria Maalum za Mawakala.
Wakala anapaswa kuchapisha simulizi ambayo ana uhakika ni ya mtunzi au mwandishi husika tu. Kuchapisha kazi isiyokuwa ya mwandishi aliyempa idhini kunaweza kusababisha kufutwa kwa akaunti.
Wakala hana haki ya kufanya mabadiliko makubwa ya muundo au maudhui ya riwaya bila idhini ya mwandishi.
Ruhusa alizopewa wakala ni za muda na zinaweza kuondolewa na mwandishi wakati wowote bila sababu โ isipokuwa kwa riwaya zilizoundwa awali na wakala mwenyewe, ambazo zinahitaji ukaguzi wa admin wa FasihiNet.
Wakala hawezi kudai umiliki wa riwaya yoyote aliyoipakua au kuisimamia kwa niaba ya mwandishi mwingine.
Ukiukaji wa masharti haya utasababisha kufutwa kwa hali ya wakala na huenda kufutwa kabisa kwa akaunti, pamoja na kupoteza mapato yote ambayo hayajalipwa.
Ufutaji wa Uwakala
Riwaya zilizoundwa na mwandishi (author-granted): Mwandishi anaweza kuondoa wakala wakati wowote bila kutoa sababu. Hata hivyo, wakala anaonya kuhusu hali hii kabla ya kukubali jukumu.
Riwaya zilizoundwa na wakala (agent-created): Mwandishi lazima atoe sababu ya kutosha ya kwa nini anataka kumfuta wakala. Ombi hilo linakaguliwa na admin wa FasihiNet, ambaye ataamua kukubali au kukataa ombi hilo ili kulinda haki za pande zote.
Tayari Kuanza?
Rudi dashibodi yako ya mwandishi na uchague wakala anayefaa kwa riwaya zako.