Hello! I'm a writer on FasihiNet, passionate about creating compelling stories that transport readers to new worlds.
Habari! Mimi ni mwandishi hapa jukwaa la FasihiNet, kazi yangu ni kuhakikisha msomaji unaburudika na kujifunza kwa wakati mmoja. Naomba mchango wako kwa kufungua baadhi ya kurasa za simulizi yangu nilizofunga🙏.
đź”” Make sure to follow me to get live updates on my latest novels and chapters as soon as they're added!
Mawasiliano
📞 Kwa mawasiliano zaidi, unaweza kunitafuta kupitia WhatsApp:
+255743 015 453
Usiishi kwa Matakwa Yako, Ishi kwa Mahitaji Yako" (Live by Your Needs, Not by Your Desires) In a world driven by constant pressure to "want more," th…
Usiishi kwa Matakwa Yako, Ishi kwa Mahitaji Yako" (Live by Your Needs, Not by Your Desires) In a world driven by constant pressure to "want more," this book invites you to take a bold step back — and live intentionally.
"Usiishi kwa matakwa yako, ishi kwa mahitaji yako" is not just a title — it’s a mindset shift. This eBook explores the difference between what we desire and what we truly need to live a fulfilled, peaceful, and purposeful life.
Through honest reflections, relatable real-life examples — like how a discarded pen taught a timeless lesson — and practical insights, you'll learn:
The dangers of chasing endless wants
How to identify your true personal and spiritual needs
Why simplicity can lead to clarity and peace
The hidden value in things and knowledge we often overlook
How to regain control of your time, mind, and energy
"Not everything that feels useless is truly without value. Sometimes, it's just not the right time."
Whether you're feeling overwhelmed by modern life or searching for deeper meaning, this book will challenge your perspective and help you rebuild your life — not on fleeting desires, but on lasting essentials.
Ni kipindi cha mwaka mmoja tangu nirudi nchini Tanzania nikitokea nje ya nchi, ambako niliishi kwa zaidi ya miaka ishirini. Kwa lugha nyepesi, tangu …
Ni kipindi cha mwaka mmoja tangu nirudi nchini Tanzania nikitokea nje ya nchi, ambako niliishi kwa zaidi ya miaka ishirini. Kwa lugha nyepesi, tangu nikiwa mdogo maisha yangu yote yalikuwa nje ya nchi — na siyo katika taifa moja tu, bali katika mataifa mbalimbali, kwenye mabara tofauti tofauti.
Sababu ya kurudi Tanzania, nchi ambayo nina kumbukumbu chache sana za utoto wangu, ilikuwa kutafuta asili yangu, wazazi walionileta duniani, lakini vilevile kutafuta utulivu na amani ya maisha. Nimepitia mengi sana nikiwa nje ya nchi — mambo ambayo kwa mtu wa kawaida hayawezi hata kufikiriwa.
Kwanza kabisa, nilifika Tanzania kwa siri sana. Hata marafiki zangu niliowaacha nje ya nchi sikuwataarifu kuwa nilikuwa nasafiri kwenda nchi gani ya Afrika. Hivyo, hata nilipoingia jijini Dar es Salaam, sikutaka kuishi maisha niliyozoea huko nje; nilitaka kuishi maisha ya kawaida, ili nijifiche dhidi ya watu wanaonifahamu.
Ndiyo, unaweza kushangaa. Ukweli ni kwamba nina maadui wengi sana wanaonitafuta kila kona, na yote hayo yanatokana na historia yangu ya maisha — kuanzia nilivyokuwa mdogo, nilivyojikuta nikiwa nje ya nchi, hadi kazi nilizowahi kufanya huko.
Basi nilipanga chumba maeneo ya Gongo la Mboto, chumba cha kawaida sana ambacho hakikuwa hata na choo ndani. Nilinunua godoro la kawaida na kulitandika chini, nikinunua pia mahitaji madogo madogo. Kwa ufupi, niliishi kama kijana anayeanza maisha ya kujitegemea.
Kwa ukweli, kuanzia hapo niliishi maisha ya kawaida. Nilianza kutumia ujuzi wangu nilioupata nje ya nchi — kuwa fundi na hata mwalimu wa tuition. Yote hayo yalikuwa kwa ajili ya kujitafutia kipato cha kuweza kumudu maisha. Unaweza kushangaa, lakini ukweli ni kwamba nina pesa nyingi sana — nina utajiri unaozidi hata wa Bill Gates au Elon Musk mwenyewe. Lakini kutokana na aina ya utajiri huo, ambao nilipata kwa njia zisizo za kawaida, sikutaka kutumia fedha hizo. Nilihitaji, kwa mara ya kwanza, kutumia hela ambazo ninazipata kwa njia halali.
Ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu niingie nchini Tanzania, hatimaye nilikuwa nimezoea jiji. Watu wengi waliniita kwa majina ya huduma nilizowapatia — wapo waliokuwa wananita fundi, wengine mwalimu, na hata wengine mwanafunzi mwenzao.
Basi bwana, siku moja nikiwa napekua pekua mtandao wa JamiiForums — mtandao ambao nilikuwa nikiupenda hata nikiwa nje ya nchi — niliona tangazo kwenye jukwaa la mahusiano. Lilikuwa tangazo la kawaida sana, lililoonekana kama mzaha.
Tangazo lenyewe lilikuwa la mwanamke aliyekuwa akitafuta mwanaume wa kuigiza kuwa mpenzi wake, kwa malipo ya mwezi. Halikuwa na maelezo mengi zaidi ya kichwa cha habari hicho. Mwanamke huyo aliandika tu sifa za mtu anayemtaka — awe mwenyeji wa jiji la Dar es Salaam, dini yoyote, umri usiozidi miaka thelathini, asiwe na watoto, na awe na urefu wa wastani.
Watu wengi, mara baada ya kuona tangazo hilo, walilidharau. Walianza kulidhihaki kwa kusema, “Ni Mtanzania gani hasa, mwanamke, anayeweza kutafuta mpenzi wa kumlipa?” Wengi walianza kumtusi na kumzushia maneno ya kashfa.
Upande wangu, nilifurahishwa na maoni hayo yote. Hata hivyo, mimi nilikuwa na mtazamo tofauti — pengine kutokana na uzoefu wangu nikiwa nje ya nchi. Kwa namna tu tangazo lilivyokuwa limeandikwa, niliamini kabisa kwamba mhusika alikuwa serious.
Kitu kilichonivutia zaidi, ambacho pia kilifanya wengi wadharau, ni kwamba mwanamke huyo aliweka wazi kiasi cha mshahara: shilingi laki saba kwa mwezi.
Kwanza nililipuuza, lakini siku ya pili nikajikuta kuna sauti ndani yangu ikisema, “Jaribu kuomba, pengine ni kweli.” Basi nikafanya hivyo. Niliandika maelezo yangu mafupi — jina langu, Hamza Mzee, umri wangu, na mwonekano wangu wa kuchanganya damu ya Mwafrika na Mzungu.
Baada ya siku kama mbili, nikiwa nimeshasahau kabisa kuhusu tangazo hilo, asubuhi moja nilipokea simu kutoka kwa namba mpya. Nilipoipokea, mtu alijitambulisha kama ndiye aliyeweka tangazo kwenye mtandao. Ee bwana eeh! Kwanza kabisa, sauti yake ilikuwa ya mwanamke, na kwa sauti hiyo tu niliweza kuhisi ni mwanamke mzuri kupindukia. Hisia zangu hazikunikosea.
Licha ya kushangazwa na ukweli kwamba nilitafutwa kwa ajili ya usaili wa kuwa boyfriend feki, nilivutwa kabisa na sauti yake tamu.
Maelezo kutoka kwa mwanamke huyo yalikuwa mafupi na wazi. Aliniambia nimechaguliwa kwa ajili ya usaili wa kazi hiyo, na kama niko tayari nifike kesho yake kwenye hoteli moja kubwa jijini Dar es Salaam. Bila kusita, nilikubali — nikiwa na shauku na maswali mengi kichwani.
Kwa ufupi, siku iliyofuata nilifika katika hoteli hiyo ambayo ilikuwa na mandhari tulivu na harufu ya kifahari. Sikuwa na wasiwasi — maeneo kama hayo nilikuwa nimezoea. Ni kwamba tu, baada ya kurudi nchini, niliamua kuishi maisha ya kimasikini.
Hapo ndipo nilipokutana na mwanamke mrembo sana aliyejulikana kwa jina la Regina. Niwaibie siri — yule mwanamke mwenye sauti tamu aliyeniambia nifike kwenye usaili hakuwa Regina!
Kukutana na Regina ndio mwanzo wa maisha yangu ya nyuma kunianza kuniwinda tena. Ndipo maadui zangu walipoanza kupata taarifa kuhusu nilipo, wakaanza kunifuatilia — na walipopata habari kwamba nina mpenzi, hata kama ni wa feki, ndipo walipopata nguvu zaidi.
Kijana Masumbuko ambae anaonekana kuwa na uwezo usiowa kawaida , uwezo wa kumfanya mtu kufanya kile anachokitaka yeye kwa kumkonyeza machoni huku…
Kijana Masumbuko ambae anaonekana kuwa na uwezo usiowa kawaida , uwezo wa kumfanya mtu kufanya kile anachokitaka yeye kwa kumkonyeza machoni huku akishidnwa kujua uwezo wake unatokana na nini , anaianza safari kutokea mkoani Tanga kuelekea mkoani Dar es salaam kwa ajili ya kutafuta maisha kama ilivyo kwa vijana wengi ambao wanaamini kuishi ndani ya jiji la Dar es salaam ndio njia rahisi ya kutoboa kimaisha. Kama ilivyokuwa jina lake hakuwa na maisha mazuri wala pesa yoyote mfukoni ya kumuwezesha kufika jijini Dar es salaam, kitu pekee ambacho alikuwa nacho na kujiamini anaweza kukamilisha safari yake hio ni uwezo wake wa kumpumbaza mtu kwa kumwangalia usoni kwa kile ambacho yeye anakiita kwamba ni masaa mawili ya kumbukumbu zake. Hatimae kwa uwezo wake huo wa ajabu anafanikiwa kula na kushiba na kupanda basi ambalo linamfikisha jijini Dar es salaam burea kabisa. Ndani ya jiji la Dar es salaam anakutana na Peter kijana msomi wa chuo kikuu cha Dar es salaam , kutokana na namna ambavyo wamekutana wanajikuta wanakuwa marafiki wa kubwa na Peter anamxchkua Masumbuko na kwenda kuishi nae. Peter ni mtoto wa Irene mwanadada ambae kazi yake ni uchangunduo kazi ya kuuza mwili wake kwa kufanya mapenzi na wanaume tofauti tofauti na kujipatia hela. Irene miaka mingi nyuma akiwa katika harakati za kazi hio , anajikuta anapata mteja tajiri afahamikae kwa jina la Samir, katika hali ya kushangaza tofauti na siku zote ambazo amefanya kazi Samiri anampatia Mimba Irene. Irene anagoma kutoa ujauzito kwa hofu ya kukosa kizazi baadae , hivyo anafanya maamuzi magumu na kulea ujauzito huo na licha ya kujua Samniri hawezi kukubali ujauzito wake anachukua maamuzi ya kijasiri na kwenda kumwambia kama amepata ujauzito wake na hawezi kuutoa kwasababu yta kuogopa kukosa mtoto baadae. Samiri anamfukuza Irene nyumbani kwake na kumwambia hatambui ujauzito huo , lakini licha ya hivyo mke wake Samiri afahamikae kwa jina la Shani anagundua juu ya swala la Irene kubeba ujauzito wa Samiri na jambo hilo linamchukiza sana na kuogopa kwa kudhania kwamba licha ya Samiri kukataa ujauzito huo mbeleni anaweza akamtafuta mtoto wa Irene na kumrisha mali za familia. Kutokana na hilo anaandaa mpango na kukodi mtu wa kumfatilia Irene kila siku na kumpa taarifa zake , miaka kadhaa mbele Peter anazaliwa na anafafikisha umri wa miaka saba na Shani anamtengenezea Irene ajali na anapoteza maisha. Peter anampoteza mama yake bila ya kujua wazazi wake na maisha yanaanza upya anafauafuru vizuri kwenda kidatoi cha kwanza ana anapata ufadhili kwa kampuni ya misaada ya F and R foundation , kampuni ambayo inaongozwa na baba yake Samiri na Peter anafanikiwa kutetea ndoto zake kama ilivyo kwa watoto wengi wenye uwezo na anafdika chuo. Siku moja akitoka kufana ununuzi wa simu katika mall za Mlimani City anajikuta kushangazwa na urembo wa binti mmoja ambae alikuwa akiingia katika maduka hayo kwa jili ya kufanya ununuzi, kitendo cha kushangaa anajikuta simu yake inakwapuiliwa na vibaka na kutokana na tukio hilo linamkiutanisha na Masumbuko ambae anamwahidi Peter anao uwezo wa kwenda kumrudishia simu yake kama tu atamslipa kiasi cha hela. Peter anashangazwa na masumbuko lakini mwisho wa siku anakubaliana na Masumbuko kwseli anafaikiwa kumrudishia Peter simu yake
Roma mbeba mizigo ndani ya soko la Mbagala Rangi Tatu anamdhania Edna Kama mwanamke anaejiuza ,baada ya mwanadada huyu kuwekewa dawa ya usingizi kwen…
Roma mbeba mizigo ndani ya soko la Mbagala Rangi Tatu anamdhania Edna Kama mwanamke anaejiuza ,baada ya mwanadada huyu kuwekewa dawa ya usingizi kwenye kinywaji na maadui zake katika ulimwengu wa Biashara akiwa ndani ya hoteli na Roma anambeba Edna na kumpeleka Geto kwake na afanya nae mapenzi.
Edna kwa Mara ya kwanza analala na Roma pasipokujitambua na kupoteza usichana wake ,baada ya tukio Hilo anaamua kuolewa na Roma kwa mkataba wa Miezi sita ili kuepuka kuolewa na mwanaume asiempenda ,baada ya Roma kufunga ndoa na Edna anakuja kugundua kuwa mke wake anamiliki kampuni kubwa Nchini huku akiwa na utajiri wa kutisha.
Edna anamuona Roma kama mtu asiyekuwa seriasi na maisha kutokana na aina ya mfumo wa maisha yake ,maisha ya kuwa na wanawake wengi swala linalomkasirisha Edna.
Edna anajitahidi kuweka ukaribu na Roma ili kujua sababu ya mume wake macho yake kubadilika Rangi anapokuwa na hasira na kuwa ya kijani huku akiwa na roho ya ukatili mno
Idara na mamlaka za kiusalama Nchini zinashangazwa na uwezo wa Roma wa kuzungumza Lugha zaidi ya ishirini na mbili na wanaanza kutafuta taarifa zinazomuhusu Roma lakini licha ya kupata taarifa inayoonyesha Roma kusomea ndani ya chuo kikubwa Duniani Cha Harvard wanakosa taarifa zingine zinazomuhusu Roma na kuishia kujiuliza Roma ni Nani haswa
Naitwa Rojaz, nikiwa mtoto wa tatu kati ya watoto sita katika familia yetu. Nimezaliwa kwa wazazi ambao walikuwa na ndoto ya kuona watoto wao wanapat…
Naitwa Rojaz, nikiwa mtoto wa tatu kati ya watoto sita katika familia yetu. Nimezaliwa kwa wazazi ambao walikuwa na ndoto ya kuona watoto wao wanapata elimu bora na kufikia malengo yao. Hii ni ndoto ya kila mzazi, kwani hakuna mzazi anayewalea watoto wake bila kutamani kuona wanapata mafanikio katika masomo yao.
Nimeweza kufika kidato cha nne, lakini matokeo yangu hayakuwa mazuri. Nilijikuta nikikosa majibu ya moja kwa moja kuhusu sababu ya kushindwa kwangu. Hata hivyo, najua kuwa uzembe wangu na uzembe wa wenzangu shuleni ulifanya niwe na matokeo duni. Wakati wengine walijitahidi na kuzingatia masomo yao, mimi niliwekeza muda wangu kwenye michezo isiyo na tija. Hii haimaanishi kuwa nilidhihaki elimu, bali mazingira yangu na familia yangu ya kipato cha chini yalichangia katika changamoto nilizokutana nazo. Elimu yangu, kuanzia kidato cha kwanza, ilitegemea michango ya familia, marafiki, na misaada kutoka kwa shangazi au mamdogo.
Kwa kifupi, nilikulia katika familia duni, lakini hiyo haikunizuia kutoka kwa juhudi yangu ya kuboresha maisha yangu.
Damiani mhitimu wa chuo kikuu cha uhasibu , anahitimu masomo yake na kurudi kijijini kwao kwa ajili ya kusubiria upepo wa ajira lakini katika hali ya…
Damiani mhitimu wa chuo kikuu cha uhasibu , anahitimu masomo yake na kurudi kijijini kwao kwa ajili ya kusubiria upepo wa ajira lakini katika hali ya kutokutegemea mama yake kipenzi anapigwa risasi mbili za kifuani na kufa hapo hapo na hio inatokana na kumpatia msaada mwanaume ambae hamfahamu mwenye asili ya ulaya (mzungu ) ambae na yeye alikuwa kwenye hatua ya mwisho ya kupoteza uhai wake kwani alikuwa na jeraha la risasi tumboni ,lakini mzungu huyo kabla ya kupoteza maisha anamkabidhi damiani nyaraka bila kumpa maelekezo ya aina yoyote ile .
Damiani anajikuta anajenga chuki na kisasi kwa watu waliohusika na mauaji ya mama yake , anajiapiza kuwatafuta mahali popote pale na kulipiza kisasi , katika harakati za kuwatafuta wabaya wake anajikuta akifahamu siri nzito iliokuwa nyuma ya kifo cha ghafla cha raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania , anapata waraka ulioachwa na raisi huyo uliopewa jina la KAULI YA MWISHO YA RAIS KABLA YA KIFO CHAKE . JE UNAFIKIRI ATAFANIKIWA KULIPIZA KISASI CHAKE ? JE NI KAULI GANI YA MWISHO ALIO ACHA MHESHIMIWA RAISII KABLA YA KIFO CHAKE ?.
simulizi hii imekamilika , mwandishi ataiweka hapa hivi punde .
Rafaeli anaingia chuo bila kujua kwamba nyumbani amempa ujauzito mfanyakazi wao wa ndani aliyejulikana kwa jina la Magreth. Kutokana na ujauzito huo,…
Rafaeli anaingia chuo bila kujua kwamba nyumbani amempa ujauzito mfanyakazi wao wa ndani aliyejulikana kwa jina la Magreth. Kutokana na ujauzito huo, na kwa kuwa hataki kumchanganya Rafaeli kimasomo, Magreth anakimbilia kijijini kwao bila kumwambia mtu yeyote kuhusu hali yake.
Rafaeli akiwa chuoni anakutana na wanawake watatu kwa nyakati tofauti na kuanzisha nao mahusiano. Hata hivyo, kati ya wanawake hao anatokea kumpenda Nifani kwa moyo wake wote — vivyo hivyo Nifani naye anatokea kumpenda sana Rafaeli. Wakiwa katika penzi zito, wanaahidiana kuoana mara tu baada ya chuo.
Upande mwingine, Magreth anahudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na kugundulika kwamba mimba yake imeota nje ya mfuko wa uzazi. Daktari anamshauri aitoe ujauzito huo kwa sababu ya uwezekano wa kupoteza uhai wake wakati wa kujifungua. Lakini Magreth anakataa kutoa ujauzito huo, akiamini kwamba huo ndio njia pekee ya kuonyesha mapenzi yake kwa Rafaeli.
Je, penzi la chuo kati ya Rafaeli na Nifani litafikia hatima ya ndoa? Na je, Magreth atathibitisha kweli mapenzi yake kwa Rafaeli licha ya kubeba mimba inayohatarisha uhai wake?