Hello! I'm a writer on FasihiNet, passionate about creating compelling stories that transport readers to new worlds.
Habari! Mimi ni mwandishi hapa jukwaa la FasihiNet, kazi yangu ni kuhakikisha msomaji unaburudika na kujifunza kwa wakati mmoja. Naomba mchango wako kwa kufungua baadhi ya kurasa za simulizi yangu nilizofunga🙏.
đź”” Make sure to follow me to get live updates on my latest novels and chapters as soon as they're added!
Mawasiliano
📞 Kwa mawasiliano zaidi, unaweza kunitafuta kupitia WhatsApp:
+255621567672
INTRO........... Usiku wa kiza kinene ambacho kilikuwa kinasindikizwa na mvua ambazo hazikuwa na mpaka wa kuweza kuz…
JIJI LA KAMARI ( GAMBLING CITY)
INTRO........... Usiku wa kiza kinene ambacho kilikuwa kinasindikizwa na mvua ambazo hazikuwa na mpaka wa kuweza kuzielezea vyema, alionekana mwanaume mmoja akiwa ndani ya nguo zake nyeusi tii na begi jeusi usiku huo huku mwili wake ukiwa umefunikwa na koti kubwa jeusi pia ambalo lilikuwa refu kiasi kwamba lilivuka mpaka magotini.
Mikono yake ilifunikwa na gloves nzito nyeusi pia ambapo mkono wake wa kulia ndio ambao alikuwa ameutumia kuweza kushika begi lake mkononi akiwa anatembea kwa mwendo wa haraka haraka huku akiwa makini mno kuonyesha wazi kwamba alikuwa anatakiwa kulifikisha begi hilo salama kabisa sehemu ambapo lilikuwa linahitajika kuweza kufika.
Akiwa kwenye mwendo wake huo wa haraka, wakati amefika katikati ya barabara ndogo ambayo ilikuwa imezungukwa na majengo marefu na pembeni yake kukiwa na vichochoro vingi, alihisi kwamba eneo hilo ni kama lilikuwa na mtu au watu wengine ukiacha yeye hivyo alizidisha hali ya umakini kwa hapo ambapo alikuwa amesimama.
Masikio yake yalimtekenya vizuri mithili ya funguo zinapokuwa zinazamishwa kwenye kufuli na kumpa taarifa hiyo, alikuwa ni mtu wa kuutumia mlango wake wa sita wa fahamu huo wa hisia kwa umakini mkubwa hivyo alikuwa na uhakika kwamba hisia zake zisingeweza kumsaliti kamwe kwani alikuwa akijiamini kwenye jambo hilo akawa na uhakika kwamba kulikuwa na ugeni ndani ya hilo eneo.
Alisimama na kutulia ili kuweza kujua kwamba huyo mgeni alikuwa anatokea upande upi huku akiwa ameyafumba macho yake kuweza kujipa hali ya utulivu zaidi kwenye masikio yake. Akiwa bado amesimama hapo alihisi kama kuna kitu kilikuwa kinakuja kwa kasi sehemu ambayo alikuwa amesimama hivyo aliinama kwa kasi mithili ya radi ya mvua.
Wakati anainama alipishana na shoka ambalo lilienda kukita kwenye ukuta mmoja wa jengo la pembeni. Aligeuka haraka ila wakati anageuka alitumia muda mrefu ambao ulimpa nafasi mtu ambaye alikuwa ameingia hapo kufanya kile ambacho alikuwa anakitaka.
Alihisi kifua kinamuwasha mithili ya mtu aliye tafuna pilipili kichaa maana spidi ambayo mvamizi aliitumia kumkita hapo kifuani haikuwa ya binadamu mwenye mifupa ya kawaida bali alikuwa ni mashine haswa kama namna umeme unavyo safiri kwenye zile njia zake. Alipokea mishindo ya haraka na mabuti makali hali iliyofanya begi kumtoka mkononi huku ikionekana wazi kwamba mabuti hayo yalitokea kwa mtu ambaye alidhamiria kabisa kumuua ndiyo maana hakumpa hata nafasi ya kuweza kumtazama maana mvamizi huyo uso wake ulifunikwa kwa kitambaa cheusi na hata mvamiwaji hakupata hiyo nafasi ya kumtazama kwa ukaribu.
Mwanaume huyo licha ya kurushwa mbali na mabuti hayo hali ambayo ingemfanya auvunje mgongo wake kwa kujibamiza kwenye kuta za mawe mazito za majengo ambayo yalikuwa pembeni, hakuwa fala kufa kijinga namna hiyo. Mkono wake ndio ambao aliutumia kukita kwenye kuta hizo na sio mgongo ambao ulitua ukutani kwa nguvu kubwa.
Kasi ambayo alitua nayo kwa mkono wake ililifanya koti lake kujivuta kidogo na kwenye mkono wake ikaonekana alama ya tatoo (tatuu) ambayo ilisomeka kama 001. Baada ya kujichomoa hapo ndipo aligeuka na kumuangalia mtu ambaye alionekana alihitaji kumuua, mtu huyo alikuwa kwenye mavazi meusi kama yeye na koti kama lake, yaani kiufupi wote walikuwa wamevaa sawa ila utofauti wao ni kwamba mvamiwaji alivaa kofia aina ya pama kichwani ila mvamiaji alikuwa amejifunika tu kitambaa kwenye uso wake hivyo sura yake haikuwa ikionekana kabisa.
Baada ya hapo ulipigwa mkono wa hatari mpaka umeme ulipo katika ghafla ndipo mvamiwaji alitulia akiwa makini maana hakuwa akimuona mtu ambaye alitakiwa kumshambulia huku akiwa amepigwa vibaya na umeme huo kukatika alishukuru japo ilikuwa ni hatari maana angeweza kuuawa bila kujua mhusika yuko wapi ila aliamini kwamba angepata dakika chache za kupumzika maana bila hivyo ni lazima angekufa.
Akiwa anaangaza kwa umakini huku na huko umeme ulirudi tena ghafla na ndipo alipo gundua kwamba ndani ya eneo hilo hapakuwa na mtu mwingine zaidi yake, mvamizi alikuwa ameondoka muda mrefu ila chini palikuwa na karatasi nyeupe ambayo ilikuwa imesainiwa kwa damu huku ikiendelea kunyeshewa na mvua.
Aligeuka na kuangalia pale ambapo begi lilikuwa limedondokea ili kujua usalama wake ila kwa bahati mbaya begi halikuwepo kabisa eneo hilo, alishtuka sana akionyesha hofu ya wazi moyoni na kwenye uso wake hivyo hakuwa na namna zaidi ya kuisogelea ile karatasi ili aweze kusoma kile ambacho kilikuwa kimeandikwa.
“KAMARI YANGU YA MWISHO, NDIYO KAMARI YAKO YA KWANZA” hayo ndiyo maneno ambayo yalikuwa yameandikwa hapo.
Aliogopa sana baada ya kuisoma huku akionekana wazi kwamba mikono yake ilikuwa inatetemeka wakati huo. Hiyo ilikuwa ni kauli ambayo alikuwa anaitumia mwanaume mmoja ambaye alimuua yeye mwenyewe kwa mkono wake miaka kadhaa ambayo ilikuwa imepita huko nyuma, huku begi ambalo lilionekana kuwa na nyaraka mhimu mno likiwa limepotea kizembe.
Inawezekanaje mwanaume ambaye alimuua kwa mkono wake mwenyewe bado awe hai? Hilo begi lina nini mpaka mtu ambaye alisemekana kwamba alikufa aweze kupotea nalo? Nini maana halisi ya JIJI LA KAMARI na jiji hilo lina mambo yapi na siri zipi labda?
Unategemea kukutana na nini humu ndani? Mimi nashika kalamu yangu sasa nakaa mezani, kazi yako wewe ni kuhakikisha unaenda nayo nukta kwa nukta ili uweze kuifunua kila kurasa kuweza kuzisoma serikali tatu kwa wakati mmoja ndani ya JIJI LA KAMARI.
I WANT TO DIE JUDGE ni hadithi ya kijana mmoja aliyeitwa Jamal, ambaye alishuhudia tukio la kutisha ambapo familia yake yote iliuawa kwa ukatili na w…
I WANT TO DIE JUDGE ni hadithi ya kijana mmoja aliyeitwa Jamal, ambaye alishuhudia tukio la kutisha ambapo familia yake yote iliuawa kwa ukatili na wanaume wawili. Jamal aliona mwanaume mmoja akikata kichwa cha baba yake na kuondoka nacho mbele yake.
Kilicho msaidia Jamal kubaki hai ni msaada kutoka kwa mtu ambaye hakujua alitokea wapi. Baadaye aligundua kuwa huyo mtu alikuwa jasusi kutoka idara ya usalama wa taifa.
Jamal alipelekwa wilayani Kyela, jiji la Mbeya, ambapo aliishi kwa miaka saba pembeni mwa mlima Livingstone akifanya mazoezi makali ambayo hakuelewa kwa nini yalifanywa.
Baada ya miaka saba, alikabidhiwa mkufu ambao aliambiwa ulinde kwa maisha yake yote, hata kama inahitajika afe ili kulinda mkufu huo (mkufu ndio chanzo cha kila kitu kilichotokea baadaye). Hapo ndipo safari ya kurudi mjini ilipoanza.
Jamal alikuzwa na kuwa kamanda mkubwa ndani ya jeshi la Tanzania chini ya usimamizi wa mkuu wa majeshi. Lakini alikumbana na matatizo makubwa alipoanza kufuatilia kundi moja lililojulikana kama M96 OWNER'Z, ambalo lilihusishwa na mauaji ya familia yake.
Baadaye, Jamal alishitakiwa kwa kuua makamu wa rais wa Tanzania, ingawa ukweli ulidhihirika baadaye kwamba makamu huyo alikuwa hai. Ilikubaliwa kuwa Jamal alifungwa gerezani kwa kosa la kumwua makamu huyo ambaye alikuwa bado yupo hai.
Jamal alipata nafasi ya kutoka gerezani kwa kushirikiana na serikali, lakini aliambiwa atakubaliana na suala la kumrudisha mwanasheria mkuu wa Tanzania, ambaye alikuwa ametekwa huko MedellĂn, Colombia. Mwanasheria huyo alikuwa ndiye aliyesababisha Jamal afungwe gerezani.
Jamal alikubali kumleta mwanasheria huyo, lakini baada ya kumaliza kazi hiyo, alijikuta akitekwa na kupangwa kuuawa kwa sababu alikuwa anajua siri nyingi za serikali na viongozi wa juu waligopa kuwa angeweza kuwaumbua.
Jamal alipigwa risasi zaidi ya kumi na mwili wake kutupwa baharini. Baada ya mwaka mmoja, kiumbe cha kutisha kilichoingia mjini kilianza kuwashambulia wale wote waliotekeleza unyama dhidi ya Jamal.
Katika ulimwengu wa watu wenye nguvu, alitokea mwanamke aitwaye Catherine, ambaye alidaiwa kuwa mtoto wa mkuu wa kambi ya MAKOMANDO nchini Cuba. Mwanamke huyu alikuwa na nguvu kubwa, na dunia iliamini kuwa hakuna aliyeweza kusimama mbele yake.
Jinsi Catherine alivyovuka mipaka ya nchi na kuingia kwenye maeneo ya hatari? Hii ni hadithi ya kutisha—unataka kujua nini kilijificha nyuma ya mauaji ya makamu wa rais na kifo chake kilichosemekana?
MASWALI YANAYOHITAJI MAJIBU
Kuna nini ndani ya kundi la M96 OWNER'Z?
Je, ni nini kilichofichwa nyuma ya mauaji ya makamu wa rais na yeye kuwa hai, ikiwa ulimwengu wote ulijua kuwa amekufa?
Mwanasheria mkuu ni nani na kwanini alitekwa MedellĂn, Colombia?
Vipi Jamal alionekana kuwa muuaji wa makamu wa rais na madaktari walithibitisha kifo chake hadharani?
Mkuu wa majeshi ni nani na kwanini hakumtetea kijana wake?
Jamal alikufa baharini baada ya kupigwa risasi kumi—ni kweli?
KUMBUKA
Yule aliyeondoka na kichwa cha baba yake, Jamal, ndiye mwanaume aliyeingia Ikulu, akamwua Rais na kuondoka akiwa amepigwa risasi moja tu. Na ndiye huyohuyo ambaye alimpiga mwanaume mwingine aliyetaka kumwokoa, kisha akamkata sehemu zake za siri na kuwarushia mbwa wale.
Hadithi hii ni ya kutisha. Ikiwa ulikuwa unawaza maisha yako kuwa ya huzuni, hakikisha unapata nafasi ya kuisoma hadithi hii bora ambayo haijawahi kuandikwa hapo awali.
Tuliza akili zako, achana na kila kitu kwa muda huu, kwani ikiwa utachanganya mambo mengi, hautaelewa, na utaishi kwa mashaka. Hii ni hadithi bora na ya ajabu ya Bux the Story Teller.
Magic fingers, kalamu ni yangu mwenyewe; Bux the Story Teller.
Inamhusu mwanaume mmoja ambaye alikuwa ni kiongozi wa genge la kihalifu ambalo lilikuwa linaitwa SARAFU KUMI NA TANO.
Mwanaume huyo …
BADO NINAISHI.
Inamhusu mwanaume mmoja ambaye alikuwa ni kiongozi wa genge la kihalifu ambalo lilikuwa linaitwa SARAFU KUMI NA TANO.
Mwanaume huyo alikuwa anasakamwa na mamlaka za usalama ndani ya taifa la TANZANIA kwa miaka kumi bila mafanikio. Ndipo alitumika mwanamke mrembo ANELIA BATON ambaye alimwingiza mwanaume huyo kwenye HONEY TRAP kwa kupitia kikosi hatari kutoka ndani ya shirika la kijasusi kiitwacho HOLY TRINITY, walifanikiwa kumpata mwanaume huyo.
Alihukumiwa kifungo cha miaka sitini gerezani na baada ya hapo angenyongwa. Alipelekwa ndani ya gereza hatari la DOMINIC, huko alikutana na tajiri mmoja ambaye alikuwa amejificha ili kuyalinda maisha ya mwanae ambaye alitekwa.
Tajiri huyo alikutana na mwanaume huyo aliye itwa REMMY CLAUDE na kumuomba akamuokoe mwanae yeye anyemsaidia kumtorosha gerezani. Walifikia makubaliano mwanaume akatoroshwa gerezani.
Huko uraiani alienda kumtafuta mtoto wa kiongozi huyo lakini wakati anafanikisha hilo tajiri huyo alikuja kupata habari kwamba mfungwa huyo aliye Mtorosha gerezani hakufungwa kwa bahati mbaya bali ilikuwa ni mipango yake yeye ili akutane na tajiri huyo.
Alishangaa sana ilikuwaje mtu ajitoe kafara kufungwa gerezani kwa sababu yake? Ndipo akaja kugundua kwamba Remmy alikuwa anautafuta umoja wa watu ambao hawakuwa wakifahamika na tajiri huyo ndiye mtu pekee ambaye angemsaidia kuwajua wote ndani ya umoja huo.
Anakuja kushtuka akiwa amechelewa, mwanaume huyo alikuwa amempata mwanae tayari na kupotea naye hali ambayo ilileta maafa makubwa sana na kulilazimu shirika la kijasusi kuanza na moja kumtafuta.
SARAFU KUMI NA TANO halikuwa pambo bali ilikuwa idadi ya wanafamilia ambao waliuawa kikatili takribani miaka ishirini iliyokuwa imepita ila kwa bahati mbaya mtu mmoja alifanikiwa kuishi.
Sitaki nikumalizie uhondo. Unataka kujua huyo Remy ni nani? Kwanini alijitoa sadaka kwenda gerezani? Huo umoja una nini hasa ndani yake na unaongozwa na nani?
Nini hatima ya maisha ya Remy Claude?
Hili ni moja kati ya andiko ambalo litakufanya ujivunie sana kuyasoma maandishi.
SIMULIZI HII INAPATIKANA HAPA HAPA HIVYO TWENDE SAWA PAMOJA ILI UWEZE KUYAGUSA MAISHA YA BWANA REMMY CLAUDE TUPATE KUMJUA NI NANI HASWA NA ANAHUSIANA VIPI NA TITLE YA BADO NINAISHI AU ASHRAFU NDILO JINA LANGU ✍️🔥
Je wewe ni mdau wa IDAIWE MAITI YANGU? Je wewe ni mdau wa SAFARI YA GAVIN LUCA? Kama jibu ni ndiyo kwanini usiisome SEHEMU YA MW…
SIKU ZA MWISHO!!!!!
Je wewe ni mdau wa IDAIWE MAITI YANGU? Je wewe ni mdau wa SAFARI YA GAVIN LUCA? Kama jibu ni ndiyo kwanini usiisome SEHEMU YA MWISHO ya mtiririko wa simulizi hizi iitwayo SIKU ZA MWISHO - GIZA LA MALAIKA (THE DARKNESS OF AN ANGEL?)........
Hii simulizi ni sehemu ya mwisho au season 3 ya IDAIWE MAITI YANGU ambazo zimetoka kwa collection kama ifuatavyo
1. IDAIWE MAITI YANGU 2. SAFARI YA GAVIN LUCA - LIONELA (THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA) 3. SIKU ZA MWISHO - GIZA LA MALAIKA kwa kiingereza THE DARKNESS OF AN ANGEL
Collection hii inaihusu familia ya GAVIN LUCA na mwanae wa pekee LIONELA GAVIN LUCA. Hivyo kama uliisoma IDAIWE MAITI YANGU ukapata maswali ambayo yalijibiwa kwenye SAFARI YA GAVIN LUCA kisha 👇
SAFARI YA GAVIN LUCA ikatuachia maswali mengi ambayo yanajibiwa ndani ya SIKU ZA MWISHO. Hivyo hakikisha unaisoma hii collection nzima ili uweze kuipata hatima nzima ya maisha ya familia Moja kubwa sana na ya Kitajiri barani Afrika, familia ya GAVIN LUCA.
SIKU ZA MWISHO (GIZA LA MALAIKA)- THE DARKNESS OF AN ANGEL..... Ni sehemu ya tatu na ya mwisho ya mwendelezo wa IDAIWE MAITI YANGU na SAFARI YA GAVIN LUCA (THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA)....
Humu utajua hatima ya familia ya GAVIN LUCA na mwanae wa pekee LIONELA na hatima ya zile nguvu zao.
Kwenye SAFARI YA GAVIN LUCA uliona JABARI akionekana msaliti, hivyo kama unataka kujua sababu nyuma yake kwamba kwanini alimsaliti mkewe wa ndoa? Basi hii ndiyo sehemu sahihi ya kupata majibu yako.
JABARI alituacha wote mdomo wazi baada ya kumuoa LIONELA kisha akaanza kuua familia ya LIONELA Lakini mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Kenya (NIS) alikuwa na ajenda gani hatari kwa Tanzania na familia ya GAVIN ?
KAA NA MIMI TWENDE SAWA MUDA HUU UANZE KULISOMA MOJA YA ANDIKO BORA SANA KUWAHI KUTOKEA TANZANIA.
Mvua ilimwagika kwa nguvu, upepo mkali ukiparaganya miti na radi zikilipuka mithili ya mapigo ya ngoma za kuzimu. Huu si msitu wa kawaida—ni Elnino, …
Mvua ilimwagika kwa nguvu, upepo mkali ukiparaganya miti na radi zikilipuka mithili ya mapigo ya ngoma za kuzimu. Huu si msitu wa kawaida—ni Elnino, kichaka kinachokomeza roho za wasiotarajia, hata mchana ukiwa na giza lisilo na mwisho.
Lakini usiku huu, kivuli kilikuwa kinakimbia kwa kasi isiyoelezeka, miguu yake ikizama kwenye tope zito. Uso wake ulikuwa umefunikwa na nywele chafu na ndevu ndefu, macho yake yakiangaza hofu isiyoelezeka. Alikuwa akitoroka—lakini kutoka kwa nani?
Nyuma yake, wanaume sita walimsakama. Wanne walikuwa wamevaa mavazi ya kininja, wakipotea na kurejea kwenye giza kama manyoya yanayorushwa na upepo, huku wawili wakiwa wamevalia magwanda ya kijeshi. Hakukuwa na huruma katika macho yao—mauti pekee ndiyo aliyoyajua.
Kisu kikubwa kiliruka kwa kasi kuelekea shingo yake, kikapita kwa milimita chache tu. Punde, alikata mwelekeo na hakuwapo tena. Mmoja wa wawinda wake alisimama, akisikiliza kwa makini—lakini upepo ulisambaza sauti kila upande, ukivuruga hisia zake. Walielekezana kimyakimya: "Muaue."
Lakini ghafla… tone la jasho likamdondokea mmoja wao. Akakoki bastola, akaiinua juu, akifyatua bila kusita. Hakuna kilichompata mtu huyo wa kutisha, aliyejirusha kutoka juu ya mti kwa kasi isiyoelezeka. Mikono yao ilikutana kwa sekunde chache, mapambano ya mwili kwa mwili yakaanza juu ya mti. Risasi sita zilifyatuka—hakuna hata moja iliyompata.
Mlio wa mifupa ukasikika. Shingo ya askari mmoja ilikatika kwa sekunde chache tu. Mwili wake ukaanguka huku damu ikimwagika kwa kasi. Mwanaume huyo mchafu hakuwa na muda wa kusherehekea ushindi. Kisu kikubwa kilikuwa kimetua mgongoni mwake, kikamdhoofisha—lakini hakuwa tayari kufa.
Mbele yake kulikuwa na maporomoko makubwa yasiyo na mwisho. Nyuma yake, waninja wanne na askari mmoja wamesimama, wakimtazama kwa macho baridi. Hakuhangaika kugeuka… alijirusha kwenye giza la maporomoko.
"He is not human, he’s completely a devil."
"But no survive, he is no more there."
"Let's go and take Donald’s body."
Walidhani kuwa msako wao umeisha. Lakini walikosea…
Mwanaume huyu alikuwa mfungwa wa miaka 10 katika gereza ambalo hakuna aliyewahi kutoroka kwa miaka 200. Gereza ambalo hakuna mfungwa anayejua lilipo. Lakini leo, mtu mmoja yuko nje.
Nani huyu? Ni kwa nini wanamtaka afe? Na je, kweli ameangamia kwenye maporomoko hayo...?
Inahusu nini, inamhusu nani, kipi kipo nyuma yake?
Mwaka 1991, ni mwaka ambao …
NAFSI ZILIZO TELEKEZWA!!!!! âś…
NINI SIRI YA NAFSI ZILIZO TELEKEZWA?
Inahusu nini, inamhusu nani, kipi kipo nyuma yake?
Mwaka 1991, ni mwaka ambao umoja wa nchi za Kisovieti ulidondoka baada ya kushindwa kwenye vita baridi dhidi ya watu wa Magharibi hususani Marekani. Baada ya vita hiyo kuisha kulikuwa na sababu nyingi sana zilizo wafanya washindwe ikiwemo utaifa na mchango wa nchi za magharibi.
Kwa madhara makubwa ambayo yalipatikana, nchi ya Urusi ilikaa chini kufanya tathmini ili kujua ni wapi walifanya makosa mpaka jambo hilo likatokea nchini mwao. Moja kati ya sababu kubwa ambazo walizipata ni kufeli kwa shirika lao la kijasusi la KGB kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kiusalama kwa asilimia miamoja, waliamini kwamba huenda kama shirika hilo lingekuwa imara mapema na kutekeleza majukumu yake kwa usahihi basi wangeishinda vita hiyo.
Sasa mjadala ukawekwa mezani, walishindwaje? Ndipo ikanukia harufu ya usaliti ndani yao, iligundulika kwamba ndani ya shirika lao kuna watu ambao walikuwa wasaliti na usaliti wao ndio ambao ulifanya shirika hilo kuyumba na kufeli. Sasa wasaliti walikuwa nani na nani? Jina ambalo lilitokezea kwenye makablasha yao ni jina la mwanamke wa miaka ishirini na mitano (IRINA ESPANOVICH). Sasa IRINA ni nani na alitokea vipi kwenye hiyo orodha ya wasaliti?
IRINA ESPANOVICH alikuwa ni jasusi mbobevu ndani ya shirika hilo, Moja kati ya wapelelezi ambao waliaminika mno kiasi kwamba akapata bahati ya kuolewa na moja kati ya maafisa wakubwa ndani ya shirika hilo la KGB. Kuolewa kwake na kiongozi mkubwa wa shirika hilo ikawa nafasi ya yeye kupata taarifa nyingi na za siri za shirika hilo kwa njia ya kawaida ama kuziiba kwa sababu huyo mwanaume alikuwa akiishi naye nyumba moja. Sasa kwenye ule mchakato wa kuwatafuta wasaliti, waligundua kwamba kuna akaunti ndani ya Urusi ilipokea mabilioni ya fedha kutoka ndani ya nchi ya Marekani na walipo jaribu kuichunguza akaunti hiyo ili wajue sababu ya msingi ya pesa nyingi kiasi hicho kutumwa kwa mtu ambaye taifa lake lilikuwa vitani na nchi hiyo ni ipi! Ndipo wakagundua kwamba akaunti hiyo ilikuwa inamilikiwa kwa siri na mwanamke huyo IRINA ESPANOVICH.
Baada ya kuunganisha doti, wakagundua kwamba hizo pesa zilitoka ndani ya shirika la kijasusi la Marekani CIA ambalo wengi huwa wanaamini kwamba ndilo shirika namba Moja kwa ubora zaidi duniani kutokana na kuwa na bajeti kubwa ya uendeshwaji wake. IRINA alipokea pesa nyingi ambazo hata angefanya kazi miaka mia-moja asingeweza kuzipata, CIA wamtumie pesa kama nani? Ikahitimishwa kwamba huyo ndiye msaliti ambaye alikuwa akiwauza kwa CIA ndiyo maana walifeli hivyo ikatolewa amri kwamba asakwe popote alipo, akamatwe, ateswe kisha auawe mrembo huyo.
Bahati ikawa upande wake, mlinzi mkuu wa mumewe akampatia taarifa kwa simu kwamba Maam you are to be killed (unatakiwa kuuawa) hawa watu wanajua kila kitu hivyo KIMBIA (RUN). Alikuwa hatarini hivyo hakuwa na muda wa kupoteza akapotea haraka, KGB hawakumpata mwanamke huyo hivyo ukaanza msako wa kimya kimya kwa sababu waliogopa kuziweka taarifa hizo wazi kwani zingewavua nguo kwa kuonekana ni wazembe mpaka yote hayo yanatokea na hawana taarifa! Hawakutaka aibu wakaamua kuifanya siri kumtafuta huyo DOUBLE AGENT IRINA ESPANOVICH.
Kupotea kwake Urusi mikononi mwa KGB ambao walimpachika jina la LUNATIC GIRL, ukawa mwanzo wake wa kuingia ndani ya nchi ya Tanzania.
Kwanini iwe Tanzania? IRINA alipiga hesabu zake akagundua kwamba kama angeenda nchi kubwa hususani ambazo zina usambaaji wa taarifa haraka wangekuja kumpata tu siku moja hivyo alihitaji kuishi sehemu ambayo hata KGB wenyewe wasingeidhania kwamba anaweza kuwepo na ile amani ambayo imetawala Tanzania ikamvutia kuishi hapa kwani ingekuwa ni ngumu kuja kujulikana kwamba yupo hapa. Yes, mpango ulikuwa sahihi sasa Tanzania angeishije na angeweza vipi kujilinda? Ukawa mwanzo wa kuanzisha jamii ya Siri ambayo aliiita LUNATIC SOCIETY, jina ambalo alipewa na KGB kwa usaliti wake. Kumbuka alikuwa mgeni hivyo asingeweza kuianzisha jamii hiyo mwenyewe ikamlazimu kumtafuta mtu.
Macho yake yakadondokea kwa Novack Nyangasa, mdogo wa raisi wa Tanzania ambaye aliamini angekuwa na nguvu ya kumpeleka anapo pataka yeye. Alimshawishi mwanaume huyo kwa urembo wake na kumpa mpango mzima juu ya utajiri ambao wangeenda kuutengeza, Novack akatokwa na mate ya uchu, akakubali. Jamii hiyo ikaanzishwa kwa nguvu ya mdogo wa raisi ambapo waliwasajili watu wakubwa; wanasiasa wakubwa, maprofesa, wanafalsafa, madaktari bingwa, wafanya biashara wakubwa na kila ambaye walimuona anafaa. Baadae raisi akazipata habari, akachukia sana na kumuita mdogo wake IKULU.
Akamtaka aifute jamii hiyo kwa mwezi mmoja tu pekee, huo mwezi ukatumika kummaliza yeye, raisi akawekwa kati akatakiwa kufa ili jamii hiyo iwepo. Moja kati ya mipango mikakati ambayo waliiweka ili kujilinda ni kuanzisha chuo cha kuwatengeneza vijana hatari kwa ajili ya ulinzi na kufanya kazi yao kwa nguvu pale ambapo ingebidi, zoezi hilo likatua mikononi mwa jasusi wa zamani wa Tanzania ambaye aliachana na kazi hiyo baada ya kuhusika na mauaji ya watu wengi sana, NIKOLAI GIBSON. Mwanaume huyo kwenye moja ya mazao yake alifanikiwa kumtengeneza kijana wa kuitwa YOHANI MAWENGE, bwana mdogo ambaye alimuokota Tandale kwa Tumbo akililia mapenzi na kutaka kujiua kisa uchi wa mwanamke.
Alimfunza namna ya kuwa mwanaume akampa begi la pesa akale maisha kwa mwezi mzima, alale na wanawake warembo ambao aliishia kuwaona kwenye runinga ili ushamba umtoke kisha baada ya hapo alikuwa na kazi naye. Alitengenezwa kikawa kiumbe cha kutisha na Kazi yake ya kwanza ikawa kwenda kumuua mcheza KAMARI mmoja huko BAMBALI Senegal na alitakiwa kurudi na bilioni 30 zilizokuwa mkononi mwa bwana huyo..... Huyu tuna mengi ya kuyasoma kwake ni mhimu sana.
Ukawa mwanzo wa mwanamke huyo wa KGB kuitawala Tanzania kwa miaka takribani thelathini. Lakini baadae Moja kati ya makosa makubwa ambayo waliyafanya ni kumuua mwanasayansi aliyedaiwa kuwa binadamu mwenye akili zaidi nchini.
NAFSI ZILIZO TELEKEZWA ni zipi na za nani? Kulikuwa na utata wa maisha ya mwanaume Edison, bwana ambaye hakuwa na kumbukumbu na kwenye mfuko wake alikuwa anatembea na picha ambayo walidai ni ya mkewe, bwana huyu alikuwa akishangaa kwa sababu yeye binafsi hakuwa na kumbukumbu yeyote kama aliwahi kuwa na mke au familia. Kitu cha kushangaza kwa EDISON ni kwamba alikuwa anatafutwa ili auawe kuliko hata pesa inavyo tafutwa na maskini mpaka yeye mwenyewe akawa anashangaa.
Hali hiyo ilimlazimu kwenda kuishi maisha ya chini sana huko Kigogo Mwisho ili awe salama kwani hakuna ambaye angempata kirahisi akiwa kwenye maisha ya kifukara huko lakini usiku mmoja mvua ikiwa inanyesha akiwa ndani ya kijumba kibovu kwenye mkeka, akapokea simu ambayo ilimtaka atoweke eneo hilo kwa dakika kumi na tano vinginevyo angekufa. Aliduwaa ila hakuwa na namna aliondoka haraka ila kabla hajafika mbali akavamiwa na wanaume wa kutisha ambapo alimuua mmoja akafanikiwa kutoroka.
Safari yake ikawa ni kwenda kwa mlezi wake ambaye ndiye alimpa taarifa hiyo na ndiye alimtaka akaishi huko Kigogo mapaka mambo yakae sawa ili akampe ukweli wa kwanini anatafutwa sana? Kufika kwa huyo mlezi wake ambaye alikuwa ni mchungaji wa KKKT pale Mabibo Mwisho karibu na hosteli za wanafunzi wa NIT, alimkuta mtu huyo yupo kwenye hatua za mwisho za uhai wake. Hakumwambia kitu zaidi ya kumtaka aende nyumbani kwake kwenye banda la mbwa akachukue kitabu ambacho kingemfunulia ukweli kwamba yeye ni nani, kwanini hana kumbukumbu, maisha yake kabla yalikuwaje na kwanini anatafutwa sana na watu ambao yeye alidai hawajui!
EDISON alishangaa baada ya kuambiwa kwamba anatafutwa kwa kuhusika na mauaji ya makomando TISA wa kikosi maamulu cha KOM (KILL ON MISSION).akabaki ameduwaaaa!!!!!!!
Ilishawahi kukukuta kwenye maisha yako ukatakiwa kumuua mama yako mzazi kwa mkono wako mwenyewe? Hilo ni jambo baya na gumu lakini Yes, kuna mwanaume alitakiwa kumuua mama yake aliye mzaa ili nchi iwe salama. Je huyu naye hatima yake ilikuwaje?
Kuna uhusiano gani kati ya hizo NAFSI ZILIZO TELEKEZWA, IRINA ESPANOVICH na EDISON?
Unataka kumjua zaidi IRINA ESPANOVICH? Unataka kuijua kiundani LUNATIC SOCIETY? Unataka kujua uhalisia wa maisha ya EDISON kabla na baada ya hapo? Hizo nafsi ZILIZO TELEKEZWA ndizo hizo za makomando TISA (9) ambao alidaiwa kuwaua au kuna mengine nyuma ya mlango wa siri? Ungana nami kwenye simulizi yangu bora zaidi kuwahi kuiandika kwa mkono wangu....
1. Storyline yake ni kali sana 2. Dialogue (majibizano) yake ni kali sana. 3.Haitabiriki kabisa (huwezi kutabiri kinacho tokea baadae) 4.Lakini pia ina actions kali mno.
Mwandishi ni Mimi FEBIANI BABUYA
KARIBU UWEZE KUZIGUSA KURASA HIZI HAPA HAPA KWA KUTUMIA Coin.
Katika Idaiwe Maiti Yangu, tulimfahamu Gavin Luca, lakini alibaki kuwa na hali ya kutatanisha. Hatukujua k…
Idaiwe Maiti Yangu Season 2 âś…
Gavin Luca
Katika Idaiwe Maiti Yangu, tulimfahamu Gavin Luca, lakini alibaki kuwa na hali ya kutatanisha. Hatukujua kama alikufa au alifanikiwa kuishi. Zaidi ya hayo, hatukuweza kugundua hatima ya nguvu zake wala mustakabali wa mtoto wake katika zile nguvu.
The Odyssey of Gavin Luca inakuja kutoa majibu ya maswali haya yote. Tutajua kilichotokea wakati ule, nini kilitokea kwa Gavin Luca, na ni nini kinatarajiwa kutokea siku zijazo.
Lionela, mtoto pekee wa Gavin Luca, anakuja kuwa kiumbe mwenye nguvu nyingi duniani, akitambua ukweli kwamba baba yake alikuwa mfu. Lakini je, ni kweli alikufa? Hatujapata uthibitisho wa kifo chake, na hakuna ishara ya uwepo wake.
Kama alikufa, kwa nini hakukuwa na dalili yoyote ya upanga wake au alama nyingine za uwepo wake? Kama alifanikiwa kuishi, alifanikiwaje kutoka kwenye hali hiyo? Alipo wapi sasa, na ni nini hatima yake?
Nini Kinaendelea Kuikumba Familia Hiyo Maarufu na Tajiri?
Je, kuna mtu alisahaulika katika The Immortals, au kuna siri nyingine nyuma ya pazia?
Nakaribisha kutazama hii simulizi inayofuata! Hautakiwi kuikosa simulizi hii kwa gharama yoyote ile.
Kabla ya kuisoma hii, hakikisha umesoma Idaiwe Maiti Yangu, kwani ni sehemu ya kwanza ya hadithi hii.
Idaiwe Maiti Yangu inapatikana hapa Fasihinet, ikiwa imekamilika kabisa. Kazi Kwako ✍️
Twende Sawa âś…
WhatsApp: +255621567672
Wao wananiita Bux the Storyteller. Jina langu ni Febiani Babuya.
Ndilo jina ambalo limeishikilia Idaiwe Maiti Yangu.
Hili ni jina la mwanamume mmoja ambaye anatusafirisha mpaka Kenya, ndani ya msitu wa…
GAVIN LUCA
Ndilo jina ambalo limeishikilia Idaiwe Maiti Yangu.
Hili ni jina la mwanamume mmoja ambaye anatusafirisha mpaka Kenya, ndani ya msitu wa Mau, ambako ndiko kila kitu kinapoanzia. Mwanzo wa simulizi hii unaanza na mwanaume huyo akiwa ametekwa na makomando wa Jeshi la Tanzania.
Aliteswa vikali, kisha akauawa kwa kupigwa risasi baada ya kuchomwa moto. Lakini muda mfupi baadaye, jambo la ajabu lilitokea. Mtu mwingine aliingia katika eneo hilo na kuwaua makomando wote, isipokuwa mwanamke mmoja tu aliyenusurika, aitwaye Sarah Martin.
Sarah alishangazwa sana kumwona mwanamume huyo, kwani alikuwa ndiye yuleyule waliyemuua dakika chache zilizopita. Inawezekanaje? Idaiwe Maiti Yangu itatupatia majibu sahihi.
Gavin Luca alikuwa akitafutwa na mamlaka za usalama kwa miaka mingi, mpaka alipokuja kujitokeza hadharani.
Kutokea kwake kulisababisha maafa makubwa ndani ya Afrika, yakiwemo mauaji ya zaidi ya marais wawili.
Mwanaume huyu anatoka katika familia yenye historia ya kutisha na utata mkubwa. Hatimaye, akawa kiumbe wa ajabu kabisa kwenye dunia ya watu wenye mabavu.
Gavin Luca pia aliaminika kuwa na nguvu zisizo za kawaida, ambazo alipata huko China. Kurejea kwake kulianza enzi mpya ya utawala wa familia yake ndani ya Afrika nzima.
Sasa Gavin Luca ni nani? Alitokea wapi? Kwa nini alitafutwa kwa miaka mingi? Ni nguvu za aina gani alizokuwa nazo? Na kwa nini alionekana akiwa hai baada ya kuuawa?
Hii ni simulizi moja bora sana kuwahi kuandikwa hapa Tanzania. Twendeni sawa, tukazifunuue kurasa za kiumbe huyu wa ajabu.
NB: Simulizi hii ni ya kutunga tu. Haina uhalisia wa maisha ya mapenzi, ujasusi, siasa, usaliti, uzandiki, watu, mauaji, nguvu za ajabu, na yote yaliyoandikwa humu ndani.
JUMBA JEUSI ni andiko ambalo linaangazia siasa kwa ujumla wake....
Inaangazia namna …
JUMBA JEUSI......
SIASA NI KAMARI....Je NANI HUIBUKA MSHINDI?
JUMBA JEUSI ni andiko ambalo linaangazia siasa kwa ujumla wake....
Inaangazia namna viongozi duniani wanavyo yatumia madaraka kuhadaa watu lakini pia kufanya mambo ya kutisha...
JUMBA JEUSI ni sanaa ya siasa ndani ya maandishi....utajifunza namna wananchi wanavyo danganywa na wanasiasa, namna wanasiasa wanavyo yafanya mambo ya kutisha nje ya macho ya kawaida ...
Je wananchi wanapaswa kufanya nini kuhakikisha wanaikimbia hiyo hali na kuyapigania maslahi ya mataifa yao?
Kumbuka tu kwenye kundi la wajinga wengi ambao wanadanganywa na wanasiasa huwa wanaibuka watu werevu, sasa watu hao huwa hawataki kwenda na ule ubaradhuli wa wanasiasa na mambo huwa yanaanza kubadilika hapo kwa sababu wanasiasa huwa hawawapendi watu wa namna hiyo.....
Unahisi inakuaje kwenye mtanange wa namna hiyo baina ya watu werevu ambao wanaamua kuyatoa maisha yao kwa ajili ya kuwapigania wengi na mataifa yao? NI WAKATI SAHIHI WA WEWE KUYAPATA MAJIBU KWA KULISOMA ANDIKO HILI.