Naam kama kichwa cha habari inavyosema hapo juu, ni simulizi ambayo inakwenda kwa jina la I WITNESSED IT ALL..
Je binadamu anaweza kuufikia Uungu? Can he/she reach Godhood? Je Uungu ni nini? Binadamu ni nani? Na ni kwa namna gani binadamu wa kawaida anafika levo ya uungu?
Naam usiwaze wala kujisumbua kutafuta majibu sababu yote yatakwenda kujibiwa katika Simulizi hii kali ya I WITNESSED IT ALL... Tutashuhudia vita dhidi ya binadamu na yeye mwenyewe, dhidi ya ubinadamu wake, dhidi ya ulimwengu, kifupi ni vita dhidi ya kila kitu. Tunakwenda kushuhudia Gods walking the lands!
Unakwenda kushuhudia ni kwa jinsi gani mwanadamu ni kiumbe cha ajabu sana.
Ni simulizi inayomuhusu kijana aitwaye Eruki ambayo ni yatima anayekulia kwenye maisha magumu mpaka anakuja kutimiza miaka 23 anakuwa amepitia mengi na bado ataendelea kupitia mengi sana tu yatakayombadilisha taratibu na kuwa kiumbe kingine kabisa. A monstet, a walking disaster, a God walking the lands
Ratiba ya simulizi ni jumanne, jumatano na Ijumaa, karibu ndugu wasomaji tufurahie simulizi hii yenye kusisimua ipatikanayo FasihiNet.
Kama mwandishi, jambo lenye furaha na kuridhisha zaidi ni kwamba bado nina ujasiri na shauku ya kutengeneza hadithi bora zaidi. Naweza pia kuona mapungufu yangu katika uandishi wangu na kupata suluhisho nzuri za kujiboresha.
Mimi sio mwandishi mwenye akili ya haraka, wala sio kijana mwenye fikra zinazochangamka kila wakati. Nahitaji muda mwingi sana kutunga kila sura. Mara nyingi naandika sura moja tu kwa siku nzima mpaka nakosa hata muda wa kupumzika na kusoma, kuandika sura mbili ni ngumu zaidi. Lakini zaidi ya yote, kile ninachotaka kuhakikisha ni ubora. Watu hukusanyika kwa sababu ya simulizi nzuri, sio vinginevyo.
Kabla sijaaanza kuandika simulizi hii, nilizungumza na marafiki zangu kuhusu kuandika hadithi za fantasia zenye ladha ya Kiingereza kidogo, lakini...
Kwa ujumla, nahitaji sapoti yenu wasomaji wangu, niombeeeni kila la kheri.
